Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matamshi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matamshi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote

3/14/2019

Neno la Mungu | Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli katika Vitendo


Mwenyezi Mungu alisema, “Wale miongoni mwa ndugu na dada ambao daima hueneza ubaya wao ni vibaraka wa Shetani na hulivuruga kanisa. Watu hawa lazima siku moja wafukuzwe na kuondolewa. Katika Imani yao kwa Mungu, ikiwa watu hawana moyo wa kumcha Mungu ndani yao, ikiwa hawana moyo ambao ni mtiifu kwa Mungu, basi hawatashindwa tu kufanya kazi yoyote ya Mungu, lakini kinyume na hayo watakuwa watu wanaovuruga kazi ya Mungu na wanaomuasi Mungu.

3/11/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 9


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 9


   Katika mawazo ya watu, Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu. Mungu haneni lugha ya mwanadamu, wala mwanadamu hawezi kunena lugha ya Mungu, na kwa Mungu, madai ya mwanadamu Kwake ni rahisi, ilhali matakwa ya Mungu kwa mwanadamu hayafikiki na hayafikiriki kwa mwanadamu. Ukweli, hata hivyo, ni kinyume kabisa: Mungu anataka tu “asilimia 0.1” ya mwanadamu.

2/22/2019

Neno la Mungu | "Jinsi ya Kuujua Uhalisi"

Neno la Mungu | "Jinsi ya Kuujua Uhalisi"


     Mwenyezi Mungu anasema, "Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi.

2/18/2019

Neno la Mungu | Maana ya Kuwa Mwanadamu Halisi

Neno la Mungu | Maana ya Kuwa Mwanadamu Halisi


Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ni kitu ambacho kilikuwa hata zaidi kimeshaamuliwa kabla Nilipoiumba dunia. Watu huenda hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho na pia huenda hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda wale walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini, adui Yangu alipoungana katika vita na Mimi, Nilikuwa Nimeshamwambia kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kufanywa watoto wake na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake.

2/15/2019

nyimbo za injili | "Kusudi la Kazi ya Usimamizi ya Mungu ni Kumwokoa Binadamu" | Wema wa Mungu

Nyimbo za Injili | "Kusudi la Kazi ya Usimamizi ya Mungu ni Kumwokoa Binadamu" | Wema wa Mungu


Upendo na huruma za Mungu 
hupenyeza kazi Yake 
ya usimamizi kwa utondoti.
I
Ikiwa mwanadamu ahisi mapenzi Yake ya huruma au la, 
Yeye hachoki kufuatilia kazi Anayohitaji kufanya.
Ikiwa mwanadamu aelewa usimamizi Wake au la, 
kazi Yake huleta usaidizi na utoaji unaoweza kuhisiwa na wote.

2/14/2019

Neno la Mungu | "Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini" | Can Your Faith Gain the Praise of God?

Neno la Mungu | "Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini" | Can Your Faith Gain the Praise of God?

Mwenyezi Mungu anasema, "Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi wewe umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako mwenyewe? Ni mara ngapi wewe umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu wewe kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha. Badala yake, haya ni kutenda ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Kutenda kama huku pekee ndiko hutosheleza Mungu. Desturi yoyote inayompendeza Mungu si kanuni bali ni kutenda ukweli."

2/11/2019

Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Uendelezo wa Sehemu ya Pili"


Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Uendelezo wa Sehemu ya Pili



Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.

Maudhui ya video hii:

Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya Mwanadamu Iliumbika Huku Mungu Akionyesha Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena

2/07/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tendeni Ukweli Mara Mnapouelewa

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tendeni Ukweli Mara Mnapouelewa


Kazi na neno la Mungu vina maana ya kuleta mabadiliko katika tabia zenu; lengo Lake si kuwafanya tu kulielewa au kulitambua na kufanya hilo kuwa mwisho wa jambo hilo. Kama mmoja wa uwezo wa kupokea, hampaswi kuwa na ugumu katika kuelewa neno la Mungu, kwa kuwa wingi wa neno la Mungu limeandikwa kwa lugha ya kibinadamu ambayo ni rahisi sana tu kuelewa. Kwa mfano, mnaweza kujua ni nini Mungu anataka muelewe na kutenda; hili ni jambo ambalo mtu wa kufaa ambaye ana uwezo wa uelewa anapaswa kuwa na uwezo wa kufanya.

2/01/2019

2. Utangulizi Mfupi Kuhusu Usuli wa Kuonekana kwa Kazi ya Kristo wa Siku za Mwisho Nchini China

2. Utangulizi Mfupi Kuhusu Usuli wa Kuonekana kwa Kazi ya Kristo wa Siku za Mwisho Nchini China

   
China ni nchi ambamo joka kubwa jekundu hukaa, na ni mahali ambapo pamempinga na kumshutumu Mungu zaidi sana katika historia. China ni kama ngome ya mapepo na gereza linalodhibitiwa na shetani, lisilopenyeka na lisiloingilika. Zaidi ya hayo, utawala wa joka kubwa jekundu husimama ukilinda katika ngazi zote na umeanzisha ulinzi katika kila kaya. Matokeo yake, hakuna mahali pagumu zaidi ya hapa kueneza injili ya Mungu na kufanya kazi ya Mungu. Wakati Chama cha Kikomunisti Cha China kiliposhika madaraka mwaka wa 1949, imani za kidini katika China bara zilizimwa kabisa na kupigwa marufuku.

1/29/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Sehemu ya Pili

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Sehemu ya Pili

Ili kuelewa tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe lazima muanzie na jambo dogo sana. Jambo hilo dogo sana mnalopaswa kuanzia ni nini? Kwanza kabisa, Nimezikusanya baadhi ya sura kutoka kwenye Biblia. Taarifa iliyo hapa chini inayo mistari ya Biblia, ambayo yote inahusiana na mada ya tabia ya Mungu, kazi ya Mungu na Mungu Mwenyewe.