6/20/2019

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu alisema, Hebu turejee kwa wateule wa Mungu. Wanapokufa, wateule wa Mungu huenda sehemu fulani tofauti kabisa na wasioamini na watu mbalimbali wenye imani. Ni sehemu ambayo wanaambatana na malaika na wajumbe wa Mungu, na ambayo inaendeshwa na Mungu binafsi. Japo katika sehemu hii, wateule wa Mungu hawawezi kumwona Mungu kwa macho yao wenyewe, si kama sehemu nyingine yoyote katika milki ya kiroho; ni sehemu ambayo hili kundi la watu huenda baada ya kufa. Wakifa, wao pia hupitia uchunguzi mkali kutoka kwa wajumbe wa Mungu. Na ni nini kinachochunguzwa? Wajumbe wa Mungu huchunguza njia zilizopitiwa na hawa watu katika maisha yao yote katika imani yao kwa Mungu, ikiwa waliwahi au hawakuwahi kumpinga Mungu wakati huo, au kumlaani, na ikiwa walitenda au hawakutenda dhambi mbaya au maovu. Uchunguzi huu unajibu swali la ikiwa mtu fulani ataondoka au atabaki. “Kuondoka” kunarejelea nini? Na “kubaki” kunarejelea nini? “Kuondoka” kunarejelea ikiwa, kulingana na mienendo yao, watabaki miongoni mwa madaraja ya wateule wa Mungu. “Kubaki” kunarejelea kuwa wanaweza kubaki miongoni mwa watu ambao wanafanywa na Mungu kuwa kamili katika siku za mwisho. Mungu ana mipango maalum kwa wale wanaobaki. Katika kila kipindi cha kazi Yake, Mungu atatuma watu kufanya kazi kama mitume au kufanya kazi ya kuyaamsha makanisa, au kuyahudumia. Lakini watu ambao wana uwezo wa kazi kama hizo hawapati miili mara kwa mara kama wasioamini, ambao wanazaliwa upya tena na tena; badala yake, wanarudishwa duniani kulingana na mahitaji na hatua ya kazi ya Mungu, na si wale wapatao mwili mara kwa mara. Je, kuna amri kuhusu ni lini wapate mwili? Je, wanakuja mara moja baada ya kila miaka michache? Je, wanakuja na hiyo haraka? Hawafanyi hivyo. Hii inategemea nini? Inategemea kazi ya Mungu, hatua ya kazi ya Mungu, na mahitaji Yake, na hakuna amri. Amri moja tu ni kwamba Mungu akifanya hatua ya mwisho ya kazi Yake katika siku za mwisho, wateule hawa wote watakuja. Wakija wote, hii itakuwa mara ya mwisho ambapo wanapata mwili. Na kwa nini hivyo? Hii inategemea matokeo yatakayopatikana katika hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu—kwani katika hatua hii ya mwisho ya kazi, Mungu atawafanya wateule hawa kuwa kamili kabisa. Hili linamaanisha nini? Ikiwa, katika hii awamu ya mwisho, watu hawa watafanywa kuwa kamili, na kufanywa wakamilifu, basi hawatapata mwili kama awali; mchakato wa kuwa wanadamu utakamilika kabisa, sawa na mchakato wa kupata mwili. Hili linawahusu wale watakaobaki. Je, wale ambao hawawezi kubaki huenda wapi? Wasioweza kubaki wanakuwa na sehemu mwafaka ya kwenda. Kwanza kabisa kwa sababu ya maovu yao, makosa waliyofanya, na dhambi walizofanya, wao pia wanaadhibiwa. Baada ya kuadhibiwa, Mungu anawatuma miongoni mwa wasioamini; kulingana na hali ilivyo, Atafanya mpango wawe miongoni mwa wasioamini, vinginevyo miongoni mwa watu mbalimbali wenye imani. Yaani, wana chaguzi mbili: Moja ni labda waishi miongoni mwa watu wa dini fulani baada ya adhabu, na nyingine ni wawe wasioamini. Kama watakuwa wasioamini, basi watapoteza kila fursa. Lakini wakiwa watu wa imani—kwa mfano, wakiwa Wakristo—bado wangali na nafasi ya kurudi miongoni mwa madaraja ya wateule wa Mungu; kwa hili kuna uhusiano changamano sana. Kwa ufupi, ikiwa mmoja wa wateule wa Mungu atafanya kitu kitakachomkosea Mungu, wataadhibiwa sawa tu na watu wengine. Chukulia Paulo, kwa mfano, ambaye tulizungumzia awali. Paulo ni mfano wa wale wanaoadhibiwa. Je, mnapata picha ya yale ninayozungumzia? Je, mipaka ya wateule wa Mungu ni ya kudumu? (Kwa kiasi kikubwa ni ya kudumu.) Kiasi kikubwa chake ni cha kudumu, lakini sehemu ndogo si ya kudumu. Kwa nini hivyo? (Kwa sababu wametenda maovu.) Nimerejelea hapa mfano mmoja dhahiri: kutenda maovu. Wanapotenda maovu, Mungu hawataki, na wakati Mungu hawataki, anawatupa miongoni mwa makabila na aina mbalimbali za watu, kitu ambacho kinawaacha bila tegemeo na kufanya kurudi kwao kuwe kugumu. Haya yote yanahusu mzunguko wa uhai na mauti wa wateule wa Mungu.
aaa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni