Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu alisema, Mtu hawezi kuchagua watu au mambo ambayo yataweza kumhimiza na kumwathiri anapokua. Mtu hawezi kuchagua ni maarifa au mbinu gani atapata, ni mazoea gani ataishia kuwa nayo. Mtu hana kauli kuhusiana na wazazi na watu wake wa ukoo, aina ya mazingira ambayo atakulia ndani; mahusiano yake na watu, matukio, na mambo yaliyo katika mazingira yake na namna yanavyoathiri maendeleo yake, vyote ni zaidi ya udhibiti wake.
Ni nani anayeamua mambo haya, basi? Ni nani anayeyapangilia? Kwa sababu watu hawana chaguo katika suala hili, kwa vile hawawezi kuamua mambo haya wao wenyewe, na kwa sababu bila shaka hayajipangi yenyewe kwa kawaida, ni wazi kabisa kwamba kuundwa kwa haya yote kunategemea mikono ya Muumba. Kama vile tu Muumba anavyopanga hali fulani za kuzaliwa kwa kila mtu, Yeye hupangilia pia hali mahususi ambazo mtu hukulia, bila shaka. Kama kuzaliwa kwa mtu kutaleta mabadiliko kwa watu, kwa matukio, na mambo yanayomzunguka yeye, basi kukua na maendeleo ya mtu huyo vyote vitaweza kuwaathiri vilevile. Kwa mfano, baadhi ya watu wanazaliwa katika familia fukara, lakini wanalelewa wakiwa wemezungukwa na utajiri; wengine wanazaliwa katika familia tajiri lakini husababisha utajiri wa familia zao kupungua, kiasi cha kwamba wanalelewa katika mazingira ya kimaskini. Hakuna kuzaliwa kwa yeyote kunatawaliwa na kanuni isiyobadilika, na hakuna anayelelewa katika hali zisizozuilika, na zisizobadilika. Haya si mambo ambayo binadamu anaweza kufikiria au kudhibiti; mambo haya yote ni mazao ya hatima ya mtu, na yanaamuliwa na hatima ya mtu. Bila shaka, kimsingi ni kwamba yote haya yaliamuliwa kabla katika hatima ya mtu na Muumba, yanaamuliwa na ukuu wa Muumba juu ya, na mipango Yake ya, hatima ya mtu huyu.
Video Husika: Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Sita
Kujua zaidi: Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki, Utongoaji wa Neno la Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni