9/04/2019

1. Biblia ni kumbukumbu tu ya hatua mbili za kazi za Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema; siyo kumbukumbu ya ukamilifu wa kazi ya Mungu

XI. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Uhusiano kati ya Mungu na Biblia

1. Biblia ni kumbukumbu tu ya hatua mbili za kazi za Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema; siyo kumbukumbu ya ukamilifu wa kazi ya Mungu

Aya za Biblia za Kurejelea:
Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).
Tazama, Simba wa kabila ya Yuda, Shina lake Daudi, ameweza kukifungua hicho kitabu, na kuzitoa muhiri saba zilizoko” (Ufunuo 5:5).
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa” (Ufunuo 2:7).
Na nikamwona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, akiwa na injili ya daima kuwahubiria hao wanaoishi katika ulimwengu, na kwa kila taifa, na ukoo, na lugha, na watu” (Ufunuo 14:6).
“Ninyi mnaohifadhiwa na nguvu zake Mungu kupitia imani hadi kwa wokovu ambao uko tayari kufichuliwa katika muda wa mwisho” (1 Petro 1:5).
Maneno Husika ya Mungu:
Biblia nzima inarekodi kazi ya enzi mbili: Moja ilikuwa kazi ya Enzi ya Sheria, na moja ilikuwa kazi ya Enzi ya Neema. Agano la Kale hurekodi maneno ya Yehova kwa Waisraeli na kazi Yake katika Israeli; Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu huko Uyahudi.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Unapaswa kujua ni sehemu ngapi ambazo Biblia inajumuisha; Agano la Kale linajumuisha Mwanzo, Kutoka…, na pia kuna vitabu vya unabii ambavyo manabii waliandika. Mwishoni, Agano la Kale linakamilika kwa kitabu cha Malaki. Linarekodi kazi ya Enzi ya Sheria, ambayo iliongozwa na Yehova; kuanzia Mwanzo hadi Kitabu cha Malaki, ni rekodi kamilifu ya kazi ya Enzi ya Sheria. Ni sawa na kusema, Agano Jipya linarekodi yote ambayo yalipitiwa na watu ambao waliongozwa na Yehova katika Enzi ya Sheria. … Biblia ya Agano la Kale kimsingi inarekodi kazi ya Mungu ya kuwaongoza Israeli, kumtumia Musa kuwaongoza Waisraeli kutoka Misri, aliyewaondoa katika shida za Farao, na kuwachukua na kuwapeleka jangwani, ambapo baada ya hapo wakaingia Kaanani na kila kitu baada ya hapa ilikuwa ni kuanza maisha yao Kaanani. Yote, isipokuwa hii ni rekodi za kazi ya Yehova katika Israeli yote. Kila kitu kilichorekodiwa katika Agano la Kale ni kazi ya Yehova katika Israeli, ni kazi Aliyoifanya Yehova katika nchi ambapo Aliwaumba Adamu na Hawa. Kuanzia wakati ambapo Mungu alianza rasmi kuwaongoza watu duniani baada ya Nuhu, yote ambayo yamerekodiwa katika Agano la Kale ni kazi ya Israeli. Na kwa nini hakuna kazi yoyote iliyorekodiwa ambayo ni nje ya Israeli? Kwa sababu nchi ya Israeli ni chimbuko la binadamu. Mwanzoni hakukuwa na nchi yoyote tofauti na Israeli, na Yehova hakufanya kazi katika sehemu nyingine yoyote. Kwa namna hii, kile kilichorekodiwa katika Biblia ni kazi katika Israeli pekee wakati huo. Maneno yaliyozungumzwa na manabii, na Isaya, Danieli, Yeremia na Ezekieli … maneno yao yanatabiri kazi Yake nyingine duniani, yanatabiri kazi ya Yehova Mungu Mwenyewe. Yote haya yalitoka kwa Mungu, ilikuwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, na tofauti na vitabu hivi vya manabii, mambo mengine yote ni rekodi ya uzoefu wa watu juu ya kazi ya Yehova wakati huo.
… Mambo yaliyorekodiwa katika Agano la Kale ni kazi ya Yehova katika Israeli, na kile kilichorekodiwa katika Agano Jipya ni kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema; ni rekodi ya kazi iliyofanywa na Mungu katika enzi mbili tofauti. Agano la Kale linarekodi kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria, na hivyo Agano la Kale ni kitabu cha kihistoria, wakati Agano Jipya ni zao la kazi ya Enzi ya Neema. Wakati kazi mpya ilipoanza, hii pia ilipitwa na wakati—na hivyo, Agano Jipya pia ni kitabu cha kihistoria. Kimsingi Agano Jipya halina mpangilio mzuri kama Agano la Kale, wala halirekodi mambo mengi. Maneno yote mengi yaliyozungumzwa na Yehova juu ya Agano la Kale yamerekodiwa katika Biblia, ambapo baadhi tu ya maneno ya Yesu yamerekodiwa katika Injili Nne. Ni kweli, Yesu pia alifanya kazi nyingi sana, lakini haikurekodiwa kwa kina. Mambo machache yamerekodiwa katika Agano Jipya ni kwa sababu ya kazi kubwa ambayo Yesu aliifanya; kiwango cha kazi Yake katika miaka mitatu na nusu duniani na kazi ile ya mitume ilikuwa ni pungufu zaidi kuliko kazi ya Yehova. Na hivyo, kuna vitabu pungufu katika Agano Jipya kuliko Agano la Kale.
Biblia ni kitabu cha aina gani? Agano la Kale ni kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria. Agano la Kale la Biblia linarekodi kazi yote ya Yehova wakati wa Enzi ya Sheria na kazi Yake ya uumbaji. Lote linarekodi kazi iliyofanywa na Yehova, na hatimaye linahitimisha maelezo ya kazi ya Yehova kwa kitabu cha Malaki. Agano la Kale linarekodi kazi mbili zilizofanywa na Mungu: Moja ni kazi ya uumbaji, na nyingine ni kuamrisha sheria. Zote ni kazi zilizofanywa na Yehova. Enzi ya Sheria inawakilisha kazi chini ya jina la Yehova Mungu; ni ujumla wa kazi iliyofanywa kimsingi chini ya jina la Yehova. Hivyo, Agano la Kale linarekodi kazi ya Yehova, na Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu, kazi ambayo kimsingi ilifanywa chini ya jina la Yesu. Umuhimu wa jina la Yesu na kazi Aliyoifanya imerekodiwa sanasana katika Agano Jipya. Wakati wa Agano la Kale Enzi ya Sheria, Yehova alijenga hekalu na madhabahu katika Israeli, Aliongoza maisha ya Waisraeli duniani, kuzingatia kwamba walikuwa watu Wake, kundi la kwanza la watu ambalo alilichagua duniani na ambao walikuwa wanautafuta moyo Wake, kundi la kwanza ambalo Yeye Mwenyewe aliliongoza; ni sawa na kusema, makabila kumi na mawili ya Israeli walikuwa ni wateule wa kwanza wa Yehova, na hivyo siku zote Alifanya kazi ndani yao, hadi ambapo kazi ya Yehova ya Enzi ya Sheria ilihitimishwa. Hatua ya pili ya kazi ilikuwa ni kazi ya Enzi ya Neema ya Agano Jipya, na ilifanyika katika kabila la Yuda, moja ya makabila kumi na mawili ya Israeli. Kwamba mawanda ya kazi yalikuwa madogo ilikuwa kwa sababu Yesu alikuwa Mungu alifanyika mwili. Yesu alifanya kazi katika eneo lote la Yudea pekee, na Alifanya tu kazi ya miaka mitatu na nusu; hivyo, kile kilichorekodiwa katika Agano la Kale kiko mbali zaidi kupitiliza kiwango cha kazi kilichorekodiwa katika Agano la Kale. Kazi ya Yesu ya Enzi ya Neema kimsingi imerekodiwa katika Injili Nne. Njia iliyopitiwa na watu wa Enzi ya Neema ilikuwa ile mabadiliko ya juu juu katika tabia yao ya maisha, nyingi zaidi ambayo imerekodiwa katika nyaraka.
kutoka katika “Kuhusu Biblia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Biblia pia huitwa Agano la Kale na Agano Jipya. Je, mnajua “agano” linarejelea nini? “Agano” katika Agano la Kale linatokana na makubaliano ya Yehova na watu wa Israeli Alipowaua Wamisri na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa Farao. Bila Shaka, uthibitisho wa haya makubaliano ulikuwa damu ya mwanakondoo iliyopakwa kwenye linta, kupitia kwayo Mungu Alianzisha agano na mwanadamu, moja ambalo ilisemwa kuwa wale wote waliokuwa na damu ya mwanakondoo juu na pembeni mwa viunzi vya mlango walikuwa Waisraeli, walikuwa wateuliwa wa Mungu, na wote wangeokolewa na Yehova (kwa kuwa Yehova wakati ule Alikuwa karibu kuwaua wazaliwa wa kwanza wa kiume wa Misri wote na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe). Agano hili lina viwango viwili vya maana. Hakuna mmoja wa watu au wanyama wa Misri angeokolewa na Yehova; Angewaua wazaliwa wa kwanza wa kiume na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe wao wote. Kwa hivyo, katika vitabu vingi vya unabii kulitabiriwa kwamba Wamisri wangeadibiwa vikali kutokana na agano la Yehova. Hiki ndicho kiwango cha kwanza cha maana cha agano. Yehova Aliwaua wazaliwa wa kwanza wa kiume wa Misri na wazaliwa wa kwanza wa mifugo wao wote, na kuwaacha Waisraeli wote, jambo lililomaanisha kuwa wale wote waliokuwa wa nchi ya Israeli walipendwa na Yehova na wote wangeokolewa; Alidhamiria kufanya kazi ya muda mrefu ndani yao, na Alianzisha agano nao kwa kutumia damu ya mwanakondoo. Tangu wakati ule kuendelea, Yehova Asingewaua Waisraeli na Alisema kuwa daima wangekuwa wateuliwa Wake. Angeianza kazi Yake ya Enzi Nzima ya Sheria Miongoni mwa makabila kumi na mawili ya Israeli, Angeziweka wazi sheria Zake zote kwa Waisraeli, na kuchagua manabii na waamuzi kutoka kati yao, na wangekuwa katikati ya kazi Yake. Yehova Agano nao: Angefanya kazi tu miongoni mwa wateuliwa isipokuwa enzi ibadilike. Agano la Yehova lilikuwa lisilobadilika kwani lilitengenezwa kwa damu, na lilianzishwa na wateuliwa Wake. La muhimu zaidi, Alikuwa Ameteua mawanda na malengo yafaayo ya kazi Yake katika enzi nzima, na kwa hivyo watu waliliona agano kuwa la umuhimu sana. Hiki ndicho kiwango cha pili cha maana ya agano. Isipokuwa kitabu cha Mwanzo, ambacho kilikuwepo kabla ya kuanzishwa kwa agano, vitabu vingine vyote vya Agano la Kale vinaeleza kuhusu kazi ya Mungu miongoni mwa Waisraeli baada ya kuanzishwa kwa agano hili. Bila shaka, yapo maelezo ya hapa na pale ya Watu wa Mataifa, ila kwa ujumla, Agano la Kale linaeleza kuhusu kazi ya Mungu nchini Israeli. Kwa sababu ya Agano kati ya Yehova na Waisraeli, vitabu vilivyoandikwa katika Enzi ya Sheria vinaitwa “Agano la Kale.” Vimepatiwa jina hili kutokana na agano la Yehova na Waisraeli.
Agano Jipya lilipatiwa jina hilo kutokana na damu iliyomwagwa na Yesu msalabani na agano Lake na wale wote waliomwamini. Agano la Yesu lilikuwa hili: Watu hawakuwa na budi kumwamini ili dhambi zao zisamehewe kwa kumwagika kwa damu Yake, na kwa njia hiyo wangeokolewa na kuzaliwa upya kupitia Kwake, na kamwe wasingeendelea kuwa wenye dhambi; watu walipaswa kumwamini ili wapokee neema Yake, na hawangeteseka jehanamu baada ya kufa. Vitabu vyote vilivyoandikwa wakati wa Enzi ya Neema vilizuka baada ya hili agano, na vyote vinaeleza kuhusu kazi na matamshi yaliyomo. Havielezi zaidi ya wokovu wa kusulubishwa kwa Bwana Yesu au hili agano; vyote ni vitabu vilivyoandikwa na wapendwa katika Bwana waliokuwa na tajriba. Kwa hivyo hivi vitabu vilevile vimepatiwa jina kutokana na agano: Vinaitwa Agano Jipya. Haya Maagano mawili yanajumuisha tu Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria na hayana uhusiano na enzi ya mwisho.
kutoka katika “Kuhusu Biblia (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna anayejua uhalisia wa Biblia: kwamba si kitu chochote zaidi ya rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu, na agano la hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, na haikupatii ufahamu wa malengo ya kazi ya Mungu. Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba inarekodi hatua mbili za kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Agano la Kale linaandika historia ya Israeli na kazi ya Yehova kuanzia wakati wa uumbaji hadi mwisho wa Enzi ya Sheria. Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu duniani, ambayo ipo katika Injili Nne, vilevile kazi ya Paulo; je, sio rekodi za kihistoria? … Kwa kusoma Biblia, angalau utakuwa umeelewa sehemu ndogo ya historia ya Israeli, utajifunza kuhusu maisha ya Abrahamu, Daudi, na Musa, utajua kuhusu namna walivyomheshimu sana Yehova, namna ambavyo Yehova aliwachoma wale waliompinga, na jinsi alivyozungumza na watu wa enzi hiyo. Utaelewa tu kuhusu kazi ya Mungu katika wakati uliopita. Rekodi za Biblia zinahusiana na jinsi ambavyo watu wa awali wa Israeli walivyomheshimu sana Mungu na kuishi chini ya uongozi wa Yehova. Kwa sababu Waisraeli walikuwa ni wateuliwa wa Mungu, katika Agano la Kale unaweza kuona utii wote wa watu wa Israeli kwa Yehova, jinsi ambavyo wale wote waliomtii Yehova walivyokuwa wanaangaliwa na kubarikiwa Naye, unaweza kujifunza kwamba Mungu alipofanya kazi katika Israeli alikuwa mwingi wa rehema na mapenzi, vilevile alikuwa na moto uteketezao, na kwamba Waisraeli wote, kuanzia watu wa chini hadi wakubwa, walimheshimu sana Yehova, na hivyo nchi yote ilibarikiwa na Mungu. Hiyo ni historia ya Israeli iliyorekodiwa katika Agano la Kale.
kutoka katika “Kuhusu Biblia (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikiwa unatamani kuiona kazi ya Enzi ya Sheria, na kuona jinsi gani Waisraeli waliifuata njia ya Yehova, basi ni lazima usome Agano la Kale; ikiwa unatamani kuelewa kazi ya Enzi ya Neema, basi ni lazima usome Agano Jipya. Lakini unawezaje kuona kazi ya siku za mwisho? Ni lazima ukubali uongozi wa Mungu wa leo, na kuingia katika kazi ya leo, maana hii ni kazi mpya na hakuna ambaye ameirekodi katika Biblia hapo nyuma. Leo, Mungu amefanyika mwili, na Amewachagua wateule wengine katika nchi ya China. Mungu anafanya kazi ndani ya watu hawa, Anaendelea na kazi Yake duniani, Anaendelea kutoka katika kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya leo ni njia ambayo mwanadamu hajawahi kuiendea, na njia ambayo hakuna mtu ambaye amewahi kuiona. Ni kazi ambayo haijawahi kufanywa hapo kabla—ni kazi ya Mungu ya hivi karibuni kabisa duniani. Hivyo, kazi ambayo haijawahi kufanywa kabla sio historia, kwa sababu sasa ni sasa, na bado haijawa muda uliopita. Watu hawajui kwamba Mungu amefanya kazi kubwa, mpya duniani, na nje ya Israeli, yaani imevuka mawanda ya Israeli, na zaidi ya unabii wa manabii, ambayo ni kazi mpya na ya kushangaza nje ya unabii, na kazi mpya kabisa nje ya Israeli, na kazi ambayo watu hawawezi kuielewa au kufikiria. Inawezekanaje Biblia kuwa na rekodi za wazi za kazi kama hiyo? Ni nani ambaye angeweza kurekodi kila hatua ya kazi ya leo, bila kuondoa kitu? Ni nani angeweza kurekodi kazi hii kubwa na yenye hekima ambayo inakataa maagano ya kitabu cha kale? Kazi ya leo sio historia, na kama vile, ikiwa unatamani kutembea katika njia ya leo, basi mnapaswa kutengana na Biblia, unapaswa kwenda mbele zaidi ya vitabu vya unabii au historia ya Biblia. Baada ya hapo tu ndipo utaweza kutembea njia mpya vizuri, na baada ya hapo ndipo utaweza kuingia katika ufalme mpya na kazi mpya.
kutoka katika “Kuhusu Biblia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni