Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Nne
Mwenyezi Mungu alisema, Kuzaliwa, kukua, na kuoa ni awamu ambazo zinaleta aina tofauti na viwango tofauti vya masikitiko. Baadhi ya watu hawatosheki na familia zao au maumbo yao ya kimwili; baadhi hawapendi wazazi wao; baadhi wanachukia au wanalalamikia mazingira ambayo walikulia ndani. Na kwa baadhi ya watu wengi, miongoni mwa masikitiko haya yote, ndoa ndiyo ambayo haitoshelezi zaidi.
Licha ya vile ambavyo unayo masikitiko kwa kuzaliwa kwako, au kukua kwako, au ndoa yako, kila mmoja ambaye amepitia awamu hizi amejua kwamba hawezi kuchagua ni wapi au ni lini alizaliwa, ni vipi anavyofanana, wazazi wake ni nani, na mume au mke wake ni nani, lakini wanaweza kukubali tu mapenzi ya Mbinguni. Lakini wakati wa watu kulea kizazi kijacho unapowadia, wataweza kuweka matamanio yao yote ambayo hayajatimizwa katika nusu ya kwanza ya maisha yao kwenye vizazi vyao, wakitumai kwamba, uzao wao utajaliza sehemu ile ambayo wao wamepitia masikitiko, kwenye nusu ile ya kwanza ya maisha yao. Kwa hivyo watu hujihusisha katika aina zote za fantasia kuhusu watoto wao: kwamba binti zao watakua na kuwa warembo ajabu, watoto wao wa kiume watakuwa wanaume wa kipekee; kwamba binti zao watakuwa na maadili na wenye vipaji nao watoto wao wa kiume watakuwa wanafunzi werevu, na wanariadha sifika; na kwamba binti zao watakuwa watulivu na waadilifu, wenye akili razini, kwamba watoto wao wa kiume watakuwa wenye akili, wenye uwezo na wanaojali. Wanatumai kwamba wawe watoto wa kike au wa kiume wataheshimu wazee wao, watajali wazazi wao, watapendwa na kusifiwa na kila mmoja…. Kufikia hapa matumaini ya maisha yanajitokeza upya, na matamanio mapya yanapata nguvu katika mioyo ya watu. Watu wanajua kwamba hawana nguvu na tumaini katika maisha haya, kwamba hawatakuwa na fursa nyingine, tumaini jingine, la kujitokeza mbele ya watu, na kwamba hawana chaguo lolote ila kukubali hatima zao. Na kwa hivyo wanatazamia matumaini yao yote, matamanio na maadili yao ambayo hayajatimizwa, hadi kwenye kizazi kijacho, wakitumai uzao wao unaweza kuwasaidia kutimiza ndoto zao na kutambua matamanio yao; na kwamba binti zao na watoto wao wa kiume wataleta utukufu katika jina la familia, kuwa muhimu, kuwa matajiri au maarufu; kwa ufupi, wanataka kuuona utajiri wa watoto wao ukizidi na kuzidi. Mipango na fantasia za watu ni timilifu; kwani hawajui kwamba idadi ya watoto walio nayo, umbo, uwezo na kadhalika wa watoto wao, si juu yao kuamua, kwamba hatima za watoto wao hazimo kamwe katika viganja vya mikono yao? Binadamu si waendeshaji wa hatima yao binafsi, ilhali wanatumai kubadilisha hatima ya kizazi kichanga zaidi; hawana nguvu za kutoroka hatima zao wenyewe, ilhali, wanajaribu kudhibiti zile za watoto wao wa kiume na kike. Je, hawazidishi ukadiriaji wao? Je, huu si ujinga na hali ya kutojua kwa upande wa binadamu? Watu huenda kwa mapana yoyote kwa minajili ya uzao wao, lakini hatimaye, idadi ya watoto aliyonayo mtu, na vile ambavyo watoto wake walivyo, si jibu la mipango na matamanio yao. Baadhi ya watu hawana hela lakini wanazaa watoto wengi; baadhi ya watu ni tajiri ilhali hawana mtoto. Baadhi wanataka binti lakini wananyimwa tamanio hilo; baadhi wanataka mtoto wa kiume lakini wanashindwa kuzaa mtoto wa kiume. Kwa baadhi, watoto ni baraka; kwa wengine, mtoto ni laana. Baadhi ya wanandoa ni werevu, ilhali wanawazaa watoto wanaoelewa polepole; baadhi ya wazazi ni wenye bidii na waaminifu, ilhali watoto wanaowalea ni wavivu. Baadhi ya wazazi ni wapole na wanyofu lakini wana watoto wanaogeuka na kuwa wajanja na wenye inda. Baadhi ya wazazi wana akili na mwili timamu lakini wanajifungua watoto walemavu. Baadhi ya wazazi ni wa kawaida na hawajafanikiwa ilhali watoto wao wanafanikiwa pakubwa. Baadhi ya wazazi ni wa hadhi ya chini ilhali watoto wanaowalea ni wenye taadhima. …
Ilisasishwa Mwisho: Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Tano
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni