5. Ni nini umuhimu na matokeo ya ulimwengu wa kidini kuikataa kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho?
Maneno Husika ya Mungu:
Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu ashikilie tu ukweli kwamba “Yehova ni Mungu” na “Yesu ni Kristo,” ambao ni ukweli unaozingatiwa katika enzi moja tu, basi mwanadamu hatawahi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu.
Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya, mwanadamu anafaa kufuata bila shaka lolote, na afuate kwa ukaribu. Kwa jinsi hii basi itakuwaje mwanadamu aondolewe na Roho Mtakatifu? Bila kujali kile anachofanya Mungu, kama mwanadamu ana uhakika ni kazi ya Roho Mtakatifu, na kushirikiana katika kazi ya Roho Mtakatifu bila mashaka yoyote, na kujaribu kufikia mahitaji ya Mungu, basi ataadhibiwaje? Kazi ya Mungu kamwe haijasimama, hatua Zake hazijakwama na kabla kukamilisha kazi Yake ya usimamizi, siku zote Mungu amekuwa mwenye kazi nyingi, na kamwe hajasimama. Lakini mwanadamu ni tofauti: Kutokana na kupata kiwango cha chini cha nguvu za Roho Mtakatifu, yeye huchukulia kwamba hakuna chochote kitakachobadilika; baada ya kupata ufahamu kidogo, hajipi msukumo wa kufuata nyayo za kazi mpya ya Mungu; licha ya kwamba ameona kiasi kazi ya Mungu, yeye anamchukulia Mungu kama kifaa, aina fulani ya umbo la sanamu ya mti, na anaamini kwamba Mungu atasalia kuwa hivyo daima kwani hali imekuwa hii tangu hapo awali na hata katika siku zijazo; akiwa amepata ufahamu wa kijuujuu, mwanadamu ni mwenye kiburi hivi kwamba hujisahau na kuanza kutangaza kwa fujo tabia ya Mungu na hali ya Mungu ambayo haipo; na akiwa na uhakika juu ya hatua moja ya Roho Mtakatifu, pasi kujali ni mtu wa aina gani ambaye anatangaza kazi mpya ya Mungu, mwanadamu huwa haikubali. Hawa ni watu ambao hawawezi kuikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu; ni watu wenye kushikilia ukale sana, na hawawezi kukubali mambo mapya. Watu kama hawa ni watu wanaomwamini Mungu lakini wakati uo huo wanamkataa Mungu. Mwanadamu anaamini kwamba wana wa Israeli walikosea “tu kumuamini Yehova na kukosa kumuamini Yesu,” huku watu wengi wakiiga jukumu ambapo “humwamini Yehova tu na kumkataa Yesu” na “kusubiri kwa hamu kurejea kwa Masihi lakini wanamkataa Masihi ambaye ni Yesu”. Ndiyo maana, basi, watu wengi bado wanaishi chini ya mamlaka ya Shetani baada ya kukubali hatua moja tu ya Roho Mtakatifu na bado hawapokei baraka za Mungu. Je, si hii ni kutokana na uasi wa mwanadamu? Wakristo ulimwenguni kote ambao hawajazingatia kazi mpya ya sasa wote wameshikilia imani kwamba wao ni wenye bahati na kwamba Mungu atawatimizia kila mojawapo ya malengo yao. Lakini hawawezi kueleza mbona Mungu atawapeleka katika mbingu ya tatu na wala hawafahamu jinsi Yesu atakavyokuja juu ya wingu jeupe na kuwachukua, wala kusema kwa uhakika kamili kama kweli Yesu atawasili akiwa juu ya wingu jeupe siku ambayo wanaiwaza. Wote wana wasiwasi, na kukanganywa; wao wenyewe hata hawafahamu kama Mungu atachukua kila mmoja wao, watu wachache sana, wanaotoka katika madhehebu yote. Kazi ambayo Mungu anafanya kwa sasa, enzi ya sasa, mapenzi ya Mungu—ni vitu ambavyo watu hawavifahamu, na hawana cha kufanya bali kusubiri na kuhesabu siku katika vidole vyao. Ni wale tu wanaofuata nyayo za Mwanakondoo hadi mwisho kabisa ndio wanaoweza kufaidi baraka za mwisho, huku wale “watu werevu,” ambao hawawezi kumfuata hadi mwisho ilhali wanaamini wamepata yote, ndio wasiokuwa na uwezo wa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Wote huamini wao ndio werevu zaidi duniani, na wanasitisha maendeleo ya kazi ya Mungu bila sababu yoyote kabisa, na huonekana kuamini pasi na shaka kwamba Mungu atawachukua mbinguni, wao “wenye uaminifu wa juu zaidi kwa Mungu, humfuata Mungu, na hutii neno la Mungu”. Hata ingawa wana “uaminifu wa hali ya juu” kwa maneno yaliyozungumzwa na Mungu; maneno yao na matendo yao bado hukera kwa sababu wao huipinga kazi ya Roho Mtakatifu, na kufanya uongo na uovu. Wale wasiofuata hadi mwisho kabisa, ambao hawazingatii kazi ya Roho Mtakatifu, na ambao wanashikilia kazi ya zamani hawajakosa tu kupata uaminifu kwa Mungu, bali kwa kinyume, wamekuwa wale wanaompinga Mungu, wamekuwa wale ambao wamekanwa na enzi mpya, na watakaoadhibiwa. Kuna wa kuhurumiwa zaidi kuliko wao?
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru—je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, zaidi ya hayo, wale wasiojua, wenye majivuno ya asili na wasioweza kutawalwa? Hata ikiwa siku itakuja ambapo watu hawa watakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, bado Mungu hatawavumilia. Hawadharau tu wale wanaofanya kazi ya Mungu, bali pia wanamkufuru Mungu Mwenyewe. Watu kama hawa jasiri pasi na hadhari hawatasamehewa, katika enzi hii ama enzi itakayokuja na wataangamia kuzimuni milele!
kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hayo ni kwa sababu walio nayo ni maji machafu yaliyolala palepale kwa maelfu ya miaka, badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, wala njia inayoweza kukuongoza kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.
kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.
kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wengi wana hisia mbaya kuhusu kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, kwa maana mwanadamu huona vigumu kuamini ya kwamba Mungu angefanya kazi ya hukumu akiwa na mwili. Hata hivyo, lazima Nikueleze kwamba mara nyingi kazi ya Mungu huzidi sana matarajio ya mwanadamu na ni vigumu kwa mawazo yao kukubali. Kwa maana wanadamu ni mabuu tu kwenye ardhi, ilhali Mungu ni mkuu Anayejaza ulimwengu mzima; mawazo ya mwanadamu ni kama shimo la maji machafu ambayo yanazalisha mabuu peke yake, ilhali kila hatua ya kazi inayoelekezwa na mawazo ya Mungu ni utoneshaji wa hekima ya Mungu. Mwanadamu hutaka kila wakati kushindana na Mungu, ambalo kwalo Nasema ni wazi nani atapata hasara mwishowe. Nawasihi nyote msijichukulie kuwa wa maana zaidi kushinda dhahabu. Ikiwa wengine wanaweza kukubali hukumu ya Mungu, ni kwa nini wewe usiikubali? Ni vipi ambavyo ninyi ni bora zaidi kuliko wengine? Iwapo wengine wanaweza kuinamisha vichwa vyao mbele ya ukweli, ni kwa nini usifanye vile pia? Mwelekeo mkuu wa kazi ya Mungu hauwezi kukomeshwa. Hatarudia kazi ya hukumu tena kwa sababu ya “kustahili” kwako, na utajawa na majuto mengi kwa kupoteza nafasi nzuri kama hiyo. Usipoyaamini maneno Yangu, basi kingoje tu kiti cheupe kikuu cha enzi kilicho angani kipitishe hukumu juu yako! Lazima ujue kwamba Waisraeli wote walimkataa kwa dharau na kumkana Yesu, ilhali uhakika wa ukombozi wa Yesu kwa wanadamu ulizidi kusambaa mpaka mwisho wa ulimwengu. Je, hili silo jambo ambalo Mungu tayari Amelitimiza? Iwapo bado unangoja Yesu aje kukupeleka mbinguni, basi Nasema kuwa wewe ni kipande sugu cha mti mkavu[a]. Yesu hatamkubali mfuasi bandia kama wewe asiye mwaminifu kwa ukweli na anayetafuta baraka pekee. Hasha, Hataonyesha huruma Anapokutupa kwenye ziwa la moto uungue kwa makumi ya maelfu ya miaka.
kutoka katika “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Dunia inaanguka! Babeli imelemaa! Dunia ya kidini—itakosa kuharibiwa vipi na mamlaka Yangu duniani?
kutoka katika “Sura ya 22” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu hataki watu zaidi kuadhibiwa, lakini badala yake Anatumai kuwa watu zaidi wataokolewa, na kuwa watu zaidi wawe kasi sawa na nyayo Zake na kuingia katika ufalme Wake. Lakini watu wakikataa kutambua makosa yao, kama hawawezi kukubali ukweli kwa moyo mnyenyekevu, lakini badala yake wayajali masuala madogo madogo, wakijaribu kutafuta makosa na kujifanya kuelewa wakati kweli hawaelewi, basi watakuwa wale wanaopoteza mwishowe. Kazi ya Mungu haisubiri yeyote. Wokovu Wake si kama kipande fulani cha taka, kuvishwa pasi kufikiria na mtu yeyote tu. Badala yake unalengwa, kwa lengo na kwa chaguo. Iwapo hujui kuutunza, basi kitu kinachokusubiri tu kitakuwa hukumu ya Mungu ya haki na adhabu. Mungu huwatendea watu wote kwa haki; bila kujali umri wako, jinsi ulivyo mkubwa au hata kiwango cha mateso umepitia, tabia ya Mungu ya haki daima haibadiliki ikiwa imekabiliwa na vitu hivi. Mungu hamtendei mtu yeyote kwa heshima kubwa, wala Hampendelei mtu yeyote. Mwelekeo Wake kwa watu unategemezwa kwa iwapo wanaweza kuukubali ukweli na kukubali kazi Yake mpya kwa kuacha vitu vyote au la. Iwapo unaweza kupokea kazi Yake mpya na kupokea ukweli Anaoonyesha, basi utaweza kupata wokovu wa Mungu. Iwapo una majivuno kwa ajili ya hadhi yako kongwe na unaringa kwa sababu ya ukubwa wako, ukimwekea Mungu masharti, basi utakanwa kutoka kwa wokovu wa Mungu. Kama tu vile Wayahudi, ambao hawakuweza kumkubali Yesu Kristo lakini walimsubiri tu Masiya, kile kilichowapata mwishowe kilikuwa laana na hasira ya Mungu; huu ni ukweli ambao uko kwa wote kuuona. …
… Maarifa na matendo ya nje ya Mafarisayo hayakuokoa uhusiano wao na Yesu Kristo. Kinyume chake, yaliwadhuru na yalikuwa maarifa na dhana zao, pamoja na taswira ya Mungu mioyoni mwao, yaliyowasababisha kumshutumu Bwana Yesu. Ilikuwa fikira na akili zao zilizowapotosha, zilizofunika macho yao ya roho, kuwasababisha kutotambua Masiya ambaye alikuwa amekuja tayari, kufanya yote waliyoweza kupata ushahidi na kupata kidato ili kumshutumu Bwana Yesu. Hii ni sura yao mbaya—kutumia kisingizio cha kutetea kazi ya asili ya Mungu kushutumu kazi halisi ya Mungu iliyopo. Bila shaka, haya ni makosa ambayo watu wanaoishi katika enzi yoyote wanaweza kufanya—kutumia mafundisho na amri za kale kupima na kushutumu ukweli ambao hawajawahi kusikia kabla, kufikiri kwamba wanashikilia njia ya kweli na kudumisha utakatifu wao mbele ya Mungu, kwamba wanakuwa waaminifu kwa Mungu. Lakini ukweli ni upi? Mungu anaendelea kufanya kazi Yake mpya, anaendeleza usimamizi Wake, daima mpya na kamwe si mzee. Na watu je? Daima wanashikilia imara vitu fulani visivyotumika siku hizi ambavyo wanafikiri kuwa ukamilifu wa maonyesho ya Mungu, wakijipongeza, wakiwa wamejaa kiburi, wakisubiri Mungu kuwapa thawabu kwa mtazamo kwamba Mungu kamwe hawezi kuwatupa, hawezi kamwe kuwatendea vibaya. Na matokeo ni yapi? Kazi ya Mungu inaendelea bila kukatizwa, huku watu zaidi wa enzi mpya wakimfuata na kukubali kazi Yake mpya, ilhali wale wanaosubiri Mungu awape thawabu wanaondolewa na kazi mpya ya Mungu, na hata watu zaidi wanapatwa na adhabu ya Mungu. Wakati huo ambapo adhabu yao inaanza, maisha yao katika kumwamini Mungu yanaisha, na mwisho wao, na hatima yao, yanahitimishwa. Hili ni jambo ambalo hakuna anayetaka kuona, lakini linatendeka pasi kujua mbele yetu. Hivyo hili linasababishwa na tabia ya Mungu kuwa isiyo na huruma kabisa, ama ni kwamba kutafuta kwa watu kuna makosa? Je, kwa kweli halistahili wanadamu kujichunguza kikamilifu?
kutoka katika Hitimisho ya Mifano Maarufu ya Adhabu kwa Kumpinga Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni