11/16/2017

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (2)


Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

 Mwenyezi Mungu alisemaMlikuwa mnatafuta kutawala kama wafalme, na leo bado hamjaacha kabisa suala hili; bado unatamani kutawala kama wafalme, kushikilia juu mbingu na kusaidia dunia. Sasa, fikiria kuhusu hilo: Je, unazo sifa kama hizo? Je, huoni unakuwa mtu usiyekuwa na maana? Je, mnachokitafuta na kujitolea umakini wenu kwacho ni cha uhalisi? Hamna hata hali ya kawaida ya ubinadamu—hilo si la kutia huruma? Hivyo, leo Nazungumzia tu juu ya kushindwa, kuwa na ushuhuda, kuboresha tabia yako, na kuingia katika njia ya kufanywa kuwa mkamilifu, na kutozungumzia kitu chochote kile. Watu wengine wanaonekana kuchoshwa na ukweli usiotiwa doa, na wanapoona mazungumzo ya ubinadamu wa kawaida na kuboresha tabia ya watu, wanakuwa wabishi.Wale ambao hawapendi ukweli sio rahisi kuwafanya wakamilifu. Ili mradi mnaingia leo, na kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, hatua kwa hatua, je, utaweza kuondolewa? Baada ya kazi kubwa sana kufanyika katika eneo bara la Uchina—kazi ya kiwango kikubwa hivyo—na baada ya maneno mengi zaidi kuwa yamezungumzwa, je, Mungu angeishia njiani? Je, angewapeleka watu katika shimo lisilokuwa na kina? Kitu ambacho ni cha msingi leo ni kwamba mnapaswa kuijua hulka ya mwanadamu, na mnapaswa kujua ni nini unapaswa kuingia kwacho; unapaswa kuzungumza juu ya kuingia katika maisha, na mabadiliko katika tabia, jinsi ya kushindwa, na jinsi ya kumtii Mungu kikamilifu, kuwa na ushuhuda wa Mungu wa mwisho, na kupata utii hata kifo. Unapaswa kutilia mkazo mambo haya, na kwamba kile ambacho si cha uhalisi au muhimu kinapaswa kuwekwa pembeni na kisizingatiwe. Leo, unapaswa kuelewa namna ya kushindwa, na jinsi watu wanavyofanya baada ya kushindwa. Unaweza kusema umeshashindwa, lakini unaweza kutii hata kufa? Unapaswa uwe na uwezo wa kufuata hadi mwisho kabisa bila kujali kama kuna matumaini yoyote, na hupaswi kupoteza imani kwa Mungu bila kujali mazingira. Mwisho wake, unapaswa kupata aina mbili za ushuhuda: ushuhuda wa Ayubu—utii hata kifo—na ushuhuda wa Petro—upendo mkuu wa Mungu. Kwa upande mmoja, unapaswa kuwa kama Ayubu: Hakuwa na mali hata kidogo, na mwili wake ukawa unateseka kwa maumivu, lakini hakulikana jina la Yehova. Huu ulikuwa ni ushuhuda wa Ayubu. Petro aliweza kumpenda Mungu hadi kifo. Alipokufa—alipoangikwa msalabani—bado alimpenda Mungu; hakufikiria juu ya maisha yake ya baadaye au kutafuta mambo yaliyo makuu au fikra za anasa, na alitafuta tu kumpenda Mungu, na kutii mipango yote ya Mungu. Hicho ndicho kiwango unachopaswa kuwa nacho kabla hujahesabiwa kuwa umebeba ushuhuda, kabla hujawa mtu ambaye amefanywa mkamilifu baada ya kushindwa. Leo, ikiwa watu wangekuwa wanajua kabisa hulka na hadhi yao, je, bado wangetafuta mambo yao na matumaini yao? Unachopaswa kujua ni hiki: Bila kujali kama Mungu atanifanya mkamilifu, ni lazima Nimfuate Mungu; kila kitu anachofanya sasa ni chema, na kwa ajili yetu, na ili kwamba tabia yetu iweze kubadilika, na tuweze kuepukana na ushawishi wa Shetani, kuturuhusu kuishi katika nchi ya uchafu na kuepukana na uchafu, kuondoa uchafu na ushawishi wa Shetani, kutuwezesha kuacha nyuma ushawishi wa Shetani. Kimsingi, hiki ndicho unachotakiwa kuwa nacho, lakini kwa Mungu ni kushinda tu, ili watu waweze kutii, na kujikabidhi kikamilifu katika mipango ya Mungu, ni kitu pekee ambacho kinahitajika. Leo, watu wengi tayari wamekwishashindwa, lakini ndani yao bado kuna mengi ambayo ni ya uasi na siyo ya utii. Kimo cha kweli wa watu bado ni mdogo sana, na wanaongezeka ikiwa tu kuna matumaini na matarajio, kama hayapo, wanakuwa na mitazamo hasi, na hata wanafikiria kumwacha Mungu. Na watu hawana shauku ya kutafuta kuishi kulingana na maisha ya ubinadamu wa kawaida. Mambo hayako hivyo! Hivyo, bado lazima Nizungumze juu ya ushindi. Kimsingi, ukamilifu unatokea wakati ule ule wa kushinda: Unaposhindwa, matokeo ya kwanza ya kufanywa mkamilifu pia yanafikiwa. Panapokuwa na tofauti kati ya kushindwa na kufanywa mkamilifu, ni kulingana na kiwango cha mabadiliko kwa watu. Kushindwa ni hatua ya kwanza ya kufanywa mkamilifu, na haimaanishi kwamba wamefanywa wakamilifu kabisa, wala kuthibitisha kwamba wamechukuliwa na Mungu kikamilifu. Baada ya watu kushindwa, kunakuwa na mabadiliko katika tabia yao, lakini mabadiliko hayo yanakuwa ya chini sana kulinganisha na mabadiliko ya watu ambao wamechukuliwa na Mungu kikamilifu. Leo, kile kinachofanywa ni kazi ya mwanzo ya kuwafanya watu kuwa wakamilifu—kuwashinda—na kama huwezi kushindwa, basi hutaweza kuwa na uwezo wa kufanywa mkamilifu na kuchukiliwa na Mungu kikamilifu. Utapata tu maneno machache ya kuadibu na hukumu, lakini hayatakuwa na uwezo wa kubadilisha kabisa moyo wako. Hivyo utakuwa mmoja wa wale ambao wameondolewa; haitakuwa na tofauti na kutazama tu karamu ya gharama mezani lakini hutakula. Je, hayo sio majanga? Na hivyo, ni lazima utafute mabadiliko: Ama iwe ni kushindwa au kufanywa mkamilifu, yote yanahusiana na kama kuna mabadiliko ndani yako, kama wewe ni mtii au la, na hii inaamua kama unaweza kuchukuliwa na Mungu au la. Elewa kwamba "kushindwa" na "kufanywa mkamilifu" kumejikita katika kiwango cha mabadiliko na utii, vilevile katika jinsi ambavyo upendo wako kwa Mungu ulivyo. Kinachotakiwa leo ni kwamba unaweza kufanywa mkamilifu, lakini mwanzoni ni lazima ushindwe, ni lazima uwe na maarifa ya kutosha juu ya kuadibu na hukumu ya Mungu, lazima uwe na imani ya kufuata, na kuwa mtu ambaye anatafuta mabadiliko na kuwa na matokeo. Baada ya hapo tu ndipo utakuwa mtu ambaye anatafuta kufanywa mkamilifu. Mnapaswa kuelewa kwamba katika mchakato wa kufanywa kuwa mkamilifu, mtashindwa, na katika mchakato wa kushindwa mtafanywa kuwa wakamilifu. Leo, unaweza kutafuta kufanywa kuwa mkamilifu au kutafuta mabadiliko katika utu wako wa nje na uboreshaji katika tabia yako, lakini muhimu kabisa ni kwamba unaweza kuelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya leo kina maana na ni cha manufaa: Kinakuwezesha wewe ambaye unaishi katika nchi ya uchafu kuepuka uchafu na kuuondoa wote, kinakuwezesha kushinda ushawishi wa Shetani na kuacha nyuma ushawishi wa Shetani—na kwa kujikita katika vitu hivi, unakuwa umelindwa katika nchi hii ya uchafu. Mwishowe, utaambiwa kutoa ushuhuda gani? Unaishi katika nchi ya uchafu lakini unaweza kuwa mtakatifu, na kutokuwa tena mchafu na mwenye najisi, unamilikiwa na Shetani, lakini unaachana na ushawishi wa Shetani, na unaacha kumilikiwa au kunyanyaswa na Shetani, na unaishi mikononi mwa Mwenyezi. Huu ndio ushuhuda na uthibitisho wa ushindi katika vita na Shetani. Unaweza kumwacha Shetani, maisha unayoishi kwa kudhihirisha hayamfichui Shetani, lakini ni kile ambacho Mungu alitaka kwamba mwanadamu apate alipomuumba mwanadamu: ubinadamu wa kawaida, urazini wa kawaida, umaizi wa kawaida, hisia za kawaida za kumpenda Mungu, na utii kwa Mungu. Huo ndio ushuhuda unaochukuliwa na kiumbe wa Mungu. Unasema, "Tunaishi katika nchi ya uchafu, lakini kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, kwa sababu ya uongozi wake, na kwa sababu ametushinda, tumejiondoa katika ushawishi wa Shetani. Kwamba tunaweza kutii leo, ni matokeo ya kushindwa na Mungu, na sio kwa sababu sisi ni wema, au kwa sababu tunampenda Mungu kwa asili. Ni kwa sababu Mungu alituchagua, na kutuamulia kabla, kwamba tumeshindwa leo, tunaweza kuwa na ushuhuda Wake, na tunaweza kumtumikia, hivyo pia, ni kwa sababu alituchagua, na kutulinda, kwamba tumechaguliwa na kutolewa katika mamlaka ya Shetani, na tunaweza kuacha kando uchafu na kusafishwa katika nchi ya joka kuu jekundu." Aidha, kile unachoishi kwa kudhihirisha nje, kitaonyesha kwamba una ubinadamu wa kawaida, kuna urazini katika kile unachosema, na unafanana na mtu wa kawaida. Watu wengine watakapowaangalia wasiweze kusema, je, hii sio sura ya joka kuu jekundu? Matendo ya dada hayaonekani kuwa ni ya dada, matendo ya kaka hayaonekani kuwa ni ya kaka, na hawana staha ya watakatifu. Hawapaswi kusema, ndio maana Mungu alisema ni wazaliwa wa Moabu, Alikuwa sahihi kabisa! Ikiwa watu wanawatazama na kusema, "Ingawa Mungu alisema wewe ni uzao wa Moabu, kile unachokiishi kwa kudhihirisha kimethibitisha kwamba umetanga mbali na ushawishi wa Shetani; ingawa mambo hayo bado yapo ndani yako, unaweza kuachana nayo," basi hii inaonyesha kwamba umeshindwa kikamilifu. Wewe ambaye umeshindwa na kuokolewa utasema, "Ni kweli kwamba sisi ni uzao wa Moabu, lakini tumeokolewa na Mungu, na ingawa uzao wa Moabu ulikataliwa na kulaaniwa, na kupelekwa uhamishoni na Waisraeli miongoni mwa Wamataifa, leo Mungu ametuokoa. Ni kweli kwamba sisi ni waovu kuliko watu wote—hii ilitamkwa na Mungu, huu ni ukweli, na haupingwi na mtu yeyote. Lakini leo tumeukwepa ushawishi huo. Tunawachukia mababu zetu, tupo radhi kuwageuzia mgongo mababu zetu, kuwatelekeza kabisa na kutii mipango yote ya Mungu, kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, na kufanikiwa kukamilisha matakwa yake kwetu, na kukidhi mapenzi ya Mungu. Moabu alimsaliti Mungu, hakutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, na alichukiwa na Mungu. Lakini tunapaswa kujali moyo wa Mungu, na leo, kwa kuwa tunaelewa mapenzi ya Mungu, hatuwezi kumsaliti Mungu, na tunapaswa kuwakana mababu zetu!" Huko nyuma Nilizungumza juu ya kumkana joka kuu jekundu—na leo, ni kukana hasa mababu wa kale. Huu ni ushuhuda mmoja wa watu kushindwa, na bila kujali, ni jinsi gani unaingia leo, ushuhuda wako katika eneo hili haupaswi kupungua.
Tabia ya watu ni duni sana, wanapungukiwa sana ubinadamu wa kawaida, maamuzi yao ni ya chini sana, ya polepole, uharibifu wa Shetani umewaacha wakiwa wapumbavu, na ingawa hawawezi kubadilika kabisa kwa kipindi cha mwaka mmoja au miwili, ni lazima watakuwa na azimio la kushiriki. Inaweza kusemwa kuwa huu pia ni ushuhuda mbele ya Shetani. Ushuhuda wa leo ni matokeo ya yaliyofikiwa na kazi ya sasa ya kushinda, vilevile mfano wa kuigwa kwa wafuasi wa baadaye. Hapo baadaye, utaenea katika mataifa yote; kile kinachofanyika China kitaenea katika mataifa yote. Uzao wa Moabu ni watu duni sana kuliko watu wote duniani. Watu wengine huuliza, je, kwani wafuasi wa Hamu sio duni kuliko wote? Kizazi cha joka kuu jekundu na uzao wa Hamu wanawakilisha vitu tofauti, na uzao wa Hamu ni suala jingine. Bila kujali ni jinsi gani walilaaniwa, bado ni uzao wa Nuhu; asili ya Moabu haikuwa safi, alitoka katika ufisadi, na hii ndiyo tofauti. Ingawa wote walilaaniwa, hali zao hazikuwa sawa, na hivyo uzao wa Moabu ni watu duni kabisa kuliko wote—hakuna ukweli unaoweza kushawishi kuliko kushindwa kwa watu duni kuliko watu wote. Kazi ya siku za mwisho inavunja kanuni zote, bila kujali kama uliadhibiwa au kulaaniwa, ilimradi tu unaisaidia kazi Yangu, na una manufaa katika kazi ya kushinda leo, na bila kujali kama wewe ni uzao wa Moabu au kizazi cha joka kuu jekundu, ili mradi tu unatimiza wajibu wa kiumbe wa Mungu katika hatua ya kazi, na kufanya kadri unavyoweza, basi matokeo yanayotarajiwa yatafikiwa. Wewe ni kizazi cha joka kuu jekundu, na ni uzao wa Moabu; kwa ujumla, wale wote walio wa mwili na damu ni viumbe vya Mungu na waliumbwa na Muumbaji. Wewe ni kiumbe wa Mungu, hupaswi kuwa na chaguo lolote, na huu ndio wajibu wako. Leo kazi ya Mungu imeelekezwa katika ulimwengu mzima. Bila kujali wewe ni uzao wa nani, zaidi ya yote, nyinyi ni uzao wa Moabu—ni sehemu ya viumbe wa Mungu, ni vile tu nyinyi mnathamini ya chini. Kwa kuwa, leo, kazi ya Mungu inafanywa miongoni mwa viumbe wote, na imelenga ulimwengu mzima, Muumbaji yupo huru kuchagua watu, masuala, au vitu vyovyote ili viweze kufanya kazi Yake. Hajali wewe ni uzao wa nani; ili mradi tu wewe ni mmoja wa viumbe wake, na ili mradi una manufaa katika kazi Yake—kazi ya kushinda na ushuhuda—ataifanya kazi yake ndani yako bila haya yoyote. Hii inaharibu kabisa dhana za watu ya kitamaduni, ambayo ni kwamba Mungu kamwe hafanyi kazi miongoni mwa Wamataifa, hususan kwa wale ambao wamelaaniwa na ambao ni duni; maana wale ambao wamelaaniwa, uzao wao nao utaendelea kulaaniwa milele, hawatakuwa na nafasi ya wokovu; Mungu hawezi kushuka na kufanya kazi katika nchi ya Wamataifa, na hatakanyaga mguu wake katika nchi yenye uchafu, maana Yeye ni mtakatifu. Elewa kwamba Mungu ni Mungu wa viumbe vyote, ni mtawala wa mbingu na nchi, na vitu vyote, na si Mungu wa watu wa Israeli pekee. Hivyo, kazi hii katika nchi ya China ni ya umuhimu mkubwa, na unadhani haitaenea katika mataifa yote? Ushuhuda mkubwa wa wakati ujao hautaishia China tu; ikiwa Mungu angewashinda nyinyi tu, je, mapepo wangeshawishika? Hawaelewi maana ya kushindwa, au nguvu kubwa ya Mungu, na ni pale tu ambapo wateuliwa wa Mungu katika nchi yote watakapoona matokeo ya mwisho ya kazi hii ndipo viumbe wote watakuwa wameshindwa. Hakuna ambao wapo nyuma sana au waovu sana kuliko uzao wa Moabu. Iwapo tu watu hawa wataweza kushindwa—wale ambao ni waovu sana, ambao hawakumtambua Mungu au kuamini kwamba kuna Mungu wameshindwa, na kumtambua Mungu katika vinywa vyao, wakimtukuza, na wanaweza kumpenda—ndipo huu utakuwa ushuhuda wa kushindwa. Ingawa nyinyi sio Petro, mnaishi kwa kudhihirisha mfano wa Petro, mnaweza kuwa na ushuhuda wa Petro, na ushuhuda wa Ayubu, na huu ni ushuhuda mkubwa sana. Hatimaye utasema: Sisi sio Waisraeli, bali ni uzao wa Moabu uliotelekezwa, sisi sio Petro, ambaye hatuwezi kuwa na tabia yake, wala sisi sio Ayubu, na hata hatuwezi kujilinganisha na azma ya Paulo ya kuteseka kwa ajili ya Mungu na kujitoa kikamilifu kwa Mungu, na sisi tupo nyuma sana, na hivyo hatufuzu kufurahia baraka za Mungu. Mungu bado ametuinua leo; hivyo tunapaswa kumridhisha Mungu, na ingawa tuna upungufu wa tabia au sifa, tupo radhi kumridhisha Mungu—tuna azma hii. Sisi ni uzao wa Moabu, na tulilaaniwa. Hii ilitangazwa na Mungu, na wala hatuwezi kuibadilisha, lakini kuishi kwetu kwa kudhihirisha na maarifa yetu yanaweza kubadilika, na tumeazimia kumridhisha Mungu. Utakapokuwa na azma hii, itathibitisha kwamba umeshuhudia kuwa umeshindwa.
kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni