5/31/2019

Wimbo wa Kuabudu 126. Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee

Wimbo wa Kuabudu 126. Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee

I
Mungu huonyesha tabia Yake ya haki kupitia mbinu na kanuni za pekee,
haidhibitiwi na watu, matukio au vitu.
Na hakuna awezaye kubadili fikira au mawazo Yake,
au kumhimiza Atumie namna nyingine.
Hii ni asili ya pekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Tabia Yake ya haki!
II
Mungu huhukumu kupitia tabia Yake ya haki matendo yote na mawazo yote ya viumbe.
Na kulingana na hili, Hutoa hasira au Hutoa rehema.
Na hakuna awezaye kubadili rehema au hasira Yake.
Na ni dutu Yake pekee yaweza kuamua njia hii.
Hii ni asili ya pekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Tabia Yake ya haki!
III
Tabia ya haki ya Mungu, takatifu na ya pekee;
hakuna awezaye kukiuka au kushuku hili.
Hakuna awezaye kuimiliki, kiumbwacho au kisichoumbwa.
Hasira ya Mungu ni takatifu; haiwezi kukosewa.
Rehema Yake pia yabeba asili hii sawa.
Hii ni asili ya pekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Tabia Yake ya haki!
IV
Hakuna mbadala wa Mungu katika Matendo Yake, kiumbwacho au kisichoumbwa.
Wala hawezi kuuharibu Sodoma au kuuokoa Ninawi kama Mungu.
Hii ni asili ya pekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Tabia Yake ya haki! Tabia Yake ya haki!
kutoka katika "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II" katika Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni