6/03/2019

Wimbo wa Kuabudu 252. Maneno ya Mungu ni Njia Ambayo Mwanadamu Anapaswa Kufuata

Wimbo wa Kuabudu 252. Maneno ya Mungu ni Njia Ambayo Mwanadamu Anapaswa Kufuata

I
Katika kila enzi, Mungu anapofanya kazi Yake duniani,
kila mara Yeye hutoa maneno juu ya wanadamu, Huwaambia ukweli fulani.
Ukweli huu hutumika kama njia ambayo mwanadamu anapaswa kuzingatia,
njia ambayo mwanadamu anapaswa kufuata
Ni njia inayomwelekeza mwanadamu kumcha Mungu na kuepuka maovu,
na kitu katika maisha yao, na katika safari ya maisha
ambayo wanapaswa kutenda, wanapaswa kuzingatia.
Hizi ndizo sababu ambazo Mungu hutoa maneno Yake juu yao.
II
Maneno haya yanatoka kwa Mungu, yanatoka kwa Mungu Mwenyewe, hivyo wanadamu wanapaswa kuzingatia.
Wakifanya hivyo, watapokea uzima;
wanadamu wasipofuata, au kuyatenda,
wasipoishi kwa kudhihirisha maneno haya ya Mungu katika maisha yao,
basi hawatendi ukweli.
Kutotenda ukweli kunamaanisha ya kuwa hawamwogopi Mungu na kuepuka maovu,
basi hawawezi kumridhisha Mungu.
Kutomridhisha Mungu kunamaanisha kutopokea sifa za Mungu,
basi mtu kama huyo hatakuwa na matokeo.
kutoka katika "Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake" katika Neno Laonekana katika Mwili
Sikiliza zaidi: Msifuni Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni