6/27/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’”



Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’”


Mwenyezi Mungu anasema, “Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea kwa ghafla kwa Yesu Kristo, ili kutimiza maneno ya Yesu akiwa duniani: “Nitarejea jinsi Nilivyoondoka”. Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe, na kuchukua mahali Pake katika mkono wa kuume wa Aliye Juu. Mwanadamu anawaza kuwa vilevile, Yesu atashuka tena juu ya wingu jeupe katika siku za mwisho (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani mno kwa maelfu ya miaka, na kwamba Atachukua mfano na mavazi ya Wayahudi. Baada ya kumwonekania mwanadamu, Atawapa chakula, na kusababisha maji ya uzima kumwagika kwa ajili yao, naye Ataishi miongoni mwa wanadamu, akiwa Amejawa na neema na upendo, Akiwa hai na halisi. Na kadhalika. Ilhali Yesu Mwokozi hakufanya hivi; Alitenda kinyume cha yale ambayo mwanadamu alidhania. Hakurejea kati ya wale ambao walikuwa wametamani kurejea Kwake, naye hakutokea kwa wanadamu wote akiwa Amepanda juu ya wingu jeupe. Amerejea tayari, lakini mwanadamu hamjui, naye anasalia kuwa mjinga kuhusu kurejea Kwake. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo, bila kujua kuwa Ameshuka tayari juu ya wingu jeupe (wingu ambalo ni Roho Wake, maneno Yake, na tabia Yake yote na yale yote Aliyo), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho.”

Jifunze zaidi: Kuhusu Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni