2. Kupata Mwili Ni Nini? Ni Nini Kiini cha Kupata Mwili?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu” (Yohana1:1).
“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).
“Mimi ndiye njia, ukweli na uhai” (Yohana 14:6).
“Yesu akasema kwake, nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua, Filipo? Yeye ambaye ameniona amemwona Baba; na unasemaje basi, Tuonyeshe Baba? Huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi? Maneno ninenayo kwenu sineni juu yangu, ila Baba aishiye ndani yangu, anazifanya kazi hizo. Niamini kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi, la sivyo niamini kwa ajili ya kazi hizo” (Yohana 14:9-11).
“Mimi na yeye Baba ang utu mmoja” (Yohana10:30).
Maneno Husika ya Mungu:
Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili, angalau, ni lazima liwe ukweli. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu.
kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kupata mwili kunamaanisha kwamba Roho wa Mungu Anakuwa Mwili, yaani, Mungu Anakuwa mwili; kazi Anayoifanya katika mwili ni kazi ya Roho, inayothibitika katika mwili, na kuonyeshwa kwa mwili. Hakuna mwingine ila tu mwili wa Mungu Anayeweza kutimiza huduma ya Mungu mwenye mwili; yaani, mwili wa Mungu kuwa mwili pekee, ubinadamu huu wa kawaida—na hakuna mwingine yeyote—anayeweza kuonyesha kazi ya uungu.
kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kristo mwenye ubinadamu wa kawaida ni mwili ambao kwao Roho Hupatikana, Akiwa na ubinadamu wa kawaida, ufahamu wa kawaida, na fikira za wanadamu. “Kupatikana” kunamaanisha Mungu kuwa mwanadamu, Roho kuwa mwili; kuiweka wazi, ni wakati ambapo Mungu Mwenyewe Anaishi katika mwili wenye ubinadamu wa kawaida, na kupitia kwenye huo mwili, Anaonyesha kazi yake ya uungu—hii ndiyo maana ya kupatikana, au kupata mwili.
kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, Kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo wa kweli sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha.
kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa sababu ni mwanadamu mwenye kiini cha Mungu, Yuko juu ya wanadamu wote walioumbwa, juu ya mwanadamu yeyote anayeweza kutekeleza kazi ya Mungu. Kwa hivyo, miongoni mwa wale wote walio na umbo la binadamu kama Lake, miongoni mwa wale wote walio na ubinadamu, Yeye pekee ndiye Mungu mwenye mwili Mwenyewe—wengine wote ni wanadamu walioumbwa. Japokuwa wote wana ubinadamu, wanadamu walioumbwa si chochote zaidi ya wanadamu, ilhali Mungu mwenye mwili ni tofauti: katika mwili Wake, si tu kwamba ana ubinadamu ila pia muhimu zaidi Ana uungu. Ubinadamu Wake waweza kuonekana katika mwonekano wa nje wa Mwili Wake na katika maisha Yake ya kila siku; ila uungu Wake ni vigumu kuonekana. Kwa kuwa uungu Wake huonyeshwa pale tu Anapokuwa na ubinadamu, na si wa kimuujiza kama watu wanavyoukisia kuwa, ni vigumu sana kwa watu kuuona. Hata leo hii ni vigumu sana kwa watu kuelewa kiini cha kweli cha Mungu mwenye mwili. Kwa kweli, hata baada ya Mimi kulizungumzia kwa mapana, Natarajia bado liwe fumbo kwa wengi wenu. Suala hili ni rahisi sana: kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili, kiini Chake ni muungano wa ubinadamu na uungu. Muungano huu unaitwa Mungu Mwenyewe, Mungu Mwenyewe duniani.
kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. Maisha Yake ya kimwili na kazi vinaweza kugawanywa katika hatua mbili. Kwanza ni maisha Anayoishi kabla ya kuanza kutekeleza huduma Yake. Anaishi katika familia ya kawaida ya binadamu, katika ubinadamu wa kawaida kabisa, Akifuata maadili na sheria za maisha ya wanadamu, Akiwa na mahitaji ya kawaida ya binadamu (chakula, nguo, makazi, na usingizi), na udhaifu wa kawaida wa binadamu na hisia za kawaida za binadamu. Kwa maneno mengine, katika hatua hii ya kwanza Anaishi maisha yasiyo na uungu, ubinadamu wa kawaida kabisa, Akijishughulisha na shughuli zote za wanadamu. Hatua ya pili ni ya maisha Anayoishi baada ya kuanza kutekeleza huduma Yake. Bado Yumo katika ubinadamu wa kawaida Akiwa na umbo la nje la binadamu bila kuonyesha ishara isiyo ya kawaida kwa nje. Lakini kimsingi Anaishi kwa ajili ya huduma Yake, na wakati huu ubinadamu Wake wa kawaida upo kikamilifu kuhudumia kazi ya kawaida ya uungu Wake; kwani wakati huo, ubinadamu Wake wa kawaida umekomaa kiasi cha kuweza kutekeleza huduma Yake. Kwa hivyo hatua ya pili ya maisha Yake ni ya kutekeleza huduma Yake katika ubinadamu Wake wa kawaida, ni maisha ya ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Sababu ya kuishi katika maisha ya kawaida kabisa ya ubinadamu katika hatua ya kwanza ya maisha Yake ni kwamba ubinadamu Wake bado ulikuwa haujalingana na ukamilifu wa kazi ya uungu, bado haujakomaa; ni baada tu ya kukomaa kwa ubinadamu Wake na kuwa na uwezo wa kustahimili huduma Yake, ndipo Anaweza kuanza kutekeleza huduma Yake. Kwa kuwa Yeye, kama mwili, Anahitaji kukua na kukomaa, hatua ya kwanza ya maisha Yake ni ile ya ubinadamu wa kawaida, ilhali katika hatua ya pili, kwa kuwa ubinadamu Wake una uwezo wa kuanza kazi Yake na kutekeleza huduma Yake, maisha ambayo Mungu mwenye mwili Anaishi katika kipindi cha huduma Yake ni ya ubinadamu na ya uungu kamili. Iwapo Mungu mwenye mwili Angeanza huduma Yake kwa dhati tangu kuzaliwa kwake, na kufanya ishara na maajabu ya mwujiza, basi Asingekuwa na kiini cha kimwili. Kwa hivyo, ubinadamu Wake upo kwa sababu ya kiini chake cha Kimwili; hakuwezi kuwepo na mwili bila ubinadamu, na mtu bila ubinadamu si mwanadamu. Kwa njia hii, ubinadamu wa mwili wa Mungu ni sifa ya ndani ya mwili wa Mungu. Kusema kwamba “Mungu Anapokuwa mwili Anakuwa na uungu kamili, kwa vyovyote vile si ubinadamu,” ni kufuru, kwa sababu huu ni msimamo usioweza kuchukuliwa, msimamo unaokinzana na kanuni ya Yesu kuupata mwili. Hata baada ya kuanza kutekeleza huduma Yake, uungu Wake bado unaishi ndani ya umbo la nje la binadamu Anapofanya kazi Yake; ni kwamba tu wakati huo, ubinadamu Wake una kusudi la pekee la kuuwezesha uungu Wake kutekeleza kazi katika mwili wa kawaida. Kwa hivyo wakala wa kazi ni uungu unaosetiriwa katika ubinadamu Wake. Ni uungu na wala si ubinadamu Wake unaofanya kazi, lakini ni uungu uliojificha katika ubinadamu Wake; kimsingi kazi Yake inafanywa na uungu Wake kikamilifu, haifanywi na ubinadamu Wake. Ila mtekelezaji wa kazi ni mwili Wake. Mtu anaweza kusema kuwa Yeye ni mwanadamu na vilevile Mungu, kwani Mungu Anakuwa Mungu Anayeishi katika mwili, mwenye umbo la mwanadamu na kiini cha binadamu lakini pia na kiini cha Mungu.
kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Maisha Aliyoishi Yesu duniani yalikuwa maisha ya kimwili ya kawaida. Aliishi katika ubinadamu wa kawaida wa mwili Wake. Mamlaka Yake—kufanya kazi Yake na kuzungumza neno Lake, au kuwaponya wagonjwa au kufukuza mapepo, kufanya hiyo kazi isiyo ya kawaida—hayakujitokeza, kwa kiasi kikubwa, hadi Alipoanza huduma Yake. Maisha Yake kabla ya umri wa miaka ishirini na tisa, kabla ya Yeye kuanza kutekeleza huduma Yake, yalikuwa uthibitisho tosha kuwa Alikuwa mwili wa kawaida. Kwa sababu ya hili, na kwa kuwa Alikuwa bado Hajaanza kutekeleza huduma Yake, watu hawakuona chochote cha uungu ndani Yake, hawakuona chochote zaidi ya ubinadamu wa kawaida, mwanadamu wa kawaida—kama vile wakati ule baadhi ya watu walimwamini kuwa mwana wa Yosefu. Watu walidhani kuwa Alikuwa mwana wa mwanadamu wa kawaida, hawakuwa na njia ya kugundua kuwa Alikuwa mwili wa Mungu; hata wakati Alipotenda miujiza mingi katika harakati za kutekeleza huduma Yake, watu wengi bado walisema Alikuwa mwana wa Yosefu, kwani Alikuwa Kristo mwenye umbo la nje la ubinadamu wa kawaida. Ubinadamu Wake wa kawaida pamoja na kazi yake vyote vilikuwepo ili kutimiza umuhimu wa kupata mwili kwa mara ya kwanza, kuthibitisha kuwa Mungu Alikuwa Amekuja katika mwili kwa ukamilifu, kuwa mwanadamu wa kawaida kabisa. Kuwa na ubinadamu wa kawaida kabla ya kuanza kazi Yake ulikuwa uthibitisho kuwa Alikuwa mwili wa kawaida; na kwa kuwa Alifanya kazi baadaye lilithibitisha pia kuwa Alikuwa mwili wa kawaida, kwa kuwa Alifanya ishara na miujiza, kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo katika mwili na ubinadamu wa kawaida. Sababu za kufanya miujiza ilikuwa kwamba mwili Wake ulikuwa umebeba mamlaka ya Mungu, ulikuwa mwili ambamo Roho wa Mungu Alikuwa Amesetiriwa. Alikuwa na mamlaka haya kwa sababu ya Roho wa Mungu, na haikumaanishi kuwa Hakuwa Mwili. Kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo ilikuwa kazi Aliyopaswa kutekeleza katika huduma Yake, onyesho la uungu Wake uliojificha ndani ya ubinadamu Wake, na haijalishi ni ishara za aina gani Alionyesha au Alidhihirisha vipi mamlaka Yake, bado Aliishi katika ubinadamu wa kawaida na bado Alikuwa mwili wa kawaida. Aliishi katika mwili wa kawaida mpaka wakati Alipofufuliwa baada ya kufa msalabani. Aliishi katika mwili wa kawaida. Akitoa neema, Akiwaponya wagonjwa, na kufukuza mapepo hayo yote yalikuwa sehemu ya huduma Yake, hiyo yote ilikuwa kazi Aliyotekeleza katika mwili Wake wa kawaida. Kabla ya kwenda msalabani, Hakuuacha mwili Wake wa kawaida, haijalishi Alikuwa Anafanya nini. Alikuwa Mungu Mwenyewe, Akifanya kazi ya Mungu, lakini kwa sababu Alikuwa Mwili wa Mungu, Alikula chakula na kuvaa nguo, Alikuwa na mahitaji ya kawaida ya binadamu, Alikuwa na fikira za kawaida za binadamu na akili za kawaida. Haya yote yalikuwa uthibitisho kwamba Alikuwa mwanadamu wa kawaida, ambayo yalithibitisha kuwa mwili wa Mungu ulikuwa mwili wenye ubinadamu wa kawaida, haukuwa wa rohoni.
kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ubinadamu wa Mungu kuwa mwili huwepo kudumisha kazi ya kawaida ya uungu katika mwili; fikira Zake za kawaida za binadamu zinadumisha ubinadamu Wake wa kawaida na shughuli Zake zote za kimwili. Mtu anaweza kusema kuwa fikira zake za kawaida za binadamu zipo ili kudumisha kazi yote ya Mungu katika mwili. Kama mwili huu usingekuwa na akili ya mwanadamu wa kawaida, basi Mungu Asingefanya kazi katika mwili, na Anachopaswa kufanya kimwili kisingetimilika. Japo Mungu mwenye mwili Ana akili ya mwanadamu wa kawaida, kazi Yake haijatiwa doa na mawazo ya binadamu; Anafanya kazi katika ubinadamu na akili ya kawaida chini ya masharti ya awali kuwa atakuwa na ubinadamu na akili ya kawaida, na si na mawazo ya kawaida ya binadamu. Haijalishi mawazo ya mwili Wake ni bora kiasi gani, kazi Yake haionyeshi alama ya mantiki au kufikiria. Kwa maneno mengine, kazi Yake haiwazwi na akili ya mwili Wake, ila ni onyesho la moja kwa moja la kazi ya uungu katika ubinadamu Wake. Kazi Yake yote ni huduma Anayostahili kutimiza, na haiwazwi hata chembe kwa akili Zake. Kwa mfano, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kusulubishwa hayakuwa mazao ya akili Zake za binadamu, yasingeweza kutimizwa na mwanadamu yeyote mwenye akili za binadamu. Vivyo hivyo, kazi ya ushindi ya leo ni huduma ambayo ni sharti itekelezwe na Mungu mwenye mwili, lakini si kazi ya mapenzi ya mwanadamu, ni kazi ambayo uungu Wake unapaswa kufanya, kazi ambayo hakuna mwanadamu wa mwili anaiweza. Kwa hivyo, Mungu mwenye mwili ni lazima Awe na akili za binadamu, ni lazima Awe na ubinadamu wa kawaida, kwa sababu ni lazima Atekeleze kazi Yake katika ubinadamu akiwa na akili za kawaida. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Mungu mwenye Mwili, kiini chenyewe cha Mungu mwenye mwili.
kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwana wa Adamu mwenye mwili alionyesha uungu wa Mungu kupitia kwa ubinadamu Wake na kuwasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Na kupitia maonyesho ya mapenzi na tabia ya Mungu, Aliwafichulia watu yule Mungu asiyeweza kuonekana au kuguswa katika ulimwengu wa kiroho. Kile watu walichoona kilikuwa Mungu Mwenyewe, anayeshikika na aliye na mwili na mifupa. Hivyo basi Mwana wa Adamu mwenye mwili Alifanya mambo kama vile utambulisho binafsi wa Mungu, hadhi, taswira, tabia, na kile Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kupewa picha ya binadamu. Ingawa sura ya nje ya Mwana wa Adamu ilikuwa na upungufu fulani kuhusiana na taswira ya Mungu, kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho yote hayo yaliweza kwa kikamilifu kuwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu—kulikuwa tu na tofauti fulani katika jinsi ya maonyesho. Bila kujali kama ni ubinadamu wa Mwana wa Mungu au uungu Wake, hatuwezi kukana kwamba Aliwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu mwenyewe. Katika kipindi hiki cha muda, hata hivyo, Mungu alifanya kazi kupitia mwili, Akaongea kutoka kwa mtazamo wa mwili, na kusimama mbele ya mwanadamu kwa utambulisho na hadhi ya Mwana wa Adamu, na hili liliwapa watu fursa ya kukumbana na kupitia maneno na kazi ya kweli ya Mungu miongoni mwa binadamu. Iliweza pia kuwaruhusu watu kuwa na utambuzi wa uungu Wake na ukubwa Wake katikati ya unyenyekevu, vilevile na kupata ufahamu wa mwanzo na ufafanuzi wa mwanzo wa uhalali na uhalisi wa Mungu.
kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ingawa kuonekana kwa Mungu mwenye mwili ni kama mwanadamu, Anajifunza maarifa ya mwanadamu na kuongea lugha ya mwanadamu, na wakati mwingine Anaonyesha hata mawazo Yake kwa jinsi na hisia za mwanadamu, namna Anavyowaona wanadamu, kiini cha vitu, na namna ambavyo watu waliopotoka wanavyomwona mwanadamu na kiini cha vitu kwa hakika si sawa kabisa. Mtazamo Wake na kimo Anachosimamia ni jambo ambalo halifikiwi na mtu aliyepotoka. Hii ni kwa sababu Mungu ni ukweli, mwili Anaouvalia unamiliki pia kiini cha Mungu, na fikira Zake na kile ambacho kinadhihirishwa na ubinadamu Wake pia ni ukweli. … Bila kujali ni vipi ambavyo mwili wa Mungu mwenye mwili ulivyo wa kawaida, ulivyo kama wengine, ulivyo wa chini, au hata namna ambavyo watu wanamdharau Yeye, fikira Zake na mwelekeo Wake kwa wanadamu ni mambo ambayo hakuna binadamu angeweza kufuatisha na wala hakuna binadamu angeweza kuiga. Siku zote Atawaangalia wanadamu kutoka kwa mtazamo wa uungu, kutoka katika kimo cha madaraka Yake kama Muumba. Siku zote Atawaona wanadamu kupitia katika kiini na akili ya Mungu. Hawezi kabisa kuwaona wanadamu kutoka katika kimo cha mtu wa kawaida na kutoka kwa mtazamo wa mtu aliyepotoka. Watu wanapowaangalia wanadamu, wanawaangalia kwa mtazamo wa binadamu, na wanatumia mambo kama vile maarifa ya binadamu na masharti na nadharia za binadamu kama kipimo. Hali hii imo ndani ya mawanda ya kile ambacho watu wanaweza kuona kwa macho yao; ni ndani ya upana ambao watu waliopotoka wanaweza kutimiza. Mungu anapowatazama wanadamu, Anawatazama kwa macho ya kiungu, na Anatumia kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho kama kipimo. Mawanda haya yanajumuisha mambo ambayo watu hawawezi kuona, na hapo ndipo Mungu mwenye mwili na wanadamu waliopotoka walivyo tofauti kabisa. Tofauti hii inaamuliwa na viini tofauti vya wanadamu na vya Mungu na ndivyo vinavyoamua utambulisho na nafasi zao pamoja na mtazamo na kimo ambacho wanaona mambo.
kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe. Kwa hiyo, Mungu mwenye mwili kamwe hangefanya kazi yoyote ambayo inasumbua usimamizi Wake Mwenyewe. Hili ndilo ambalo binadamu wote wanapaswa kuelewa. Kiini cha kazi ya Roho Mtakatifu ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya usimamizi wa Mungu Mwenyewe. Vile vile, kazi ya Kristo ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Kutokana na kwamba Mungu Anapata mwili, Anatambua dutu Yake ndani ya mwili Wake, kama kwamba mwili Wake ni wa kutosha kufanya kazi Yake. Kwa hivyo, kazi zote za Roho wa Mungu zinabadilishwa na kazi ya Kristo wakati wa kupata mwili, na kwenye msingi wa kazi zote wakati wa kupata mwili ni kazi ya Kristo. Haiwezi kuchanganyika na kazi yoyote ile kutoka enzi nyingine yoyote. Na kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili, Yeye Anafanya kazi katika utambulisho wa mwili Wake; kwa kuwa Yeye hukuja katika mwili, kisha Yeye humaliza katika mwili kazi hiyo Anayoazimia kufanya. Iwe ni Roho wa Mungu au ni Kristo, wote ni Mungu Mwenyewe, na Anafanya kazi hiyo Anayoazimia kufanya na hufanya huduma hiyo Anayopaswa kufanya.
Dutu ya Mungu yenyewe hushika na kutumia mamlaka, lakini Yeye Anao uwezo wa kuwasilisha kwa ukamilifu mamlaka ambayo hutoka Kwake. Iwe ni kazi ya Roho au kazi ya mwili, hakuna ambayo itazozana na nyingine. Roho wa Mungu ndiyo mamlaka juu ya viumbe vyote. Mwili na dutu ya Mungu pia inayo mamlaka, bali Mungu katika mwili Anaweza kufanya kazi yote inayotii mapenzi ya Baba wa mbinguni. Hii haiwezi kupatikana au kufanyika na binadamu yeyote. Mungu Mwenyewe ni mamlaka, lakini mwili Wake unaweza kunyenyekea kwa mamlaka Yake. Hii ndiyo maana ya ndani ya maneno: “Kristo hutii mapenzi ya Mungu Baba.” Mungu ni Roho na Anaweza kufanya kazi ya wokovu, kama vile Mungu Anavyoweza kuwa mwanadamu. Hata hivyo, Mungu Mwenyewe Anafanya kazi Yake Mwenyewe; Yeye wala hazuii wala kuathiri, wala kufanya kazi inayozipinganisha pande zote mbili, kwa kuwa kiini cha kazi iliyofanywa na Roho na mwili yote ni sawa. Iwe ni Roho au mwili, vyote hufanya kazi kutimiza nia moja na kusimamia kazi sawa. Ingawa Roho na mwili huwa na sifa mbili tofauti, dutu yao ni sawa; zote zina dutu ya Mungu Mwenyewe, na utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Mungu Mwenyewe hana mambo ya kuasi; dutu Yake ni nzuri. Yeye ni udhihirisho wa uzuri wote na wema, vile vile upendo wote. Hata katika mwili, Mungu hafanyi lolote linalomuasi Mungu Baba. Hata kwa gharama ya kutoa sadaka maisha Yake, Angekuwa kwa ukamilifu tayari na kutofanya uchaguzi mwingine. Mungu hana mambo ya ukamilifu wa kibinafsi na umuhimu wa kibinafsi, au yale wa kujiona na kiburi; Hana mambo yasiyo aminifu. Yote yanayomuasi Mungu yanatoka kwa Shetani; Shetani ni chanzo cha ubaya na uovu wote. Sababu kwamba mwanadamu anayo sifa sawa na ile ya Shetani ni kwa sababu mwanadamu amelaghaiwa na kufinyangwa Shetani. Kristo hajawahi kupotoshwa na Shetani, hivyo Anazo tu tabia za Mungu na hakuna hata moja ya Shetani. Haijalishi ugumu wa kazi, au udhaifu wa mwili, Mungu, wakati Anapoishi katika mwili, kamwe hatafanya kitu chochote kitakachopinga kazi ya Mungu Mwenyewe, wala kuacha mapenzi ya Mungu Baba kwa njia ya uasi. Ni afadhali Ateseke maumivu ya mwili kuliko kwenda kinyume na matakwa ya Mungu Baba; ni kama vile Yesu Alisema katika sala, “Baba, kama inawezekana, kikombe hiki kiniondokee: hata hivyo si kama Mimi Nipendavyo, bali kama Wewe upendavyo.” Wanadamu watachagua, bali Kristo hawezi. Ingawa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe, bado Yeye Anatafuta mapenzi ya Mungu Baba, na Anatimiza kile Alichokabidhiwa na Mungu Baba, kutoka kwa mtazamo wa mwili. Hili ni jambo ambalo haliwezi kupatikana kwa binadamu. Hilo ambalo huja kutoka kwa Shetani haliwezi kuwa na dutu ya Mungu, bali mojawapo ya yale ambayo hukosa kutii na kumpinga Mungu. Haliwezi kumtii Mungu kikamilifu, wala kutii mapenzi ya Mungu kwa hiari. Wanadamu wote isipokuwa Kristo wanaweza kufanya yaliyo ya kumpinga Mungu, na hakuna anayeweza moja kwa moja kufanya kazi aliyoaminiwa na Mungu; hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuzingatia usimamizi wa Mungu kama wajibu wake wenyewe kutekeleza. Kuwasilisha mapenzi ya Mungu Baba ni kiini cha Kristo; uasi dhidi ya Mungu ni tabia ya shetani. Sifa hizo mbili hazipatani, na yeyote aliye na sifa za shetani hawezi kuitwa Kristo. Sababu ambayo binadamu hawezi kufanya kazi ya Mungu kwa niaba Yake ni kwa sababu mwanadamu hana kiini chochote cha Mungu. Binadamu humfanyia Mungu kazi kwa ajili ya maslahi binafsi ya binadamu na ya matarajio Yake ya baadaye, lakini Kristo Anafanya kazi ya kufanya mapenzi ya Mungu Baba.
kutoka katika “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ubinadamu wa Kristo unaongozwa na uungu Wake. Ingawa yuko katika mwili, ubinadamu Wake si kama ule wa binadamu wa mwili kabisa. Anao upekee wa tabia Yake Mwenyewe, na hii pia huongozwa na uungu Wake. Uungu Wake hauna udhaifu; udhaifu wa Kristo unaelezea ule wa ubinadamu Wake. Kwa kiasi fulani, udhaifu huu huzuia uungu Wake, lakini mipaka hiyo ipo tu kati ya wigo fulani na wakati, na sio zisizo na mipaka. Linapokuja suala la muda wa kufanya kazi ya uungu Wake, hufanyika bila kujali ubinadamu Wake. Ubinadamu wa Kristo kabisa huongozwa na uungu Wake. Mbali na maisha ya kawaida ya ubinadamu Wake, matendo mengine yote ya ubinadamu Wake ni ya kushawishiwa, inayoathirika na kuelekezwa na uungu Wake. Ingawa Kristo Anao ubinadamu, haukatizi kazi ya uungu Wake. Hii hasa ni kwa sababu ubinadamu wa Kristo unaongozwa na uungu Wake; ingawa ubinadamu Wake haujakomaa katika mwenendo Wake mbele ya wengine, hauathiri kazi ya kawaida ya uungu Wake. Ninaposema kwamba ubinadamu Wake haujapotoshwa, Ninamaanisha kwamba ubinadamu wa Kristo unaweza moja kwa moja kuongozwa na uungu Wake, na kwamba Yeye ni mwenye hisia kubwa kuliko ile ya mwanadamu wa kawaida. Ubinadamu Wake unafaa zaidi kwa kuongozwa na uungu katika kazi Yake; ubinadamu Wake una uwezo wa kuonyesha kazi ya uungu, kama vile unao uwezo wa kutii kazi kama hiyo. Mungu Anapofanya kazi katika mwili, hajawahi kamwe kupoteza maono ya wajibu wa mwanadamu katika mwili Anaopaswa kutimiza; Anao uwezo wa kumwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli. Anayo dutu ya Mungu, na utambulisho Wake ni mfano wa Mungu Mwenyewe. Ni kwamba tu Amekuja duniani na kuwa kiumbe aliyeumbwa, na ganda la nje la kiumbe, na sasa Amemiliki ubinadamu ambao hakuwa nao mwanzo; Yeye anao uwezo wa kumwabudu Mungu mbinguni. Hiki ni kiumbe cha Mungu Mwenyewe na hakiigwi na binadamu. Utambulisho Wake ni Mungu Mwenyewe. Ni kutokana na mtazamo wa mwili ndio Yeye huabudu Mungu; Kwa hivyo, maneno “Kristo huabudu Mungu mbinguni” si kwa makosa. Kile Anachouliza binadamu hasa ni nafsi Yake Mwenyewe; Yeye tayari Ameshafanikisha yote Anayotarajia kutoka kwa binadamu kabla ya kuwauliza wafanye hayo. Asingeweza kudai wengine wakati Yeye Mwenyewe Anapata kwao bure, kwa kuwa haya yote yanayotengeneza nafsi Yake. Bila kujali jinsi Yeye hufanya kazi Yake, wala Naye hangewahi kutenda kwa namna inayomuasi Mungu. Haijalishi Analomuuliza mwanadamu, hakuna mahitaji Yake yanayozidi uwezo wa mwanadamu kupata. Yote Afanyayo ni kutenda mapenzi ya Mungu na ni kwa ajili ya usimamizi Wake. Uungu wa Kristo ni zaidi ya wanadamu wote, kwa hivyo Yeye Anayo mamlaka ya juu ya viumbe vyote vilivyoumbwa. Mamlaka haya ni uungu Wake, yaani, nafsi na tabia ya Mungu Mwenyewe, ambayo huamua utambulisho Wake. Kwa hiyo, haijalishi jinsi ubinadamu Wake ni wa kawaida ni wazi kuwa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe; haijalishi upande Anaosimama Akiongea na kwa vyovyote vile Yeye hutii mapenzi ya Mungu, haiwezi kusemwa kwamba Yeye si Mungu Mwenyewe.
kutoka katika “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu huendelea na matamshi Yake, akitumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya kuhusu kile tunachofaa kufanya na wakati uo huo akipea moyo Wake sauti Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi Anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuvutiwa na hisia za ndani kabisa za mwanadamu huyu asiye wa ajabu. Yeye hutema damu ya moyo Wake kwa niaba yetu, hupoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa akigumia kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na uasi wetu na kufa ganzi kwetu kunatoa machozi na damu kutoka kwa moyo Wake. Njia hii ya kuwa na kumiliki si ya mtu wa kawaida, wala haiwezi kumilikiwwa au kufikiwa na mtu yeyote aliyepotoka. Anaonyesha uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake si kitu ambacho kiumbe chochote kimepewa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu. Yeye huonyesha moyo wa ndani zaidi wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na kuleta mbingu na nchi mpya na kazi mpya, na ametuletea matumaini, akimaliza maisha ambayo tuliishi katika hali isiyo dhahiri, na kuwezesha nafsi yetu nzima kuona njia ya wokovu kwa udhahiri kamili. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zimepata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, huyu si ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, tukiwa tumeamka au kuota, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu! Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima!
kutoka katika “Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu ni mwili wa Mungu mwenyewe. Roho wa Mungu ni mkubwa, Yeye ni mwenyezi, mtakatifu, na mwenye haki—na vilevile ndivyo ambavyo mwili Wake ulivyo pia mkubwa, wenye uwezo, mtakatifu, na wenye haki. Mwili kama huo unaweza kufanya tu kile ambacho ni chenye haki na manufaa kwa mwanadamu, kile ambacho ni kitakatifu, chenye utukufu, na uweza, na hakiwezi kukifanya chochote ambacho kinakiuka ukweli au uadilifu na haki, isitoshe hata kile ambacho kinaasi dhidi ya Roho wa Mungu.
kutoka katika “Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu anaweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika ushawishi wa Shetani, lakini kazi hii haiwezi kukamilishwa moja kwa moja na Roho wa Mungu; badala yake, inaweza kufanywa tu na mwili ambao Roho wa Mungu anauvaa, na mwili wa Mungu mwenye mwili. Mwili huu ni mwanadamu na pia ni Mungu, ni mwanadamu aliye katika ubinadamu wa kawaida na pia ni Mungu ambaye ana uungu wote. Na hivyo, hata kama mwili huu sio Roho wa Mungu, na unatofautiana kwa kiasi kikubwa na Roho, bado ni Mungu mwenye mwili Mwenyewe ambaye Anamwokoa mwanadamu, ambaye ni Roho, pia ni mwili. Haijalishi Anaitwa majina gani, hatimaye bado ni Mungu Mwenyewe anayemwokoa mwanadamu. Maana Roho wa Mungu hatenganishwi na mwili, na kazi ya mwili pia ni kazi ya Roho wa Mungu; ni kwamba tu kazi hii haifanywi kwa kutumia utambulisho wa Roho, lakini inafanywa kwa kutumia utambulisho wa mwili.
kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni nini kilichomo katika maonyesho ya Roho? Wakati mwingine Mungu wa vitendo hufanya kazi miongoni mwa ubinadamu, na wakati mwingine katika uungu—lakini kwa jumla, Roho anatawala katika pande zote mbili. … Mungu wa vitendo Mwenyewe ambaye Anazungumziwa leo hufanya Kazi katika uungu na ubinadamu. Kupitia kwa kujitokeza kwa Mungu wa vitendo, kazi Yake ya kawaida ya binadamu na maisha na kazi Yake kamilifu ya uungu vinapatikana. Ubinadamu na uungu wake vimeungwa kuwa kitu kimoja, na kazi ya pande zote mbili inakamilishwa[a] kupitia maneno; iwe katika ubinadamu au uungu, Ananena maneno. Mungu anapofanya Kazi katika ubinadamu, Anazungumza lugha ya ubinadamu, ili watu waweze kushiriki na kuelewa. Maneno Yake yanasemwa waziwazi, na ni rahisi kueleweka, kiasi kwamba yanaweza kutolewa kwa watu wote; bila ya kujali kuwa hawa watu wana ufahamu au hawajasoma vyema, wote wanaweza kupokea maneno ya Mungu. Kazi ya Mungu katika uungu vilevile inaweza kufanywa kupitia maneno, lakini imejawa na riziki, imejawa na uzima, haijatiwa dosari na mawazo ya mwanadamu, haihusishi mapenzi ya mwanadamu, na haina mipaka ya binadamu, iko nje ya mipaka ya ubinadamu wowote wa kawaida; vilevile, inafanywa katika mwili, lakini ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. … Kuonekana kwa Mungu katika mwili kunamaanisha kuwa kazi yote na maneno ya Roho wa Mungu yanafanywa katika ubinadamu wake wa kawaida, na kupitia mwili Wake uliopatikana. Kwa maneno mengine, Roho wa Mungu huelekeza kazi Yake ya ubinadamu na hutekeleza kazi Yake ya uungu katika mwili, na katika Mungu kupata mwili unaweza kuona kazi ya Mungu katika ubinadamu na kazi kamili ya uungu; huu ndio umuhimu wa utendaji hata zaidi wa kuonekana kwa Mungu wa vitendo katika mwili. Ukiweza kuliona hili wazi, utaweza kuhusisha sehemu zote za Mungu, na utaacha kuthamini sana kazi Yake ya uungu, na kuwa mwenye kupuuza sana kazi Yake katika ubinadamu, na hautazidi mipaka wala kupita njia za michepuo. Kwa jumla, maana ya Mungu wa vitendo ni kuwa kazi Yake ya ubinadamu na kazi Yake ya uungu, kama inavyoelekezwa na Roho, inaonyeshwa kupitia mwili Wake, ili watu waone kuwa Yeye ni wazi na mwenye kufanana na kiumbe chenye uhai, na ni halisi na wa hakika.
kutoka katika “Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe” katika Neno Laonekana katika Mwili
Tufuate : Mwenyezi Mungu Hutumia Neno Lake Kumwokoa Mwanadamu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni