6/02/2019

Wimbo wa Kuabudu 251. Maana ya Kweli ya Maneno ya Mungu Haijawahi Kueleweka

Wimbo wa Kuabudu 251. Maana ya Kweli ya Maneno ya Mungu Haijawahi Kueleweka

I
Wanadamu hawajui jinsi ya kufurahia
baraka walizopangiwa mikononi mwa Mungu,
maana hawawezi tofautisha mateso kutoka baraka.
Hivyo si wakweli katika kumtaka Mungu.
Kama kesho isipofika,
ni nani kati yenu, akisimama mbele za Mungu,
angekuwa mweupe kama theluji inayoendeshwa,
kama kito safi bila doa lolote.
Hakika upendo wako kwa Mungu hauwezi
kubadilishwa na chakula kitamu
au kubadilishwa na nguo za kifahari
au ofisi kubwa ya malipo mazuri?
Inaweza kubadilishwa na upendo wa wengine
au kuachwa sababu ya majaribu?
Hakika dhiki haitasababisha
malalamiko dhidi ya mipango ya Mungu?
II
Hakuna mwanadamu kweliameelewa
upanga ulio ndani ya kinywa cha Mungu.
Anajua maana tu ya juu,
maana ya ndani hawezi kuielewa.
Kama wanadamu kweli wangeaona
ukali halisi wa upanga wa Mungu,
Wangekimbia kujificha kama panya,
wakikimbia kwenye mashimo yao.
Wamekufa ganzi sana wasijue ukweli wa maneno ya Mungu,
hawana ufahamu wa nguvu yake,
ni kiasi gani upotovu wao unahukumiwa,
au kiasi gani asili yao inafunuliwa.
Kulingana na mawazo yasiyo kamili kuhusu maneno ya Mungu,
wengi wana mtazamo ulio vuguvugu.
kutoka katika "Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I" katika Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni