Maonyesho ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu" Sehemu ya Tano
Aina ya Tano: Hatua ya Maisha Yaliyokomaa, au Hatua ya Mtu Mzima
Mwenyezi Mungu alisema, Baada ya kupitia awamu ya mtoto mchanga hadi ya utoto, awamu hii ya ukuaji uliojaa kupindua kunakojirudia, maisha ya watu tayari yamekuwa thabiti, hatua yao ya kusonga mbele haisiti tena, wala hakuna yeyote anayeweza kuwazuia. Ingawaje njia iliyo mbele ingali na mabonde na misukosuko, si wanyonge tena au wenye woga; hawayumbiyumbi tena huko mbele au kupoteza mwelekeo wao. Misingi yao imekita mizizi kwenye hali halisi ya neno la Mungu. Mioyo yao imevutwa na heshima na ukubwa wa Mungu. Wanatamani kufuata nyayo za Mungu, kujua hali halisi ya Mungu, kujua Mungu kwa uzima Wake.
Watu katika awamu hii tayari wanajua waziwazi ni nani wanayemsadiki, na wanajua waziwazi kwa nini wanafaa kumsadiki Mungu na maana ya maisha yao husika; wanajua pia waziwazi kwamba kila kitu ambacho Mungu huelezea ndicho ukweli. Kwenye miaka yao mingi ya uzoefu, wametambua kwamba bila ya hukumu na kuadibu kwa Mungu, mtu hatawahi kuweza kutosheleza au kumjua Mungu, wala mtu huyo hataweza kuja mbele ya Mungu. Ndani ya mioyo ya watu hawa husika kunalo tamanio thabiti la kujaribiwa na Mungu, ili kuona tabia ya haki ya Mungu huku wakiendelea kujaribiwa, kufikia upendo safi zaidi, na wakati uo huo kuweza kuelewa na kujua Mungu kwa njia ya kweli zaidi. Wale walio katika awamu hii tayari wameaga kwaheri awamu ya mtoto, awamu ya kufurahia neema ya Mungu na kula mkate na kushiba. Hawaweki tena matumaini mengi katika kumfanya Mungu kuvumilia na kuwaonyesha huruma; badala yake, wanao ujasiri wa kupokea na kutumai kupata kuadibu na hukumu isiyosita ya Mungu, ili kuweza kujitenga na tabia yao potovu na hivyo basi kutosheleza Mungu. Maarifa yao kwa Mungu, kufuatilia kwao au shabaha za mwisho za kufuatilia kwao: mambo haya yote yako wazi kabisa katika mioyo yao. Hivyo basi, watu katika awamu ya mtu mzima tayari wameaga kwaheri kabisa awamu ya imani isiyo dhahiri, kwenye awamu ambayo wanategemea neema kupata wokovu, kwenye awamu ya maisha yasiyo komavu yasiyoweza kustahimili majaribio, hadi kwenye awamu ya kutokuwa bainifu, hadi kwenye awamu ya kuyumbayumba, hadi kwenye awamu ya mara kwa mara kutokuwa na njia ya kufuata, hadi kwenye kipindi kisichokuwa thabiti cha kubadilisha kati ya joto na baridi ya ghafla, na hadi kwenye awamu ambapo mtu anafuata Mungu huku ameyafumba macho yake. Aina hii ya mtu hupokea nuru na mwangaza wa Mungu mara kwa mara, na pia mara kwa mara hujihusisha katika ushirikiano na mawasiliano ya kweli na Mungu. Mtu anaweza kusema kwamba watu wanaoishi katika awamu hii tayari wameng’amua sehemu ya mapenzi ya Mungu; wanaweza kupata kanuni za ukweli katika kila kitu wanachofanya; wanajua namna ya kutosheleza tamanio la Mungu. Isitoshe, wamepata pia njia ya kumjua Mungu na wameanza kuwa na ushuhuda wa maarifa yao kwa Mungu. Kwenye mchakato huu wa ukuaji wa utaratibu, wanao ufahamu wa taratibu na maarifa ya mapenzi ya Mungu, ya mapenzi ya Mungu katika kuumba ubinadamu, ya mapenzi ya Mungu katika kusimamia binadamu; vilevile, kwa utaratibu wanao ufahamu na maarifa ya tabia ya haki ya Mungu kwa mujibu wa hali halisi. Hakuna dhana ya binadamu au kufikiria kunaweza kubadilisha maarifa haya. Huku mtu hawezi kusema kwamba kwenye awamu ya tano maisha ya mtu yamekomaa kabisa au kumwita mtu huyu mwenye haki au mkamilifu, aina hii ya mtu tayari amechukua hatua ya kuelekea kwenye awamu ya ukomavu katika maisha; mtu huyu tayari anaweza kuja mbele ya Mungu, kusimama ana kwa ana na neno la Mungu na kuwa ana kwa ana na Mungu. Kwa sababu mtu wa aina hii tayari amepitia mengi sana yanayohusu neno la Mungu, amepitia majaribio yasiyokadirika na kupitia matukio yasiyokadirika ya nidhamu, hukumu na kuadibu kutoka kwa Mungu, unyenyekevu wake kwa Mungu si wa kutegemea chochote bali ni kamili. Maarifa yao kwa Mungu yamebadilika kutoka kwenye kufichika akilini hadi kwa maarifa wazi na hakika, kutoka kwenye hali ya juujuu hadi kina, kutoka kwenye hali ya kutoeleweka na kutokuwa bainifu hadi hali ya umakinifu na uyakinifu, na wamebadilika kutoka kwenye kutafutatafuta kwa bidii na kutafuta kwa njia iliyo baridi hadi katika hali ya kuwa na maarifa kwa hakika na utoaji ushuhuda wenye mnato. Inaweza kusemekana kwamba watu katika awamu hii wamemiliki uhalisi wa ukweli wa neno la Mungu, kwamba wamepitia kwenye njia ya utimilifu kama vile Petro alivyopita. Huyu ndiye mtu wa aina ya tano, yule anayeishi katika hali ya kuwa mkomavu—awamu ya kuwa mtu mzima.
Desemba 14, 2013
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni