Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Haki-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Haki-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

7/25/2018

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Nne

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Nne


Ili kuwazuia watu wote kutiwa kiburi na kujisahau baada ya mabadiliko yao kutoka kwa ubaya hadi kwa uzuri, katika fungu la maneno la mwisho la matamshi ya Mungu, mara tu Mungu akishazungumza kuhusu matakwa yake ya juu zaidi kwa watu Wake—mara tu Mungu akishawaambia watu kuhusu mapenzi Yake katika hatua hii ya mpango wa usimamizi Wake—Mungu huwapa nafasi ya kuyatafakari maneno Yake, kuwasaidia kufanya uamuzi wa kuridhisha mapenzi ya Mungu mwishowe.

6/28/2018

Hakuna Utendewaji Maalum katika Kanisa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

   Hakuna Utendewaji Maalum katika Kanisa

Liu Xin     Mji wa Liaocheng, Mkoa wa Shandong
Baada ya kumfuata Mungu kwa miaka hii, nilihisi kuwa nilikuwa nimevumilia mateso na kulipa gharama fulani, kwa hiyo nilianza kuyategemea mapato yangu ya zamani na kuringia ukubwa wangu. Niliwaza: Nimeondoka nyumbani kwa miaka mingi na familia yangu haijaisikia kutoka kwangu kwa muda mrefu. Katika hali hii, kanisa hakika litanitunza. Hata nisipofanya kazi yangu vizuri hawatanituma nyumbani. Si zaidi ya hayo wataniondoa tu na kunielekeza kufanya kazi nyingine. Kutokana na kufikiri kama huko, sikuwa na mzigo wowote kamwe katika kazi yangu. Nilipuuza kila kitu, na hata nikaiona kazi ya injili kama mzigo, daima nikiishi katika matatizo na visingizio.

12/11/2017

Sura ya 13. Maana ya Utendaji wa Watu Kuamua Matokeo Yao

1. Hakuna Ambaye Angeokolewa iwapo Mungu Angeangalia Tu Maonyesho ya Asili ya Watu

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa sasa, utendaji wa watu unaamua matokeo yao, lakini huu utendaji ni upi? Je, unaujua? Nyinyi mnaweza kufikiri kwamba hili linarejelea tabia ya watu iliyopotoka ikijionyesha kazini mwao, lakini halimaanishi lile. Utendaji huu unanena kuhusu ikiwa unaweza kuweka ukweli kwenye vitendo au la na ikiwa unaweza kusalia mwaminifu na kujizatiti unapotenda wajibu wako au la, na vilevile mtazamo wako wa kumwamini Mungu, msimamo wako kwa Mungu, uamuzi wako wa kuteseka kwa ajili ya ugumu, mtazamo wako kwa kukubali hukumu na kupogolewa, kiwango chako cha mabadiliko na idadi ya dhambi kubwa.