4. Kueneza kwa Injili ya Ufalme wa Mwenyezi Mungu Nchini China
Mwaka wa 1995, kazi ya kushuhudia kwa injili ya ufalme ya Mwenyezi Mungu ilianza rasmi China Bara. Kwa njia ya shukrani kwa Mungu na kwa upendo ambao ulikuwa wa kweli, tulishuhudia kwa kuoenekana na kazi ya Mwenyezi Mungu kwa ndugu wa kiume na kike katika madhehebu mbalimbali na makundi ya kidini. Hatukutarajia hata kidogo kukumbwa na upinzani na kukashifiwa kulikokithiri kutoka kwa viongozi wao.
Tungeweza tu kuja mbele ya Mwenyezi Mungu kusali kwa ari, tukimsihi Mungu kufanya kazi binafsi. Kutoka 1997 na kuendelea, tulimwona Roho Mtakatifu akifanya kazi kwa kiwango kikubwa. Kulikuwa na ongezeko la haraka la washirika wa makanisa katika maeneo mbalimbali. Wakati huo huo, ishara nyingi na maajabu vilitokea, na watu wengi katika madhehebu mbalimbali na makundi ya kidini yakarudi kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kupokea ufunuo au kuona hizi ishara na maajabu. Kama Roho Mtakatifu hangekuwa amefanya kazi, mtu angefanya nini? Hili lilitufanya kutambua: Ingawa tulielewa baadhi ya ukweli, hatungeweza kutoa ushuhuda kwa Mwenyezi Mungu kwa nguvu zetu za kibinadamu pekee. Baada ya watu hawa kutoka madhehebu mbalimbali na makundi ya kidini kumkubali Mwenyezi Mungu, wao hatua kwa hatua walipata uhakika wa Mwenyezi Mungu katika mioyo yao kupitia kula na kunywa na kufurahia neno la Mwenyezi Mungu, na baada ya muda fulani, kulifanyika ndani yao imani halisi na utii. Watu kutoka kila dhehebu na kundi la kidini kwa hivyo waliinuliwa mbele ya kiti cha enzi, na hawakutarajiwa tena "kukutana na Bwana angani" kama walivyokuwa wamefikiri.
Tungeweza tu kuja mbele ya Mwenyezi Mungu kusali kwa ari, tukimsihi Mungu kufanya kazi binafsi. Kutoka 1997 na kuendelea, tulimwona Roho Mtakatifu akifanya kazi kwa kiwango kikubwa. Kulikuwa na ongezeko la haraka la washirika wa makanisa katika maeneo mbalimbali. Wakati huo huo, ishara nyingi na maajabu vilitokea, na watu wengi katika madhehebu mbalimbali na makundi ya kidini yakarudi kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kupokea ufunuo au kuona hizi ishara na maajabu. Kama Roho Mtakatifu hangekuwa amefanya kazi, mtu angefanya nini? Hili lilitufanya kutambua: Ingawa tulielewa baadhi ya ukweli, hatungeweza kutoa ushuhuda kwa Mwenyezi Mungu kwa nguvu zetu za kibinadamu pekee. Baada ya watu hawa kutoka madhehebu mbalimbali na makundi ya kidini kumkubali Mwenyezi Mungu, wao hatua kwa hatua walipata uhakika wa Mwenyezi Mungu katika mioyo yao kupitia kula na kunywa na kufurahia neno la Mwenyezi Mungu, na baada ya muda fulani, kulifanyika ndani yao imani halisi na utii. Watu kutoka kila dhehebu na kundi la kidini kwa hivyo waliinuliwa mbele ya kiti cha enzi, na hawakutarajiwa tena "kukutana na Bwana angani" kama walivyokuwa wamefikiri.
Tangu injili ya ufalme ilipoanza kuenea, tumewindwa na kuteswa kikatili na serikali ya China. Hata la kusikitisha zaidi, tumetukanwa pia, kusingiziwa, kushutumiwa, na kukataliwa na Kanisa Katoliki na madhehebu yote ya Kikristo na makundi ya kidini. Hili limetusumbua sana, na hata kusitisha kazi ya injili kwa muda. Tukiwa tumekabiliwa na hali hiyo, tulichanganyikiwa tusijue la kufanya; ilikuwa ni kama kwamba tulikuwa tumezingirwa pande zote. Wakati huo huo, tulikemewa maradufu: Tumefurahia wokovu mkuu kutoka kwa Mungu na kuelewa ukweli mwingi, lakini hatuwezi kueneza Injili. Kwa kweli hatustahili kuwa mashahidi wa Mungu, na kwa kweli tumeshindwa kutimiza agizo Lake. Katika hali hii ya mawazo, sote tulihisi kuwa tumeshindwa katika wajibu wetu, hatukujua ni hatua gani ya kuchukua, na hatukujua jinsi ya kujieleza mbele ya Mungu—hata hatukujua jinsi ya kukabiliana na mashauri ya Mungu na imani. Tukiwa tumechanganyikiwa, bado tulihisi kuwa moyo wa Mungu ulikuwa unatuita na kumwita kila kondoo Aliyetaka kumpata. Hivyo, sisi sote tulikuja mbele ya Mungu tukiwa tunawiwa, hatia, na kiu kuomba kwa Mungu na kufungua mioyo yetu kwa Mungu: "Mungu! Tafadhali tupe nguvu na Ututunukie hekima, ili tuweze kuwapata kondoo Wako wote. Mapenzi Yako yafanyike ndani yetu na injili Yako ya ufalme ienezwe. Neno Lako liwalete watu zaidi ndani ya nyumba Yako. Mradi tunaweza kueneza injili Yako, tuko tayari kupitia mateso makubwa zaidi, hata kama itatubidi kuyatoa maisha yetu. Tunaomba tu kwamba ungetupa nguvu zaidi. Tuko radhi kushirikiana na mwongozo Wako hatua kwa hatua. Ee Mungu, kwa sababu kimo chetu ni kidogo na kwa sababu tu wadhaifu, hatuwezi kukamilisha agizo Lako vizuri. Tafadhali zifunge hizo nguvu za uadui ambazo huingilia uenezaji wa injili Yako, Walaani wazawa wa shetani ambao si Wako mwenyewe, viondolee mbali vikwazo vyote ambavyo huzuia uenezaji wa injili Yako, na utufungulie njia.” Tuliamini kwamba maombi yetu yaliyafikia masikio ya Mungu, kwa sababu maombi yetu yalilenga mapenzi ya Mungu na yalifanywa kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Baada ya muda mfupi, Mungu kweli Alifanya kazi kubwa, ambayo ilileta msisimko na furaha kwa kiasi ambacho hatukuwahi kukihisi kabla. Mungu alitufadhili na hekima na kutupa imani na nguvu, hivi kwamba kazi ya injili ilienea kwa haraka na kufikia kilele chake. Kila mmoja wetu alijua, na zaidi ya hayo, kuamini kwamba hii ilikuwa habari njema ambayo Mungu alileta kwetu, na kwamba ilikuwa pia utiwaji moyo na Mungu na thawabu kwetu. Mateso tuliyokuwa tumeyapitia yalilipwa. Katika vina vya mioyo yetu, tulipata hata zaidi ufahamu wa maana ya kweli ya maneno: “Ni Mungu Mwenyewe Pekee Ndiye anayeweza kufanya kazi Yake.” Mungu hakufanya mambo yawe magumu kwetu, na Hakutufanya kutahayari. Alitupa tu majaribu madogo hapo mwanzo. Tukiwa na furaha, tulikuwa na shukurani kwa mwongozo wa Mungu, msaada, na utunzaji na ulinzi kutoka kina cha mioyo yetu. Wakati huo huo, tuliuona pia ukuu wa matendo ya Mungu na utukufu wa tabia ya Mungu; zaidi ya hayo, tuliona haki ya Mungu na kutovumilia Kwake kwa makosa ya mtu, kwa kuwa wakati huo huo wa kumwokoa mtu, Mungu pia Aliwaadhibu maadui wengi waliompinga Yeye. Miongoni mwa viongozi wa madhehebu yote katika majimbo 24 na miji ya manispaa katika China Bara, kuna matukio ya mfano mmoja ya watu kuadhibiwa kwa upinzani wao wenye wayowayo, kumshutumu, na kumkufuru Mwenyezi Mungu. Idadi hii ni kubwa mara nyingi kuliko ile ya watu waliopewa adhabu kwa sababu ya kupinga kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria. Inaweza kuonekana kuwa, katika siku za mwisho, binadamu amepitia upotovu usio na kadiri, na hata ameweka bidii zaidi katika upinzani wake kwa Mungu. Watu wengi sana wameadhibiwa na kuondolewa, jambo ambalo limetimiza kabisa unabii katika Biblia kwamba “Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa.” Kama Roho Mtakatifu hakufanya kazi kubwa kama hiyo, mtu hangekuwa na nguvu za kufanya kazi ya kueneza injili ya ufalme. Kutoka mwanzo hadi mwisho, kazi ya Mungu na kazi ya kueneza injili ya ufalme zimestahimili upinzani wenye wayowayo na mateso ya kikatili kutoka kwa Chama cha Kikomunisti cha Kichina kinachotawala, joka kubwa jekundu. Angalau, zaidi ya laki moja ya watu kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu wametiwa mbaroni na kufungwa, na kuvumilia kila aina ya maangamizi na mateso. Watu wengi sana wanatafutwa na kuwindwa na Chama cha Kikomunisti cha Kichina, bila uwezo wa kurudi nyumbani, wanaweza tu kutangatanga hapa na pale na kutumia fedha kwa ajili ya Mungu. Watu wengi sana wanapelelezwa na wameshindwa kutekeleza wajibu wao. Watu wengi sana wamedhibitiwa na Chama cha Kikomunisti cha Kichina na hawawezi kutoka nje ya nyumba zao. ... Katika kuipinga na kuivunja kazi ya Mungu, serikali ya joka kubwa jekundu imetumia kila aina ya njia za kudharauliwa na kutumia kiasi kikubwa cha rasilimali mkiwemo watu na fedha. Licha ya kumaliza mbinu zake zote mbovu na za kudhuru kisiri, haiwezi kamwe kusimamisha kasi ya kazi ya Mungu. Mungu hutumia werevu kwa vitu vyote katika utumishi kwa utimizaji wa mapenzi yake. Joka kubwa jekundu liko chini kabisa ya mpango wa Mungu, kuwa limeamuriwa hivyo na Mungu ili kulichanganya kabisa, bila njia ya kutoka. Mara nyingi sana, joka kubwa jekundu lilikaribia kutekeleza ukamatwaji wa watu nchini kote, lakini mpango wake ulivurugwa na mpango wa Mungu; mara nyingi sana, joka kubwa jekundu lilitaka kunyoosha mkono wake ili kuliangamiza Kanisa la Mwenyezi Mungu, lakini halikufanikiwa; mara nyingi sana, joka kubwa jekundu lilijaribu kuchukua hatua kubwa zaidi ili kuimaliza kazi ya Mungu, lakini lilishindwa chini ya ukuu na werevu wa Mungu. Wakati kama huo, joka kubwa jekundu lilikata tamaa kwa hasira, lakini halikuwa na mipango ya kutekeleza. Hivyo halikuwa na budi kukubali kuwa lilikuwa na bahati mbaya—Mbingu haisaidii! Ni kweli kwamba Mbingu huharibu Chama cha Kikomunisti cha Kichina! Kutokana na kuenea kwa injili ya ufalme, tumeona uenyezi wa Mungu: Bila kujali jinsi nguvu za Shetani zilivyo katili na jinsi wanavyojiunga ili kuipinga kazi ya Mungu, ni kazi ya bure tu. Katika takriban miaka kumi tu, injili ya ufalme imeenea kotekote katika China Bara. Neno la Mungu na jina la Mungu zimeenea katika mamia ya mamilioni ya kaya, na mamilioni ya watu wamekuja chini ya jina la Mwenyezi Mungu. Miongoni mwa madhehebu mbalimbali katika China Bara, wengi wa wale ambao hufuatilia ukweli na kwa kweli kumtafuta Mungu wamerudi mbele ya Mwenyezi Mungu. Mamilioni ya watu wanafurahia neno la Mwenyezi Mungu, wakipokea kazi ya Mungu na wokovu, na kuyasifu matendo ya ajabu ya Mungu. Mungu amefanya kundi la washindi katika China na Amepata kundi la watu ambao ni wa moyo mmoja na akili moja naye. Hili limefungua njia ya kuonekana kwa Mungu kwa umma. Kazi ya Mungu hatimaye imefika mwisho katika utukufu. Mungu ameanza kuadibu joka kubwa jekundu, na baada ya hapo Ataonekana hadharani kwa kila taifa na sehemu duniani.
Mwaka wa 1992, Mwenyezi Mungu - Kristo wa siku za mwisho—Alianza rasmi kutoa sauti Yake na kusema kwa utambulisho wa Mungu wa asili. Yeye alionyesha mamilioni ya maneno na kabisa alishinda na kuwaokoa watu wa Mungu waliochaguliwa nchini China. Kulifuatiwa na upanuzi wa haraka katika ushuhuda kwa kazi ya Mungu wa siku za mwisho katika China Bara, na kazi ya Roho Mtakatifu ikafuatana na wateule wa Mungu. Watu wengi sana kutoka madhehebu mbalimbali walishindwa na neno la Mungu, wakitambua kuwa lilikuwa ni neno la Mungu kamili na wakawa wameaminishwa kabisa. Kondoo wa Mungu hatimaye walisikia sauti ya Mungu na kurudi mbele ya Mungu. Katika kipindi hiki, Roho Mtakatifu akifanya ishara mbalimbali na maajabu, Akiwaongoza watu wa Mungu waliochaguliwa katika kurejea kwa nyumba ya Mwenyezi Mungu kutoka madhehebu mbalimbali. Kama watu wa Mungu waliochaguliwa walivyorudi siku baada ya siku, madhehebu yote yalianguka na yakakoma kuwepo, na ni kana kwamba dunia nzima ya dini ilikuwa imefutika kabisa.
Wakati wa kuenea kwa injili ya ufalme, kila aina ya mashetani na wapinga Kristo waliokuwa wamempinga Mungu walipata adhabu ya haki ya Mwenyezi Mungu. Hivyo watu waliona tamati ya kwenda kinyume na Mungu. Joka kubwa jekundu lilijaribu kuinyonga na kuimaliza kazi ya Mungu, lakini hatimaye lilishindwa. Nguvu zote mbovu ambazo zilimpinga Mungu ziliaibishwa kabisa, na kushindwa. Joka kubwa jekundu hatimaye limemaliza huduma zake na kuanza kupokea adhabu ya Mungu. Mwenyezi Mungu wakati mmoja Alisema: “Je, unalichukia kwa kweli lile joka kuu jekundu? Unalichukia kwa kweli? Mbona Nimekuuliza mara nyingi? Mbona Nimekuuliza swali hili, mara tena na tena? Kuna picha gani ya joka kuu jekundu katika moyo wako? Picha hiyo imeondolewa? Haumchukulii kwa kweli kama “baba” yako joka hili? Watu wote wanafaa kuona nia Yangu katika maswali Yangu. Sio kuwafanya watu wawe na hasira, au kuchochea uasi kati ya mwanadamu, au ili mwanadamu agundue njia yake mwenyewe, bali ni kuwawezesha watu wajifungue kutoka kwa minyororo ya lile joka kuu jekundu. Ila mtu yeyote asiwe na wasiwasi. Yote yatakamilika na maneno Yangu; hakuna mwanadamu atakayekula, na hakuna mwanadamu anayeweza kufanya kazi ambayo Nitaifanya. Nitaifanya hewa ya nchi yote iwe safi na Nitatoa madoadoa yote ya mapepo duniani. Tayari Nimeanza, na Nitaanzia kazi Yangu ya kuadibu katika nyumba ya lile joka kuu jekundu. Hivyo inaonekana kuwa kuadibu Kwangu kumeifikia dunia nzima, na lile joka kuu jekundu na mapepo yote machafu yatashindwa kuepuka kuadibu Kwangu, kwa kuwa Ninaangazia nchi zote. Kazi Yangu duniani itakapokamilika, hapo ndipo, kipindi cha hukumu Yangu kitakamilika, Nitamuadibu kirasmi lile joka kuu jekundu. Watu Wangu wataona kuadibu Kwangu kwa haki kwa lile joka kuu jekundu, watamwaga sifa zao mbele kwa sababu ya haki Yangu, na milele watalisifu jina Langu takatifu kwa sababu ya haki Yangu. Hivyo basi, utatenda wajibu wako kirasmi, na kirasmi utanisifu katika kila nchi milele na milele! Kipindi cha hukumu kitakapofika kilele, Sitaharakisha kumaliza kazi Yangu, bali Nitajumuisha ndani “ushahidi” wa enzi ya kuadibu na kuruhusu ushahidi huo kuonekana na watu Wangu wote; na katika haya kutazaliwa matunda mengi zaidi. “Ushahidi’ huu ndio njia ambayo Nitaadibu lile Joka kuu jekundu, na Nitafanya watu Wangu kuliona kwa macho yao ili wajue zaidi kuhusu tabia Yangu. Wakati watu Wangu wananifurahia ni wakati lile joka kuu jekundu linaadibiwa. Kuwafanya wale watu wa lile joka kubwa jekundu kusimama na kuasi joka hilo ndiyo nia Yangu, na ndiyo njia ambayo Nitawafanya wakamilifu watu Wangu, na ni nafasi nzuri ya watu Wangu kukua maishani.”
Kuenea kwa injili ya ufalme kumefikia hali isiyo na kifani. Mamilioni ya watu wamekuja chini ya jina la Mwenyezi Mungu. Jina la Mwenyezi Mungu limeenea kotekote China Bara, na makanisa ya Mwenyezi Mungu yameonekana katika kila mkoa na kanda. Wale wote ambao wameikubali kazi ya Mwenyezi Mungu wanafurahia uchungaji wa neno la Mungu na kupitia kazi ya Mungu ya wokovu. Kama vile Mwenyezi Mungu alisema: “Katika ulimwengu mzima Mimi Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, kutikisa dini zote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo iliyoleta watu katika wakati wa sasa. Nimeiwacha sauti Yangu kuwa inayowashinda wanadamu; wote wanaingia katika mkondo huu na wote wananyenyekea mbele Zangu, kwa maana Mimi kwa muda mrefu uliopita Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote na Nikaupeleka upya Mashariki. Ni nani asiye na hamu ya kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuuona uzuri Wangu? Ni nani asiyetaka kuja kwenye mwanga? Ni nani asiyeona utajiri wa Kanaani? Ni nani asiyengoja kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mkuu Mwenyezi? Sauti Yangu lazima ienee kote duniani; Ningependa kuzungumza zaidi na watu Wangu wateule. Maneno Ninayotamka yanatikisa milima na mito kama radi yenye nguvu; Nasema na ulimwengu wote na kwa watu wote. Hivyo maneno Yangu yanakuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni jinsi kwamba mtu huchukia kuyaacha na pia kuyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote, mwanadamu anayafurahia. Kama watoto wachanga waliozaliwa karibuni, watu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu. Kwa sababu ya sauti Yangu, Nitawaleta watu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia kirasmi kati ya wanadamu ili waje kuniabudu Mimi. Utukufu Ninaotoa na maneno Yangu yatawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki, na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye "Mlima wa Mizeituni" wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari kwa muda mrefu Nimekuwa duniani, si tena Mwana wa Wayahudi lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwa maana ni muda mrefu tangu Nimekwishafufuka, Nimekwenda kutoka miongoni mwa wanadamu, na Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu kwa utukufu. Mimi ndiye Nilichiwa kabla ya enzi, na "mtoto mchanga" aliyeachwa na Israeli kabla ya enzi. Aidha, Mimi ndimi mwenye utukufu wote mtukufu Mwenyezi Mungu wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, kusikia sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vilevile madhumuni ya usimamizi Wangu. Basi kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na kila mtu awe mmoja wa wale walio chini Yangu!”
Kazi ya Mungu katika China Bara hatimaye imeishia katika utukufu. Mungu Yu karibu kuonekana kwa umma kwa kila taifa na sehemu. Wale katika kila taifa na sehemu ambao walitamania kuonekana kwa Mungu kamwe hawakufikiri kwamba Mungu waliyemtamania sana kuonekana kwa umma tayari Amekuja kwa siri China na kutekeleza hatua moja ya kazi ya ushindi na wokovu. Kuna watu wengi ambao bado wanahukumu kazi ya Mungu katika China, na watu wengi ambao bado wanakufuru dhidi ya kazi ya Roho Mtakatifu pale. Ni wakati tu Mungu Atakapoonekana hadharani ndipo watakapozinduka kama kutoka kwa ndoto, na kujawa na majuto: Sikufikiri kwamba Mwenyezi Mungu niliyempinga ndiye Bwana Yesu ambaye amekuja tena. Lakini wanaweza tu kulia na kusaga meno yao. Hili limetimiza kabisa maneno ya Ufunuo wa Biblia: “Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake.” Hukumu ya kiti kikubwa cheupe cha enzi hatimaye imeanza.
Mwenyezi Mungu alisema: “Katika ufalme, vitu vingi visivyohesabika vya uumbaji vinaanza kufufuka na kupata nguvu ya maisha yao. Kwa sababu ya mabadiliko katika hali ya dunia, mipaka kati ya nchi moja na nyingine pia inaanza kusonga. Hapo awali, Nimetabiri: Wakati ardhi itagawanywa kutoka kwa ardhi, na ardhi kujiunga na ardhi, huu ndio utakuwa wakati ambao Nitayapasua mataifa kuwa vipande vidogo. Katika wakati huu, Nitafanya upya uumbaji wote na kuugawa tena ulimwengu mzima, hivyo kuweka ulimwengu katika mpangilio, Nikibadilisha hali yake ya awali kuwa mpya. Huu ndio mpango Wangu. Hii ni kazi Yangu. Wakati mataifa na watu wa dunia watakaporudi mbele ya kiti Changu cha enzi, basi Nitachukua fadhila ya mbinguni na kuiweka kwa sababu ya ulimwengu wa binadamu, ili, kwa mujibu Wangu, itajazwa na fadhila isiyo ya kufananisha. Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikipitisha wazi amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta adhabu kwa yeyote anayeyakiuka: Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapata adhabu Yangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadhibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa viwango tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa “Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe.” Binadamu wote watafuata aina yao, na watapokea adhabu itakayotofautiana kulingana na walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni