6/24/2018

Upendo wa Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maombi

  Upendo wa Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu

Danyi     Mkoa wa Sichuan
Kuna hisia ya hatia ambayo huchemka moyoni mwangu kila wakati ninapoona maneno haya ya Mungu: “Tatizo kubwa mno kwa mwanadamu ni kuwa yeye hufikiria tu kuhusu hatima yake na matarajio, na kuyaabudu. Mwanadamu humfuata Mungu kwa ajili ya hatima yake na matarajio; yeye hamwabudu Mungu kwa sababu ya upendo wake kwake. Na kwa hivyo, katika ushindi kwa mwanadamu, ubinafsi wa mwanadamu, uroho na vitu ambavyo sana sana huzuia ibada yake kwa Mungu ni sharti viondolewe. Kwa kufanya hivyo, matokeo ya ushindi kwa mwanadamu yatatimizwa. Hivyo, katika ushindi wa kwanza wa mwanadamu ni muhimu kwanza kuondoa matarajio makubwa ya mwanadamu na udhaifu unaohuzunisha kabisa, na, kupitia hili, kufichua upendo wa mwanadamu kwa Mungu, na kubadilisha maarifa yake kuhusu maisha ya binadamu, mtazamo wake kwa Mungu, na maana ya kuwepo kwake. Kwa njia hii, upendo wa mwanadamu kwa Mungu unatakaswa, ambapo ni kusema, moyo wa binadamu unashindwa” (“Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Imekuwa tu kwa sababu ya hukumu ya Mungu na adabu ya mara kwa mara ambapo hatimaye nimejirudi na kutambua kwamba kile ambacho Mungu hutaka ni upendo wa wanadamu ambao ni dhabiti, safi, na kwamba ni sahihi na sawa kwa viumbe wote kutafuta kumpenda Mungu na kutimiza wajibu wao. Nilitambua pia kwamba wakati watu hawazuiliwi tena na kudura yao ya baadaye na wanaweza kuishi kwa ajili ya Mungu, kazi ya ushindi kwao itazaa matunda. Hata hivyo, nilipokuwa nikifanya kazi kama kiongozi, sikuwa nikiweka juhudi yangu katika kufuatilia ukweli; daima nilitawaliwa na mawazo ya kudura yangu ya baadaye. Kwa sababu ya hili, mara kwa mara ningepitia usafishwaji hadi kiasi kwamba nilikuwa hasi, na hii haikuwa tu hasara katika maisha yangu mwenyewe, lakini pia iliharibu kazi yangu katika nyumba ya Mungu. Hata hivyo, Mungu hakunishughulikia kwa msingi wa makosa yangu. Alinipa fursa nyingi za kutubu. Kulikuwa na hukumu na kuadibu na vilevile kusafishwa kuchungu kutoka kwa maneno ya Mungu, riziki, faraja, msaada, na uchungaji kutoka kwa maneno Yake, Roho Mtakatifu akiniongoza, akinipa nuru, na akinimulikia njia mara kwa mara—ni kupitia mambo haya tu nilipoweza hatua kwa hatua kujinasua kutoka kwa mtego wa Shetani, kutopoteza njia yangu, na kuanza njia sahihi maishani. Ninapofikiria juu ya wokovu wa Mungu kwangu, zamani ni dhahiri sana.
Nilizaliwa vijijini. Nilikuwa na dada watatu, na kwa sababu baba yangu alikuwa mwenye uelekeo wa wazo la desturi la kuendeleza nasaba, aliona heri kupigwa faini ya kuwa na watoto zaidi kuliko sheria ilivyoruhusu badala ya kutokuwa na mwana wa kiume. Kwa sababu suala la kuwapendelea wavulana kuliko wasichana ni kubwa sana vijijini, kaya yoyote ambayo haina mtoto wa kiume huonekana kuwa imekata nasaba yao. Hili lilikuwa jambo lililomsikitisha baba yangu mno, na wazazi wangu walibishana juu ya hilo mara kwa mara. Kulikuwa na vitisho vya talaka mara kadhaa na baba yangu alikuwa akivunjavunja vitu mara nyingi. Siku zote nilikuwa na matumaini ya siku ambayo wazazi wangu hawangepigana tena. Nakumbuka wakati mmoja ambapo binamu yangu alinisemea kwa sauti kubwa "Nasaba ya familia yenu umevunjika!" kwa sababu ya suala fulani dogo. Sikusema chochote niliposikia maneno hayo ya kuhuzunisha sana. Kutoka wakati huo kwendelea, sumu za Shetani za "Nani anayesema wasichana si wazuri kama wavulana," “Mtu anapaswa kuleta heshima kwa wahenga wake,” na “kupata fanaka” zilipata mshiko wa kina katika uketo wa roho yangu. Nilikuza lengo la siri: Mimi ndiye binti mkubwa katika familia, na nitajitahidi kupata utambuzi kwa ajili ya wazazi wangu. Siku moja nitaonyesha kwamba ingawa wazazi wangu hawana mwana wa kiume, kuwa na binti ni bora hata zaidi.
Nilikuwa mwanafunzi mwenye bidii katika shule ya msingi na nilishiriki kwa shauku katika shughuli zote za shule. Mara nyingi nilisifiwa na walimu wangu na pia nilishinda tuzo kiasi. Katika darasa langu nilikuwa mwanachama wa kamati ya sanaa, mwanachama wa kamati ya masomo, nahodha wa timu, na mwanachama wa Shirikisho la Kikomunisti la Vijana. Nilipofika shule ya kati nilikuwa mwakilishi wa darasa la lugha ya Kichina na nilishinda tuzo kadhaa katika kusanyiko la kila mwaka la michezo. Katika kata yetu, walitengeneza video kwa kila Siku ya Waalimu na shule iliandaa utaratibu wa maonyesho. Mwalimu wangu hasa aliomba kwamba nishiriki katika nafasi ya mhusika mkuu. Wakati huo mwalimu wangu aliniheshimu sana, na wanafunzi wenzangu walikuwa na wivu. Baba yangu alipoona kwamba nilikuwa kwa televisheni alitabasamu kwa shauku na kunijivunia sana. Nilipoona tabasamu yake yenye furaha, nilisisimka kwamba ningeshinda utambuzi huu kutoka kwa baba.
Mwishoni mwa mwaka wa 1999, familia yetu yote ilikubali kazi mpya kutoka kwa Mungu, na kwa sababu nilikuwa nikiongozwa na mawazo ya kubarikiwa, nilianza maisha ya kuondoka nyumbani ili kutimiza wajibu wangu. Ili kupata idhini ya kiongozi pamoja na msaada wa ndugu zangu wa kiume na wa kike, nilifanya ilivyowezekana kuvumilia shida katika kutimiza wajibu wangu, na ningefanya kila nililoweza kufanya kazi yoyote iliyohitajika na nyumba ya Mungu au iliyopangwa na kiongozi. Wakati huo, nilikuwa mmoja wa watu wa juu miongoni ma wafanyakazi wenzangu katika kazi ya injili, na kila mradi wangu ulikuwa ukizaa matunda. Ijapokuwa ufahamu wangu wa ukweli ulikuwa wa juujuu, wakati ndugu zangu wa kiume na wa kike walipokuwa na hoja nyumbani, matatizo katika kazi zao, au shida na kuingia kwao kwa maisha, daima ningetafuta maneno ya Mungu na kufanya ushirika nao. Ndugu zangu wa kiume na wa kike walielewana vizuri nami na kiongozi aliniheshimu sana. Hatua kwa hatua nilianza kujihisi kuwa nilikuwa mwenye kipaji adimu katika nyumba ya Mungu. Mwanzoni mwa mwaka wa 2006, nilipandishwa cheo kuwa kiongozi wa eneo, na nilipoona kwamba matunda kutoka eneo ambalo niliwajibikia yalikuwa bora kiasi kuliko katika maeneo mengine, niliwaza mwenyewe: Ingawa sijatekeleza wajibu wa aina hii, mimi hutekeleza kila mradi haraka zaidi kuliko wengine na matokeo ya kazi yangu pia ni bora. Kiongozi pia anataka kunifundisha; kama wazazi wangu wangejua kwamba ningeweza kutekeleza wajibu huu sijui wangekuwa na furaha kiasi gani. Hasa nilipokwenda kwa makazi yangu ya kudumu, daima kulikuwa na hisia ya kurudi nyumbani kwa utukufu, na nilitumaini kuwa ningewaona ndugu wa kiume na wa kike zaidi ambao walinijua ili waweze kujua kwamba wajibu nilioutekeleza ulikuwa kwa daraja hilo. Nilikuwa nikiishi katika hali ya kuwa wa kujishukuru, na hata jinsi yangu ya kuzungumza ilikuwa imebadilika. Nilikuwa nimeanza kulenga kuhusu picha yangu kwa macho ya watu wengine. Kwa wakati huo, sikuwa nimelenga tena kuweka jitihada yangu katika neno la Mungu na sikutafuta tena kuingia kwa maisha. Badala yake, nililenga maoni ya kiongozi na ukadiriwaji wangu, na kama watu niliowafanyia kazi waliniunga mkono. Baada ya muda, sikuwa na uwezo tena wa kutatua masuala kanisani au michepuko au matendo ya kuacha katika kazi ya wale niliowafanyia kazi. Wakati wa kukutana na wafanyakazi wenzangu sikuweza kushiriki tena ushirika wowote nao. Hili lilikuwa chungu sana kwangu, na nilijihisi kama dubwana, anayeishi gizani. Mwishowe, sikukosa kupandishwa maaraka tu, lakini nilibadilishwa. Wakati huo nilikuwa nimesononeka sana, na nikawaza mwenyewe: Kama wazazi wangu na ndugu wa kiume na wa kike wanaonijua wakijua kwamba nimebadilishwa, wangenifikiria nini? Sitaweza kupata ufahari wa familia au kwenda mbele. Inaonekana kama nimekwisha, na sina mustakabali wa kuongelea. Nilikuwa nimekata tamaa sana na sikuwa tayari kusoma neno la Mungu, kuomba, na sembuse kuwa tayari kuwaona au kuwasiliana na ndugu zangu wa kiume na wa kike. Udhaifu na hali hasi katika moyo wanguno haya kutoka kwa Mungu: “Katika kutafuta kwenu, mna dhana, matumaini, na siku za baadaye nyingi sana za kibinafsi. Kazi ya sasa ni ili kushughulikia tamaa yenu ya hadhi na tamaa zenu badhirifu. Matumaini, tamaa ya[a] hadhi, na dhana yote ni mifano bora kabisa ya tabia ya kishetani. Sababu ambayo vitu hivi vipo katika mioyo ya watu ni kwa sababu hasa sumu ya Shetani daima inaharibu fikira za watu, na watu daima hawawezi kuondoa majaribu haya kutoka kwa Shetani. Wanaishi katikati ya dhambi ilhali hawaiamini kuwa dhambi, na bado wanaamini: ‘Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima Atupe baraka na kupanga kila kitu kwa ajili yetu ipasavyo. Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima tuwe wa cheo cha juu kuliko wengine, na lazima tuwe na hadhi zaidi na maisha zaidi ya baadaye kuliko mtu mwingine yeyote. Kwa kuwa tunaamini katika Mungu, lazima Atupe baraka bila kikomo. Vinginevyo, hakungeitwa kuamini katika Mungu’” (“Mbona Huko Tayari Kuwa Foili[b]?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila sentensi ya maneno haya ya ufunuo na Mungu iliushika moyo wangu. Kwamba nilibadilishwa ilikuwa ni tabia ya Mungu ya haki iliyonifika, na ilikuwa ni kushughulikia shauku za hadhi moyoni mwangu. Tangu nilipokuwa msichana mdogo, sumu ya Shetani ya “Mtu anapaswa kuleta heshima kwa wahenga wake,” “Mtu anapaswa kuleta heshima kwa wahenga wake,” na “kupata fanaka” ilikuwa ikipotosha mawazo yangu kwa mfululizo kiasi kwamba maoni yangu kuhusu imani katika Mungu yalikuwa yamekuwa mabaya kwa namna isiyovumilika. Kwa uelekeo wa utawala na aina hizi za mawazo, nilikuwa nimefanya kazi kwa bidii mno katika kutimiza wajibu wangu, nilikuwa nimekimbia kwa bidii hapa na pale kwa miaka mingi, lakini kwa kweli nilikuwa nimetaka kumtumia Mungu kufikia malengo yangu ya kufanikiwa na kupata ufahari wa familia. Nilikuwa wa kudharauliwa sana! Hunde sana! Kupitia ukweli na hukumu ya maneno Yake, Mungu alifichua kwamba taswira zangu za ndani juu ya ukimbizaji zilikuwa kabisa sawa na Shetani. Nilikuwa kwa njia ya kushindwa, na bila hukumu ya Mungu na kuadibu za wakati wa kufaa, ningeendelea kushikilia aina hii ya ukimbizaji na mwisho, ningeweza tu kuanguka kwa uangamizwaji wangu na kufika mwisho sawa na wa Paulo.
Nilifikiria kuwa kulistahili kuwe na mabadiliko kiasi baada ya kupata ufahamu huu, lakini kulikuwa na ufunuo mwingine mnamo mwaka wa 2008 ambao ulinilazimisha kuona kwamba mabadiliko katika tabia hayakuwa rahisi kama nilivyokuwa nimefikiria. Sikuweza kubadilika tu kutokana na kuwa na ufahamu mdogo wa maoni yangu ya ukimbizaji baada ya kupitia usafishwaji kiasi. Ni kwa kupitia tu hukumu ya muda mrefu na kuadibiwa ambapo mabadiliko yanaweza kupatikana. Wakati huo nilikuwa nimepewa kazi ya unyunyiziaji kwa ajili ya Mungu katika eneo jingine. Wakati mkutano na dada aliyekuwa msimamizi wa kazi ulipokwisha, nilianza kupima moyoni mwangu ni nani kati yetu aliyekuwa hodari katika ushirika, na cheo changu kilikuwa kipi. Nilizingatia hasa maoni na mitazamo kunihusu ya dada msimamizi wa kazi hiyo. Nilipoona kwamba alikuwa akimsikiliza dada mwingine, nilihisi kwa kweli nimechanganywa. Aliponiitaka kwenda kuwanyunyizia viongozi wa kanisa na mashemasi, nilidhani ilikuwa tu kupoteza uwezo wangu na nilihisi kuwa hakujua jinsi ya kusimamia watu. Ningeweza angalau kuwanyunyizia viongozi wa wilaya na wafanyakazi. Kwa sababu hii nikawa bila rajua na kusikitika na nikapoteza hiari yangu ya ukimbizaji. Nilikuwa nikiishi katika hali hasi. Ingawa nilikuwa nimezuiwa na matatizo mara kadhaa, sikuwa nimeliwazia jambo hilo kwa vyovyote. Baadaye tabia ya Mungu ya haki ilinijia na ugonjwa wa kibole ulinirudia, lakini bado sikuugeuza moyo wangu mgumu. Hilo lilikuwa, hadi wakati mmoja nilipoweka chupa ya dawa ya kutibu ukavu na mwatuko wa mguu nyuma ya kiweko cha usiku katika nyumba ya familia mwenyeji. Msichana mwenye umri wa miaka saba alifikiria kilikuwa ni kitu kizuri na kukinywa kwa siri, na baadaye alikuwa chini, akifumbata tumbo kwa maumivu na kulia. Wakati huo nilikuwa na hofu kiasi kwamba sikujua cha kufanya. Dada yangu katika familia mwenyeji kwa haraka alimpeleka mtoto kwa zahanati ya jamii ili kumwokoa, na daktari akasema: "Tumbo la mtoto ni nyembamba sana, lakini hukumpeleka kwa Hospitali ya Watoto. Unataka kumngojea tu afe?" Miguu yangu ilionekana kama imekufa, na wakati nilifikiria kile daktari alichokisema, nilikuwa na wasiwasi sana. Sikujua hata jinsi nilivyotembea kurudi kwa familia mwenyeji wangu kutoka kwa zahanati. Niliwaza mwenyewe: Kama mtoto kwa kweli atafariki, wazazi wake watachunguza kilichotokea …. Nilivyozidi kufikiria kulihusu ndivyo niilivyozidi kuogopa sana. Nilitaka kulia lakini hakuna machozi yaliyotoka. Wakati ulipita sekunde moja na dakika moja kwa wakati mmoja. Sikuweza kujituliza—nilikuwa nateseka kweli. Nilipitia maneno ya Mungu na niliona yafuatayo: “Naamini kwamba ni bora zaidi kwetu kutafuta njia rahisi sana ya kumridhisha Yeye, yaani, kutii mipango Yake yote, na ikiwa utatimiza hili kwa kweli utakamilishwa. Je, hili si jambo rahisi, la kufurahisha? … Katika kazi ya Mungu leo, Yeye hakasiriki kwa urahisi, lakini watu wakitaka kuvuruga mpango Wake Anaweza kubadilisha sura Yake mara moja na kuigeuza kutoka kuwa yenye kung'aa hadi ya kuhuzunisha. Kwa hiyo, Nakushauri kutulia na kutii mipango ya Mungu, mruhusu akufanye uwe mkamilifu. Hii ndiyo njia pekee ya kuwa mtu stadi” (“Njia… (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kutoka kwa maneno ya Mungu niliona kuwa tabia ya Mungu huwa haivumilii makosa ya watu; niligundua kuwa matendo yangu yalikuwa yameleta karaha ya Mungu na kuamsha hasira Yake. Ili kunionyeshea njia, Alikuwa ameniacha nijue jinsi ninavyopaswa kushiriki katika ukimbizaji. Nilipokuwa mgonjwa na katika maumivu, sikujichungua hata kidogo. Mungu tena alitumia tukio la msichana mdogo kula dawa ili kuniadibu, kunifanya niteseke, kunifanya niweze kuweka mambo haya kando, nifuatilie ukweli, na kutii mipango ya Mungu. Mungu hakuweza kuvumilia kuniruhusu nipumbazwe na Shetani, kupigana sana na kukurupuka kwa ajili ya sifa na hadhi. Aina hii ya kuadibu, hukumu, na utakaso kwangu ilikuwa juhudi Yake ya mwisho, kunifanya nione shimo lenye uketo la hadhi ambamo nilikuwa nimenaswa. Uzoefu wa mara kadhaa wa kuadibiwa haukuwa umeuamsha moyo wangu; bado sikuweza kujinasua kutoka kwa udhibiti na mateso ya asili ya kishetani ndani yangu. Kwa kuwazia, wakati nilipoanza kufanya kazi hiyo, nilijidai kwa kujipambanua, na niliamini mwanzo kuwa ningepandishwa cheo kwa lengo muhimu; sikuwa nimefikiria ya kwamba ningeshushwa cheo hadi kazi ya kiwango cha chini. Watu ambao nilifikiri kuwa hawakufikia kiwango changu walikuwa wakiwanyunyizia ndugu wa kiume na wa kike katika ngazi za uongozi kwa wilaya, na baadhi yao hata walipandishwa vyeo huku matarajio yangu yakionekana kudidimia. Niliwaza: Kurudi nyumbani kutakuwa bora zaidi kuliko kutimiza wajibu wangu hapa. Kwa hiyo, nilipokutana na viongozi wa kanisa, nilianza tu kufanya mambo kwa namna isiyo ya dhati. Sikuchukua wajibu wowote juu ya maisha yao, na sikubeba mzigo wowote wa kweli kwa masuala mbalimbali ndani ya kanisa, sembuse kuzingatia mapenzi ya Mungu. Wakati huo, nilipokabiliwa na maneno ya Mungu yaliyojaa fadhili na upendo, nilihisi kuwa na deni kubwa Kwake. Mawazo ya Mungu ni kwa maisha ya wanadamu, na Yeye hutoa kila kitu kwa ajili ya binadamu; huku ni kuwaokoa kabisa wanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Lakini sikuwa tayari kutoa chochote katika kazi yangu kwa ajili ya Mungu. Kiini cha shida kilikuwa kwamba daima nilikuwa nimefungwa na kutawaliwa na sumu ya Shetani. Nilikuwa kama mtoto mjinga ambaye hakuwa na ufahamu wa nia njema za wazazi wake; nilikuwa nimepoteza fursa nyingi sana za kukamilishwa na Mungu. Ni kuwa tu na uzinduzi mara moja mambo yalipofikia kiwango hicho—si kulikuwa kumechelewa mno? Nilianguka chini, kama nimejaa majuto na kujilaumu: "Ee Mungu! Hukumu na adabu vilivyonijia leo yote ni haki Yako. Niko tayari kutii. Kama bado kuna fursa, niko tayari kujibadilisha mwenyewe, kutohangaika tena kwa ajili ya jaala yangu ya baadaye. Niko tayari kuwa tu kiumbe mdogo mkononi Mwako, kutimiza wajibu wangu ya kunyunyizia vizuri niwezavyo, na kuufariji moyo Wako." Baada ya kumaliza kuomba, moyo wangu ulitulizwa. Nilikuwa tayari kujitoa kabisa kwa Mungu, na tayari hata zaidi kumkabidhi huyo msichana mdogo kwa Mungu kabisa. Baada ya muda mfupi, nikasikia sauti ya huyo dada katika familia yangu mwenyeji akifungua mlango, na yule msichana mdogo akasema kwa sauti: "Shangazi, utanishika?" Kisha akaniambia kimya kimya: "Shangazi, ni lazima uliweke jambo hili kama siri kabisa; huwezi kumwambia bibi yangu kwamba nilikunywa maji yako!" Wakati huo huo moyo wangu hatimaye uliwekwa huru, kuona kuwa Mungu alikuwa ametumia werevu wa ninani anayewajua watu wangapi, matukio, na vitu ili kuniokoa, "jiwe" hili. Nilihisi kama nilikuwa asiyestahili kabisa. Kutoka wakati huo na kwendelea, nia zangu hazikuwa tena kwa ajili ya jaala yangu ya baadaye. Nilikuwa tu mwenye busara na hekima na nikafanya lililowezekana ili kutimiza wajibu wangu wa kunyunyizia ili kuufariji moyo wa Mungu. Sikufanya tena mambo kwa namna isiyo ya dhati tu, na wakati niligundua kwamba kulikuwa na michepuko na matendo ya kuacha katika kazi za ndugu zangu wa kiume na wa kike, niliwasiliana nao tu kwa uvumilivu, nikawasaidia, na kuwaauni. Kupitia ushirika wangu na ndugu zangu wa kiume na wa kike nilipata ukweli kiasi, na wakati huo huo kujifunza masomo fulani kutoka kwao. Wakati huo sikuwa ninaamini tena kwamba uwezo wangu ulikuwa unapotelea bure. Nilielewa nia njema za Mungu, na kwamba kutimiza wajibu huu kulikuwa kilichohitajika katika maisha yangu. Ilikuwa ni Mungu akinikusudia mazingira kulingana na dosari zangu, kuzifidia. Ninamshukuru Mungu! Kuanzia wakati huo na kwendelea, niliweza kutimiza wajibu wangu kwa amani. Sikuwa nimewaza kwamba kabla ya muda mrefu mno, kiongozi alizungumza nami na kuniuliza kuwanyunyizia viongozi na wafanyakazi wa wilaya zilizokuwa katika maeneo mawili. Kisha nikaona tabia ya Mungu ya haki, kwamba Yeye huchunguza vina vya moyo wa mwanadamu na anasimamia kila kitu. Kile Mungu anachopenda ni mtu mwenye kuhusika na mambo halisi na ambaye hutimiza wajibu wake. Ninamshukuru Mungu kwa kunipa fursa ya kutimiza wajibu wangu. Nilipokuwa nikikutana na viongozi wa wilaya niligundua masuala fulani na kuyashughulikia kwa bidii. Pia niliandika masuala yaliyotambuliwa katika kila mkutano, matatizo yaliyokuwa yameenea sana, jinsi nilivyokuwa nikiyatatua, na ni matatizo gani niliyokuwa sijayatatua. Baada ya muda nilihisi kuwa kutimiza wajibu wangu kwa njia hii lilikuwa jambo lenye uhalisi. Moyo wangu ulikuwa na utilivu na amani, na sikuwa tena chini ya utawala wa sumu ya "kwendelea mbele." Nilihisi kama nilikuwa nimejiandaa na kuelewa baadhi ya ukweli katika vipengele mbalimbali, kwamba ningeingia na ndugu zangu wa kiume na wa kike, kwamba nilikuwa mtu asiyetaka kujitangaza. Nilielewa kuwa kutimiza wajibu wangu kama kiumbe ni kanuni isiyoweza kubadilika, na kwamba ni lazima niwe kama askari tu, kutii amri kama wajibu wangu mtakatifu, sio kuzingatia au kujipangia mwenyewe, lakini katika kila kitu kufanya maslahi ya nyumba ya Mungu kuwa muhimu. Hili ndilo viumbe wanalopaswa kufanya.
Mwishoni mwa Februari mwaka wa 2012, nilihamishiwa kwenda jimbo jingine kutekeleza wajibu wangu. Wakati huo moyo wangu ulikuwa na utulivu sana, na sikuwa naangalia kwa wivu kama nilivyokuwa nimefanya awali. Nilipokuwa nimekwisha tu kwenda kuchukua nafasi hiyo ilitokea kuwa ni wakati ambapo kaya ya Mungu ilikuwa ikisafisha kanisa. Ya hapo juu yakisemwa katika mpango wa kazi: "Kazi ya kusafisha aina tano za watu katika kanisa inapaswa kukamilika kabla ya likizo ya Sikukuu ya Wafanyakazi ya mwaka wa 2012. Kwa sababu kazi ya kusafisha ni kuandaa njia ya kupanua kazi ya injili ya ufalme, ni lazima kabisa isiathiri kazi ya injili" ("Mungu Hutukuzwa Kikamilifu Tu kwa Kusafisha kabisa Kanisa na Kuhakikishia Upanuzi Sawa wa Injili ya Ufalme" katika Kumbukumbu za Ushirika na Mipango ya Kazi II). Viongozi fulani na wafanyakazi walihitajika kubadilishwa kwa haraka; kila kipengele cha kazi kilikuwa karibu kusimama. Kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, sikumezwa na matatizo kwa wakati huo. Nilipokuwa nikiwarekebisha viongozi na wafanyakazi, nilikuwa nikiwaanda watu wafaao wakusanye vifaa vya wale waliokuwa wameondoshwa na kufukuzwa. Hata hivyo, ilipofika mwishoni mwa Machi, niliona kuwa bado hakukuwa na taarifa hata moja ya kumfuta mtu iliyokuwa imetolewa. Kwa kweli nilipitia usafishwaji katika moyo wangu. Nilikuwa nimejaa sababu na nyudhuru; nilijiwazia mwenyewe kwamba nilikuwa nikifanya mazoezi tu ya kutekeleza wajibu huu, kwamba sikuwa wazi kuhusu ukweli, na singeweza kuendelea tena na kazi yangu ya kuongoza juhudi hii. Nilipokuwa tu nikipata usafishwaji, dada aliyesimamia kazi hiyo aliniita ili kunishughulikia. Nilikuwa na hasira sana wakati huo na sikuwa tayari kukubali. Nilihisi kukosewa katika moyo wangu. Niliwaza: Ndiyo tu nimewasili hapa, unajua vizuri sana kazi yangu ilivyo. Nimekuwa nikifanya kila kitu ninachoweza ili kushirikiana, na hunifariji, lakini badala yake kunishughulikia. Hivi tu, nilikuwa nikiishi katikati ya usafishwaji na neno "kubadilishwa" lilikuwa linanisumbua akili. Ingawa nilikuwa nikifanya kazi hiyo, nilikuwa nimepoteza imani yangu, na daima nilikuwa nikifikiri: Wakati huu huenda nibadilishwa kwa sababu inasema katika mpango wa kazi kwamba viongozi ambao hawawezi kufanya kazi ya kuwaondosha na kuwafukuza aina tano ya watu ni lazima wabadilishwe. Baadaye, nilifikiri juu ya wimbo wa neno la Mungu ambao nilikuwa nikiuimba mara kwa mara: "Usafishwaji wa Mungu unavyozidi kuwa mkubwa, ndivyo mioyo ya watu inavyoweza kumpenda Mungu. Maumivu makubwa katika mioyo yao ni ya manufaa kwa maisha yao, wanaweza zaidi kuwa na amani mbele ya Mungu, uhusiano wao na Mungu ni wa karibu zaidi, na wanaweza kuona upendo mkuu wa Mungu na wokovu wake mkuu vyema. Petro alipitia usafishwaji mara mia kadhaa, na Ayubu akapitia majaribu kadhaa. Kama unataka kukamilishwa na Mungu, wewe pia ni lazima upitie usafishwaji mara mia kadhaa; ni kama tu unapaswa kupitia mchakato huu, na unapaswa kutegemea hatua hii, unapoweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu, na kufanywa mkamilifu na Mungu. Usafishwaji ndiyo njia bora kabisa ambayo kwayo Mungu huwafanya watu wawe wakamilifu; ni usafishwaji tu na majaribu machungu yanayoweza kuleta upendo wa kweli kwa Mungu katika mioyo ya watu. Bila shida, watu hawana upendo wa kweli kwa Mungu; kama hawajapimwa ndani, na kwa hakika hawaelekezwi kwa usafishwaji, basi nyoyo zao zitaendelea kuelea katika ulimwengu wa nje. Baada ya kusafishwa kwa kiwango fulani, utaona udhaifu na shida zako mwenyewe, utaona ni kiasi gani unakosa na kwamba huwezi kuyashinda matatizo mengi yanayokukabili, utaona uasi wako ni mkubwa kiasi gani, na kwa hakika utaweza kujijua mwenyewe. Ni kama tu unapaswa kupitia mchakato huu, na unapaswa kutegemea hatua hii, utakapoweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu, na kufanywa mkamilifu na Mungu" ("Usafishwaji Ndiyo Njia Bora Zaidi Ambayo Kwayo Mungu Huwafanya Watu Kuwa Wakamilifu" katika Mfuateni MwanaKondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kupitia mwongozo wa maneno ya Mungu, nilitambua kwamba usafishwaji ndiyo njia bora zaidi ya Mungu kuwakamilisha watu, na kama dada yangu hangekuwa amenishughulikia, moyo wangu ungekuwa unazurura huku na huko. Kwa sababu uvivu na unyonge wangu vilikuwa na nguvu sana, ilikuwa ni kwa aina hii ya mazingira tu ambapo ningekuwa amilifu na kutoka kwa sababu zangu na nyudhuru. Kwa aina hii ya usafishwaji tu ambapo ningeweza kuona wazi kwamba sikuwa na maana na kwamba nilikuwa na makosa mengi sana, lakini pia lilidhihirisha kuwa bado nilikuwa chini ya uelekeo wa mawazo ya jaala yangu ya baadaye. Licha ya ukweli kwamba nilikuwa nimekuwa na uzoefu kiasi wa adhabu kwa miaka michache iliyopita, sikuwa tayari kufuatilia aina yoyote ya sifa isiyo na thamani au hadhi, na nilikuwa nimekwishakuwa mwaminifu zaidi kwa nje, katika kina cha nafsi yangu sumu ya Shetani ilikuwa bado ipo. Nilifikiria nyuma kwa hali zilivyokuwa nilipofika hapa: Zilinionyesha kwamba kiongozi wa zamani hakuwa amefanya kazi ya vitendo, lakini alikuwa ameongea tu mafundisho, sio kufanya kazi ya kuondoa vitu kwa kanisa. Nikawaza mwenyewe: Siwezi kuwa mtu ambaye huongea tu mafundisho lakini hafanyi kazi ya vitendo. Ni lazima nifanye kazi yangu vizuri, na kuondoa kabisa aina hizi tano za watu kabla ya Sikukuu ya Wafanyakazi ili wale ninaowafanyia kazi waone kuwa mimi ni bora zaidi kuliko kiongozi wa zamani, ili kwamba mtu anayesimamia atanitambua. Ilielekea kuwa nilitembea pote na kufanya kazi kwa bidii kufanikisha tamaa hiyo. Mungu ni mwenye haki sana—Ana maarifa ya kina ya uchafu ulio moyoni mwangu. Sikuwa nikifanya kazi ili kusimama kwa upande wa Mungu, au kudumisha maslahi ya kaya ya Mungu au kulinda ndugu zangu wa kiume na wa kike, lakini nilikuwa napanga kujiasisi. Wapinga Kristo wanavuruga na kuangamiza kazi ya nyumba ya Mungu, lakini sikuweza kuwafukuza pepo hawa kutoka kwa nyumba ya Mungu na kuufariji moyo Wake. Kwa hakika ninastahili kufa! Katikati ya mateso na kujilaumu, nilianguka sakafuni: "Ee Mungu! Kwamba ningeweza kutimiza wajibu huu ni kuinuliwa kukubwa mno kutoka kwako, lakini sikuwa na shukrani na sikujali kuhusu mapenzi Yako. Mimi kweli ni mwenye kustahili dharau. Leo, nimeonja tabia Yako ya haki, na ingawa upotovu wangu bado ni mwingi, niko tayari kukubali Wewe kunifanya mkamilifu. Niko tayari kutakaswa ndani ya mazingira haya, na niko tayari kufanya kila liwezekanalo kufanya kazi na Wewe, na hata zaidi niko tayari kushikamana na ndugu zangu wa kiume na wa kike kuyaondoa mapepo yote ya wapinga Kristo." Baada ya kuomba, niliona kifungu cha maneno ya Mungu: “Watu humwamini Mungu kwa nia ya kutaka kupata baraka siku zijazo. Watu wote wana kusudi na tumaini hili. Hata hivyo, upotovu ndani ya asili ya binadamu ni lazima uondolewe kupit majaribu. Katika hali yoyote usiyoipita, ni katika hizi hali ambamo ni lazima usafishwe—huu ni mpango wa Mungu. Mungu anakutengenezea mazingira, Akikulazimisha usafishwe hapo ili ujue upotovu wako mwenyewe. Hatimaye unafika hatua ambapo unaona heri kufa na kuziacha njama na tamaa zako, na kutii mamlaka na mipango ya Mungu.
Hivyo ikiwa watu hawana miaka kadhaa ya usafishaji, ikiwa hawana kiwango fulani cha mateso, hawataweza kuepuka utumwa wa upotovu wa mwili katika mawazo na mioyo yao. Katika hali zozote zile bado ungali mtumwa wa Shetani, katika hali zozote bado ungali na tamaa zako mwenyewe, matakwa yako mwenyewe—ni katika hali hizi ambamo unapaswa kuteseka. Mafunzo yanaweza kupatikana tu katika mateso, yaani, kuweza kupata ukweli, na kuelewa kusudi la Mungu. Kwa kweli, ukweli mwingi unafahamika katika uzoefu wa majaribu makali. Hakuna asemaye kuwa kusudi la Mungu linajulikana, kwamba uweza na busara Yake vinafahamika, kwamba tabia ya haki ya Mungu inaonekana katika mazingira ya utulivu au katika hali zinazofaa. Hilo haliwezekani!” (“Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kutoka kwa maneno ya Mungu, nilitambua kuwa wasiwasi wangu na jaala yangu ya baadaye vilikwisha kuwa ni jambo la mauti zaidi katika asili yangu. Kwa sababu ningeivuruga kazi ya nyumba ya Mungu kwa ajili yalo, na bado ningeweza kutawaliwa nalo, Mungu tena alitengeneza mazingira ya kunisafisha. Kutoka kwa hili, nikaona kwamba majaribu na usafishwaji vilikuwa mpango wa Mungu, na kama singekuwa nimeshughulikiwa na kusafishwa kwa miaka michache hii, kama singekuwa nimepitia hali hizi zenye taabu, maoni katika nafsi yangu na akili juu ya mambo ya mwili hayangebadilika. Baada ya duru kadhaa za kushughulikiwa na kusafishwa, ukimbizaji wangu hatimaye ulipitia mabadiliko. Sikuwa tayari tena kumwamini Mungu kwa madhumuni ya baraka au kufanya biashara na Mungu, kuweka umuhimu mwingi sana juu ya sifa na hadhi au jaala yangu ya baadaye. Nilikuwa wazi sana pia juu ya mapenzi ya Mungu katika kuwaokoa wanadamu.
Tangu wakati huo, wakati wa kutimiza wajibu wangu, bila kujali kama ninabadilishwa au majukumu yangu yamerekebishwa, mimi ni mtulivu zaidi moyoni mwangu na sijishughulishi tena juu ya kile ninachoweza kupata au kupoteza kama awali. Ninahisi tu kwamba ni jukumu moja zaidi na wajibu zaidi. Bila kujali ni wajibu gani nimepangiwa, niko tayari kutii tu mapenzi ya Mungu na kufanya chochote ninachoweza. Wajibu wote ninaoutimiza umeagizwa na Mungu, na niko tayari kushikilia msimamo na kufuatilia ukweli, kufidia makosa yangu ya zamani na madeni, kufuata mfano wa Petro katika kuishi kwa kudhihirisha upendo wa vitendo wa Mungu. Kama tu maneno ya Mungu katika wimbo huu: "Ee Mungu! Tumetengana kwa muda, na tumekuwa pamoja kwa muda. Sijakutendea Wewe chochote, lakini Unanipenda zaidi ya vyote. Nimeasi mara kwa mara dhidi Yako na mara kwa mara nimekuhuzunisha Wewe. Ninawezaje kusahau vitu kama hivyo? Kazi uliyofanya ndani yangu na yale uliyoniaminia nitakumbuka daima, mimi kamwe sisahau. Pamoja na kazi Uliyofanya ndani yangu nimejaribu linalowezekana. Unajua kile ninachoweza kufanya, na zaidi Unajua zaidi jukumu ninaloweza kutenda. Nitatoa kila kitu nilicho nacho Kwako. Ingawa Shetani amenifanya mpumbavu sana na mara kwa mara nimekuasi Wewe, ninaamini Wewe hunikumbuki kwa ajili ya makosa hayo, kwamba Wewe hunitendei kulingana nayo. Napenda kujitolea maisha yangu yote Kwako. Siombi kitu, wala sina matumaini au mipango mingine; ninataka tu kutenda kulingana na nia Yako na kufanya mapenzi Yako. Nitakunywa kutoka kikombe Chako kichungu. Niko tayari kujitolea moyo wangu na mwili na upendo wangu wote wa kweli Kwako, kuyaweka mbele Yako, kuwa mtiifu kabisa Kwako, na niyafikirie kabisa mapenzi Yako. Sio kwa ajili ya mwili, wala kwa ajili ya familia, bali kwa ajili ya kazi Yako" ("Maombi ya Petro" katika Mfuateni Mwana Kondoo na Kuimba Nyimbo Mpya).
Sasa, nimemwamini Mungu kwa zaidi ya miaka 14. Kwa sababu ya neema ya Mungu daima nimetimiza wajibu wangu katika kaya ya Mungu. Kumekuwa na matatizo mengi; kumekuwa na kicheko, kumekuwa na machozi ya huzuni, kumekuwa na furaha kutokana na kuelewa mapenzi ya Mungu na hisia za hatia kutokana na madeni kwa Mungu. Hata zaidi, kumekuwa na furaha na amani kutokana na kuweka ukweli katika matendo. Kwa kweli nimepata mengi sana. Nimepitia uzuri wa hukumu ya Mungu na kuadibiwa—ni halisi mno! Bila hukumu Yake na kuadibiwa singekuwa nimepitia kamwe mabadiliko niliyo nayo. Katika siku zangu tangu sasa na kwendelea, niko tayari kukubali zaidi hukumu za Mungu na adabu, kukubali zaidi majaribu machungu ambayo Mungu hunipangia ili nipate kutakaswa, kuokolewa na kufanywa mkamilifu na Mungu kutoka kwa hukumu Zake na adabu. Kwa njia hii ninaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana na thamani!
Tanbihi:
a. Nakala ya asili inaacha "tamaa ya."
b. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Kujua zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni