Neno la Mungu | "Jinsi ya Kuujua Uhalisi"
Mwenyezi Mungu anasema, "Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi.
Kadiri watu wanavyoujua uhalisi zaidi, kadiri wanavyoweza kugundua ikiwa maneno ya wengine ni halisi; kadiri watu wanavyojua uhalisi, ndivyo wanavyokuwa na dhana kidogo zaidi; kadiri watu wanavyopitia uhalisi zaidi, kadiri wanavyojua zaidi matendo ya Mungu wa uhalisi, na ndivyo inavyokuwa rahisi kwao kuacha nyuma tabia zao potovu na za kishetani; kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyomjua Mungu zaidi na kuuchukia mwili zaidi na kupenda ukweli; na kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyofika karibu na ubora wa mahitaji ya Mungu."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni