Matamshi ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)" Sehemu ya Kwanza
Mwenyezi Mungu alisema, Mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Ndiyo maonyesho ya sifa ya, na hali halisi maalum ya, utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Hakuna kiumbe ambacho kiliumbwa wala kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki maonyesho ya sifa kama hizi na hali halisi maalum; Muumba tu ndiye anayemiliki aina hii ya mamlaka. Hivyo ni kusema kwamba, ni Muumba tu—Mungu Yule wa kipekee—ambaye anaonyeshwa kwa njia hii na ndiye aliye na hali halisi hii.
Kwa nini tuzungumzie mamlaka ya Mungu? Mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanatofautiana vipi na mamlaka yaliyomo kwenye akili ya binadamu? Ni nini maalum sana kuyahusu? Na kunao umuhimu gani haswa kuyazungumzia hapa? Kila mmoja wenu lazima aweze kutilia maanani kwa umakinifu suala hili. Kwa watu wengi zaidi, “Mamlaka ya Mungu” ni fikira isiyoeleweka, ile ambayo ni ngumu sana kupata kuielewa, na mazungumzo yoyote kuihusu huenda yasizae matunda mazuri. Kwa hivyo lazima kutakuwepo na pengo kati ya maarifa ya mamlaka ya Mungu ambayo binadamu anaweza kumiliki, na hali halisi ya mamlaka ya Mungu. Ili kuliziba pengo hili, mtu lazima kwa utaratibu aweze kuelewa mamlaka ya Mungu kwa njia ya watu halisi-maishani, matukio, vitu au mambo muhimu yanayopatikana katika uwezo wa binadamu, na ambayo binadamu wanaweza kuyaelewa. Ingawaje kauli hii “Mamlaka ya Mungu” inaweza kuonekana kama isiyoeleweka, mamlaka ya Mungu kwa kweli si ya dhahania kamwe. Yeye yupo na binadamu kila dakika ya maisha yake, akimwongoza kila siku. Kwa hivyo, katika maisha ya kila siku ya kila mtu ataweza haswa kuona na kupitia dhana halisi ya mamlaka ya Mungu. Uhalisi huu ni ithibati tosha kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo, na unakuruhusu kabisa kutambua na kuelewa hoja hii kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya.
Tazama Zaidi: Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Saba
Tufuate: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni