Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Sita
Mwenyezi Mungu alisema, Wakati ule ambao mtu anazaliwa, nafsi ya mtu iliyo pweke inaanza kupitia maisha hapa duniani, inapitia mamlaka ya Muumba ambayo Muumba ameipangilia. Ni wazi kwamba, kwa mtu husika, ile nafsi, hii ni fursa nzuri kabisa ya kupata maarifa kuhusu ukuu wa Muumba, kujua mamlaka Yake na kuyapitia binafsi. Watu wanaishi maisha yao kulingana na sheria za hatima zilizowekwa wazi kwao na Muumba, na kwa mtu yeyote mwenye akili razini aliye na dhamiri, kuelewa ukuu wa Muumba na kutambua mamlaka yake kwenye mkondo wa miongo yao mbalimbali hapa nchini si jambo gumu kufanya.
Kwa hivyo inafaa kuwa rahisi sana kwa kila mtu kutambua, kupitia kwa yale ambayo yeye mwenyewe amepitia maishani kwa kipindi cha miongo mbalimbali, kwamba hatima zote za binadamu zimeamuliwa kabla, na kung’amua au kujumlisha ni nini maana ya kuishi. Wakati uo huo ambao mtu anakumbatia mafunzo haya ya maisha, mtu ataelewa kwa utaratibu ni wapi maisha yanatokea, kunga’mua hasa ni nini ambacho moyo unahitaji kwa kweli, nini kitaongoza mtu kwenye njia ya kweli ya maisha, kazi maalum na shabaha ya maisha ya binadamu inafaa kuwa nini; na mtu ataanza kutambua kwa utaratibu kwamba kama mtu hataabudu Muumba, kama mtu hataingia kwenye utawala Wake, basi mtu anakabiliana na kifo—wakati nafsi iko karibu kukabiliana na Muumba kwa mara nyingine—moyo wa mtu utajazwa hofu na ugumu usio na mipaka. Kama mtu amekuwepo ulimwenguni kwa miongo kadhaa ilhali hajajua ni wapi maisha ya binadamu hutoka, angali hajatambua ni kwenye viganja vya mikono ya nani hatima ya binadamu huwa, basi si ajabu hataweza kukabiliana na kifo kwa utulivu. Mtu aliyepata maarifa ya ukuu wa Muumba baada ya kupitia miongo kadhaa ya maisha, ni mtu aliye na shukrani sahihi ya maana na thamani ya maisha; mtu aliye na kina cha maarifa kuhusu kusudi la maisha, aliye na hali halisi aliyopitia na anaelewa ukuu wa Muumba; na hata zaidi, mtu anayeweza kunyenyekea mbele ya mamlaka ya Muumba. Mtu kama huyo anaelewa maana ya uumbaji wa Mungu wa mwanadamu, anaelewa kwamba binadamu anafaa kumwabudu Muumba, kwamba kila kitu anachomiliki binadamu kinatoka kwa Muumba na kitarudi kwake siku fulani isiyo mbali sana kwenye siku za usoni; mtu kama huyo anaelewa kwamba Muumba hupangilia kuzaliwa kwa binadamu na ana ukuu juu ya kifo cha binadamu, na kwamba maisha na kifo vyote vimeamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba. Kwa hiyo, wakati mtu anapong’amua mambo haya, mtu ataanza kuweza kukabiliana na kifo kwa utulivu na kwa kawaida, kuweka pembeni mali yake yote ya dunia kwa utulivu, kukubali na kunyenyekea kwa furaha kwa yote yatakayofuata, na kukaribisha awamu ya mwisho ya maisha iliyopangiliwa na Muumba badala ya kutishika vivyo hivyo tu na kung’ang’ana dhidi ya kifo. Ikiwa mtu anayaona maisha kama fursa ya kupitia ukuu wa Muumba na kujua mamlaka yake, ikiwa mtu anayaona maisha yake kama fursa nadra ya kutekeleza wajibu wake akiwa binadamu aliyeumbwa na kutimiza kazi yake maalum, basi mtu atakuwa ana mtazamo sahihi wa maisha, ataishi maisha yaliyobarikiwa na yanayoongozwa na Muumba, atatembea kwenye nuru ya Muumba, atajua ukuu wa Muumba, atakuwa katika utawala Wake, atakuwa shahidi wa matendo Yake ya kimiujiza na mamlaka Yake. Ni wazi kwamba, mtu kama huyo atahitajika kupendwa na kukubaliwa na Muumba, na mtu kama huyo ndiye anaweza kushikilia mtazamo mtulivu mbele ya kifo, na anayeweza kukaribisha awamu hii ya mwisho kwa furaha. Bila shaka Ayubu alikuwa na mtazamo kama huu kwa kifo; alikuwa katika nafasi ya kukubali kwa furaha awamu ya mwisho ya maisha, na baada ya kuhitimisha safari yake ya maisha vizuri, baada ya kukamilisha kazi yake maalum alirudi upande wa Muumba.
Tazama Video: Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Saba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni