“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Nne
Mwenyezi Mungu alisema, Je, mielekeo kumwelekea Mungu ya watu hawa wa aina mbalimbali waliotajwa hapo juu ipo miongoni mwenu? (Ipo.) Kama, katika imani yao katika Mungu, moyo wa mtu una mwelekeo wowote kati ya hii, je, kweli wanaweza kuja mbele za Mungu? Kama watu wana mwelekeo wowote kati ya hii katika mioyo yao, je, wanamwamini Mungu? Je, wanamwamini Mungu Mwenyewe yule wa kipekee? (La.) Kwa kuwa humwamini Mungu wa kipekee Mwenyewe, unamwamini nani? Kama unachoamini si Mungu Mwenyewe wa kipekee, kuna uwezekano unaamini katika sanamu, mtu maarufu, au Bodhisattva, kuwa unamwabudu Budha moyoni mwako.
Zaidi ya hayo, kuna uwezekano unaamini katika mtu wa kawaida. Kwa muhtasari, kwa sababu ya aina tofautitofauti za imani za watu na mielekeo kwa Mungu, watu humweka Mungu wa utambuzi wao wenyewe katika nyoyo zao, wanamlazimishia Mungu fikira zao, wanaweka fikira na mielekeo yao kuhusu Mungu sambamba na Mungu Mwenyewe wa kipekee, na kisha wanayanyanyua juu kuyashangilia. Ina maana gani watu wakiwa na mielekeo hiyo isiyofaa kwa Mungu? Ina maana kuwa wamemkataa Mungu wa kweli Mwenyewe na kuabudu Mungu bandia, na ina maana kuwa wakati uleule wanapomwamini Mungu, wanamkataa Mungu, wanampinga, na kuwa wanakana uwepo wa Mungu wa kweli. Kama watu watazidi kushikilia imani za aina hiyo, matokeo yao yatakuwa gani? Kwa aina hiyo ya imani, je, wanaweza kufikia karibu na kutimiza matakwa ya Mungu? (La, hawawezi.) Kinyume cha hayo, kwa sababu ya dhana na fikira zao, watu watazidi kuwa mbali na njia ya Mungu, kwa kuwa njia wanayoifuata ni kinyume cha njia ambayo Mungu anawahitaji waifuate. Umekwisha kusikia hadithi ya “kwenda kusini kwa kuendesha gari la farasi kuelekea kaskazini”? Hii yaweza kuwa ni mfano wa kwenda kusini kwa kuendesha gari la farasi kuelekea kaskazini. Watu wakimwamini Mungu kwa njia hii ya kipumbavu, basi kadiri unavyojaribu kwa nguvu, ndivyo utakavyokuwa mbali zaidi na Mungu. Na kwa hiyo nakuonya hivi: Kabla ya kufunga safari, ni lazima kwanza ujue kama unaenda njia iliyo sawa. Lenga katika juhudi zako, kuwa na uhakika na kujiuliza, “Je, Mungu ninayemwamini ni Mtawala wa vitu vyote? Je, huyu Mungu ninayemwamini ni mtu tu wa kunipa riziki ya kiroho? Ni sanamu yangu? Je, huyu Mungu ninayemwamini anataka nini kutoka kwangu? Mungu huwa anakubali chochote ninachokifanya? Je, kila kitu ninachokifanya na kutafuta kinalingana na kazi ya kumjua Mungu? Je, kinalingana na mahitaji ya Mungu kwangu? Je, njia ninayoifuata inajulikana na kukubaliwa na Mungu? Je, Mungu anaridhishwa na imani yangu?” Aghalabu na mara kwa mara unafaa ujiulize haya maswali. Kama ungetaka kuutafuta ufahamu wa Mungu, basi lazima uwe na dhamiri safi na malengo wazi ndipo uweze kumridhisha Mungu.
Chanzo: “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Nne
Jifunze zaidi: Kuhusu Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni