“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Kwanza
Mwenyezi Mungu alisema, Baada ya kuzungumza juu ya baadhi ya vitu hivi, sasa mna uelewa fulani wa mada kuu ambayo tumeijadili hivi punde? Je, mmeielewa kwa kiasi fulani? Kuna sababu ambayo nimeongea kuhusu mambo haya ndani ya mada pana–sasa mnapaswa kuwa mmeelewa angalau kwa muhtasari. Mnaweza kuniambia mmeelewa kwa kiasi gani. (Binadamu wote wamelelewa kwa sheria tu ambazo ziliamuliwa na Mungu kwa ajili ya vitu vyote. Mungu alipokuwa anaamua sheria hizi, Aliandaa mbari tofautitofauti zikiwa na mazingira tofauti, mitindo tofauti ya maisha, vyakula tofauti, na hali ya hewa na halijoto tofauti. Hii ilikuwa hivyo ili binadamu wote waweze kuishi duniani na kuendelea kuishi. Kutokana na hili naweza kuuona mpango wa usimamizi wa Mungu na mipango yake angalifu na sahihi vilevile hekima na ukamilifu Wake.) (Ili kumlea binadamu, Mungu ameamua sheria hizi kwa ajili yetu na Ameandaa mazingira ya kijiografia na vilevile aina tofauti za vyakula. Na ili tuweze kuendelea kuishi ndani ya aina hii ya mazingira Aliandaa sehemu tofauti za kuishi. Kutokana na hili ninaweza kuona kwamba kazi ya Mungu na mipango ipo sahihi sana, na ninaweza kuona upendo Wake kwa sisi binadamu.) Je, kuna mtu yeyote aliye na cha kuongeza? (Sheria na mawanda yaliyoamuliwa na Mungu hayawezi kubadilishwa kabisa na mtu yeyote, tukio, au kitu. Yote ipo chini ya kanuni Yake.) Tukiangalia kwa mtazamo wa sheria zilizoamriwa na Mungu kwa ukuaji wa vitu vyote, yote hii si kwa ajili ya mwanadamu, haijalishi ni wa aina gani, anaishi chini ya uangalizi wa Mungu–je, wote hawaishi chini ya malezi Yake? Ikiwa sheria hizi zingeharibiwa au Mungu hakuanzisha aina hizi za sheria kwa ajili ya binadamu, majaliwa yao yangekuwa ni nini? Baada ya binadamu kupoteza mazingira yao ya msingi kwa ajili ya kuendelea kuishi, je, wangekuwa na chanzo chochote cha chakula? Inawezekana kwamba vyanzo vya chakula vingekuwa tatizo. Ikiwa watu wangepoteza vyanzo vyao vya chakula, yaani, hawawezi kupata kitu chochote kwa ajili ya kula, pengine wasingeweza kuvumilia hata kwa mwezi mmoja. Watu kuendelea kuishi lingekuwa ni tatizo. Kwa hiyo kila kitu ambacho Mungu anafanya kwa ajili ya watu kuendelea kuishi, kwa ajili ya wao kuendelea kuwepo na kuongezeka ni muhimu sana. Kila kitu ambacho Mungu anafanya miongoni mwa vitu vyote vinahusiana kwa karibu na haviwezi kutenganishwa na watu kuendelea kuishi. Hakiwezi kutenganishwa na wao kuendelea kuishi. Ikiwa kuendelea kuishi kwa binadamu kulikuwa tatizo, je, usimamizi wa Mungu ungeweza kuendelea? Je, usimamizi wa Mungu bado ungekuwepo? Kwa hiyo usimamizi wa Mungu unakwenda sambamba na kuendelea kuishi kwa binadamu wote ambao Anawalea, na haijalishi Mungu anaandaa kitu gani kwa ajili ya vitu vyote na kile Anachofanya kwa ajili ya binadamu, hii yote ndiyo lazima Kwake, na ni muhimu sana kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Ikiwa sheria zote hizi ambazo Mungu aliziamua kwa ajili ya vitu vyote zingekuwa zimeachwa, ikiwa sheria hizi zingekuwa zimevunjwa au zimeharibiwa, vitu vyote visingeweza kuwepo, mazingira ya binadamu ya kuendelea kuwepo yasingekuwepo, na wala riziki zao za kila siku, na wala wao wenyewe. Kwa sababu hii, Usimamizi wa Mungu wa wokovu wa binadamu wala nao usingekuwepo. Hiki ni kitu ambacho watu wanapaswa kuona waziwazi.
Tazama Zaidi Video: Matamshi ya Mungu | “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Moja”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni