Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ukaidi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ukaidi. Onyesha machapisho yote

1/24/2018

Sura ya 92. Njia ya Utendaji katika Kusuluhisha Ukaidi | Umeme wa Mashariki

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

Umeme-wa-Mashariki-Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo

Mwenyezi Mungu alisema, Mtu huwa na tatizo lipi anapopenda kupeana visingizio? Ni nini kiini chake? Yeye ni mkaidi. Watu wakaidi hawakubali ukweli kwa urahisi; sio watiifu, na wanaposikia neno moja ambalo haliambatani na dhana, mitazamo, wanayopenda, hisia au mihemko yao wenyewe, basi hawalikubali; husema, “Sijali iwapo liko sahihi au ni mbaya, ni nani aliyelinena, lilinenwa katika muktadha gani, au iwapo linahusiana na majukumu na wajibu wangu; siyajali mambo haya. Kuziridhisha hisia zangu mwenyewe ni suala muhimu .” Hii sio ukaidi? Ukaidi huwafanya watu kupoteza nini mwishowe? Huifanya vigumu kwao kupata ukweli.