Sura ya 44. Kuutoa Ukweli Ndiyo Njia ya Kweli ya Kuwaongoza Wengine
Mwenyezi Mungu alisema, Ikiwa mnataka kufanya kazi nzuri katika kuwaongoza wengine na kuhudumu kama mashahidi wa Mungu, la muhimu zaidi, lazima uwe na ufahamu wa kina wa kusudi la Mungu katika kuwaokoa watu na kusudi la kazi Yake. Lazima uyaelewe mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake mbalimbali ya watu. Unapaswa kuwa mwenye utendaji katika juhudi zenu; upitie tu kiasi unachoelewa na kuwasiliana tu kile unachokijua. Usijisifu, usitie chumvi, na usiseme maneno yasiyopaswa.