Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yehova. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yehova. Onyesha machapisho yote

1/14/2019

Umeme wa Mashariki | 2. Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

Umeme wa Mashariki | 2. Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

(1) Lengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ambayo Yehova Alifanya kwa Waisraeli ilianzishwa miongoni mwa binadamu mahali pa asili pa Mungu hapa ulimwenguni, pahali patakatifu ambapo Alikuwepo. Hii kazi Aliiwekea mipaka miongoni mwa watu wa Israeli tu. Kwanza, hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Alichagua watu Alioona kwamba walifaa ili kuwawekea mipaka upana wa kazi Yake. Israeli ndipo mahali ambapo Mungu Aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka kwenye vumbi la mahali hapo, Yehova Alimwumba mwanadamu; ndio msingi wa kazi Yake ya hapo ulimwenguni. Waisraeli, ambao ni kizazi cha Nuhu na Adamu, ndio waliokuwa msingi wa kazi ya Yehova ulimwenguni.

1/14/2018

Sura ya 58. Upendo wa Kweli wa Mungu kwa Wanadamu

Sura ya 58. Upendo wa Kweli wa Mungu kwa Wanadamu

    Mwenyezi Mungu alisema, Katika kukifahamu kiini cha Kristo, kipengele kimoja ni kuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya kupata mwili Kwake na binadamu; aidha, watu ambao wanafahamu kiini cha Kristo wana uwezo zaidi kuwa hakika kuhusu Mungu kuwa mwili na uwezo zaidi wa kuamini kuwa Yeye kweli Yupo, kuwa Yeye si nabii, mtume, wala mwenye kufunua, na hasa si mtu mdogo aliyetumwa hapa na Mungu; bali Yeye ni mwenye mwili, Yeye ni Kristo, Naye ni Mungu Mwenyewe. Hata kama mwili ulikuwa sehemu miongoni mwa watu, Alikuwa mtu wa kawaida na kiini cha Uungu.

12/26/2017

Sura ya 33. Jinsi ya Kufahamu Tabia Yenye Haki ya Mungu

Sura ya 33. Jinsi ya Kufahamu Tabia Yenye Haki ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wanaweza kupangwa kwa makundi, ambayo hubainishwa kwa roho zao. Watu wengine wana roho za binadamu, na wao huchaguliwa kwa njia iliyoamuliwa kabla. Ndani ya roho ya binadamu kuna sehemu iliyoamuliwa kabla. Watu wengine hawana roho; wao ni pepo ambao wamepenyeza. Hawajaamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mungu. Ingawa wamekuja ndani, hawawezi kuokolewa, na hatimaye wataondolewa na pepo.

11/28/2017

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)



Mwenyezi Mungu alisema, Wanadamu kwakupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa.

11/23/2017

Kazi Katika Enzi ya Sheria

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

 Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani. 

11/16/2017

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (2)


Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

 Mwenyezi Mungu alisemaMlikuwa mnatafuta kutawala kama wafalme, na leo bado hamjaacha kabisa suala hili; bado unatamani kutawala kama wafalme, kushikilia juu mbingu na kusaidia dunia. Sasa, fikiria kuhusu hilo: Je, unazo sifa kama hizo? Je, huoni unakuwa mtu usiyekuwa na maana? Je, mnachokitafuta na kujitolea umakini wenu kwacho ni cha uhalisi?

11/15/2017

Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu

Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Enzi ya Neema ilihubiri injili ya toba, na alimradi mwanadamu aliamini, basi angeokolewa. Leo, badala ya wokovu kuna majadiliano tu ya ushindi na ukamilifu. Haisemwi katu kwamba mtu mmoja akiamini, familia yake yote itabarikiwa, au kwamba wokovu ni ya mara moja na kwa wote. Leo, hakuna mtu anayezungumza maneno haya, na vitu kama vile vimepitwa na wakati.

10/26/2017

Umeme wa Mashariki | Je, Utatu Mtakatifu Upo?


Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu
Ni baada tu ya ukweli wa Yesu kuwa mwili kutokea ndipo mwanadamu alipogundua hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana ya kawaida aliyonayo mwanadamu, kwamba kuna Mungu wa aina hii mbinguni: Utatu ambao ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote katika nafsi moja. 

10/22/2017

Umeme wa Mashariki | Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku Ya Ghadhabu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu
Leo, Nawaonya hivi kwa ajili ya kusalimika kwenu wenyewe, ili kazi Yangu iendelee vizuri, na ili kazi Yangu ya uzinduzi kote ulimwenguni iweze kufanyika kwa njia inayofaa na kikamilifu, ikifichua maneno Yangu, mamlaka, adhama na hukumu kwa watu wa nchi zote na mataifa. Kazi Ninayoifanya miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi Yangu katika ulimwengu wote. 

10/05/2017

Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi"


1. Wanadamu kwa kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa. Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote. Hili ndilo linapaswa kufanywa katika hatua hii ya kazi. 

9/18/2017

Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote | Umeme wa Mashariki


  Hatua moja ya kazi ya enzi mbili za awali ilifanyika Israeli; nyingine ilifanyika Uyahudi. Kuzungumza kwa jumla, hakuna hatua ya kazi hii iliyotoka Israeli; zilikuwa ni hatua za kazi zilizofanywa miongoni mwa wateule wa mwanzo. Hivyo, kwa mtazamo wa Wanaisraeli, Yehova Mungu ni Mungu wa Wanaisraeli pekee. Kwa sababu ya kazi ya Yesu huko Uyahudi, na kwa sababu ya kukamilisha Kwake kwa kazi ya kusulubiwa, kwa mtazamo wa Wayahudi, Yesu ni Mkombozi wa watu wa Kiyahudi. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi tu, sio wa watu wengine wowote; Yeye si Bwana anayewakomboa Waingereza, wala Bwana anayewakomboa Wamarekani, lakini Yeye ni Bwana anayewakomboa Wanaisraeli, na katika Israeli ni Wayahudi ndio Anaokomboa. Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote. Yeye ndiye Mungu wa viumbe vyote. Yeye si Mungu wa Wanaisraeli pekee, na si Mungu wa Wayahudi pekee; ni Mungu wa viumbe vyote.

9/15/2017

Kuhusu Biblia (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia
Biblia pia huitwa Agano la Kale na Agano Jipya. Je, wajua “agano” linarejelea nini? “Agano” katika “Agano Jipya” linatokana na makubaliano ya Yehova na watu wa Israeli Alipowaua Wamisri na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa Farao. Bila Shaka, uthibitisho wa haya makubaliano ulikuwa damu ya mwanakondoo iliyopakwa kwenye linta kupitia kwayo Mungu Alianzisha agano na mwanadamu, moja ambalo ilisemwa kuwa wale wote waliokuwa na damu ya mwanakondoo juu na pembeni mwa viunzi vya mlango walikuwa Waisraeli, walikuwa wateuliwa wa Mungu, na wote wangeokolewa na Yehova (kwa kuwa Yehova wakati ule Alikuwa karibu kuwaua wazaliwa wa kwanza wa kiume wa Misri wote na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe).