3/07/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tabia Yako Ni Duni Sana!


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tabia Yako Ni Duni Sana!


    Ninyi nyote mmeketi katika viti vya kifahari, mkiwafundisha wale wa vizazi vijana ambao ni wa aina yenu, ukiwafanya waketi nawe. Je, mngekosaje kujua kwamba wale “watoto” wenu walikuwa tayari hawana pumzi, na kwamba hawakuwa na kazi Yangu zamani? Utukufu Wangu huangaza kutoka nchi ya Mashariki hadi nchi ya Magharibi, lakini wakati utukufu Wangu huenea mpaka mwisho wa dunia na wakati unapoanza kuinuka na kuangaza, Nitaondoa utukufu wa Mashariki na kuuletea Magharibi ili kwamba watu hawa wa giza katika Mashariki ambao wameniacha Mimi watakuwa bila mwanga unaong’aa kuanzia hapo kwendelea. Wakati huo, mtaishi katika bonde la kivuli. Ingawa watu leo ni wazuri mara mia zaidi kuliko awali, bado hawawezi kuyatosheleza mahitaji Yangu, na bado wao si ushahidi mtukufu Kwangu. Kwamba nyinyi mnaweza kuwa wazuri mara mia zaidi kuliko awali yote ni matokeo ya kazi Yangu—ni tunda la kazi Yangu duniani. Hata hivyo, bado Ninahisi maudhi kwa maneno na matendo yenu, na tabia yenu, na Ninahisi hasira ya ajabu sana kwa matendo yenu mbele Yangu, kwa maana hamna ufahamu wowote Wangu. Kwa hiyo mnawezaje kuwa walio hai kutoka kwa utukufu Wangu, na mnawezaje kuwa waaminifu kabisa kwa kazi Yangu ya baadaye? Imani yenu ni nzuri sana; mnasema kwamba mko radhi kutoa maisha yenu kwa kazi Yangu, kufanya chochote na kila kitu kwa ajili yake, lakini tabia yenu haijabadilika sana. Kumekuwa tu na maneno ya kiburi, na matendo yenu halisi ni duni sana. Inaonekana kwamba ulimi na midomo ya mtu iko mbinguni lakini miguu ya mtu iko mbali sana duniani, hivyo maneno na matendo yake na sifa yake bado yako katika hali mbaya sana. Sifa zenu tayari zimeharibiwa, mwenendo wenu unashuka hadhi, njia yenu ya kuzungumza ni ya chini, maisha yenu ni ya kudharauliwa, na hata ubinadamu wenu wote ni wa chini. Nyinyi ni wa mawazo finyu kwa watu na nyinyi hubishana juu ya kila kitu kidogo. Nyinyi hugombana juu ya sifa zenu na hadhi zenu wenyewe, hata kufikia kiasi kwamba mko radhi kushuka kuzimu, katika ziwa la moto. Maneno na matendo yenu ya sasa yanatosha kiasi kwamba Ninaweza kuamua kuwa nyinyi ni wenye dhambi. Mtazamo wenu juu ya kazi Yangu unatosha Kwangu kutambua kuwa nyinyi ni wale wadhalimu, na tabia zenu zote zinatosha kusema kuwa nyinyi ni roho chafu ambazo zimejaa machukizo. Maonyesho yenu na kile mnachofichua ni tosha kusema kuwa nyinyi ni watu ambao mmekunywa damu ya kutosha ya pepo wachafu. Wakati kuingia katika ufalme kunapozungumzwa hamfichui hisia zenu. Mnaamini kuwa jinsi mlivyo sasa kunatosha kwenu kuingia katika lango la ufalme Wangu wa mbinguni? Je, mnaamini kuwa mnaweza kupata kuingia katika nchi takatifu ya kazi na maneno Yangu bila maneno na vitendo vyenu kupitia majaribio Yangu? Ni nani anayeweza kwa ufanisi kuyadanganya macho Yangu mawili? Je, tabia zenu za mazungumzo ya kudharauliwa na duni, zawezaje kuepuka Mimi kuona? Maisha yenu yameamuliwa na Mimi kama maisha ya kunywa damu ya pepo hizo chafu na kula nyama ya pepo hao wachafu kwa sababu mnachukua sura yao mbele Yangu kila siku. Mbele Yangu tabia zenu zilikuwa mbaya hasa, hivyo, ni vipi Mimi singeweza kuchukizwa? Katika kile mnachosema kuna najisi ya pepo wachafu: Nyinyi hudanganya, huficha, na kujipendekeza kama wale tu wanaofanya uchawi, kama wale wanaodanganya na kunywa damu ya wasio wa haki. Maonyesho yote ya wanadamu ni madhalimu sana, hiyo watu wote wanawezaje kuwekwa katika nchi takatifu ambako wenye haki wapo? Je, unafikiri kwamba tabia hiyo yako ya kudharauliwa inaweza kukubainisha kama mtakatifu dhidi ya wale wadhalimu? Huo ulimi wako unaofanana na nyoka hatimaye utaangamiza mwili wako ambao huleta maangamizi na hufanya machukizo, na mikono yako hiyo ambayo imefunikwa na damu ya pepo wachafu pia itavuta roho yako kuzimu hatimaye, hiyo kwa nini usichukue fursa hii kuitakasa mikono yako iliyofunikwa na uchafu? Na kwa nini huchukui fursa hii kuukata ulimi wako huo ambao husema maneno maovu? Inawezekana kuwa uko radhi kuteseka chini ya moto wa kuzimu kwa sababu ya mikono yako miwili na ulimi wako na midomo? Mimi huilinda mioyo ya watu wote kwa macho Yangu mawili kwa sababu muda mrefu kabla ya kuwaumba wanadamu, Nilikuwa Nimeishika mioyo yao ndani ya mikono Yangu. Zamani Nilibaini moyo wa mwanadamu, kwa hiyo mawazo ya ndani ya moyo wa mwanadamu yanawezaje kuyaepuka macho Yangu? Na wanawezaje kuwepo mapema ili kuepuka kuchomwa kwa Roho Wangu?

Midomo yako ni yenye huruma zaidi kuliko njiwa lakini moyo wako ni mbaya zaidi kuliko nyoka ya kale, hata midomo yako ni mizuri kama mwanamke Mlebanoni, lakini moyo wako si mwema kama ule wa wanawake Walebanoni na hakika hauwezi kulinganishwa na uzuri wa Wakanaani. Moyo wako ni mdanganyifu sana. Ninachochukia ni midomo ya wadhalimu na mioyo ya wadhalimu pekee. Mahitaji Yangu kwa watu si ya juu kuliko watakatifu, ni vile tu kwamba Mimi huhisi chukizo kwa matendo maovu ya wadhalimu na Natumaini kwamba wadhalimu huenda waweze kuondoa kuchafuka kwao na kukimbia kutoka kwa mashaka yao ya sasa ili waweze kutofautishwa na wale wadhalimu, na kuishi na kuwa watakatifu pamoja na wale wenye haki. Nyinyi mko katika hali sawa na Mimi, lakini mmefunikwa na uchafu, hakuna hata mfano kidogo wa wanadamu walioumbwa hapo mwanzo ndani yenu, na kwa sababu kila siku mnaiga mfano wa hao pepo wachafu na mnafanya kile wanachokifanya na kusema kile wanachokisema, kila sehemu zenu na hata ndimi zenu na midomo yenu imelowa katika maji yao mabaya. Ni kwa kiwango ambacho mmefunikwa kabisa na hayo mawaa na hakuna sehemu hata moja ambayo inaweza kutumiwa kwa kazi Yangu. Ni jambo la kusikitisha sana! Mnaishi katika ulimwengu huu wa farasi na ng’ombe lakini bado kwa kweli hamjihisi kuwa na wasiwasi; na mmejaa furaha na nyinyi huishi kwa uhuru na kwa urahisi. Mnaogelea katika maji haya mabaya lakini kwa kweli hamjui kwamba mmeanguka katika mazingira haya. Kila siku unaafikiana na pepo wachafu na una shughuli na “kinyesi.” Uhai wako ni duni sana, lakini hujui kwamba bila shaka huendelei kuishi katika ulimwengu wa kibinadamu na kwamba humo ndani ya ufahamu wako mwenyewe. Je, hujui kwamba maisha yako yalikanyagwa na pepo wachafu zamani, kwamba tabia yako ilivunjiwa hadhi na maji machafu zamani? Je, unadhani kuwa unaishi katika paradiso ya kidunia, kwamba uko katikati ya furaha? Je, hujui kwamba umeishi maisha na pepo wachafu, na kwamba umeishi maisha na kila kitu ambacho wamekuandalia? Je, kuishi kwako kungewezaje kuwa na maana yoyote? Je, maisha yako yangewezaje kuwa na thamani yoyote? Umekuwa ukienda huku na huko kwa ajili ya wazazi wako pepo wachafu, hadi sasa, lakini hujui kwamba wale ambao wanakunasa mtegoni ni hao pepo wachafu, wazazi wako ambao walikuzaa na kukulea. Aidha, hujui kuwa uchafu wako hakika ulipewa wote na wao; yote unayojua ni kwamba wanaweza kukupa “ridhaa,” hawakuadibu, wala hawakuhukumu, na hasa hawakulaani. Hawajawahi kukulipukia kwa ghadhabu, lakini hukutendea kwa bashasha na kwa ukarimu. Maneno yao hulisha moyo wako na kukupendeza mno ili ukanganywe na bila kulitambua, unavutwa ndani na uko radhi kuwa wa huduma kwao, uwe mlango wao na kadhalika mtumishi wao. Huna malalamiko kamwe lakini uko radhi kutumiwa nao—unadanganywa nao. Kwa sababu hii, bila shaka huna majibizo yoyote kwa kazi ambayo Mimi hufanya—si ajabu kwamba wewe daima hutaka kuponyoka kwa siri kutoka kwa mikono Yangu, na si ajabu kwamba wewe daima hutaka kutumia maneno matamu ili kuidanganya fadhila Yangu. Inadhihirika kwamba tayari ulikuwa na mpango mwingine, mpangilio mwingine. Unaweza kuona sehemu ndogo ya vitendo Yangu, vitendo vya Mwenyezi, lakini hujui chembe ya hukumu na kuadibu kwangu. Hujui wakati kuadibu kwangu kulianza; unajua tu jinsi ya kunidanganya Mimi, lakini hujui kuwa Sivumilii ukiukaji na mwanadamu. Kwa kuwa tayari umeweka uamuzi wako kunitumikia Mimi, sitakuacha uende. Mimi ni Mungu mwenye wivu, na Mimi ni Mungu ambaye ana wivu kwa mwanadamu. Kwa kuwa tayari umewekelea maneno yako juu ya madhabahu, Sitakuvumilia wewe kuhudumia mabwana wawili. Je, ulifikiri ungepata upendo mwingine baada ya kuweka maneno yako juu ya madhabahu Yangu, baada ya kuyaweka mbele ya macho Yangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo? Je, ulidhani kwamba ungeweza kuweka nadhiri kikawaida, kula kiapo kunielekea Mimi na ulimi wako? Je, ungewezaje kula kiapo kunielekea kiti Changu cha enzi, Aliye Juu Zaidi? Je, ulifikiri kwamba viapo vyako vilikuwa tayari vimekufa? Nawaambia, hata kama miili yenu ikifa, viapo vyenu haviwezi kufa. Hatimaye, Nitawahukumu kwa msingi wa viapo vyenu. Lakini mnadhani kwamba mnaweza kuweka maneno yenu mbele Yangu ili kunivumilia Mimi na kwamba mioyo yenu inaweza kuwatumikia pepo wachafu na pepo wabaya. Je, hasira Yangu ingewezaje kuwavumilia hao watu mithili ya mbwa na nguruwe wanaonidanganya? Lazima Nitekeleze amri Zangu za kiutawala, na kuwapokonya kutoka kwa mikono ya pepo wachafu wale wote wenye fukuto, “wacha Mungu” ambao wanaamini katika Mimi “kunitumikia” Mimi kwa njia ya mpango, kuwa ng’ombe Wangu, kuwa farasi Wangu na kudhibitiwa na Mimi. Nitakufanya ushike uamuzi wako wa awali na kunitumikia Mimi tena. Siwezi kuvumilia kiumbe yeyote kunidanganya Mimi. Je, ulifikiria kwamba ungeweza kufanya maombi tu kiutukutu na kudanganya kiutukutu mbele Yangu? Je, ulifikiri kwamba Mimi sikuwa nimesikia au kuona maneno na matendo yako? Je, maneno yako na matendo yako yangekosaje kuwa katika mtazamo Wangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo?

Nimekuwa miongoni mwenu, Nimeshirikiana nanyi kwa majira kadhaa ya kuchipua na kwa majira kadhaa ya kupukutika, Nimeishi kati yenu kwa muda mrefu—ni kiasi gani cha tabia yenu ya kudharaulika kimeponyoka mbele ya macho Yangu? Maneno yenu hayo ya dhati daima yarudisha mwangwi ndani ya masikio Yangu; mamilioni na mamilioni ya matarajio yenu yamewekwa juu ya madhabahu Yangu—hayawezi hata kuhesabiwa. Lakini kwa kujitolea kwako na kile mnachokitumia, hakuna hata kidogo. Hakuna hata tone dogo la uaminifu wenu kwenye madhabahu Yangu. Yako wapi matunda ya imani yenu Kwangu? Mmepokea neema isiyo na mwisho kutoka Kwangu na mmeona mafumbo yasiyo na mwisho kutoka mbinguni, na Nimewaonyesha hata miale ya mbinguni lakini Sijawahi kuwa na moyo wa kuwachoma, na ni kiasi gani mmenipa Mimi kama malipo? Je, mko radhi kunipa Mimi kiasi gani? Kama umeshikilia chakula Nilichokupa, unageuka na kunitolea Mimi, hata ukisema kuwa ni kitu ambacho umepata kama malipo kwa jasho la kazi yako ngumu, kwamba unatoa yote uliyo nayo Kwangu. Je, unawezaje kukosa kujua kwamba “michango” yako Kwangu ni vitu vyote vilivyoibwa kutoka kwa madhabahu Yangu? Na sasa unavitoa Kwangu—si wewe unanidanganya Mimi? Unawezaje kukosa kujua kuwa vitu Ninavyovifurahia leo ni matoleo yote juu ya madhabahu Yangu, na sicho kile ulichokichuma kama malipo ya kazi yako ngumu halafu ukanitolea Mimi? Kwa kweli mnathubutu kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa hiyo ni kwa jinsi gani Ninaweza kuwasamehe? Ninawezaje kuvumilia hili zaidi? Nimewapa kila kitu. Nimewafungulia kila kitu, Nikakimu mahitaji yenu, na kuyafungua macho yenu, lakini bado mnanidanganya Mimi kwa njia hii, mkipuuza dhamiri yenu. Bila ubinafsi Nimewapa kila kitu, ili kwamba hata kama mnateseka, mmepata kutoka Kwangu kila kitu Nilichokileta kutoka mbinguni. Lakini hamna kujitolea kamwe, na hata kama mna mchango mdogo, mnalipa deni baada ya hapo. Je, si mchango wako utakuwa bure? Kile ambacho umenipa si chochote isipokuwa chembe moja ya mchanga, lakini kile ulichouliza kutoka Kwangu ni tani moja ya dhahabu. Je, si wewe unakuwa muhali? Ninafanya kazi miongoni mwenu. Hakuna kabisa dalili ya asilimia kumi ambayo Ninapaswa kupata, sembuse dhabihu za ziada. Zaidi ya hayo, asilimia kumi inayochangwa na wale ambao ni wacha Mungu inachukuliwa na wale waovu. Je, si nyinyi wote mmetawanyika kutoka Kwangu? Je, si nyinyi nyote mna uhasama na Mimi? Je, si nyinyi nyote mnaharibu madhabahu Yangu? Je, mtu wa aina hii anawezaje kuonekana kama hazina machoni Pangu? Je, si yeye ni nguruwe, mbwa ambao Ninawachukia? Ningewezaje kurejelea uovu wenu kama hazina? Kazi Yangu kwa kweli ni ya nani? Inawezekana kuwa tu ni ya kuwapiga nyinyi nyote ili kufichua mamlaka Yangu? Je, si maisha yenu yameshikiliwa na neno moja kutoka Kwangu? Ni kwa nini Ninatumia maneno tu kuwaagiza na Sijayageuza maneno kuwa ukweli ili kuwapiga haraka iwezekanavyo? Je, maneno Yangu na kazi Yangu ni ya kuwapiga wanadamu tu? Je, Mimi ni Mungu ambaye huwaua wasio na hatia bila ubaguzi? Hivi sasa, ni wangapi wenu ambao wako hapo mbele Yangu ambao wanatafuta njia sahihi ya maisha ya mwanadamu na nafsi zao nzima? Ni miili yenu tu iliyo mbele Yangu, lakini mioyo yenu iko huru, na iko mbali, mbali na Mimi. Kwa sababu hamjui kwa kweli kazi Yangu ni nini, kuna baadhi yenu ambao mnataka kuondoka Kwangu, mnaojitenga na Mimi, na mnataka kuishi katika mahali hapo pa raha ambapo hakuna kuadibu, hakuna hukumu. Je, hili ndilo watu wanatamani katika mioyo yao? Mimi hakika sikulazimishi. Njia yoyote utakayoichukua ni uchaguzi wako mwenyewe, na njia ya leo huenda sambamba na hukumu na laana, lakini nyote mnapaswa kujua kwamba kile Niliyowapa, iwe ni hukumu au kuadibu, zote ni zawadi bora kabisa Ninazoweza kuwapa, na vyote ni vitu ambavyo mnahitaji kwa dharura.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni