1/12/2019

Wimbo wa Maneno ya Mungu | Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee

Wimbo wa Maneno ya Mungu Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee

I
Mungu huonyesha tabia Yake ya haki
kupitia mbinu na kanuni za kipekee,
haidhibitiwi na watu, matukio au vitu.
Na hakuna awezaye kubadili dhana au mawazo Yake,
au kumshawishi Ajaribu njia tofauti.
Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Tabia Yake ya haki!
II
Mungu huhuku matendo na mawazo yote
ya viumbe kwa tabia Yake ya haki.
Na kulingana na hili, Hutoa ghadhabu au kupeana rehema.
Na hakuna awezaye kubadili rehema au ghadhabu Yake.
Na ni kiini Chake tu kiwezacho kuamua njia hii
Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Tabia Yake ya haki!
III
Tabia ya haki ya Mungu, takatifu na ya kipekee;
hakuna awezaye kiuka au kushuku hili.
Hakuna awezaye kuimiliki, kiumbwacho au kisichoumbwa.
Ghadhabu ya Mungu ni takatifu; haiwezi kukosewa.
Rehema Yake pia yabeba asili hii
Hii ni asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Tabia Yake ya haki!
IV
Hakuna mbadala wa Mungu katika Matendo Yake,
kiumbwacho au kisichoumbwa.
Wala hawezi kuuharibu Sodoma au
kuuokoa Ninawi kama alivyofanya Mungu.
Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Tabia Yake ya haki! Tabia Yake ya haki!

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni