Umeme wa Mashariki | "Kuona Ni Kuamini" Haipaswi Kuaminiwa
Xiaowen Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Awali, nilipokuwa nikisikia watu wakitoa maoni juu ya kitu fulani, mara nyingi wangesema "kuona ni kuamini." Muda ulivyoendelea kupita, pia nilichukua huu kama msingi wa kuangalia mambo, na ilikuwa vivyo hivyo kuhusu maneno ya Mungu. Matokeo yake ni kwamba niliishia kutoweza kuamini maneno mengi ya Mungu ambayo hayakuwa yametimizwa. Kama wakati wangu uliotumiwa kumwamini Mungu ulipoongezeka, niliona maneno ya Mungu kwa viwango tofauti vya kutimizwa , nikaona ukweli wa mafanikio ya maneno ya Mungu na sikuwa tena na shaka juu ya chochote ambacho Mungu alisema.
Nilidhani hii ilikuwa mimi kuwa na ufahamu kiasi wa uaminifu wa Mungu, na kwamba niliweza kuamini kwamba kila kitu ambacho Mungu alisema kilikuwa halisi.
Lakini siku moja, nilipoyasoma maneno haya yaliyotamkwa na Mungu, "bila wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi Mungu Angekuwa Ashawaangamiza wanadamu wote kuzimu kitambo sana; bila kuwepo kwa mwili huu," tena singeweza kuliamini wazo hilo. Niliwaza, kama lingekuwa limesema "bila ya wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi binadamu wote waovu lazima hatimaye waangamizwe," basi ningeweza kuliamini kabisa, kwa sababu nilijua jinsi Mungu mwenye mwili alivyo muhimu sana kwetu. Lakini kusema kwamba bila ya wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi Mungu angekuwa amewaangamiza wanadamu wote kuzimuni zamani sana, nilifikiri kwamba hii ilikuwa ni tafsiri tu. Wakati nilipotafakari hili, nilihisi kuwa na wasiwasi sana. Ilinibidi kuja mbele ya Mungu kutafuta msaada na uongozi: Ee Mungu! Sitaki kuwa na mtazamo huu kwa maneno Yako na nachukia kuwa mimi ni mjanja sana. Nimekufuata kwa muda mrefu sana na nimeona ukweli mwingi wa kutimizwa kwa maneno Yako, kwa hiyo nawezaje bado kuwa nikifikiri kwa njia hii? Ee Mungu! Natamani kuamini kila neno Unalolisema na kuwa na imani ya kweli katika maneno Yako. Natamani kuwa Wewe uniongoze katika uhalisi huu!
Baadaye, nilisoma ushirika kutoka hayo ya juu unaosema: "Mtu lazima atambue kwamba kila neno alisemalo Mungu litatimizwa na kufanikishwa, lakini mwanadamu hawezi kuyatambua au kuyaona yote. Kwa sababu kutimizwa kwa maneno ya Mungu bila shaka hakuwezi kufanana na kile ambacho mtu hufikiria kabisa na wakati mwingine yatafichwa na sura nyingi za nje, na mtu hawezi kuyatambua kwa urahisi; ni Mungu peke yake anayejua jinsi maneno ya Mungu yatakavyotimizwa. Kuna baadhi ya mambo ambayo kwayo utimizwaji wa maneno ya Mungu unaweza kuonekana kwa dhahiri na wanadamu, na baadhi ambayo kwayo si rahisi kuyaona kwa dhahiri, kwa hiyo wanadamu hawapaswi kuweka msingi wa maamuzi yao kwa kama maneno ya Mungu yametimizwa kwa mawazo yao wenyewe au la. Hata wale ambao kwa ulinganishi wana ufahamu bora wa ukweli hawawezi kuona dhahiri kabisa jinsi kila neno la Mungu hutimizwa. Mambo ambayo kwayo mtu anaweza kuona kwa dhahiri utimizwaji wa maneno ya Mungu yana mipaka kwa sababu mtu hawezi kuelewa hekima ya Mungu asilani. Jinsi neno lolote la Mungu hutimizwa ni juu Yake kabisa kufafanua na yote yana hekima ya Mungu—kwa hiyo mtu anawezaje kulielewa?" ("Mabadiliko ya Msingi katika Mtazamo Ni Ishara ya Kuelewa Ukweli Kwa Dhati" katika Kumbukumbu za Ushirika na Mipango ya Kazi ya Kanisa I). Kwa kusoma kifungu hicho, kwa ghafla nilifikiria Yona. Uovu wa watu wa Ninawi ulimfika Yehova, na Mungu alimtuma Yona kwenda Ninawi kuwahubiria "Baada ya siku arobaini mji wa Ninawi utaangamizwa" (Yona 3: 4). Lakini Yona hakuwa tayari kufanya kama Bwana alivyotaka kwa sababu alijua kwamba Yehova Mungu alikuwa na neema na huruma, alikuwa na upendo mwingi na hakukasirika kwa urahisi. Yona aliogopa kwamba, kama angeenda na kutangaza kama Bwana alivyotaka, basi baada ya siku 40 kama Mungu hangeleta maafa kwa watu wa Ninawi, wangesema kuwa alikuwa mwongo na mdanganyifu. Miaka elfu kadhaa baadaye, nilikuwa naupitia mchakato huu wote ambao unaweza kuonekana umeandikwa katika Biblia. Nilijua kwa dhahiri kwamba, wakati huo, kwa kweli Mungu alitaka hasa kuuangamiza mji wa Ninawi, lakini kwa sababu ya toba yao hakufanya hivyo. Lakini kama ningekuwa mtu aliyeishi katika enzi ya Yona, ambaye hakuwa na ufahamu wa kile Yona alikuwa amepitia na yote niliyoyaona ni kwamba yote yalikuwa sawa mjini Ninawi, ningefikiria basi kuwa Yona alikuwa muongo na mdanganyifu? Bila shaka ningefikiria hivyo.
Ni hapo tu nilipoelewa kuwa kuyapima mambo kwa msingi wa ukweli unaoonekana kutoka nje ni kwa upande mmoja mno, sahili mno. Hakufikirii ukweli ukiwa mzima, sio hali halisi ya mambo na si sahihi hata kidogo. Hii ni kwa sababu vitu vinavyoonekana kwa macho ya mwanadamu ni vichache sana, vyenye mipaka mno na ni vya juujuu mno. Ni kuona tu mambo kwa mujibu wa maneno ya Mungu ndiko sahihi zaidi, kupana sana, na hufichua hali halisi. Kama vile tu wakati Yehova alitaka kuuangamiza mji wa Ninawi. Kuangalia ukweli ambao watu waliweza kuuona, wakati wote kutoka kabla ya Yona kusema maneno hayo mpaka baadaye, yote yalikuwa shwari katika mji huo, bila dalili kwamba Yehova alitarajia kuuangamiza mji huu. Hali ya kweli, hata hivyo, ilikuwa kwamba, kwa tabia ya haki ya Mungu, watu wa mji huo walikuwa wapotovu sana kiasi kwamba Hakuwa na budi kuuangamiza. Lakini Mungu alionyesha rehema kwa wanadamu na aliwapenda, na hivyo akamtuma Yona kuwaambia watubu. Baadaye, Mungu aliona kwamba walitubu kweli na kwa hiyo, kwa moyo wa huruma, Hakushusha maafa ili kuwaangamiza. Kama hawakuwa wametubu, Mungu angefanikisha kile Alichokuwa amekisema: "Baada ya siku arobaini mji wa Ninawi utaangamizwa." Hali halisi wakati huo ilijitokeza kwa njia hii, lakini haikuwezekana kwa watu waliohusika kuitambua au kuiona yote. Hivyo ni kusema, kila kitu ambacho Mungu anasema kitatimizwa na kufanikishwa—hili ni la uhakika. Hii ni kwa sababu mtu hawezi asilani kufahamu hekima ya Mungu, na jinsi neno lolote la Mungu hutimizwa ni juu ya Mungu kabisa kufafanua na yote ina hekima ya Mungu, ni mwanadamu tu ambaye hawezi kulielewa, sembuse kulipenya kabisa.
Ninamshukuru Mungu kwa kutumia jambo hili kunipatia nuru, kunifanya nielewe kwamba kirai "kuona ni kuamini" ambacho mara nyingi watu hunena si sahihi, na kwamba kupima maneno ya Mungu kulingana na maoni haya ni makosa kabisa. Baada ya kufika kwa utambuzi huu, kisha nilisoma tena maneno haya ambayo Mungu alikuwa ameyanena, "bila wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi Mungu Angekuwa Ashawaangamiza wanadamu wote kuzimu kitambo sana; bila kuwepo kwa mwili huu," na ningeweza kuyaamini kutoka moyoni mwangu na kuyakubali kwa njia sahihi. Kutokana na upotovu wetu na haki ya Mungu, tunapaswa kuwa tumeangamizwa zamani sana, lakini tu kwa sababu Mungu alituonyesha rehema na kurudi tena kama mtu katika mwili kutuokoa, tunaweza kuishi mbele ya Mungu leo. Ni sasa tu ninapofahamu wazi kwamba kila moja ya maneno ya Mungu yanafaa kuaminiwa, na kutoka moyoni mwangu ninahisi kwamba Mungu ni mwenye haki sana na mwenye upendo sana kwa mwanadamu.
Ninashukuru kunurishwa kwa Mungu ambako kulinifanya nielewe kipengele hiki cha kweli, na ambako kumegeuza maoni yangu ya awali ya makosa. Kuanzia sasa na kwendelea, kama ni juu ya jinsi ninavyoona watu au jinsi ninavyoona vitu, daima nitafanya hivyo kwa mujibu wa maneno ya Mungu, kwa sababu maneno ya Mungu ni sahihi zaidi. Bali na maneno ya Mungu, maoni yoyote kama "kuona ni kuamini" ambayo watu huona kama ni sahihi, bila kujali kama yametendwa na kupimwa au yana historia ndefu, bado si sahihi. Maneno ya Mungu ndicho kiwango cha pekee ambacho mimi huangalia au kupimia vitu vyote.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni