Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 9
Katika mawazo ya watu, Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu. Mungu haneni lugha ya mwanadamu, wala mwanadamu hawezi kunena lugha ya Mungu, na kwa Mungu, madai ya mwanadamu Kwake ni rahisi, ilhali matakwa ya Mungu kwa mwanadamu hayafikiki na hayafikiriki kwa mwanadamu. Ukweli, hata hivyo, ni kinyume kabisa: Mungu anataka tu “asilimia 0.1” ya mwanadamu. Hili si la kushangaza tu kwa kila mtu, lakini pia huwafanya wahisi kukanganyikiwa sana, kama kwamba wote wamechanganyikiwa. Ni kwa msaada wa kupata nuru kwa Mungu, na neema ya Mungu tu, ndio watu hupata maarifa kidogo ya mapenzi ya Mungu. Lakini mnamo Machi 1, watu wote kwa mara nyingine walibaki wakiwa wamekanganyikiwa na wakikuna vichwa vyao. Mungu alitaka kwamba watu Wake wawe theluji inayong’aa, si mawingu yaendayo pepe. Kwa hiyo hii “theluji inayong’aa” inahusu nini? Na “mawingu yaendayo pepe” yanaashiria nini? Wakati huu, Mungu hasemi lolote kwa makusudi kuhusu maana ya ndani ya maneno haya. Hili linawatumbukiza watu katika kiwewe, na hivyo kuongeza imani yao wanapotafuta—kwani ni matakwa maalum kwa watu wa Mungu, na si kitu kingine, na kwa hiyo kila mtu hujikuta akitumia muda mwingi zaidi kwa hiari akifikiri kuhusu maneno haya yasiyoeleweka. Kutokana na hilo, mawazo mbalimbali huchipua ndani ya akili zao, chembe za theluji ziendazo pepe zinakuja ghafla mbele ya macho yao, na mawingu yaendayo pepe angani mara moja yanatokea katika mawazo yao. Kwa nini Mungu anataka watu Wake wawe kama theluji inayong’aa, na sio kama mawingu yaendayo pepe? Maana ya kweli hapa ni gani? Maneno haya hasa yanahusu nini? “Theluji inayong’aa” haifanyi tu mandhari yaonekane mazuri, lakini pia ni nzuri kwa ardhi ya ukulima—ni nzuri katika kuua bakteria. Baada ya kuanguka kwa theluji nyingi, bakteria zote hufunikwa na theluji inayong’aa, na uwanda wote mara moja hujaa kabisa na uhai. Vivyo hivyo, watu wa Mungu hawatakiwi tu kumjua Mungu mwenye mwili, bali pia kujinyenyekeza kwa ukweli wa kupata mwili kwa Mungu, na hivyo kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida. Hivi ndivyo theluji huyafanya mandhari kuonekana mazuri; hatimaye, ukomavu wa watu wa Mungu utalimaliza joka kuu jekundu, kuanzisha ufalme wa Mungu duniani, kueneza na kutukuza jina takatifu la Mungu, ili ufalme wote duniani ujazwe haki ya Mungu, hung’arisha miali ya Mungu, na kumemetuka na utukufu wa Mungu, na kila mahali kuna na maonyesho ya amani na ridhaa, furaha na utimizo, na uzuri unaofanya upya daima. Tauni mbalimbali zilizopo wakati wa sasa—tabia potovu ya kishetani, kama vile udhalimu, uhalifu na udanganyifu, tamaa mbovu na kadhalika—zote zinakomeshwa, na hivyo mbingu na dunia vyote vinafanywa upya. Hii ni maana ya kweli ya “baada ya kuanguka kwa theluji nyingi.” Wale ambao ni mawingu yaendayo pepe ni kama aina ya watu ambao hufuata kundi linalozungumziwa na Mungu; kama kuna majaribu ya Shetani, au majaribio ya Mungu, wataenda pepe mara moja, na kukosa kuwepo tena. Hata kiini chao hakitasalia, kitakuwa kimetoweka kitambo sana. Kama watu ni mawingu yaendayo pepe, hawawezi tu kuishi kulingana na sura ya Mungu, lakini pia huleta aibu kwa jina la Mungu, kwani watu kama hao wako katika hatari ya kunyakuliwa wakati wowote au mahali popote, wao ni chakula ambacho Shetani hula, na wakati ambapo Shetani anawachukua kuwa mateka, watamsaliti Mungu na kumtumikia Shetani. Hili kwa dhahiri huleta aibu kwa jina la Mungu, ni kile ambacho Mungu huchukia zaidi ya yote, na ni adui za Mungu. Hivyo, wao hawana kiini cha watu wa kawaida na hawana thamani halisi ya matumizi. Ni kwa sababu ya hili ndio Mungu huwa na matakwa kama haya kwa watu Wake. Lakini baada ya kuelewa kitu fulani kuhusu maneno haya, watu huwa hawajui wafanye nini baada ya hapo, kwani mada ya maneno ya Mungu imemgeukia Mungu Mwenyewe, ambalo huwaweka katika hali ngumu: “Kwa sababu Nilitoka katika nchi takatifu, si kama yungiyungi, ambalo lina jina tu na halina dutu kwa sababu lilikuja kutoka katika matope na si kutoka nchi takatifu.” Mbona, baada ya kuzungumza juu ya matakwa Yake kwa watu Wake, Mungu anaeleza kuzaliwa kwa Mungu Mwenyewe? Yawezekana kwamba kuna uwiano wa asili kati ya hayo mawili? Kweli, kuna uwiano wa asili kati ya hayo—la sivyo, Mungu hangezungumza hivyo kwa watu. Kati ya majani mabichi, yungiyungi huyumba nyuma na mbele katika upepo mwanana. Linapendeza machoni na kuthaminiwa sana. Watu hawawezi tu kutosheka nalo, na wana hamu sana ya kuogelea majini kuchuma kikonyo na kukitazama kwa karibu. Lakini Mungu asema yungiyungi linatoka matopeni, na lina jina tu wala si dutu. Inaonekana kwamba Mungu haweki umuhimu wowote kwa mayungiyungi, na kutokana na maneno Yake inaweza kuonekana kwa dhahiri kwamba Ana chuki kiasi fulani kwayo. Kotekote katika enzi, wengi wamemimina sifa kwa mayungiyungi kwa sababu hayo hutoka kwa uchafu pasipo mawaa, kiasi kwamba takriban hayawezi kulinganishwa, ni ya ajabu ya kushangaza. Lakini machoni pa Mungu, mayungiyungi hayana thamani—ambayo hasa ni tofauti kati ya Mungu na mwanadamu. Hii inatosha kuonyesha umbali ulioko kati ya Mungu na mwanadamu, ulio mkuu kama ule ulioko kati ya juu ya anga na chini ya ardhi. Kwa kuwa yungiyungi hutoka matopeni, virutubishi vyote linavyohitaji hutoka humo. Ni vile tu yungiyungi linaweza kujigeuza umbo, na hivyo kufurahisha macho. Watu wengi huona tu uzuri wa nje wa yungiyungi, lakini hakuna yeyote kati yao aonaye kwamba uzima ulio ndani ya yungiyungi ni mchafu na wenye najisi. Hivyo, Mungu asema kwamba lina jina tu bila dutu—ambayo ni sahihi kabisa na kweli. Na hivi hasa sivyo walivyo watu wa Mungu leo? Wao hutii na kumwamini Mungu kwa nje tu. Mbele ya Mungu, wao hujipendekeza na kujionyesha kumfanya Mungu aridhike nao; ndani, hata hivyo, wamejazwa tabia potovu ya kishetani, matumbo yao yamejaa uchafu. Hivyo, Mungu anatoa maswali kwa mwanadamu, Akiuliza kama uaminifu wake kwa Mungu umeozeshwa na uchafu, kama ni safi na kamili. Walipokuwa watendaji huduma, watu wengi walimsifu Mungu vinywani mwao lakini walimlaani mioyoni mwao. Katika vinywa vyao, walikuwa watiifu kwa Mungu, lakini mioyoni mwao, walimuasi Mungu. Vinywa vyao vilitamka maneno hasi, na ndani ya mioyo yao walificha upinzani kwa Mungu. Kulikuweko hata na wale ambao matendo yao yalikuwa ya kulingana sawa: Waliachilia uchafu kwa vinywa vyao na kuashiria kwa mikono yao, wapotovu kabisa, wakitoa onyesho wazi na lenye kufanana na kiumbe chenye uhai la uso wa kweli wa joka kubwa jekundu. Wanastahili kweli kuitwa mayai ya joka kubwa jekundu. Lakini leo, wanasimama katika nafasi ya watendaji huduma waaminifu na kutenda kama watu waaminifu wa Mungu—aibu iliyoje! Si ajabu; walitoka matopeni, kwa hiyo hawana budi ila kuonyesha tabia yao ya halisi. Kwa kuwa Mungu ni mtakatifu na safi, na halisi na wa kweli, mwili Wake unatoka kwa Roho. Hili ni wazi, na bila shaka. Sio tu kuweza kushuhudia kwa Mungu Mwenyewe, bali pia kuweza kutekeleza kabisa mapenzi ya Mungu: huu ni upande mmoja wa dutu ya Mungu. Kwamba mwili unatoka kwa Roho na sura kuna maana kwamba mwili ambao Roho anajivisha ni tofauti kimsingi na mwili wa mwanadamu, na tofauti hii hasa iko ndani ya roho zao. Kile ambacho Roho aliye na sura kinahusu ni jinsi, kutokana na kufunikwa na ubinadamu wa kawaida, uungu unaweza kufanya kazi kwa kawaida ndani, ambacho si cha muujiza kabisa, na hakiwekewi mipaka na ubinadamu. “Sura ya Roho” inahusu uungu kamili, na haiwekewi mipaka na ubinadamu. Hasa, tabia ya Mungu ya asili na sura ya kweli vinaweza kuishi kwa kudhihirishwa kabisa ndani ya mwili, ambao si wa kawaida na thabiti tu, lakini wenye uadhama na ghadhabu. Mwili wa kwanza ungeweza tu kuwasilisha Mungu wa dhana za watu, yaani, Angeweza tu kutekeleza ishara na miujiza na kunena unabii. Hivyo, Hakuishi kwa kudhihirisha kabisa uhalisi wa Mungu, na kwa hiyo hakuwa mfano halisi wa Roho mwenye sura; Alikuwa tu kuonekana kwa kweli kwa uungu. Na kwa kuwa Alizidi sana uwezo wa ubinadamu wa kawaida, Hakuitwa Mungu Mwenyewe wa vitendo kamili, bali Alikuwa na kiasi kidogo cha Mungu asiye dhahiri aliye mbinguni kumhusu, alikuwa Mungu wa dhana za watu. Hii ndiyo tofauti muhimu kati ya miili miwili.
Kutoka mahali palipo juu zaidi ulimwenguni, Mungu huchunga kila mwendo wa mwanadamu, huchunga yote ambayo watu husema na kutenda. Hata kila wazo lao la ndani zaidi Hulichunguza na ubayana kabisa, bila kulipuuza—na kwa hiyo maneno ya Mungu hupenya hadi ndani ya mioyo ya watu, yakigonga kila wazo lao, na maneno Yake ni mepesi kung’amua na bila kosa. “Ingawa mwanadamu anajua Roho Yangu, yeye pia huikosea Roho Yangu. Maneno Yangu yanaweka wazi uso mbaya wa wanadamu wote, na kuweka wazi mawazo ya ndani kabisa ya watu wote, na kusababisha wote duniani kuanguka chini katikati ya uchunguzi Wangu makini.” Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba, ingawa matakwa ya Mungu kwa mwanadamu si ya juu, watu bado hawawezi kustahimili uchunguzi makini wa Roho wa Mungu. “Ijapokuwa mwanadamu anaanguka chini, moyo wake hauthubutu kwenda mbali Nami. Miongoni mwa viumbe, ni nani asiyekuja kunipenda kwa sababu ya matendo Yangu?” Hili hata linaashiria zaidi hekima kamili ya Mungu na kudura, na hivyo kufichua yote ambayo watu wa Mungu walifikiri walipokuwa katika cheo cha watendaji huduma: Ingawa, baada ya “biashara” iliyoishia kushindwa, “mamia ya maelfu” au “mamilioni” katika vichwa vyao ziliambulia patupu, kwa sababu ya amri za usimamizi za Mungu, na kwa sababu ya uadhama wa Mungu na ghadhabu, ingawaje waliinamisha vichwa vyao kwa huzuni, bado walimhudumia Mungu katikati ya uhasi, utendaji wao wote wa siku zilizopita ukawa maneno matupu, yaliyosahaulika kabisa; badala yake walifanya mambo kwa hiari yao ambayo yaliwafanya wao na kila mtu mwingine afurahi ili kuendelea kujiburudisha, ili kupitisha muda… Hiki ndicho kilikuwa kikiendelea kwa kweli miongoni mwa wanadamu. Hivyo, Mungu anakuwa wazi kwa mwanadamu na kusema: “Ni nani asiyekuwa na hamu kwa ajili ya kuyasikia maneno Yangu? Ni nani asiyezaliwa ndani mwake na hisia za ibada kwa sababu ya upendo Wangu?” Kusema kweli, watu wote wako radhi kukubali maneno ya Mungu, na hakuna yeyote kati yao asiyependa kusoma maneno ya Mungu—ni vile tu hawawezi kutia maneno ya Mungu katika vitendo kwa sababu wanazuiliwa na asili zao. Baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu wengi hawawezi kustahimili kujitenga na maneno ya Mungu, na upendo kwa Mungu hufurika ndani yao. Hivyo, Mungu kwa mara nyingine Anamlaani Shetani, na mara tena Anafichua sura yake mbaya. “Enzi ambayo Shetani anaendesha ghasia na ni mdhalimu mkuu” pia ni enzi ile ile ambayo Mungu anaanza kazi Yake kuu, rasmi duniani. Kufuatia, Anaanza kazi ya kuangamiza ulimwengu. Ambalo ni kusema, kadri Shetani anavyozidi kuendesha ghasia, ndivyo siku ya Mungu inavyokaribia zaidi, na kwa hiyo ndivyo Mungu anenavyo zaidi kuhusu utukutu wa Shetani, hivyo inaonyeshwa kwamba siku ambayo Mungu ataangamiza ulimwengu inakaribia. Huu ndio utangazaji wa Mungu kwa Shetani.
Kwa nini Mungu alisema tena na tena “…na, nyuma Yangu, wao wanashiriki katika zile shughuli chafu “zenye kusifika.” Je, unafikiri kwamba mwili Ninaouvaa, haufahamu chochote kuhusu matendo yako, tabia zako, na maneno yako?” Hakusema tu maneno hayo mara moja au mbili—Kwa nini? Mara tu watu wakishafarijiwa na Mungu, na wanafahamu huzuni ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu, ni rahisi kwao kusahau yaliyopita wanapong’ang’ana kuendelea mbele. Lakini Mungu si mwenye huruma kabisa kwa mwanadamu: Yeye huendelea kujaribu kupata fikira za watu. Hivyo Huwauliza watu mara nyingi wajijue, waache upotovu wao, kutoshiriki tena katika shughuli chafu “za kusifika,” na kutowahi kamwe kumdanganya tena Mungu aliye katika mwili. Ingawa asili za watu hazibadiliki, kuna manufaa katika kuwakumbusha mara chache. Baada ya hili, Mungu anena kutokana na mtazamo wa mwanadamu ili kufichua mafumbo yaliyo ndani yake: “Nimestahimili mvua na upepo kwa miaka mingi, na vile vile Nimepitia machungu ya ulimwengu wa binadamu, lakini ukitafakari kwa karibu, hakuna kiasi cha mateso kinachoweza kumfanya mwanadamu aliye katika nyama za mwili kupoteza matumaini ndani Yangu, kama vile hakuna utamu wowote unaoweza kumfanya mwanadamu wa mwili awe bila hisia, mwenye kuvunjika moyo au mwenye kunipuuza Mimi Je, upendo wa mwanadamu Kwangu ni mdogo kiasi kwamba upo tu katikati ya ama kutokuwa na maumivu au kutokuwa na utamu?” “Yote chini ya jua ni tupu,” maneno haya kweli yana maana ya ndani. Hivyo Mungu asema kwamba hakuna chochote kinachoweza kumfanya mwanadamu akate tamaa Kwake au kumdharau. Ikiwa watu hawampendi Mungu, ni heri basi wafe; ikiwa hawampendi Mungu, basi mateso yao ni bure, na baraka zao ni tupu, na kuongezewa kwa dhambi zao. Kwa vile hakuna hata mtu mmoja anayempenda Mungu kweli, hivyo Asema, “Je, upendo wa mwanadamu Kwangu ni mdogo kiasi kwamba upo tu katikati ya ama kutokuwa na maumivu au kutokuwa na utamu?” Katika ulimwengu wa mwanadamu, mtu yeyote angewezaje kuishi bila maumivu au utamu? Mara kwa mara, Mungu asema, “Hakuna hata mtu mmoja amewahi kuuona uso Wangu kweli na amewahi kusikia sauti Yangu kweli, kwani mwanadamu hanijui kweli.” Mungu asema kwamba mwanadamu hamjui Yeye kweli, lakini kwa nini Anataka mwanadamu amjue? Je, huu si ukinzani? Kila mojawapo ya maneno ya Mungu lina lengo fulani. Kwa kuwa mwanadamu amekuwa sugu, Mungu anatumia kanuni ya kufanya 100% ya kazi Yake ndani ya mwanadamu ili hatimaye kutimiza asilimia 0.1 ndani ya moyo wa mwanadamu. Hiyo ndiyo mbinu ambayo Mungu hufanyia kazi, na Mungu lazima atende hivyo ili kutimiza malengo Yake. Hii pia ni hekima ya maneno ya Mungu kabisa. Je, mmeelewa hili?
Mungu asema “Ninapozionyesha siri Zangu wazi na kufanya wazi mapenzi Yangu katika mwili, hamwoni haya yote; mnaisikiliza sauti, lakini hamwelewi maana yake. Mimi hukumbwa na huzuni kuu. Ingawa Mimi Niko katika mwili, Ninakosa uwezo wa kufanya kazi ya huduma ya mwili.” Katika suala moja, maneno haya huwafanya watu, kwa ajili ya usugu wao, kuanza kushirikiana na Mungu; katika suala lingine, Mungu hufichua sura ya kweli ya uungu Wake katika mwili. Kwa kuwa kimo cha watu ni kidogo sana, ufunuo wa uungu wakati wa kipindi ambacho Mungu yuko ndani ya mwili ni kufuatana tu na uwezo wa mwanadamu wa kukubali. Wakati wa hatua hii ya kazi, watu wengi hubaki wasioweza kuwa na ridhaa kamili, ambalo linaonyesha kwa kiasi cha kutosha vile uwezo wao wa ridhaa ni hafifu. Hivyo, uungu hautekelezi kwa ukamilifu kazi yake ya asili unapofanya kazi; hii ni sehemu ndogo tu. Hili linaonyesha kwamba katika kazi ya siku za baadaye, uungu utafichuliwa polepole kufuatana na hali ya kupatikana tena kwa mwanadamu. Uungu, hata hivyo, haukui polepole, lakini ni kile ambacho Mungu mwenye mwili anacho kimsingi, na si kama kimo cha mwanadamu.
Kulikuwa na lengo na maana kwa Mungu kumuumba mwanadamu, na hivyo Mungu asema, “Kama mwanadamu angeangamizwa na ghadhabu Yangu, umuhimu wa kuumba Kwangu kwa mbingu na dunia ungekuwa nini?” Baada ya mwanadamu kupotoshwa, Mungu alipanga upataji wa sehemu ya watu kwa sababu ya kujifurahisha Kwake; si kweli kwamba watu wote wanatakiwa kuangamizwa, au kwamba watang’olewa wakikiuka hata kidogo amri za usimamizi za Mungu. Haya si mapenzi ya Mungu. Kama alivyosema Mungu, hilo halingekuwa na maana. Ni hasa kwa sababu ya “kutokuwa na maana” huku ndiyo hekima ya Mungu inafanywa kuwa wazi. Je, hakuna umuhimu mkuu zaidi kwa Mungu kuzungumza na kutenda kazi kwa njia nyingi ili kuadibu, kuhukumu, na kuwagonga watu wote, hatimaye kuchagua wale wanaompenda kweli? Na ni kwa njia hii hasa ndio matendo ya Mungu hufichuliwa, kwa hiyo uumbaji wa mwanadamu unakuwa wa maana zaidi. Hivyo, mengi ya maneno ya Mungu huelea yakienda; hili ni ili kutimiza lengo, na huu pekee ndio uhalisi wa baadhi ya maneno Yake.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni