Umeme wa Mashariki | Kupotea Njia na Kupata Njia
Xiaobing Jijini Xuanzhou, Mkoani Anhui
“Kile ambacho unafurahia leo ndicho kilekile ambacho kinaharibu mustakabali wako, huku yale maumivu unayopitia leo ndiyo yaleyale ambayo yanakulinda. Lazima ufahamu waziwazi kuhusu jambo hilo ili ukuwe mbali na mtego wa majaribio na kukuepushwa kuingia kwenye ukungu mzito unaozuia jua katika maisha yako.” Kila mara ninapoimba wimbo huu wa neno la Mungu “Kufurahia Anasa za Mwili Kutaharibu Siku Zako za Baadaye,” mara kwa mara nafikiri kuhusu wakati nilipomjaribu na kumsaliti Mungu, na nahisi huruma isiyo na mwisho na shukrani kubwa.
Mnamo mwaka wa 1997, nilikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, na baada ya muda mfupi nilikuwa nimejishughulisha kwa shauku katika kazi ya kueneza injili na nilikuwa nimeweka uamuzi wangu kuwa mbele ya Mungu, ningejitumia kwa ajili Yake bila vikwazo ili kuridhisha moyo Wake. Lakini vile kazi ya Mungu ilibadilika, wakati kazi ya Mungu haikuendana na mawazo yangu mwenyewe na maombi yangu hayakutimizwa, “kujitoa” kwangu kwa Mungu basi kulipotea kusijulikane kulikoenda na asili yangu ya kumsaliti Mungu ilikuwa wazi kabisa.
Kulikuwa na siku moja mwaka wa 1999 wakati nilipokuwa nikirudi nyumbani baada ya safari ya kutekeleza wajibu wangu, na nikakutana na mwanafunzi tuliyekuwa naye darasa moja ambaye sikuwa nimemwona kwa miaka. Niliona suti yake na tai, rununu yake—kichwani hadi kidoleni, alionekana tajiri sana. Nilikuwa na wivu ajabu; kwa upande mwingine, nilionekana chakavu sana. Siku chache baadaye, kitu ambacho bibi yangu alisema mara nyingine ilinijia tena katika mahali pale pachungu: “Wewe hufanyi kazi na hupati pesa sasa—je, wewe hujizuii mwenyewe? Nani atakuheshimu bila fedha? Angalia mwanafunzi mliyekuwa naye darasa moja, akitoka na kupata pesa nyingi, kununua kila aina ya vitu ... lakini wewe je? Huna kitu!” Ghafla, niliwaza wa sura hiyo ya pekee ambayo mwanafunzi tuliyekuwa darasa moja alikuwa nayo. Nilihisi maskini na kutaka kabisa kutambaa ndani ya shimo ndogo! Kisha bibi yangu akasema: “Kiwanda cha karatasi ya maandiko ambacho mjomba wako anaendesha kinatokea kuwa kinahitaji watu na alitaka ufanye kazi huko.” Niliropokwa: “Sawa! Nitaenda!” Usiku huo, nilijilaza macho wazi nikigaagaa na kugeuka, nikiteswa na mawazo haya: Je, nitapata fedha kweli? Na ikiwa nitakabiliwa na majaribu na nisiweze kujinasua? Lakini kwa sababu ya ubatili wangu mwenyewe na ulaghai wa pesa pamoja na mashaka halisi, nilianza kuwa na shaka kwa maneno ya Mungu. Nilifikiria: Haiwezi kuwa kupata pesa kidogo kutafanya kuwa vigumu kwangu kujinasua. ... Baada ya mapambano, nilikuwa bado siwezi kupinga jaribu la pesa, kwa hiyo nilijifariji na hili: “Haijalishi; baada ya kupata pesa kidogo na kubadilisha hali hiyo, bila shaka nitaweka kila kitu katika kutimiza wajibu wangu. Sitakuwa kama watu wa kidunia ambao hawawezi kupata pesa za kutosha.” Kwa hiyo, siku iliyofuata nilikwenda kwenye kiwanda cha karatasi ya maandiko.
Nilipoanza kwanza, nilikuwa ninafanya kazi na kuishi maisha ya kikanisa. Nilijikumbusha mara nyingi: Siwezi kumkana Mungu! Lakini hatua kwa hatua nikazama chini na kuanza kuhisi kuchoshwa na kula na kunywa neno la Mungu. Sikutaka kuwaona ndugu zangu. Hata ingawa katika kila mkusanyiko nilisema kuwa fedha hazikuwa muhimu kama maisha, mara tu niliporudi kiwandani, nilishughulika sana bila kufikiri kuihusu. Wakati mwingine hata nilijitia ganzi kwa kufanya kazi daima ili kuwa nilishughulika sana kufikiria yasio ya kawaida, maafa ya mara moja kwa milenia ambayo Mungu ameandaa. Ilikuwa hivyo ndivyo nilikuja kupendelea kuishi maisha yasiyo na kusudi kama watu wa kidunia na sikutaka kutafuta maisha mazuri ya kweli katika maneno ya Mungu.
Baadaye, katika mkusanyiko, nilihisi maumivu ya ghafla ndani ya tumbo langu kama kwamba nilikuwa nimepigwa na nyundo. Kwa kweli sikuweza kuyavumilia, na nikaingia chumbani kulala. Lakini hayakuacha—nilikuwa nikizunguka kitandani kwa maumivu. Ndugu zangu walipoona kilichokuwa kinatendeka, waliharakisha kunikimbiza hospitalini, lakini daktari hakuweza kupata kitu chochote kibaya nami. Ndugu zangu walinishauri nijichunguze ndani, lakini sikufikiria kujihusu tu, lakini niliamini hata zaidi kuwa haikuwa sahihi kutokuwa na pesa. Nilifikiria: “Na kama siku moja nitakuwa mgonjwa sana, na nife kwa sababu sina pesa za matibabu?” Kwa sababu hiyo, nilianza kuchukia kuwa mshahara wangu wa kila mwezi katika kiwanda cha karatasi ya maandiko ilikuwa yuan 400 tu na niliamua kurudi nyumbani na kujitupa katika amali yangu. Kwa hiyo niliomba yuan 6,000 na kuanza kiwanda cha karatasi ya maandiko. Lakini ili kuepuka maafa ya siku za mwisho, nilishikilia pesa yangu kwa mkono mmoja na ukweli kwa mwingine, kutoruhusu yoyote kutoka. Nani angejua kuwa miezi sita baadaye, sio tu kwamba sikuwa nimepata pesa yoyote, lakini na riba niliyodaiwa zaidi ya yuan 10,000. Nilipoteza mantiki yangu hapo, na kulalamikia Mungu: “Ee Mungu, Hutanibariki kwa kupata pesa, lakini Haupaswi kuruhusu kupoteza pesa! Kwa nini nikuwe na mapenzi ya kukufuata wakati Unafanya hivi? Kwa nini nikuwe na mapenzi ya kukufuata wakati Unafanya hivi? ... “Wakati huo, nilivutiwa sana na pesa na Mungu hakuwa na hata nafasi ndogo kabisa ndani ya moyo wangu; Sikujua kabisa kuwa tabia adilifu ya Mwenyezi Mungu ilikuwa imenipata. Nilibaki nisiyetubu; kwa kweli nilimsaliti Mungu tena, kuacha kanisa kwenda kujifunza kuwa msusi. Nilijizamisha dhambini na kusahau kuhusu Mungu kabisa.
Hiyo ilikuwa mpaka siku moja nilipokuwa nikiendesha baiskeli yangu kwenda kukutana na baba yangu. Nilifika kileleni mwa mlima, na ghafla mbwa mbaya akakimbia kutoka upande wa barabara, akanirukia mbele kwa ukali. Niliendesha kwa bidii niwezavyo, nikishuka chini ya mteremko, lakini mbwa bado alikuwa karibu, akikenua meno yake na kubweka. Niliogopa sana nilikuwa nikitetemeka kutoka kichwani hadi kidoleni. Nilikuwa na hofu na nikainua miguu yangu yote juu. Kwa mshindo, nilianguka ghafla kutoka kwa baiskeli kwenye barabara, ambayo ilikuwa imefunikwa na miamba wenye ncha kali. Nilibingirika bingirika kwenye shimo karibu na barabara, kisha hatimaye kusimama. Sikuweza kusongesha miguu yangu, mikono yangu ilikuwa na ganzi, na nilikuwa na hofu. Nilifikiria: Na ikiwa hii itanifanya mimi mlemavu? Na ikiwa kitu cha kutisha kitatokea? Nilivumilia uchungu na kulala shimoni, nikitumaini baba yangu angerudi nyumbani karibuni. Hatimaye, baba yangu alirudi na, akitazama jinsi nilivyokuwa nimegongwa gongwa, aliniuliza nini kilichotokea. Bila kujua ikiwa nicheke au nilie , nikasema: “Nilitishwa na mbwa!” “Ajabu! Mbwa haumi mtu mwingine, kwa nini akuume wewe? “Mwishowe, baba yangu alifanya jitihada za kuhitaji nguvu na hatimaye akanitoa nje ya shimo na kuniweka kwenye baiskeli, na akanisukuma nyumbani. Nikilala kitandani, sikuwa na budi ila kufikiria maneno ya baba yangu tena: “Ajabu! Mbwa haumi mtu mwingine, kwa nini akuume wewe?” Ghafla, nikaona nuru na kumshukuru Mungu! Nilifikiria: Anguko hili limenibingirisha kwenye mwamko! Ikiwa ningebingirika hadi nife leo baada ya kuanguka au kuumwa na mbwa na kufa, basi haijalishi ni kiasi gani cha fedha nilichokipata, ingekuwa na matumizi gani? Zaidi nilivyofikiri kuihusu, ndivyo nilivyoogopa sana, na kwa ghafla, nilifikiria maneno ya Mungu: “Je, dunia ni mahali pako pa mapumziko kweli? Je, unaweza kupata tabasamu ya afueni kutoka kwa dunia kwa kuepuka kuadibu Kwangu? … Nawashauri: ni heri kutumia nusu ya maisha yako Kwangu kwa dhati kuliko kuishi maisha yako yote katika hali hafifu na kujishughulisha kwa ajili ya mwili, kuvumilia mateso yote ambayo ni vigumu binadamu kuvumilia. Kutakuwa na faida gani ya wewe kujipenda sana mpaka kiwango cha kuikimbia kuadibu Kwangu? Utafaidi nini ukijificha kutoka kwa kuadibu Kwangu kwa muda mfupi tu, na mwishowe upate aibu ya milele, na kuadibu kwa milele? Mimi, kwa hakika, Sitamlazimisha yeyote kufanya mapenzi Yangu. Iwapo mtu kweli anayo nia ya kujiwasilisha kwa mipango Yangu yote, Sitamtendea vibaya. Lakini Nahitaji kwamba watu wote waamini ndani Yangu …” (“Maana ya Mwanaadamu Halisi” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Labda umelalamika hapo awali, lakini haijalishi umelalamika kiasi gani Mungu hakumbuki hayo kukuhusu wewe. Leo imekuja na hakuna haja ya kuchunguza masuala ya jana” (“Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari” katika Neno Laonekana katika Mwili). Wakati huo, hisia ya shukrani ilinijaa moyoni wangu. Maisha ya wanadamu yote yako mikononi mwa Mungu, na ni Mwenyezi Mungu Amenipa uzima. Lakini wakati huo ningewezaje kuwa na ujasiri wa kurudi kanisani! Nilikuwa nimejaa majuto na nilichukia kuwa nilikuwa nimetawaliwa kumsaliti Mungu. Sio tu kwamba sikuweza kutoa ushuhuda kwa Mungu katika mazingira ambayo Aliumba kwa ajili yangu, lakini pia nilikuwa nimejaribu kujadiliana na Mungu na kulalamika, na nilikuwa nimefuata mwili wangu katika kufanya mabaya na Shetani. Nilipojifikiria nikijaribu tabia ya Mungu, kukataa kuwepo Kwake, macho Yake ya kuchunguza yakiwa kwa wanadamu, na nidhamu Yake, na mara kwa mara kuwa bila haya, bila aibu nilijaribu kujadiliana na Mungu, sikuwa na budi ila kulia machozi ya majuto. Licha ya maumivu, nilipiga magoti kitandani na kumwomba Mungu: “Mwenyezi Mungu! Mimi ni muasi sana. Nilikuamini Wewe lakini nikakuwa na shaka Kwako, nilikuamini Wewe lakini nikasonga mbali na Wewe. Sikukutendea kabisa kama Mungu; kwa kweli napaswa kulaaniwa! Kulingana na vitendo vyangu leo, ningeumwa hadi kufa na mbwa huyo. Kwa sababu huruhusu mtu mmoja kumtumikia Mabwana wawili, na hasa humruhusu mtu kukuamini lakini asikuweke katika moyo wake. Ni leo tu nilipoona kuwa bila Wewe mimi ni wa kusikitisha sana. Nilikuwa nikiishi uchafuni lakini sikuhisi kirihi, lakini sikuhisi kuwa nilikuwa nikidanganywa na Shetani. Ee Mungu! Niko tayari kujitoa Kwako kabisa. Ninakuomba Unihurumie tena, Uulinde moyo wangu, kuruhusu moyo wangu kukurudia. Baada ya majeruhi yangu yamepona, nitaacha kazi ya kutengeneza nywele na kujitupa katika kazi ya injili ili kutimiza wajibu wa uumbaji, kulipa upendo Wako, kuifariji moyo Wako, na kutojishughulisha tena kwa ajili ya pesa au kushughulika kwa ajili ya mwili.”
Ninashukuru upendo wa Mwenyezi Mungu; Alitumia adabu na hukumu kuniokoa tena kutoka kwa dhambi, kuniruhusu nipate njia yangu ya kurudi dhidi ya kupotea, ili kutafuta maisha yenye kusudi, na thamani. Upendo wa Mwenyezi Mungu kweli ni pana na kubwa; unaniacha nisiweze kuuelezea kwa maneno. Niko tayari kuweka uamuzi huu mbele ya Mungu: Kuanzia leo, sitamkana Mungu tena; Nitamfuata kwa karibu hadi mwisho ili kumlipa Mungu anayewapenda wanadamu kama mwili na damu Yake mwenyewe!
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Kujua zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Kujua zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni