5/02/2018

Swahili Gospel Praise Music "Kila Kitu Kinaishi Chini ya Sheria na Masharti Yaliyowekwa na Mungu"




Swahili Gospel Praise Music "Kila Kitu Kinaishi Chini ya Sheria na Masharti Yaliyowekwa na Mungu"

Miaka elfu kadhaa imepita,
na mwanadamu angali anafurahia nuru na hewa aliyopewa na Mungu,
angali anapumua pumzi iliyotolewa na Mungu Mwenyewe,
angali anafurahia maua, ndege, samaki na wadudu walioumbwa na Mungu,
na kufurahia viumbe vyote vilivyotolewa na Mungu;
mchana na usiku zingali zinabadilishana nafasi zao bila kusita;
hiyo misimu minne inabadilishana kama kawaida;
nayo batabukini wanaopaa wanaondoka msimu huu wa kipupwe,
lakini bado watarudi kwenye msimu ujao wa machipuko;
samaki ndani ya maji hawajawahi kuondoka kwenye mito, maziwa—maskani yao.


Adudu aina ya nyenje (cicadas) kwenye mchanga wanaimba kwelikweli kwenye siku za kiangazi;
nyenje kwenye nyasi wanaimba kwa sauti ya polepole huku wakikaribisha msimu wa mapukutiko;
wale batabukini wanaanza kutembea kwa makundi, huku nao tai wanabakia pweke;
fahari za simba wakijitosheleza wenyewe kwa kuwinda;
nao kunguni wa kaskazini wa ulaya hawatoki kwenye nyasi na maua….
Kila aina ya kiumbe kilicho hai miongoni mwa viumbe vyote kinaondoka na kurudi, kisha kinaondoka tena,
mabadiliko milioni yanafanyika kwa muda wa kufumba na kufumbu—
lakini kile kisichobadilika ni silika zao na sheria za kusalia.
Wanaishi katika ruzuku na kustawishwa na Mungu,
na hakuna mtu anayeweza kubadilisha silika zao,
na vilevile hakuna mtu yeyote anayeweza kukiuka sheria hizi za kuishi,
vilevile hakuna mtu yeyote anayeweza kukiuka sheria hizi za kuishi.


kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili 

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Nyimbo


Umeme wa MasharikiKanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni