![]() |
Umeme-wa-Mashariki-Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo |
Sura ya 46. Ni Kwa Kuujua Uweza wa Mungu Pekee Ndipo Unaweza Kuwa na Imani ya Kweli
Mwenyezi Mungu alisema, Wengi wa watu hawaelewi kazi ya Mungu na si rahisi kuelewa kipengele hiki. Kitu cha kwanza ambacho lazima ujue ni kwamba kunawakati ulioteuliwa wa kazi yote ya Mungu na bila shaka si kama ilivyodhaniwa na watu. Mwanadamu hawezi kamwe kuelewa kazi ambayo Mungu ataifanya ama wakati Ataifanya. Anafanya sasa kile kinachostahili kufanywa sasa na hiki ni kitu ambacho hakuna anayeweza kukiharibu; Anafanya baadaye kile kinachostahili kufanywa baadaye, na hachelewi hata kwa sekunde moja, na hakuna anayeweza kuharibu jambo hilo pia.
