10. Kwa nini ni kwa kupitia na kuitii kazi ya Mungu mwenye mwili pekee ndipo mtu anaweza kumjua Mungu?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).
“Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu. Kama ninyi mngelinijua, pia mngelimjua Baba yangu: na kuanzia sasa mnamjua, na mmemwona” (Yohana 14:6-7).
“Mimi na yeye Baba yangu tu mmoja” (Yohana 10:30).
Maneno Husika ya Mungu:
Wakati Mungu alikuwa bado hajawa mwili, watu hawakuelewa mengi ya Alichosema kwa sababu kilitoka katika uungu kamilifu. Mtazamo na muktadha wa kile Alichosema ulikuwa hauonekani na haufikiwi na mwanadamu; ulionyeshwa kutoka katika ulimwengu wa kiroho ambayo watu wasingeweza kuiona. Kwa watu walioishi katika mwili, wasingeweza kupita katika ulimwengu wa kiroho. Lakini baada ya Mungu kuwa mwili, Aliongea na mwanadamu kutoka katika mtazamo wa ubinadamu, na Alitoka kwa na, na akazidi mawanda ya ulimwengu wa kiroho. Angeweza kuonyesha tabia Yake ya uungu, mapenzi, na mtazamo, kupitia mambo yale ambayo binadamu wangeweza kufikiria na mambo yale wangeweza kuona na kukumbana nayo katika maisha yao, kwa kutumia mbinu ambazo binadamu wangeweza kukubali, kwa lugha ambayo wangeweza kuelewa, na maarifa ambayo wangeweza kuelewa, ili kuruhusu mwanadamu kumwelewa na kumjua Mungu, kufahamu nia Yake na viwango Vyake hitajika ndani ya mawanda ya uwezo wao; hadi kufikia kiwango ambacho wangeweza. Hii ndiyo iliyokuwa mbinu na kanuni ya kazi ya Mungu kwa ubinadamu. Ingawa njia za Mungu na kanuni Zake za kufanya kazi katika mwili ziliweza kutimizwa sana kwa, au kupitia kwa ubinadamu, ziliweza kwa kweli kutimiza matokeo ambayo yasingeweza kutimizwa kwa kufanya kazi moja kwa moja katika uungu. Kazi ya Mungu katika ubinadamu ilikuwa thabiti zaidi, halisi, na yenye malengo, mbinu zilikuwa zaweza kubadilika kwa urahisi zaidi, na kwa umbo iliweza kupita Enzi ya Sheria.
kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu anafanya kazi mpya katika siku za mwisho. Atafichua tabia Yake zaidi, na haitakuwa huruma na upendo wa wakati wa Yesu. Kwa kuwa Ana kazi mpya, kazi hii mpya itaandamana na tabia mpya. Kwa hiyo kama kazi hii ingefanywa na Roho—kama Mungu hangepata mwili, na badala yake Roho angenena moja kwa moja kupitia radi ili mwanadamu hangekuwa na njia ya kuwasiliana na Yeye, je, mwanadamu angejua tabia yake? Kama Roho tu Angefanya kazi, basi mtu hangekuwa na njia yoyote ya kujua tabia Yake. Watu wanaweza tu kuona tabia ya Mungu kwa macho yao wenyewe wakati Anapopata mwili, wakati ambapo Neno laonekana katika mwili, na Anaonyesha tabia Yake yote kupitia mwili. Mungu kweli huishi kati ya wanadamu. Anaonekana; mwanadamu anaweza kweli kujihusisha na tabia Yake na kile Anacho na Alicho; ni kwa njia hii tu ndiyo mwanadamu anaweza kumjua kweli.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kimsingi, ujio wa Mungu katika mwili ni kuwawezesha watu kuona matendo halisi ya Mungu, kumfanya Roho asiye na umbo kuwa bayana katika mwili, na kuwapa watu fursa ya kumwona na kumgusa. Kwa njia hii, wanaokamilishwa Naye wataishi kwa kumfuata Yeye, watamfaidi na kuupendeza moyo Wake. Mungu angalinena kutoka mbinguni tu, na hakika asije duniani, basi bado watu hawangeweza kumjua, wangeweza tu kuyahubiri matendo ya Mungu kwa kutumia nadharia tupu, na hawangekuwa na maneno ya Mungu kama uhalisi. Mungu amekuja duniani kimsingi kuwa mfano na kielelezo kwa wale ambao wamepatwa na Mungu; ni kwa njia hii pekee ndio watu wanaweza kumjua Mungu kwa hakika, na kumgusa Mungu, na kumwona, na hapo ndipo wanaweza kupatikana na Mungu kwa kweli.
kutoka katika “Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ndani ya upana wa kazi ambayo Bwana Yesu alikamilisha katika Enzi ya Neema, unaweza kuona kipengele kingine cha kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho. Kilionyeshwa kupitia kwa mwili Wake, na kikawezeshwa kwa watu kuiona na kufahamu zaidi kupitia kwa ubinadamu Wake. Ndani ya Mwana wa Adamu, watu waliweza kuona namna ambavyo Mungu katika mwili alivyoishi kwa kudhihirisha ubinadamu Wake, na wakaona uungu wa Mungu ulioonyeshwa kupitia kwa mwili. Aina hizi mbili za maonyesho ziliwaruhusu watu kuweza kumwona Mungu aliye halisi sana, na kuwaruhusu kuwa na dhana tofauti ya Mungu. Hata hivyo, katika kipindi cha muda kati ya uumbaji wa ulimwengu na mwisho wa Enzi ya Sheria, yaani, kabla ya Enzi ya Neema, kile kilichoonekana, kilichosikizwa, na kupitiwa na watu kilikuwa tu kipengele kitakatifu cha Mungu. Kilikuwa kile ambacho Mungu alifanya na kusema katika himaya ile isiyoshikika, na mambo ambayo Aliyaonyesha kutoka katika nafsi Yake halisi ambayo yasingeweza kuonekana au kuguswa. Mara nyingi, mambo haya yaliwafanya watu kuhisi kwamba Mungu alikuwa mkubwa sana, na kwamba wasingeweza kusonga karibu na Yeye. Picha ambayo Mungu kwa kawaida aliwapa watu ilikuwa kwamba Alionekana akipotea, na watu walihisi hata kwamba kila mojawapo ya fikira na mawazo Yake yalikuwa yenye mafumbo mno na yasiyoeleweka mno kiasi kwamba hakukuwa na njia ya kuyafikia, isitoshe hata kujaribu kuelewa na kuyashukuru. Kwa watu, kila kitu kuhusu Mungu kilikuwa cha mbali—mbali mno kiasi kwamba watu wasingeweza kukiona, wasingeweza kukigusa. Ilionekana Alikuwa juu katika mbingu, na ilionekana kwamba Hakukuwepo kamwe. Hivyo basi kwa watu, kuelewa moyo na akili ya Mungu au kufikiria Kwake kokote kusingeweza kutimizika, na hata kufikika. … Katika kipindi cha Muda ambacho Bwana Yesu alikuwa akifanya kazi, watu wangeweza kuona kwamba Mungu alikuwa na maonyesho mengi ya kibinadamu. Kwa mfano, Aliweza kucheza, Aliweza kuhudhuria harusi, Aliweza kuwasiliana kwa karibu na watu, kuongea na wao, na kujadili mambo pamoja nao. Aidha, Bwana Yesu aliweza pia kukamilisha kazi nyingi zilizowakilisha uungu Wake, na bila shaka kazi Yake yote ilikuwa ni maonyesho na ufichuzi wa tabia ya Mungu. Katika kipindi hiki, wakati uungu wa Mungu ulitambuliwa kupitia kwa mwili wa kawaida ambao watu wangeweza kuona na kugusa, hawakuhisi tena kwamba Alikuwa akionekana na kutoweka, na kwamba wangeweza kumkaribia. Kinyume cha mambo ni kwamba, wangejaribu kuelewa mapenzi ya Mungu au kuuelewa uungu Wake kupitia kila hatua, maneno, na kazi ya Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu mwenye mwili alionyesha uungu wa Mungu kupitia kwa ubinadamu Wake na kuwasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Na kupitia maonyesho ya mapenzi na tabia ya Mungu, Aliwafichulia watu yule Mungu asiyeweza kuonekana au kuguswa katika ulimwengu wa kiroho. Kile watu walichoona kilikuwa Mungu Mwenyewe, anayeshikika na aliye na mwili na mifupa. Hivyo basi Mwana wa Adamu mwenye mwili Alifanya mambo kama vile utambulisho binafsi wa Mungu, hadhi, taswira, tabia, na kile Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kupewa picha ya binadamu. Ingawa sura ya nje ya Mwana wa Adamu ilikuwa na upungufu fulani kuhusiana na taswira ya Mungu, kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho yote hayo yaliweza kwa kikamilifu kuwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu—kulikuwa tu na tofauti fulani katika jinsi ya maonyesho. Bila kujali kama ni ubinadamu wa Mwana wa Mungu au uungu Wake, hatuwezi kukana kwamba Aliwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu mwenyewe. Katika kipindi hiki cha muda, hata hivyo, Mungu alifanya kazi kupitia mwili, Akaongea kutoka kwa mtazamo wa mwili, na kusimama mbele ya mwanadamu kwa utambulisho na hadhi ya Mwana wa Adamu, na hili liliwapa watu fursa ya kukumbana na kupitia maneno na kazi ya kweli ya Mungu miongoni mwa binadamu. Iliweza pia kuwaruhusu watu kuwa na utambuzi wa uungu Wake na ukubwa Wake katikati ya unyenyekevu, vilevile na kupata ufahamu wa mwanzo na ufafanuzi wa mwanzo wa uhalali na uhalisi wa Mungu.
kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili
Miliki na uwepo wa Mungu, kiini cha Mungu, tabia ya Mungu—yote yamewekwa wazi katika maneno Yake kwa binadamu. Anapopitia maneno ya Mungu, katika mchakato wa kuyatekeleza mwanadamu atapata kuelewa kusudi la maneno Anayonena Mungu, na kuelewa chemichemi na usuli wa maneno ya Mungu, na kuelewa na kufahamu matokeo yaliotarajiwa ya maneno ya Mungu. Kwa binadamu, haya ni mambo yote ambayo mwanadamu lazima ayapitie, ayatambue, na kuyafikia ili kuufikia ukweli na uzima, kutambua nia ya Mungu, kubadilishwa katika tabia yake, na kuweza kutii mamlaka ya Mungu na mipango. Katika wakati huo ambao mwanadamu anapitia, anafahamu, na kuvifikia vitu hivi, atakuwa kupata kumwelewa Mungu polepole, na katika wakati huu atakuwa pia amepata viwango tofauti vya ufahamu kumhusu Yeye. Kuelewa huku na maarifa havitoki katika kitu ambacho mwanadamu amefikiria ama kutengeneza, ila kutoka kwa kile ambacho anafahamu, anapitia, anahisi, na anashuhudia ndani yake mwenyewe. Ni baada tu ya kufahamu, kupitia, kuhisi, na kushuhudia vitu hivi ndipo ufahamu wa mwanadamu kumhusu Mungu utapata ujazo, ni maarifa anayopata katika wakati huu pekee ndio ulio halisi, wa kweli na sahihi, na mchakato huu—wa kupata kuelewa kwa kweli na ufahamu wa Mungu kwa kuelewa, uzoefu, kuhisi, na kushuhudia maneno Yake—sio kingine ila ushirika wa kweli kati ya mwanadamu na Mungu. Katikati ya aina hii ya ushirika, mwanadamu anakuja kuelewa kwa dhati na kufahamu nia za Mungu, anakuja kuelewa kwa dhati na kujua miliki na uwepo wa Mungu, anakuja na kuelewa kujua kwa kweli kiini cha Mungu, anakuja kuelewa na kujua tabia ya Mungu polepole, anafikia uhakika wa kweli kuhusu, na ufafanuzi sahihi wa, ukweli wa mamlaka ya Mungu juu ya vitu vyote vilivyoumbwa, na kupata mkondo kamili kwa na ufahamu wa utambulisho wa Mungu na nafasi Yake.
kutoka katika “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kipindi hiki akimfuata Yesu, Petro alikuwa na maoni mengi kuhusu Yeye na siku zote Alimhukumu kutokana na mtazamo wake. Ingawa alikuwa na kiwango fulani cha ufahamu wa Roho Mtakatifu, Petro hakuwa ametiwa nuru sana, na haya yanaonekana katika maneno yake aliposema: “Lazima nimfuate yeye aliyetumwa na Baba wa mbinguni. Lazima nimtambue yule aliyechaguliwa na Roho Mtakatifu.” Hakuelewa mambo yale ambayo Yesu alifanya na wala hakupata nuru yoyote. Baada ya kumfuata kwa muda fulani alivutiwa kwa kile alichofanya Yeye na kusema, na kwa Yesu Mwenyewe. Alikuja kuhisi kwamba Yesu alivutia upendo na heshima; alipenda kujihusisha na Yeye na kuwa kando Yake, na kusikiliza maneno Yake Yesu kulimpa ruzuku na msaada. Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. Alipata ufahamu wa kina kwamba Yesu hakuwa kama binadamu wa kawaida. Ingawa mwonekano Wake wa binadamu ulikuwa wa kawaida kabisa, Alijaa upendo, huruma, na ustahimilivu kwa binadamu. Kila kitu alichokifanya au kusema kilikuwa chenye msaada mkubwa kwa wengine, na akiwa kando Yake, Petro aliona na kujifunza mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyasikia awali. Aliona kwamba ingawa Yesu hakuwa na kimo kikubwa wala ubinadamu usio wa kawaida, Alikuwa na umbo la ajabu na lisilo la kawaida kwa kweli. Ingawa Petro hakuweza kuyafafanua kabisa, aliweza kuona kwamba Yesu alikuwa na mwenendo tofauti na kila mtu mwingine, kwani Aliyafanya mambo yaliyokuwa tofauti kabisa na yale yaliyofanywa na binadamu wa kawaida. Tangu wakati huo akiwa na Yesu, Petro alitambua pia kwamba hulka Yake ilikuwa tofauti na ile ya binadamu wa kawaida. Siku zote alikuwa na mwenendo dhabiti na hakuwahi kuwa na haraka, hakupigia chuku wala kupuuza chochote, na aliyaishi maisha Yake kwa njia iliyokuwa ya kawaida na ya kuvutia. Katika mazungumzo, Yesu alikuwa mwenye madaha na uzuri, mwenye uwazi na mchangamfu ilhali pia mtulivu, na Hakuwahi kupoteza heshima Yake katika utekelezaji wa kazi Yake. Petro aliona kwamba Yesu wakati mwingine alikuwa mnyamavu, ilhali nyakati nyingine alizungumza kwa mfululizo. Wakati mwingine Alikuwa na furaha sana kiasi cha kwamba aligeuka na kuwa mwepesi na mchangamfu kama njiwa, na ilhali nyakati nyingine Alihuzunika sana kiasi cha kwamba hakuzungumza kamwe, ni kana kwamba alikuwa mama aliyeathirika na hali ya hewa. Nyakati nyingine Alijawa na hasira, kama askari jasiri anayefyatuka kuwaua adui, na wakati mwingine hata kama simba anayenguruma. Nyakati nyingine Alicheka; nyakati nyingine aliomba na kulia. Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na ukali vyote vikamfanya kuja kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache.
kutoka katika “Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Upendo wa Mungu umeonyeshwa katika kazi Yake: ni baada tu ya kupitia kazi Yake ndipo wanaweza wakagundua upendo Wake, ni katika matukio wanayopitia ya hakika tu ambapo wanaweza kufahamu upendo wa Mungu. Kuna mengi ya kupendeza kumhusu Mungu, lakini bila ya kujihusisha na Yeye kwa hakika watu wengi hawana uwezo wa kuyagundua. Hivi ni kusema, kama Mungu asingefanyika mwili, watu wasingekuwa na uwezo wa kujihusisha na Yeye, na kama wasingekuwa na uwezo wa kujihusisha na Yeye, pia wasingeweza kupitia Kazi Yake—na kwa hivyo upendo wao kwa Mungu ungetiwa doa la uongo mwingi na mawazo. Upendo wa Mungu ulio mbinguni si halisi kama upendo wa Mungu ulio ulimwenguni, kwa kuwa ufahamu wa watu kuhusu Mungu aliye mbinguni umejengwa katika mawazo yao, bali si kwa yale ambayo wameyaona kwa macho yao, na yale ambayo wameyapitia wao wenyewe. Mungu anapokuja ulimwenguni, watu wanaweza kuyaona matendo Yake halisi na upendo wake, na wanaweza kuona kila kitu katika matendo na tabia Zake za kawaida, ambayo ni mara elfu halisi kuliko ufahamu wa Mungu aliye mbinguni. Bila kujali ni vipi ambavyo watu wanampenda Mungu aliye mbinguni, hakuna kitu halisi kuhusu huu upendo, na umejaa mawazo ya kibinadamu. Haijalishi udogo wa upendo wao kwa Mungu aliye duniani, huu upendo ni halisi; hata kama ni kidogo, ungali ni halisi. Mungu huwafanya watu kumjua kupitia kazi halisi, na kupitia ufahamu huu Anapata upendo wao. Ni kama Petro: kama hangeishi na Yesu, haingewezekana yeye kumwabudu Yesu. Aidha, huu uaminifu ulijengwa kwenye uhusiano wake na Yesu. Ili kumfanya mwanadamu ampende, Mungu amekuja miongoni mwa wanadamu na kuishi na wanadamu, na yote Anayomfanya mwanadamu kuona na kupitia ni uhalisi wa Mungu.
kutoka katika “Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikiwa Mungu hangekuwa mwili ili kufanya kazi na kumwongoza mwanadamu uso kwa uso, ikiwa Hangeathiriana na mwanadamu na kuishi na mwanadamu wakati wote, basi kuuelewa upendo wa Mungu kwa kweli kisingekuwa kitu rahisi kufanya.
Mwanadamu na Mungu kimsingi hawafanani na wanaishi katika dola mbili tofauti. Mwanadamu hawezi kuielewa lugha ya Mungu, sembuse kuyaelewa mawazo ya Mungu. Ni Mungu pekee ndiye Anayemwelewa mwanadamu na haiwezekani kwa mwanadamu kumwelewa Mungu. Kwa hiyo, Mungu ni lazima Awe mwili na awe wa aina sawa na mwanadamu (akionekana kwa nje kuwa sawa, kuvumilia fedheha na maumivu mengi ili kuwaokoa binadamu, ili waweze kuielewa na kuifahamu kazi ya Mungu. Kwa nini Mungu siku zote Anamwokoa mwanadamu na hajawahi kukata tamaa? Hii si kwa sababu ya upendo Wake kwa mwanadamu? Anamwona binadamu akiharibiwa na Shetani na Hawezi kuvumilia kuacha au kukata tamaa. Kwa hivyo ana mpango wa usimamizi. Kama ingekuwa wanavyofikiri watu na Angewaangamiza binadamu punde tu anaposhikwa na hasira, basi kusingekuwa na haja ya kuteseka kwa njia hii kumwokoa mwanadamu. Na hasa ni kwa sababu ya maumivu yaliyopitiwa na kupata mwili Kwake ndiyo upendo Wake unavumbuliwa kidogokidogo na binadamu na unafahamika kwa watu wote. Kama Mungu asingefanya kazi ya aina hii sasa, watu wangejua tu kwamba kuna Mungu mbinguni na kwamba Anawapenda binadamu. Hali ingekuwa hivi, hiyo ingekuwa mafundisho tu, na watu kamwe wasingeweza kuuona na kuupitia upendo wa Mungu wa kweli. Ni kwa Mungu tu kufanya kazi Yake katika mwili ndipo watu wanaweza kuwa na uelewa wa kweli juu Yake. Ufahamu huu si wa kufikirika au mtupu na wala siyo mafundisho ambayo mtu anayaunga mkono kwa maneno matupu, lakini badala yake ni ufahamu wa kweli sana, kwa sababu upendo ambao Mungu anampatia mwanadamu ni wa manufaa ya kweli. Kazi hii inaweza kufanywa tu kupitia kupata mwili Kwake; Roho Mtakatifu hawezi kufanya kazi hiyo badala Yake.
kutoka katika “Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kwa wale wote ambao wanaishi katika mwili, kubadilisha tabia zao kunahitaji kuwe na malengo ya kufuata, na kumjua Mungu kunahitaji kushuhudia matendo halisi na sura halisi ya Mungu. Yote haya yanaweza kufikiwa tu na Mungu mwenye mwili, na yote yanaweza kukamilishwa na mwili wa kawaida na halisi. Hii ndiyo maana kufanyika mwili ni muhimu, na kwa nini kunahitajika na wanadamu wote wapotovu. Kwa kuwa watu wanahitajika kumjua Mungu, taswira za Mungu wa kufikirika na wa kimiujiza inapaswa iondolewe kutoka katika mioyo yao, na kwa kuwa wanahitajika kutupilia mbali tabia yao iliyopotoka, kwanza wanapaswa kujua tabia yao iliyopotoka. Ikiwa mwanadamu anafanya kazi ili kuondoa taswira za Miungu wasio dhahiri kutoka katika mioyo ya watu, basi atashindwa kupata matokeo sahihi. Taswira za Miungu wasio dhahiri katika mioyo ya watu haziwezi kuwekwa hadharani, kutupwa, au kufukuzwa kabisa kwa maneno pekee. Kwa kufanya hivyo, mwisho wake haitawezekana kuondoa vitu hivi vilivyokita mizizi kwa watu. Ni Mungu anayeonekana tu na mwenye taswira halisi ya Mungu ndiyo inayoweza kuchukua nafasi ya vitu hivi visivyo dhahiri na vya kimiujiza ili kuwaruhusu watu kuvielewa taratibu, na ni kwa njia hii pekee ndipo matokeo mazuri yanaweza kupatikana. Mwanadamu anatambua kwamba Mungu aliyekuwa anamtafuta huko nyuma ni asiye dhahiri na wa kimiujiza. Kile ambacho kinaweza kufanikisha matokeo haya sio uongozi wa moja kwa moja wa Roho, sembuse mafundisho ya mtu fulani, bali ni Mungu mwenye mwili. Dhana za mwanadamu zinakuwa wazi pale ambapo Mungu mwenye mwili atafanya kazi Yake rasmi, kwa sababu ukawaida na uhalisi wa Mungu mwenye mwili ni kinyume na nadharia za Mungu asiye dhahiri na wa kufikirika katika fikra za mwanadamu. Dhana asili za mwanadamu zinaweza tu kudhihirishwa kupitia tofauti zao na Mungu mwenye mwili. Bila ulinganisho na Mungu mwenye mwili, dhana za mwanadamu zisingefichuliwa; kwa maneno mengine, bila tofauti ya uhalisi vitu visivyo dhahiri visingefichuliwa. Hakuna anayeweza kutumia maneno ili kufanya kazi hii, na hakuna anayeweza kuizungumzia kazi hii kwa kutumia maneno. Ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kufanya kazi Yake, na hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hii kwa niaba Yake. Haijalishi lugha ya mwanadamu ni pevu kiasi gani, hawezi kuzungumzia uhalisi na ukawaida wa Mungu. Mwanadamu anaweza tu kumjua Mungu zaidi kwa utendaji, na anaweza tu kumwona kwa uwazi zaidi, ikiwa Mungu binafsi anafanya kazi miongoni mwanadamu na anaonyesha kikamilifu sura Yake na uungu Wake. Athari hii haiwezi kupatwa na mwanadamu yeyote yule mwenye mwili. … Kwa hiyo, mwanadamu aliyepotoka anahitaji zaidi wokovu wa Mungu mwenye mwili, na anahitaji zaidi kazi ya moja kwa moja ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anamhitaji Mungu mwenye mwili ili kumchunga, kumsaidia, kumnywesha maji, kumlisha, kumhukumu na kumwadibu, na anahitaji neema zaidi na wokovu mkubwa kutoka kwa Mungu mwenye mwili. Ni Mungu katika mwili pekee ndiye anayeweza kuwa msiri wa mwanadamu, mchungaji wa mwanadamu, msaada wa mwanadamu uliopo kila mara, na hii yote ni ulazima wa kufanyika mwili leo na katika nyakati za nyuma.
kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili
Leo unaweza kumwabudu huyu mtu, lakini kwa hakika unamwabudu Roho. Hiki ndicho kiwango cha chini kabisa kinachopaswa kufahamiwa kuhusu ufahamu wa watu kuhusu Mungu aliyepata mwili: kujua kiini cha Roho kupitia kwa mwili, kujua kazi ya uungu ya Roho katika mwili na kazi ya wanadamu katika mwili, kukubali maneno yote ya Roho na matamshi katika mwili, na kuona jinsi Roho wa Mungu anauelekeza mwili na kudhihirisha uwezo Wake katika mwili. Hivi ni kusema kuwa, mwanadamu anapata kumjua Roho aliye mbinguni kupitia kwa mwili; kuonekana kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe miongoni mwa wanadamu kumemwondoa Mungu asiye yakini kutoka katika dhana za wanadamu; ibada ya watu kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe imeongeza utiifu wao kwa Mungu; na kupitia kwa uungu wa kazi ya Roho wa Mungu katika Mwili, na kazi ya wanadamu katika miili, mwanadamu hupata ufunuo, na kuongozwa, na mabadiliko hupatikana katika tabia ya maisha yake. Hii tu ndiyo maana halisi ya ujio wa Roho katika mwili, kimsingi, ili kwamba watu waweze kushirikiana na Mungu, kumtegemea Mungu, na kuupata ufahamu wa Mungu.
kutoka katika “Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kikundi cha watu ambao Mungu mwenye mwili Anataka kupata leo ni wale wanaokubali mapenzi Yake. Watu wanahitaji tu kutii kazi Yake, sio daima kujishughulisha na mawazo ya Mungu aliye mbinguni, waishi ndani ya hali isiyo dhahiri, au kufanya mambo kuwa magumu kwa Mungu mwenye mwili. Wale ambao wanaweza kumtii ni wale wanaoyasikia kabisa maneno Yake na kutii mipango Yake. Watu hawa hawajali kamwe jinsi Mungu mbinguni alivyo kwa kweli au ni kazi ya aina gani Mungu wa mbinguni Anafanya sasa kwa wanadamu, lakini wao humpa Mungu aliye duniani mioyo yao kabisa na kuweka nafsi zao zote mbele Yake. Kamwe hawazingatii usalama wao wenyewe, na hawalalamiki juu ya ukawaida na utendaji wa Mungu katika mwili. Wale wanaomtii Mungu katika mwili wanaweza kukamilishwa na Yeye. Wale wanaomwamini Mungu mbinguni hawatapata kitu. Hii ni kwa sababu si Mungu mbinguni, lakini ni Mungu hapa duniani ndiye Anayetoa ahadi na baraka juu ya watu. Watu hawapaswi daima kumtukuza Mungu aliye mbinguni na kumwona Mungu duniani kama mtu wa wastani. Hii si haki. Mungu mbinguni ni mkuu na wa ajabu na mwenye hekima ya ajabu, lakini hii haipo kabisa. Mungu duniani ni wa wastani sana na asiye na maana; Yeye pia ni wa kawaida sana. Hana mawazo ya ajabu au vitendo vya kimiujiza. Anatenda tu na kuongea kwa njia ya kawaida na ya matendo. Ingawa Hazungumzi kwa njia ya ngurumo au kuita upepo na mvua, Yeye kwa kweli ni mwili wa Mungu aliye mbinguni, na kwa kweli ni Mungu anayeishi kati ya wanadamu. Watu hawapaswi kumtukuza yule wanayeweza kumwelewa na ambaye analingana na mawazo yao wenyewe kama Mungu, au kumwona Yeye ambaye hawawezi kumkubali na kabisa hawawezi kufikiria kama wa chini. Yote haya ni uasi wa watu; yote ni chanzo cha upinzani wa wanadamu kwa Mungu.
kutoka katika “Watu Wanaoweza Kuwa Watiifu Kabisa Kwa Utendaji wa Mungu Ndio Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni