1/29/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Sehemu ya Pili

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Sehemu ya Pili

Ili kuelewa tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe lazima muanzie na jambo dogo sana. Jambo hilo dogo sana mnalopaswa kuanzia ni nini? Kwanza kabisa, Nimezikusanya baadhi ya sura kutoka kwenye Biblia. Taarifa iliyo hapa chini inayo mistari ya Biblia, ambayo yote inahusiana na mada ya tabia ya Mungu, kazi ya Mungu na Mungu Mwenyewe.
Nilipata dondoo hizi mahususi kama nyenzo za marejeleo ili kuwasaidia kujua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Hapa Nitayashiriki nanyi ili muweze kuona ni aina gani ya tabia na kiini cha Mungu ambacho kimefichuliwa kupitia kwa kazi Yake ya kitambo lakini watu hawajui kukihusu. Sura hizi zinaweza kuwa nzee, lakini mada tunayowasiliana ni kitu kipya ambacho watu hawana na hawajawahi kusikia. Baadhi yenu huenda mkapata hazieleweki—je, kule kuwataja Adamu na Hawa na kurudi kwa Nuhu si kurudia hatua sawa tena? Haijalishi ni nini mnafikiria, sura hizi ni zenye manufaa kwa mawasiliano ya mada hii na zinaweza kutumika kama maandishi ya mafunzo au nyenzo za matumizi ya kwanza katika ushirika wa leo. Mtaelewa nia Zangu za kuchagua sehemu hizi kufikia wakati Nitakapoumaliza ushirika huu. Wale ambao wamesoma Biblia awali huenda wameona mistari hii michache lakini huenda hawajaelewa. Hebu tuangalie haraka kwanza kabla ya kupitia mistari hii mmoja baada ya mwingine kwa kina zaidi.

Adamu na Hawa ni mababu wa mwanadamu. Kama itabidi tutaje wahusika kutoka kwenye Biblia, basi lazima tuanzie kwa wawili hawa. Kisha Nuhu, mababu wa pili wa mwanadamu. Mnaona haya? Mhusika wa tatu ni nani? (Ibrahimu.) Je, nyote mnaijua hadithi ya Ibrahimu? Baadhi yenu mnaweza kuijua, lakini kwa baadhi yenu huenda isiwe wazi sana. Nani ndiye mhusika wa nne? Ni nani anayetajwa kwenye hadithi ya kuangamizwa kwa Sodoma? (Lutu.) Lakini Lutu hajarejelewa hapa. Ni nani anayerejelewa? (Ibrahimu.) Kitu kikuu kilichotajwa kwenye hadithi ya Ibrahimu ni kile Yehova Mungu alikuwa amesema. Je mnaona haya? Nani ndiye mhusika wa tano? (Ayubu.) Je, Mungu hataji mengi kwenye hadithi ya Ayubu wakati wa awamu hii ya kazi Yake? Basi mnajali sana kuhusu hadithi hii? Kama mnajali sana, je mmeisoma hadithi ya Ayubu kwenye Biblia kwa umakini? Je, mnajua ni mambo gani Ayubu alisema, ni mambo gani aliyofanya? Wale ambao wameisoma hadithi hiyo sana, ni mara ngapi mmeisoma? Je, mnaisoma mara kwa mara? Akina dada kutoka Hong Kong, tafadhali tuambieni. (Mimi niliisoma mara kadhaa hapo awali tulipokuwa katika Enzi ya Neema.) Hamjawahi soma tena tangu hapo? Kama ni hivyo, basi hiyo ni aibu kubwa. Wacha Niwaambie: Katika awamu hii ya kazi ya Mungu Alimtaja Ayubu mara nyingi, na hilo ni onyesho la nia Zake. Kwamba Alimtaja Ayubu mara nyingi lakini umakini wenu haukuzinduliwa ni thibitisho kwa ukweli kwamba: Hamna haja ya kuwa watu ambao ni wazuri na watu wanaomcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hii ni kwa sababu mnatosheka tu na kuwa na wazo la juujuu kuhusu hadithi ya Ayubu iliotajwa na Mungu. Mnatosheka na uelewa wa juujuu wa hadithi yenyewe, lakini hamjali kuhusu na hamtaki kufahamu maelezo ya Ayubu ni nani na kusudio linalomfanya Mungu kumrejelea Ayubu mara kadhaa. Kama hata hamjali mtu kama huyo ambaye Mungu amesifu, basi ni nini hasa mnayotilia maanani? Kama hamjali kuhusu na hamjaribu kuelewa mhusika muhimu sana kama huyu ambaye Mungu amemtaja, basi hiyo inasema nini kuhusu mwelekeo wenu katika neno la Mungu? Hilo si jambo baya? Je, hiyo haithibitishi kwamba wengi wenu hawajihusishi katika mambo ya kimatendo na nyinyi nyote hamfuatilii ukweli? Kama unafuatilia ukweli, utatilia maanani kwa lazima watu ambao Mungu ameidhinisha na hadithi za wahusika ambazo Mungu amezungumzia. Haijalishi kama unaweza kuithamini au kuipata kuwa hadithi ya dhahiri shahiri, utaenda haraka na kuisoma, kujaribu kuifahamu, kupata njia za kufuata mfano wake, na kufanya kile unachoweza kwa uwezo wako bora zaidi. Hiyo ndiyo tabia ya mtu anayetamani ukweli. Lakini ukweli ni kwamba wengi wenu mlioketi hapa hamjawahi kuisoma hadithi ya Ayubu. Hii kwa kweli inaniambia kitu.

Hebu turudi katika mada niliyokuwa Nikizungumzia muda mfupi uliopita. Sehemu hii ya maandiko inayoshughulikia Enzi ya Sheria ya Agano la Kale ni haswa hadithi za wahusika Nilizokuwa nimedondoa. Hizi ni hadithi zilizoeleweka kwa watu wengi ambao wamesoma Biblia. Wahusika hawa ni wawakilishi sana. Wale waliosoma hadithi hizi wataweza kuhisi kwamba kazi ambayo Mungu amewafanyia wao na maneno ambayo Mungu amewazungumzia yanashikika na yanafikika kwa watu wa leo. Unaposoma hadithi hizi na rekodi hizi kutoka kwenye Biblia, utaweza kuelewa namna ambavyo Mungu alivyofanya kazi Yake na namna alivyoshughulikia watu wakati huo. Lakini kusudio la Mimi kutafuta sura hizi leo si eti kwamba uweze kujaribu kung'amua hadithi hizi na wahusika ndani zao. Badala yake, ni ili uweze kupitia kwa hadithi za wahusika hawa, kuona vitendo vya Mungu na tabia Yake, na hivyo kurahisisha kujua na kuelewa Mungu, kuuona upande halisi Wake yeye, kusitisha kufikiria kwako, na kukomesha dhana zako kuhusu Yeye, na kusitisha imani yako na kuitoa katika hali ya kutokuwa na hakika. Kujaribu kuifahamu tabia ya Mungu na kuielewa na kupata kujua Mungu mwenyewe bila ya msingi, kunaweza mara nyingi kukufanya kuhisi kama mtu asiyeweza, asiye na nguvu, na asiye na hakika ni wapi wataanzia. Na ndiyo maana Nilifikiria ni wazo zuri kutumia mbinu kama hii na mtazamo ili kukufanya kumwelewa Mungu kwa njia bora zaidi, na kwa uhalisia zaidi kutambua na kushukuru mapenzi ya Mungu na kupata kuijua tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe na kukufanya kuhisi kwa dhati uwepo wa Mungu na kushukuru mapenzi Yake kwa wanadamu. Je, haya si ya manufaa kwenu? Sasa mnahisi vipi ndani ya mioyo yenu mnapoziangalia hadithi hizi na maandiko haya tena? Je, mnafikiria maandiko haya Niliyoyachukua yamezidi kuliko kawaida? Lazima Nitilie mkazo tena kile Nimetoka tu kuwaambia. Nia ya kuwaruhusu kusoma hadithi hizi za wahusika ni kuwasaidia kuelewa namna ambavyo Mungu anafanya kazi Yake kwa watu na mwelekeo Wake kwa wanadamu. Ni kupitia nini ndipo mtaweza kuelewa haya? Kupitia kwa kazi ambayo Mungu amefanya kitambo, na kuunganisha pamoja na kazi ambayo Mungu anafanya sasa hivi kuwasaidia kuelewa mambo mbalimbali kuhusu Yeye. Mambo haya mbalimbali ni ya kweli, na lazima yajulikane na yatambulike na wale wanaotaka kumjua Mungu.

Tutaanza sasa na hadithi ya Adamu na Hawa. Kwanza, hebu tuyasome maandiko.

1. Adamu na Hawa

1) Amri ya Mungu kwa Adamu

Mwa 2:15-17 Naye Yehova Mungu akamchukua mtu huyo, na kumweka ndani ya bustani ya Edeni ili ailime na kuihifadhi. Yehova Mungu akamwamrisha mtu huyo, akisema, Unaweza kula kwa uhuru matunda kutoka miti yote ya bustani: Lakini kutoka mti wa maarifa ya mema na maovu, usiyale: kwa kuwa katika siku ambapo utakula matunda kutoka mti huo bila shaka utakufa.

Je, mlielewa chochote kutoka kwenye mistari hii? Je, ni vipi ambavyo sehemu hii ya maandiko inavyo wafanya kuhisi? Kwa nini "Amri ya Mungu kwa Adamu" ilidondolewa kutoka kwa maandiko? Je, kila mmoja wenu sasa anayo picha ya Mungu na Adamu katika akili yenu? Mnaweza kujaribu kufikiria: Kama ni nyinyi mliokuwa katika tukio hilo, je, Mungu katika moyo wenu angekuwa vipi? Ni hisia gani ambazo picha hii zinafanya mhisi? Hii ni picha ya kusisimua na ya kutuliza moyo. Ingawaje kunaye Mungu tu na binadamu ndani yake, ule ukaribu kati yao unastahili kuonewa wivu: Upendo mwingi wa Mungu amepewa binadamu kwa ukarimu, unamzunguka binadamu; binadamu ni mnyofu na asiye na hatia, aliye huru kabisa na asiyejali chochote, anayeishi kwa furaha kwa uangalizi wa jicho la Mungu; Mungu anaonyesha hali ya kujali binadamu huku naye binadamu anaishi katika ulinzi na baraka za Mungu; kila kitu binadamu anachofanya na kusema kinaunganishwa kwa karibu na Mungu na hakiwezi kutofautishwa.

Mnaweza kusema kwamba hii ndiyo amri ya kwanza ya Mungu aliyoitoa kwa binadamu tangu kumuumba yeye. Je, amri hii ina nini? Amri hii inayo mapenzi ya Mungu, lakini pia inayo wasiwasi Wake kwa wanadamu. Hii ndiyo amri ya kwanza ya Mungu na pia ndio mara ya kwanza Mungu anakuwa na wasiwasi kuhusu binadamu. Hivi ni kusema, Mungu analo jukumu kwa binadamu tangu ule wakati alipomuumba yeye. Jukumu Lake ni lipi? Lazima amlinde binadamu, kumwangalia binadamu. Anatumai kwamba binadamu anaweza kuamini na kutii maneno Yake. Hili pia ndilo tarajio la kwanza la Mungu kwa binadamu. Na ni kwa tarajio hili kwamba Mungu anasema yafuatayo: "Unaweza kula kwa uhuru matunda kutoka miti yote ya bustani: Lakini kutoka mti wa maarifa ya mema na maovu, usiyale: kwa kuwa katika siku ambapo utakula matunda kutoka mti huo bila shaka utakufa." Maneno haya rahisi yanawakilisha mapenzi ya Mungu. Yanafichua pia kwamba moyo wa Mungu tayari umeanza kuonyesha hali ya kujali binadamu. Miongoni mwa mambo yote, ni Adamu pekee aliyeumbwa kwa taswira ya Mungu; Adamu alikuwa kiumbe wa pekee aliye hai aliye na pumzi ya uhai ya Mungu; angeweza kutembea na Mungu, kuzungumza na Mungu. Na ndiyo maana Mungu alimpa amri kama hiyo. Mungu aliweka wazi katika amri hii kile binadamu anaweza kufanya, na vilevile akaweka wazi kile asichoweza kufanya.

Katika maneno haya machache rahisi, tunauona moyo wa Mungu. Lakini ni aina gani ya moyo tunaouona? Je, kunao upendo katika moyo wa Mungu? Je, upendo huo unao hali yoyote ya kujali ndani yake? Upendo wa Mungu na kujali kwake katika mistari hii hakuwezi kutambulika na kuthaminiwa tu na watu, lakini unaweza pia kuhisiwa vizuri na kwa kweli. Hayo ni kweli? Kwa vile nimesema tayari mambo haya, bado mnafikiria kwamba haya ni maneno machache tu rahisi? Si rahisi hivyo, kweli? Mngeweza kuona hivi awali? Kama Mungu mwenyewe angekuambia maneno hayo machache mngehisi vipi ndani yenu? Kama wewe si mtu mwenye utu, kama moyo wako ni baridi kama barafu, basi usingehisi chochote, usingethamini upendo wa Mungu, na usingejaribu kuuelewa moyo wa Mungu. Lakini kama wewe ni mtu mwenye dhamiri, mwenye ubinadamu, basi utahisi tofauti. Utahisi joto, utahisi kuwa umetunzwa na umependwa, na utahisi furaha. Je, hayo ni kweli? Unapohisi mambo haya, utatenda vipi kwa Mungu? Utahisi ukiwa umeunganishwa kwa Mungu? Utampenda na kumheshimu Mungu kutoka kwenye sakafu ya moyo wako? Moyo wako utakuwa karibu zaidi na Mungu? Unaweza kuona kutoka kwa haya namna ambavyo upendo wa Mungu ulivyo muhimu kwa binadamu. Lakini kile kilicho muhimu zaidi ni kuthamini na kufahamu kwa binadamu upendo huu wa Mungu. Kwa hakika, Mungu hasemi mambo mengi yanayofanana kwenye awamu hii ya kazi Yake? Lakini je, watu wa leo wanauthamini moyo wa Mungu? Je, mnaweza kung'amua mapenzi ya Mungu Niliyoyazungumzia muda mfupi uliopita? Hamwezi hata kutambua mapenzi ya Mungu wakati yanaonekana waziwazi, yanaweza kushikika na ni halisi. Na ndiyo maana Nasema hamna maarifa na uelewa halisi wa Mungu. Je, haya si kweli? Hayo tu ndiyo yote tutakayowasiliana nanyi kwenye sehemu hii.

2) Mungu Amuumba Hawa

Mwa 2:18-20 Yehova Mungu akasema, Si vizuri kuwa mtu huyo akuwe peke yake; nitamuumbia msaidizi anayefanana na yeye. Na kutoka kwa ardhi Yehova Mungu akaumba wanyama wote wa msituni, na ndege wote wa angani; na akawaletea kwa Adamu ndiyo aone majina ambayo angewapa: na chochote ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, hilo ndilo likawa jina lake kuanzia hapo. Naye Adamu akawapa wanyama wote wa kufugwa majina, na ndege wa hewani, na wanyama wote wa mwituni; lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi ambaye alifanana na yeye.

Mwa 2:22-23 Nao ubavu, ambao Yehova Mungu aliuchukua kutoka kwa Adamu, yeye akaufanya uwe mwanamke, na akampeleka kwa Adamu. Naye Adamu akasema, Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu, na nyama ya nyama zangu: ataitwa Mwanamke, kwa kuwa amechukuliwa kutoka kwa Mwanamume.

Kunazo kauli kuu chache kwenye sehemu hii ya maandiko. Tafadhali zichoree mstari chini: "chochote ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, hilo ndilo likawa jina lake kuanzia hapo." Kwa hivyo ni nani aliyepatia viumbe wote haya majina yao? Alikuwa Adamu, si Mungu. Kauli hii inamwambia mwanadamu ukweli: Mungu alimpa binadamu werevu alipomuumba Yeye. Hivi ni kusema kwamba, werevu wa binadamu ulitoka kwa Mungu. Hili ni kweli. Lakini kwa nini? Baada ya Mungu kumuumba Adamu, Adamu alienda shuleni? Je, alijua namna ya kusoma? Baada ya Mungu kuwaumba viumbe hai mbalimbali, je Adamu aliwatambua wanyama hawa wote? Je, Mungu alimwambia majina ya viumbe hao? Bila shaka, Mungu pia hakumfunza namna ya kutunga yale majina ya viumbe hawa. Huo ndio ukweli! Basi alijua vipi namna ya kupatia viumbe hawa hai majina yao na aina gani ya majina ya kuwapatia? Haya yote yanahusiana na swali kuhusu ni nini ambacho Mungu aliongezea kwa Adamu alipomuumba yeye. Ukweli unathibitisha kwamba wakati Mungu alipomuumba binadamu Alikuwa ameongezea werevu kwake. Huu ni ukweli muhimu sana. Je, nyinyi nyote mmesikiliza kwa makini? Kunao ukweli mwingine muhimu ambao unafaa kuwa wazi kwenu? Baada ya Adamu kuwapatia viumbe hai majina yao, majina haya yalipangwa kwenye msamiati wa Mungu. Kwa nini Ninasema hivyo? Hii pia inahusisha tabia ya Mungu, na lazima Niielezee.

Mungu alimuumba binadamu, Akapumua maisha ndani yake, na pia Akampa baadhi ya werevu Wake, uwezo Wake, na kile Anacho na alicho. Baada ya Mungu kumpa binadamu mambo haya yote, binadamu aliweza kufanya baadhi ya mambo haya kwa uhuru na kufikiria pekee yake. Kama kile binadamu anaunda na kufanya ni kizuri machoni mwa Mungu, basi Mungu anakikubali na haingilii kati. Kama kile binadamu anafanya ni sahihi, basi Mungu atakiacha tu kiwe hivyo milele. Kwa hivyo kauli hii "chochote ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, hilo ndilo likawa jina lake kuanzia hapo" inaonyesha nini? Inaopendekeza kwamba Mungu hakufanya marekebisho yoyote kwa majina ya wale viumbe mbalimbali hai. Jina lolote lile ambalo Adamu alimwita, Mungu alisema "Ndiyo" na akasajili jina hilo hivyo. Je, Mungu alionyesha maoni yoyote? La, hilo ni hakika. Kwa hivyo, mnaona nini hapa? Mungu Alimpa binadamu werevu naye binadamu akautumia werevu wake aliopewa na Mungu kufanya mambo. Kama kile binadamu anafanya ni kizuri machoni mwa Mungu, basi kinathibitishwa, kutambulika, na kukubalika na Mungu bila ya utathmini au upinzani wowote. Hili ni jambo ambalo hakuna mtu wala roho wa maovu, wala Shetani, anaweza kufanya. Je, mnauona ufunuo wa tabia ya Mungu hapa. Je, mwanadamu, mwanadamu aliyepotoshwa, au Shetani anaweza kuwakubali wengine kuwawakilisha katika kufanya mambo huku wakitazama? Bila shaka la! Je, wanaweza kupigania cheo na yule mtu mwingine au nguvu nyingine ambayo ni tofauti na wao? Bila shaka wangefanya hivyo! Na kwa muda huo, kama angekuwa ni mtu aliyepotoshwa au Shetani aliyekuwa na Adamu, bila shaka wangekataa kile ambacho Adamu alikuwa akifanya. Ili kuthibitisha kwamba wanao uwezo wa kufikiria kwa uhuru na wanayo maono yao binafsi na ya kipekee, wangekataa kabisa kila kitu alichofanya Adamu: "Unataka kukiita hivyo? Kwa kweli, sitakiita hivyo, nitakiita hivi; ulikiita Tom lakini mimi nitakiita Harry. Lazima nionyeshe ustadi wangu." Haya ni aina gani ya asili? Hii ni asili ya kiburi kisicho na mipaka? Lakini Mungu anayo tabia kama hii? Je, Mungu alikuwa na upinzani wowote usiokuwa wa kawaida kwa mambo haya ambayo Adamu alifanya? Jibu ni bila shaka la! Kati ya tabia ambayo Mungu anafichua, hakuna hata chembe ya ubishi, ya kiburi, au kujigamba kwa nafsi. Hilo liko wazi kabisa hapa. Hili ni jambo dogo tu, lakini kama huelewi kiini cha Mungu, kama moyo wako hautajaribu kujua namna ambavyo Mungu anatenda na mwelekeo wa Mungu ni ipi, basi hutajua tabia ya Mungu au kuyaona maonyesho na ufunuo wa tabia ya Mungu. Je, hayo si kweli? Je, unakubali kile Nimetoka tu kukuelezea? Kwa kujibu matendo ya Adamu, Mungu hakutangaza kwa sauti kwamba, "Umefanya vyema. Umefanya sahihi Ninakubali." Katika Moyo Wake, hata hivyo, Mungu aliidhinisha, akathamini, akashangilia kile Adamu alikuwa amefanya. Hili ndilo jambo la kwanza tangu uumbaji ambalo binadamu alikuwa amemfanyia Mungu akifuata maagizo Yake. Ni jambo ambalo binadamu alifanya badala ya Mungu na kwa niaba ya Mungu. Mbele ya macho yake, hili lilitokana na werevu Aliokuwa amempa binadamu. Mungu aliliona kama jambo zuri, kitu kizuri. Kile ambacho Adamu alifanya wakati huo kilikuwa maonyesho ya kwanza ya werevu wa Mungu kwa binadamu. Hili lilikuwa onyesho zuri kutoka kwa maoni ya Mungu. Kile Ninachotaka kuwaambia nyinyi hapa ni kwamba nia ya Mungu katika kuongezea sehemu ya kile Anacho na alicho na werevu wake kwa binadamu ilikuwa ili mwanadamu aweze kuwa kiumbe hai anayemwonyesha Yeye. Kwa kiumbe hai kama huyo kufanya mambo hayo kwa niaba yake, ilikuwa ndicho hasa kile Mungu alikuwa akitamani kuona.

3) Mungu Awatengenezea Adamu na Hawa Nguo za Ngozi

Mwa 3:20-21 Adamu akampa mke wake jina la Hawa; kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa mama ya wote wenye uhai. Pia Yehova Mungu akawatengenezea Adamu na mke wake nguo za ngozi; na akawavisha.

Hebu tuangalie kifungu hiki cha tatu, kinachosema kwamba, kunayo maana katika jina Adamu alimpa Hawa, kweli? Hii inaonyesha kwamba baada ya kuumbwa, Adamu alikuwa na fikira zake na alielewa mambo mengi. Lakini kwa sasa, hatutasoma na kuchunguza kile alichoelewa au kwa kiwango kipi alielewa kwa sababu hiyo si hoja kuu Ninayotaka kuzungumzia kwenye kifungu hiki cha tatu. Hivyo hoja kuu katika kifungu cha tatu ni gani? Hebu na tuuangalie mstari huo, "Pia Yehova Mungu akawatengenezea Adamu na mke wake nguo za ngozi; na akawavisha." Kama hatutakuwa na ushirika kuhusu mstari huu wa maandiko leo, huenda hamtawahi kutambua uzito ulio katika maneno haya. Kwanza, hebu niwape vidokezo fulani. Panua kufikiria kwenu na kuona picha ya bustani ya Edeni, huku Adamu na Hawa wakiishi ndani. Mungu anaenda kuwatembelea lakini wanajificha kwa sababu wako uchi. Mungu hawezi kuwaona, na baada ya kuwaita wao, wanasema, "Hatuwezi kuthubutu kukuona kwa sababu tuko uchi." Hawathubutu kumwona Mungu kwa sababu wako uchi. Kwa hivyo Yehova Mungu anawafanya nini? Maandishi asilia yanasema: "Pia Yehova Mungu akawatengenezea Adamu na mke wake nguo za ngozi; na akawavisha." Sasa mnajua kile Mungu alitumia kutengeneza nguo zao? Mungu alitumia ngozi za wanyama kutengeneza nguo zao. Hivyo ni kusema, nguo ambazo Mungu alitengenezea binadamu zilikuwa za koti la manyoya. Hiki ndicho kilichokuwa kipande cha kwanza cha nguo ambacho Mungu alitengenezea binadamu. Koti la manyoya ni mavazi ya soko la vitu vya bei ghali kwa viwango vya leo, kitu ambacho si kila mtu anaweza kumudu kuvaa. Kama mtu atakuuliza: Kipande cha kwanza cha nguo kilichovaliwa na wazee wa wanadamu kilikuwa kipi? Unaweza kujibu: Kilikuwa ni koti la manyoya. Nani aliyetengeneza hilo koti la manyoya? Unaweza kujibu zaidi: Mungu alilitengeneza! Hiyo ndiyo hoja kuu: Nguo hii ilitengenezwa na Mungu. Je, hilo ni jambo la kutilia maanani, sivyo? Kwa vile sasa nimetoka kukifafanua, picha imeibuka katika akili zenu? Kunafaa kuwa angaa na mpangilio wa juu kukihusu. Hoja ya kuwaambia haya leo si kuwafahamisha kuhusu kipande cha kwanza cha nguo cha binadamu kilikuwa nini. Hivyo hoja ni gani? Hoja si lile koti la manyoya, lakini namna ya kujua tabia na uwepo na nafsi zilizofichuliwa na Mungu alipokuwa Akifanya hivi.

Katika picha hii ya "Pia Yehova Mungu akawatengenezea Adamu na mke wake nguo za ngozi; na akawavisha," ni wajibu gani ambao Mungu anatekeleza anapokuwa na Adamu na Hawa? Na ni katika aina gani ya uajibu ambao Mungu anajitokeza katika ulimwengu akiwa tu na wanadamu wawili? Kutekeleza wajibu wa Mungu? Kaka na dada kutoka Hong Kong, tafadhali jibuni. (Kutekeleza wajibu wa mzazi.) Kaka na dada kutoka Korea Kusini, ni wajibu wa aina gani mnafikiria Mungu anatekeleza hapa? (Kiongozi wa familia.) Kaka na dada kutoka Taiwan, mnafikiria nini? (Wajibu wa mtu katika familia ya Adamu na Hawa, wajibu wa mwanafamilia.) Baadhi yenu mnafikiria kuwa Mungu anajitokeza kama mwanafamilia wa Adamu na Hawa, huku baadhi wakisema kwamba Mungu anajitokeza kama kiongozi wa familia na wengine wanasema kwamba Anajitokeza kama mzazi. Haya yote yanafaa sana. Lakini ni nini hasa Ninachotilia mkazo hapa? Mungu aliwaumba watu hawa wawili na kuwashughulikia kama mtu na mwandani Wake. Akiwa ndiye mwanafamilia pekee wao, Mungu aliangalia kuishi kwao na pia akakidhi mahitaji yao ya kimsingi. Hapa, Mungu anajitokeza kama mzazi wa Adamu na Hawa. Huku Mungu akifanya haya, binadamu haoni namna ambavyo Mungu alivyo mkuu; haoni mamlaka ya juu zaidi ya Mungu, hali Yake ya mafumbo, na hasa haoni hasira au adhama Yake. Kile anachoona tu ni unyenyekevu wa Mungu, upendo Wake, kujali Kwake binadamu na jukumu Lake na utunzaji Wake kwake yeye. Mwelekeo na njia ambayo Mungu alishughulikia Adamu na Hawa ni sawa na namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyoonyesha hali ya kuwajali watoto wao binafsi. Ni kama pia namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyopenda, kuangalia, na kutunza watoto wao binafsi wa kiume na kike—halisia, namna ya kuonekana, na kushikika. Badala ya kujiweka Yeye Mwenyewe katika cheo cha juu na cha utukufu, Mungu mwenyewe alitumia ngozi kutengeneza nguo za binadamu. Haijalishi kama koti hili la manyoya lilitumika kufunika uchi wao au wao kujikinga dhidi ya baridi. Kwa ufupi, nguo hii iliyotumika kuufunika mwili wa binadamu ilitengenezwa na Mungu mwenyewe kwa mikono Yake mwenyewe. Badala ya kuitengeneza tu kupitia kwa fikira au kwa mbinu za kimiujiza kama watu wanavyofikiria, Mungu alikuwa amefanya kitu cha halali kwa binadamu ambacho binadamu anafikiria Mungu hawezi na hafai kufanya. Kitu hiki kinaweza kuwa rahisi ambacho baadhi huenda hata wasifikirie kwamba kinastahili kutajwa, lakini kinawaruhusu pia wale wote wanaomfuata Mungu lakini awali walikuwa na mawazo yasiyoeleweka kuhusu Yeye kuweza kupata maono kuhusu ukweli na uzuri Wake, na kuuona uaminifu Wake na asili Yake ya unyenyekevu. Kinawafanya watu wenye kiburi kisicho na kifani wanaofikiria kwamba wako juu na wanao utukufu kuinamisha vichwa vyao kwa aibu mbele ya ukweli na unyenyekevu wa Mungu. Hapa, ukweli na unyenyekevu wa Mungu unawezesha zaidi watu kuona namna ambavyo Anapendeka. Kwa kinyume cha mambo, yule Mungu mkubwa sana, Mungu anayependeka na yule Mwenyezi Mungu katika mioyo ya watu ni mdogo sana, asiyevutia, na asiyeweza kuhimiliwa hata mara moja. Unapouona mstari huu na kuisikia hadithi hii, unamkasirikia Mungu kwa sababu Alifanya kitu kama hiki? Baadhi ya watu wanaweza kufanya hivyo, lakini kwa wengine itakuwa ni tofauti kabisa. Watafikiri Mungu ni mkweli na anapendeka, na hasa ni ule ukweli na uzuri wa Mungu ndiyo unaowafurahisha. Kwa kadri wanavyoona ule upande wa kweli wa Mungu, ndipo wanapothamini uwepo wa kweli wa upendo wa Mungu, umuhimu wa Mungu katika mioyo yao, na namna anavyosimama kando yao kila muda.

Kwa wakati huu, tunafaa kuunganisha mazungumzo yetu na sasa. Kama Mungu angeweza kufanya mambo haya madogo mbalimbali kwa binadamu Aliowaumba hapo mwanzo kabisa, hata vitu vingine ambavyo watu hawangethubutu kufikiria ama kutarajia, basi naye Mungu angewafanyia watu leo mambo kama hayo? Baadhi ya watu husema, "Ndiyo!" Kwa nini hivyo? Kwa sababu kiini cha Mungu si bandia, uzuri Wake si bandia. Kwa sababu kiini cha Mungu kwa kweli kipo, na si kitu kilichoongezewa tu na wengine na bila shaka si kitu ambacho kinabadilika na mabadiliko ya muda, mahali, na enzi. Ukweli na uzuri wa Mungu unaweza kwa kweli kuonyeshwa kupitia kufanya jambo ambalo watu wanafikiria si la kipekee na ni dogo, jambo ambalo ni dogo sana kiasi cha kwamba watu hata hawafikirii angeweza kufanya. Mungu si mnafiki. Hakuna kupiga chuku, kufunika ukweli, majivuno au kiburi katika tabia na kiini Chake. Siku zote Hajigambi, lakini badala yake Anapenda, Anaonyesha hali ya kujali, Anaangalia, na kuwaongoza wanadamu Aliowaumba kwa uaminifu na dhati. Haijalishi ni kiwango kipi ambacho watu wanaweza kuthamini, kuhisi, au kuona, Mungu kwa hakika anafanya mambo haya. Je, kujua kwamba Mungu anacho kiini kama hicho kunaweza kuathiri upendo wa watu kwake Yeye? Kutaweza kushawishi namna wanavyomcha Mungu? Ninatumai utakapoelewa upande halisi wa Mungu utaweza kuwa hata karibu zaidi na Yeye na kuweza kuthamini hata zaidi na kwa kweli upendo Wake na utunzaji Wake kwa wanadamu, huku wakati huohuo pia kumpa moyo wako na kutowahi tena kuwa na shaka au wasiwasi wowote kwake Yeye. Mungu anafanya kimyakimya kila kitu kwa ajili ya binadamu, akifanya kimyakimya kupitia ukweli, uaminifu, na upendo Wake. Lakini siku zote Hana hofu au majuto yoyote kwa yale yote Anayofanya, wala hahitaji mtu yeyote kumlipa Yeye kwa njia yoyote au kuwa na nia za kuwahi kupokea kitu kutoka kwa wanadamu. Kusudio tu la kila kitu Alichowahi kufanya ni ili Aweze kupokea imani na upendo wa kweli kutoka kwa wanadamu. Hebu tuhitimishe mada hii ya kwanza hapa.

Je, mazungumzo haya yamewasaidia? Yamewasaidia kwa kiasi kipi? (Uelewa na maarifa zaidi kuhusu upendo wa Mungu.) (Mbinu hii ya mawasiliano inaweza kutusaidia katika siku za mbele ili kuweza kuthamini zaidi neno la Mungu, kufahamu hisia alizokuwa nazo na maana ya mambo Aliyoyasema Alipoyasema, na kuhisi namna Alivyohisi wakati huo.) Je, yupo yeyote kati yenu anayehisi hata zaidi uwepo halisi wa Mungu baada ya kuyasoma maneno haya? Je, mnahisi uwepo wa Mungu si mtupu wala wa kutiliwa mashaka tena? Pindi mnapokuwa na hisia hii, mnahisi kwamba Mungu yupo tu kando yenu? Pengine hisia hiyo si ya dhahiri kwa sasa hivi au hamtaweza kuihisi sasa hivi bado. Lakini siku moja, mtakapokuwa na shukrani ya kina na ya kweli na maarifa halisi kuhusu tabia na kiini cha Mungu ndani ya moyo wako, utahisi kwamba Mungu yupo tu kando yako—ni vile tu kwamba haujawahi kumkubali kwa kweli Mungu ndani ya moyo wako. Haya ni halisi.

Mnafikiria vipi kuhusu mbinu hii ya mawasiliano? Mnaweza kuiendeleza? Mnafikiria aina hii ya ushirika kuhusu mada ya kazi ya Mungu na tabia ya Mungu ni nzito? Mnahisi vipi? (Vizuri sana, kuchangamka.) Ni nini kilichowafanya kuhisi vizuri? Kwa nini mlichangamka? (Ilikuwa sawa na kurudi kwenye Bustani ya Edeni, kurudi kuwa kando ya Mungu.) "Tabia ya Mungu" kwa kweli ni mada ambayo haijazoeleka sana na kila mmoja, kwa sababu kile ambacho unafikiria kwa kawaida, kile unachosoma kwenye vitabu au kusikia kwenye ushirika, siku zote hukufanya kuhisi kama mtu asiyeona akimgusa ndovu—unahisi tu kila pahali kwa kutumia mikono yako, lakini kwa hakika huoni chochote kwa macho yako. "Mguso wa mkono" hauwezi tu kukupa mpangilio wa kimsingi wa maarifa ya Mungu, wacha hata dhana iliyo wazi. Kile ambacho mguso wa mkono unakupatia ni kufikiria zaidi, kiasi kwamba huwezi kufafanua kwa uhakika tabia ya Mungu na kiini halisi. Badala yake, masuala haya ya kutokuwa na uhakika yanayotokana na kufikiria kwako huwa siku zote yanaonekana kujaza moyo wako na shaka. Wakati ambapo huwezi kuwa na uhakika kuhusu kitu na ilhali bado unajaribu kukielewa, ndani ya moyo wako bado siku zote kutaendelea kuwa na mambo yanayopingana na kukinzana, na wakati mwingine huenda hata yakabadilika na kuwa shida, na kukufanya kuhisi ni kana kwamba umepoteza kitu. Je, si jambo la kusikitisha sana unapotaka kumtafuta Mungu, kumjua Mungu, na kumwona Yeye waziwazi, lakini siku zote kutoweza kupata majibu? Bila shaka, maneno haya yanalengwa kwa wale wanaotamani kutafuta uwezo wa kumuheshimu sana Mungu na kuridhisha Mungu. Kwa wale watu ambao hawatilii maanani mambo kama haya, hili kwa hakika si muhimu kwa sababu wanatumaini kwamba ni bora zaidi kuwa uhalisi na uwepo wa Mungu uwe ni ngano ya kale au ndoto, ili waweze kufanya chochote wanachotaka, ili waweze kuwa wale wakubwa zaidi na wenye umuhimu zaidi, na kuweza kutenda vitendo vya maovu bila ya kujali athari zake, na hivyo basi kutoweza kukabiliana na adhabu au kulazimika kuwajibika, ili hata mambo ambayo Mungu anasema kuwahusu watendaji maovu hayataweza kuwahusu wao. Watu hawa hawako radhi kufahamu tabia ya Mungu, wamechoshwa na kujaribu kujua Mungu na kila kitu kuhusu Yeye. Wangependelea kwamba Mungu asiwepo. Watu hawa wanampinga Mungu na wao ndio watakaoondolewa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni