VIII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu
2. Kuna tofauti ipi kati ya kazi ya wale wanaotumiwa na Mungu na kazi ya viongozi wa kidini?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Naye akasema … Mtumishi wangu Musa hayuko hivyo, ambaye ni mwaminifu nyumbani mwangu mwote” (Hesabu 12:6-7).
“Na Yesu akajibu na kumwambia, … Na pia nakuambia, Kwamba wewe ni Petro, na nitalijenga kanisa langu juu ya mwamba huu; na milango ya jahanamu haitashinda dhidi ya kanisa hilo.
Na nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni: na chochote utakachofunga duniani kitafungwa mbinguni: na chochote utakachoweka huru duniani kitawekwa huru mbinguni” (Mathayo 16:17-19).
“Ole wao wachungaji wa Israeli wajilishao! Wachungaji hawapaswi kuwalisha kondoo? Mnawala kondoo walio wanono, na kuvalia sufu zao, mnawaua wale ambao wamenona: lakini hamwalishi kondoo. Hamjawapa nguvu wagonjwa, wala hamjawaponya waliougua, wala hamjawafunga waliovunjika, wala hamjawarudisha wale waliofukuzwa, wala hamjawatafuta wale waliopotea; lakini mmewatawala kwa nguvu na ukatili. Nao walitapanyika, kwa kuwa hakuna mchungaji: na wakawa chakula kwa wanyama wa porini, walipotapanyika. Kondoo wangu walizurura katika milima yote, na juu ya kila kilima kirefu: ndiyo, kondoo wangu walitapanyika juu ya uso wote wa dunia, na hakuna aliyewatafuta au kuwaulizia” (Ezekieli 34:2-6).
“Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie. Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwani mnazila nyumba za wanawake wajane, na mnatoa sala ndefu kwa kujifanya: kwa hivyo mtapokea laana kubwa zaidi. Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnazingira bahari na ardhi kwa ajili ya kumfanya mtu kubadili imani, na anapobadili, mnamfanya awe mwana wa kuzimu mara dufu zaidi kuwaliko” (Mathayo 23:13-15).
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi inayotekelezwa na yule anayetumiwa na Mungu ni kwa ajili ya kushirikiana na kazi ya Kristo au Roho Mtakatifu. Mtu huyu anainuliwa na Mungu miongoni mwa wanadamu, yuko pale kuongoza wateule wote wa Mungu, na pia yeye anainuliwa na Mungu ili kufanya kazi ya ushirikiano wa mwanadamu. Na mtu kama huyu, ambaye anaweza kufanya kazi ya ushirikiano wa mwanadamu, matakwa mengi zaidi ya Mungu kwa mwanadamu na kazi ambayo Roho Mtakatifu lazima Afanye miongoni mwa wanadamu inaweza kutimizwa kupitia kwake. Njia nyingine ya kulisema ni hivi: Lengo la Mungu katika kumtumia mtu huyu ni ili wote wanaomfuata Mungu waweze kuelewa bora mapenzi ya Mungu, na waweze kufikia matakwa zaidi ya Mungu. Kwa vile watu hawawezi kuyaelewa maneno ya Mungu na mapenzi ya Mungu moja kwa moja, Mungu amemuinua mtu fulani ambaye anatumiwa kutekeleza kazi kama hiyo. Mtu huyu anayetumiwa na Mungu anaweza kuelezwa kama chombo ambacho Mungu hutumia kuwaongoza watu, kama “mfasiri” anayewasiliana kati ya Mungu na watu. … Kuhusu kiini cha kazi yake na usuli wa kutumiwa kwake, mwanadamu anayetumiwa na Mungu huinuliwa na Yeye, hutayarishwa na Mungu kwa kazi ya Mungu, na yeye hushirikiana katika kazi ya Mungu Mwenyewe. Hakuna mtu anayeweza kushikilia nafasi ya kazi yake, ni ushirikiano wa mwanadamu ndio muhimu katika kazi takatifu. … Yule anayetumiwa na Mungu, kwa upande mwingine, ni mtu ambaye ametayarishwa na Mungu, na aliye na ubora fulani wa tabia, na ana ubinadamu. Ametayarishwa na kukamilishwa mapema na Roho Mtakatifu, na anaongozwa kabisa na Roho Mtakatifu, na, inapofikia kazi yake hasa, yeye huongozwa na kuamriwa na Roho Mtakatifu—kutokana na hilo hakuna mkengeuko katika njia ya kuwaongoza wateule wa Mungu, kwani Mungu kwa hakika huwajibikia kazi Yake mwenyewe, na Mungu hufanya kazi Yake nyakati zote.
kutoka katika “Kuhusu Mungu Kumtumia Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa nini inasemekana kwamba vitendo vya walio katika makanisa ya kidini vimepitwa na wakati? Ni kwa kuwa wanayoyaweka katika vitendo ni tofauti na kazi ya leo. … Kazi ya Roho Mtakatifu daima inasonga mbele, na wote walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu wanafaa waendelee mbele na kubadilika, hatua kwa hatua. Hawapaswi kukwama katika hatua moja. Ni wale tu wasioifahamu kazi ya Roho Mtakatifu ndio wanaweza kubaki katika hatua ya kazi ya Mungu ya awali na wasikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu. Ni wale tu walio waasi ndio watakosa uwezo wa kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ikiwa vitendo vya mwanadamu haviendani na mwendo wa kazi mpya ya Roho Mtakatifu, basi vitendo vya mwanadamu hakika vimetengana na kazi ya leo na kwa hakika havilingani na kazi ya leo. Watu waliopitwa na wakati kama hawa hawawezi kutimiza mapenzi ya Mungu, na zaidi hawawezi kuwa wale watu wa mwisho ambao watamshuhudia Mungu. Aidha, kazi nzima ya usimamizi haiwezi kutimilika miongoni mwa kundi la watu kama hao. Kwa wale walioshikilia sheria za Yehova kipindi fulani, na wale walioumia wakati fulani chini ya msalaba, ikiwa hawawezi kukubali hatua ya kazi ya siku za mwisho, basi yale yote waliyofanya ni bure na yasiyofaa. Dhihirisho la wazi zaidi wa kazi ya Roho Mtakatifu ni kwa kuyakumbatia ya sasa, sio kushikilia ya zamani. Wale ambao hawajiendelezi na kazi ya leo, na wale ambao wametengwa na utendaji wa leo, ni wale wanaopinga na hawaikubali kazi ya Roho Mtakatifu. Watu kama hao wanaipinga kazi ya Mungu ya sasa.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho ya kina hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho makuu ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali kuhusu viini vya watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufunua fikira zao, sembuse kurekebisha hali yao ya dhambi. Watu wengi wanaowafuata wanahudumia kwa karama zao za asili, na kile wanachokionyesha ni maarifa na ukweli wa kidini usioeleweka, ambao hauambatani na uhalisi na hauwezi kabisa kuwapa watu uzima. Kwa kweli, kiini cha kazi yao ni kulea talanta, kumlea mtu kuwa mhitimu mwenye talanta aliyemaliza mafunzo ya kidini ambaye baadaye anakwenda kufanya kazi na kuongoza.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda kufanya, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi kufanya, na unaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi katika kazi yako. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe; badala yake, utakuwa msumbufu hata zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na hii itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hili ni funzo kutokana na uzoefu wa kibinadamu. Ni falsafa ya maisha ya binadamu. Watu kama hawa ni wa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hatimaye watageuka na kuwa wale Makristo wa uwongo watakaoonekana katika siku za mwisho, na watu kuwa wanaowadanganya wanadamu. Makristo wa uwongo na wadanganyifu waliozungumziwa watatokana na mtu wa aina hii. Kama wale wanaomhudumia Mungu watafuata hulka yao na kutenda kulingana na mapenzi yao binafsi, basi wamo katika hatari ya kutupwa nje wakati wowote. Wale wanaotumia miaka yao mingi ya uzoefu kwa kumhudumia Mungu ili kutega mioyo ya watu, kuwasomea na lengo la kusimanga na kuwadhibiti na wale katu hawatubu, katu hawakiri dhambi zao, katu hawakatai manufaa ya cheo—watu hawa wataanguka mbele ya Mungu. Hawa ni watu walio kama Paulo, waliojaa majivuno ya vyeo vyao na wanaoonyesha ukubwa wao. Mungu hatawakamilisha watu kama hawa. Aina hii ya huduma huzuia kazi ya Mungu.
kutoka katika “Njia ya Huduma ya Kidini Lazima Ipigwe Marufuku” katika Neno Laonekana katika Mwili
Tazama tu viongozi wa kila madhehebu—wote ni wa kujigamba na kujidai, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ufahamu fulani, na wanaweza kuhubiri kuhusu mafundisho fulani, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa. Wanatumia haya kuwaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu, lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na mtu akihubiri njia ya kweli, baadhi yao husema, “Lazima tutafute ushauri kwa kiongozi wetu imani.” Imani yao lazima impitie mwanadamu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli?
kutoka katika “Ukimbizaji wa Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini. Mtu kama huyu anawezaje kutii kazi na maneno ya Mungu ambayo hayafuati fikira za mwanadamu? Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu?
kutoka katika “Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?
kutoka katika “Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni