6/18/2019

Wimbo wa Injili 87. Mandhari Mapya Kila siku ya Ufalme

Wimbo wa Injili 87. Mandhari Mapya Kila siku ya Ufalme

I
Katika Mashariki, jua linalochomoza linaangaza katika anga zenye ukungu,
na ufalme wa uzuri mkuu
umekamilishwa katika ulimwengu huu.
Ulimwengu unayakubali maisha mapya, vitu vyote vinapewa nguvu mpya.
Eh! Pambazuko limefika sasa.
Eh! Mwangaza uko mbele ya macho yetu.
Tumaini la miaka elfu mbili hatimaye limefanikishwa.
Miaka ya huzuni imeisha, hakuna tena mchana na usiku yenye huzuni.
Haleluya! (Haleluya!) Haleluya! (Haleluya!)
Haleluya! (Haleluya!) Haleluya! (Haleluya!)
II
Maua yanachanua na kunukia vema,
vipozamataza wanaimba juu angani.
Habari njema inasambazwa kote.
Watu wa Mungu wanahisi upendo Wake,
wanatoa maoni yao kwa uhuru, wote kama kitu kimoja.
Eh! Omba kwa kujitolea. Eh! Sifu kwa sauti.
Sujudu mbele ya kiti cha enzi.
Tunampa Mungu utukufu. Ndugu zetu wanazivuka bahari,
hebu tusherehekee pamoja, familia zetu za mbali.
Haleluya! (Haleluya!) Haleluya! (Haleluya!)
Haleluya! (Haleluya!) Haleluya! (Haleluya!)
III
Mungu, Bwana wa ulimwengu, amepata mwili
na anafanya kazi Yake miongoni mwa mwanadamu.
Analeta maisha ya ufalme,
anaonyesha maneno kutukimu.
Aha, mioyo yetu inanyunyiziwa na maji ya uzima,
inahisi kubarikiwa na utamu.
Sisi ndicho kizazi ambacho Mungu amekichagua.
Sisi ndicho kizazi ambacho Mungu amekiteua.
Haleluya! (Haleluya!) Haleluya! (Haleluya!)
Haleluya! (Haleluya!) Haleluya! (Haleluya!)
IV
Kuingia katika ufalme wa Mungu, hicho ni kitu tunachotamani sote.
Kuishi kwa kudhihirisha ukweli tukamilishwe,
ahadi ya Mungu tutapata.
Eh, tuendelee mbele kwa nguvu zetu zote.
Eh, tung’ang’ane kwa uwezo wetu wote.
Turidhishe mapenzi ya Mungu,
na tutang’aa kwa nuru kuu zaidi.
Roho ya Petro, tuko imara kung’ang’ana,
na tuyatende mapenzi ya Mungu sasa ili tuishi maisha ya kweli ya mwanadamu.
Haleluya! (Haleluya!) Haleluya! (Haleluya!)
Haleluya! (Haleluya!) Haleluya! (Haleluya!)
Haleluya! (Haleluya!) Haleluya! (Haleluya!)
Haleluya! (Haleluya!) Haleluya! (Haleluya!)

Chanzo: 87. Mandhari Mapya Kila siku ya Ufalme
Tufuate: Asili ya  Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni