Nyimbo za kusifu | 235. Mmempa Mungu Nini Kama Malipo?
I
Mungu amekuwa kati yenu
kwa majira kadhaa ya kupuputika na ya kuchipua.
Ameishi nanyi kwa muda mrefu.
Mbele Yake ni matendo yenu mangapi maovu yamenyiririka?
Maneno ya dhati mnayoyasema, yanarudisha mwangwi katika masikio ya Mungu.
Mamilioni ya matakwa yenu hayawezi kuhesabiwa,
juu ya madhabahu Yake yamewekelewa.
Na bado hakuna kujitolea, hakuna chembe ya uaminifu
Madhabahu yake mnayalalia.

