Sura ya 1 Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Ambaye Aliumba Kila kitu
1. Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Anayetawala Juu ya Vitu Vyote
Maneno Husika ya Mungu:
Yote yaliyo duniani humu yanabadilika haraka sawasawa na mawazo ya Mwenye uweza, na chini ya macho Yake. Mambo ambayo wanadamu hawajawahi kuyasikia yanaweza kuja kwa ghafla, ilhali vitu ambavyo wanadamu wamemiliki kwa muda mrefu vinaweza kutoweka bila wao kujua.
Hakuna anayeweza kutambua mahali alipo Mwenye uweza sembuse yeyote kuweza kuhisi kuzidi uwezo wa mwanadamu na ukuu wa nguvu za uzima za Mwenye uweza. Anazidi uwezo wa mwanadamu kwa vile Anavyoweza kufahamu yale ambayo wanadamu hawawezi. Yeye ni mkuu kwa vile ni Yeye anayekataliwa na wanadamu na bado Anawaokoa wanadamu. Yeye anajua maana ya maisha na mauti na, isitoshe, Anajua ni kanuni gani zinazofaa katika kuongoza uwepo wa wanadamu Aliowaumba. Yeye ndiye msingi ambao kwao uwepo wa wanadamu hutegemea, na ndiye Mkombozi ambaye hufufua wanadamu tena. Yeye huilemea mioyo yenye furaha kwa huzuni na kuiinua mioyo yenye huzuni kwa furaha, yote kwa ajili ya kazi Yake, na kwa ajili ya mpango Wake.
kutoka katika “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni viumbe wangapi wanaoishi na kuzaana katika ulimwengu mpana, wakifuata sheria ya maisha tena na tena, wakifuata sheria isiyobadilika. Wanaokufa huenda na hadithi za walio hai, na walio hai hurudia historia hii yenye huzuni ya wale waliokufa. Na kwa hivyo wanadamu hawawezi kujizuia ila kujiuliza wenyewe; Kwa nini tunaishi? Na kwa nini inatulazimu kufa? Nani anayeitawala dunia hii? Na ni nani muumbaji wa mwanadamu? Je, kweli wanadamu waliumbwa na mazingira asilia? Je, kweli wanadamu wana uamuzi juu ya hatima yao? … Kwa maelfu ya miaka wanadamu wameyauliza haya maswali, tena na tena. Kwa bahati mbaya, jinsi wanadamu wanavyopagawa na haya maswali, ndivyo kiu yao ya sayansi huendelea kukua. Sayansi hupatiana kutosheleza kwa muda na raha ya muda ya mwili, ila haitoshi kumpa mwanadamu uhuru kutokana na upweke, ukiwa, na hofu isiyodhihirika na kutosaidika ndani ya moyo wake. Wanadamu hutumia ujuzi wa kisayansi unaoweza kuonekana kwa macho na ambao akili zaweza kuufahamu kutuliza moyo wake, na bado hili haliwezi kuwazuia wanadamu kutafiti yasiyofahamika. Wanadamu hawajui ni nani Mkuu wa kila kitu katika ulimwengu huu, aidha hajui mwanzo na mustakabali wa wanadamu. Wanadamu wanaishi tu, bila budi, katikati ya hii sheria. Hakuna anayeweza kuiepuka wala kuibadilisha kwani katika vitu vyote na katika mbingu kuna Mmoja kutoka milele hadi milele ambaye ni Mkuu wa kila kitu. Ni Yeye ambaye Hajawahi kuonekana na mwanadamu, ambaye wanadamu hawajawahi kumjua, ambaye wanadamu hawajawahi kuamini kuwepo Kwake, na bado ni Yeye Aliyewapulizia pumzi mababu wa wanadamu na kuwapa wanadamu uhai. Ni Yeye ndiye Huruzuku na kustawisha wanadamu kwa kuishi kwao, na huwaongoza wanadamu hadi siku ya leo. Aidha, Yeye na Yeye pekee ni wa kutegemewa na wanadamu ili kuendelea kuishi. Ni Mkuu wa kila kitu na Hutawala viumbe vyote vyenye uhai chini ya dunia. Huamrisha misimu yote minne, na ni Yeye huita upepo, jalidi, theluji na mvua. Huwapa wanadamu mwangaza wa jua na huleta machweo ya jioni. Ni Yeye Aliyeumba mbingu na ardhi, Akampa mwanadamu milima, maziwa na mito na kila kitu kilicho na uhai ndani yake. Matendo Yake yamo kila mahali, nguvu Zake ziko kila mahali, busara Zake ziko kila mahali na mamlaka Yake yako kila mahali. Kila mojawapo ya hizi sheria na kanuni ni mfano mzuri wa matendo Yake, na kila mojawapo inafichua hekima na mamlaka Yake. Nani anayeweza kujiondoa kutoka kwa ukuu Wake? Na ni nani anayeweza kujitoa mwenyewe katika njia Zake? Kila kitu kinaishi chini ya uangalizi Wake, zaidi ya hayo, kila kitu huishi chini ya ukuu Wake. Matendo na nguvu Zake huwaacha wanadamu bila chaguo ila kutambua ukweli kwamba ni Yeye pekee Anayeishi na Ana ukuu juu ya kila kitu. Hakuna kitu chochote ila Yeye kinachoweza kuamuru dunia, wala kuwajibikia wanadamu bila kukoma. Bila kujali kama unaweza kutambua vitendo vya Mungu, bila kujali kama unaamini katika kuwepo kwa Mungu, hakuna shaka kuwa hatima yako inaegemea katika mipango ya Mungu, na hakuna shaka kuwa Mungu atakuwa na ukuu juu ya kila kitu. Uwepo na utawala Wake haviwezi kutabiriwa ikiwa vinatambulika na kufahamika na binadamu au la. Ni Yeye pekee Anayejua kuhusu yaliyopita ya mwanadamu, yaliyomo na yanayojiri, na Yeye pekee ndiye mwamuzi wa hatima ya wanadamu. Haijalishi kama unaukubali huu ukweli, haitachukua muda mrefu kabla mwanadamu kushuhudia haya yote kwa macho yake mwenyewe, na huu ni ukweli ambao hivi karibu Mungu Ataudhihirisha. Wanadamu huishi na hufa chini ya macho yake Mungu. Wanadamu huishi kwa usimamizi wa Mungu, na wakati macho Yake yatafumbika kwa mara ya mwisho, hio pia ni kwa usimamizi Wake. Tena na tena, mwanadamu huja na kwenda, nyuma na mbele. Bila mapendeleo, yote ni sehemu ya ukuu na michoro ya Mungu. Usimamizi wa Mungu ungali unaendelea mbele na haujawahi kusimama. Atawafanya wanadamu wafahamu uwepo Wake, waamini katika ukuu Wake, watazame matendo Yake, na warudi katika ufalme Wake. Huu ni mpango Wake, na kazi ambayo Amekuwa Akiitekeleza kwa maelfu ya miaka.
kutoka katika “Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee” katika Neno Laonekana katika Mwili
Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa. Mungu kamwe hajawahi kosa kwa moyo wa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa binadamu wakati wote. Amekuwa nguvu ya kuendesha maisha ya mwanadamu, chanzo cha kuwepo kwa binadamu, na amana ya fahari ya kuwepo kwa binadamu baada ya kuzaliwa. Husababisha binadamu kuzaliwa upya, na kumwezesha kwa ushupavu kuishi kwa kila jukumu lake. Kwa sababu ya uwezo Wake, na nguvu ya maisha Yake yasiyopungua, binadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, ambapo nguvu ya uhai wa Mungu umekuwa uti wa mgongo wa kuwepo kwa binadamu, na ambayo Mungu amelipia gharama ambayo hakuna mtu wa kawaida amewahi kulipa. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha si rahisi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za maisha ya Mungu zipo, na hung’aa mwangaza wake ulio mzuri sana, bila ya kujali muda au mahali. Maisha ya Mungu, huishi milele bila kubadilika katika kusumbuka kwa mbingu na nchi. Mambo yote hupita, lakini maisha ya Mungu hubaki, kwa maana Mungu ni chanzo cha kuwepo kwa mambo yote, na mizizi ya kuwepo kwao. Asili ya maisha ya mwanadamu hutoka kwa Mungu, kuwepo kwa mbingu ni kwa sababu ya Mungu, na kuwepo kwa ardhi kunatokana na nguvu ya uhai wa Mungu. Hakuna kitu kinachomiliki nguvu kinachoweza kuzidi ukuu wa Mungu, na hakuna kitu chenye nguvu kinachoweza kuvunja mipaka ya mamlaka ya Mungu. Kwa njia hii, bila kujali wao ni nani, kila mtu lazima ajiwasilishe kwa utawala wa Mungu, kila mtu lazima aishi chini ya amri za Mungu, na hakuna mtu anayeweza kutoroka kutoka katika utawala Wake.
kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kabla ya binadamu hawa kujitokeza, viumbe vyote—sayari zote, nyota zote kule mbinguni—tayari vilikuwepo. Kwenye kiwango cha vitu vikubwa, vyombo hivi vya mbinguni vimekuwa vikizunguka mara kwa mara chini ya udhibiti wa Mungu, kwa uwepo wavyo wote, hata hivyo miaka mingi imepita. Ni sayari gani inaenda wapi na wakati gani haswa; ni sayari gani inafanya kazi gani, na lini; ni sayari gani inazunguka katika mzingo gani, na ni lini inatoweka au inabadilishwa—vitu hivi vyote vinasonga mbele bila ya kosa lolote dogo. Nafasi za sayari na umbali kati yazo ni masuala yanayofuata ruwaza maalum, ni masuala ambayo yanaweza kufafanuliwa kwa data yenye uhakika; njia ambazo zinasafiria, kasi na ruwaza ya mizingo yao, nyakati ambapo zinapatikana kwenye nafasi mbalimbali zinaweza kufafanuliwa kwa hakika na kufafanuliwa kwa sheria maalum. Kwa miaka na mikaka sayari zimefuata sheria hizi na hazijawahi kupotoka hata chembe. Hakuna nguvu inaweza kubadilisha au kutatiza mizingo yazo au ruwaza zao ambazo zinafuata. Kwa sababu sheria maalum zinazotawala mzunguko wazo na data yenye uhakika inayozifafanua iliamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba, zinatii sheria hizi zenyewe, kulingana na ukuu na udhibiti wa Muumba. Kwenye kiwango cha mambo makubwamakubwa, si vigumu kwa binadamu kujua zaidi kuhusu ruwaza fulani, data fulani, pamoja na sheria au matukio fulani yasiyoeleweka au yasiyoelezeka. Ingawaje binadamu hawakubali kwamba Mungu yupo, haukubali hoja kwamba Muumba aliumba na anatawala kila kitu na zaidi ya yote hautambui uwepo wa mamlaka ya Muumba, wanasayansi wa kibinadamu, wanafalaki, nao wanafizikia wanachunguza na kugundua zaidi na zaidi kwamba uwepo wa kila kitu kwenye ulimwengu, na kanuni na ruwaza zinazoonyesha mzunguko wavyo, vinatawaliwa na kudhibitiwa na nishati nyeusi kubwa na isiyoonekana. Hoja hii inampa binadamu mshawasha wa kukubaliana na kutambua kwamba kunaye Mwenyezi aliye miongoni mwa ruwaza hizi za mzunguko, anayepangilia kila kitu. Nguvu zake si za kawaida, na ingawaje hakuna anayeweza kuona uso Wake wa kweli, Yeye hutawala na kudhibiti kila kitu kila dakika. Hakuna binadamu au nguvu zozote zile zinazoweza kuuzidi ukuu Wake. Huku binadamu akiwa amekabiliwa na hoja hii, lazima atambue kwamba sheria zinazotawala uwepo wa kila kitu haziwezi kudhibitiwa na binadamu, haziwezi kubadilishwa na yeyote; na wakati uo huo binadamu lazima akubali kwamba, binadamu hawezi kuelewa kikamilifu sheria hizi. Na hizi sheria hazitokei kiasili lakini zinaamrishwa na Bwana na Mungu. Haya yote ni maonyesho na mamlaka ya Mungu yanayoonyesha kwamba mwanadamu anaweza kuelewa katika kiwango cha mambo makubwa.
Kwenye kiwango cha mambo madogomadogo, milima, mito, maziwa, bahari, na maeneo ya ardhi yote ambayo binadamu anatazama nchini, misimu yote ambayo yeye anapitia, mambo yote yanayopatikana kwenye ulimwengu, kukiwemo mimea, wanyama, vijiumbe na binadamu, vyote viko chini ya ukuu wa Mungu na vinadhibitiwa na Mungu Mwenyewe. Katika ukuu na udhibiti wa Mungu, vitu vyote vinakuwepo au vinatoweka kulingana na fikira Zake, maisha ya vitu hivi yanatawaliwa na sheria fulani, na vinakua na kuzaana kulingana nazo. Hakuna binadamu au kiumbe chochote kilicho juu ya sheria hizi.
kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu alipoviumba vitu vyote, Aliweka mipaka kwa ajili ya milima, tambarare, majangwa, vilima, mito, na maziwa. Duniani kuna milima, tambarare, majangwa, vilima, vilevile vyanzo mbalimbali vya maji. Je, hayo si mandhari tofautitofauti? Mungu aliweka mipaka kati ya mandhari haya yote tofautitofauti. Tunapozungumza juu ya kuweka mipaka, ina maana kwamba milima ina mipaka yake, tambarare zina mipaka yake, majangwa yana mawanda fulani, na vilima vina eneo mahususi. Pia kuna kiwango mahususi cha vyanzo vya maji kama vile mito na maziwa. Yaani, Mungu alipoumba vitu vyote aligawanya kila kitu vizuri kabisa. … Ndani ya mandhari haya yote tofautitofauti na mazingira ya kijiografia yaliyoumbwa na Mungu, Anasimamia kila kitu kwa njia iliyopangwa na kwa mpangilio. Kwa hiyo mazingira haya yote ya kijiografia bado yapo kwa miaka elfu kadhaa, makumi elfu ya miaka baada ya kuwa yameumbwa na Mungu. Bado yanatimiza kila wajibu wao. Ingawa wakati wa vipindi fulani volkano hulipuka, wakati wa vipindi fulani matetemeko ya ardhi hutokea, na kuna mabadiliko makubwa ya ardhi, hakika Mungu hataruhusu aina yoyote ya mandhari kupoteza kazi yake ya asili. Ni kwa sababu tu ya usimamizi huu unaofanywa na Mungu, utawala Wake na udhibiti wa sheria hizi, kwamba yote haya—yote haya yanayofurahiwa na binadamu na kuonwa na binadamu—yanaweza kuendelea kuishi duniani kwa njia ya mpangilio.
…………
… kando na kuanzisha mipaka kwa ajili ya mazingira mbalimbali ya kijiografia, Mungu pia Aliweka mipaka kwa ajili ya ndege na wanyama, samaki, wadudu mbalimbali, na mimea yote. Pia alianzisha sheria. Kwa sababu ya tofauti za mazingira mbalimbali ya kijiografia na kwa sababu ya uwepo wa mazingira tofauti ya kijiografia, aina tofautitofauti za ndege na wanyama, samaki, wadudu, na mimea vina mazingira tofauti kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ndege na wanyama na wadudu wanaishi miongoni mwa mimea, samaki wanaishi majini, na mimea inakua kwenye nchi kavu. … vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu—haijalishi kama vimewekwa katika sehemu moja au vinapumua kupitia mapua—vyote vina sheria zao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Zamani kabla Mungu hajaumba viumbe hai hivi Alikuwa ameviandalia makazi yao, mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai hivi vilikuwa na mazingira yao yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi, chakula chao, makazi yao yasiyobadilika, sehemu zao zisizobadilika zinazowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi, maeneo yenye halijoto inayowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa njia hiyo wasingezungukazunguka au kuhafifisha hali ya mwanadamu kuendelea kuishi au kuathiri maisha yao. Hivi ndivyo Mungu anavyosimamia viumbe vyote. Ni kumwandalia binadamu mazingira mazuri kabisa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai chini ya viumbe vyote kila kimoja kina chakula kinachokimu maisha ndani ya mazingira yao wenyewe kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa chakula hicho, vinajifunga katika mazingira yao ya asili kwa ajili ya kuendelea kuishi. Katika aina hiyo ya mazingira bado vinaendelea kuishi, kuzaliana, na kuendelea kulingana na sheria za Mungu alizozianzisha kwa ajili yao. Kwa sababu ya aina hizi za sheria, kwa sababu ya majaaliwa ya Mungu, viumbe vyote vinaingiliana na binadamu kwa upatanifu, na binadamu na viumbe vyote vinategemeana.
kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX” katika Neno Laonekana katika Mwili
Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Kwa kuchukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu Wake, unaanza safari yako katika maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeunda, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake mwenyewe, kwa maana yule Anayetawala kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa akitenda kazi Yake kwa njia hii, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mifuatano ya mabadiliko katika mambo yote na njia ambazo yanasongea. Pamoja na vitu vyote vingine, mwanadamu polepole na bila kujua anastawishwa na utamu na mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote vingine, mwanadamu bila kujua, anaishi chini ya mpango wa mkono wa Mungu. Moyo na roho ya mwanadamu vimeshikwa katika mkono wa Mungu, na maisha yake yote yanatazamwa machoni mwa Mungu. Haijalishi kama unayaamini mambo haya au la, vitu vyote, viwe hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, kufanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hii ndiyo njia ambayo Mungu huongoza vitu vyote.
Usiku uingiapo polepole, mwanadamu huwa hafahamu, kwani moyo wa mwanadamu hauwezi kujua jinsi giza linapokaribia au wapi linakotoka. Usiku unapotoweka polepole, mwanadamu hukaribisha mwanga wa mchana, lakini ikija kwa kulikotoka nuru na jinsi imeliondoa giza la usiku, mwanadamu anajua hata machache na hata ana ufahamu mchache zaidi Mabadiliko haya ya kawaida ya mchana na usiku humpitisha mwanadamu kutoka kipindi kimoja hadi kingine, kutoka kipindi kimoja cha kihistoria hadi kingine, wakati huu wote yakihakikisha kwamba kazi ya Mungu katika kila kipindi na mpango Wake wa kila enzi unatekelezwa.
kutoka katika “Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Tangu uumbaji wa ulimwengu Nimeanza kuamulia kabla na kuchagua kundi hili la watu, yaani, ninyi leo. Tabia yako, ubora wa tabia, sura, kimo, familia ambayo ulizaliwa kwayo, kazi yako na ndoa yako, nafsi yako yote, hata rangi ya nywele yako na ngozi yako, na wakati wa kuzaliwa kwako vyote vilipangwa na mikono Yangu. Hata mambo unayofanya na watu unaokutana nao kila siku hupangwa na mikono Yangu, sembuse ukweli kwamba kukuleta katika uwepo Wangu leo kwa kweli ni mpango Wangu. Usijitupe katika vurugu; unapaswa kuendelea kwa utulivu.
kutoka katika “Sura ya 74” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Hatima za binadamu na zile za ulimwengu zimeingiliana kwa ndani na ukuu wa Muumba, zimefungamanishwa na haziwezi kutenganishwa na mipango ya Muumba; na hatimaye, haziwezi kutenganishwa na mamlaka ya Muumba. Kupitia kwenye sheria za mambo yote binadamu huja kuelewa mipango ya Muumba na ukuu Wake; kupitia kwenye sheria za namna ya kuishi ambazo anaona katika utawala wa Muumba; kutoka kwenye hatima za mambo yote anapata hitimisho kuhusu njia ambazo Muumba huonyesha ukuu Wake na kuvidhibiti; na kwenye mzunguko wa maisha ya binadamu na mambo yote ambayo binadamu kwa kweli hupitia ile mipango na mipangilio ya Muumba kwa mambo yote na kwa viumbe vyote vilivyo hai na anashuhudia kwa kweli namna ambavyo mipango na mipangilio hiyo inavyozidi sheria zote za nchi, kanuni, na taasisi, mamlaka na nguvu zote nyingine. Kwa mujibu wa haya, binadamu wanashawishiwa kutambua kwamba, ukuu wa Muumba hauwezi kukiukwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, kwamba hakuna nguvu zinazoweza kuharibu au kubadilisha matukio na mambo yaliyoamuliwa kabla na Muumba. Ni kupitia kwenye sheria na kanuni hizi takatifu ambapo binadamu na viumbe vyote wanaweza kuishi na kuzalisha, kizazi baada ya kizazi. Je, huu si mfano halisi wa mamlaka ya Muumba?
kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili
(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)
Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote
Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wa sisi wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya kusudi la haki la mwanadamu, basi nafsi zetu hazina thamani kwa wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo la Mungu, na thamani ndogo zaidi kwa Mungu, aliyetupa kila kitu.
Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa muasisi wa utamaduni wa zamani wa Giriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu tu anayemfariji huyu mwanadamu, na ni Mungu tu anayemtunza mwanadamu huyu usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatengani na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu ni zisizochangulika kutoka kwa miundo ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu. Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga.
Angalia nyuma wakati wa safina ya Nuhu: Wanadamu walikuwa wapotovu sana, walikuwa wamepotea kutoka katika baraka za Mungu, hawakuwa wanatunzwa na Mungu tena, na walikuwa wamepoteza ahadi za Mungu. Waliishi gizani, bila mwangaza wa Mungu. Hivyo wakawa waasherati kwa asili, wakajiachilia katika mkengeuko wa kutisha. Watu kama hao hawangeweza tena kupokea ahadi za Mungu; hawakufaa kushuhudia uso wa Mungu, wala kusikia sauti ya Mungu, kwani walikuwa wamemwacha Mungu, kuweka kando yote Aliyowapa, na kusahau mafunzo ya Mungu. Mioyo yao ilipotea mbali zaidi na zaidi na Mungu, na ilivyofanya hivyo, wakawa wapotovu zaidi ya mantiki na ubinadamu wote na wakazidi kuwa waovu. Hivyo walikaribia kifo zaidi, na kukabiliwa na ghadhabu na adhabu ya Mungu. Ni Nuhu tu aliyemwabudu Mungu na kuepukana na uovu, na hivyo aliweza kusikia sauti ya Mungu, na kusikia maelekezo ya Mungu. Alijenga safina kulingana na maelekezo ya neno la Mungu, na kukusanya aina yote ya viumbe hai. Na kwa njia hii, wakati kila kitu kilikuwa kimetayarishwa, Mungu aliangamiza dunia. Nuhu tu na wanachama saba wa familia yake walinusurika maangamizi, kwani Nuhu alimwabudu Yehova na kuepukana na uovu.
Kisha angalia enzi ya sasa: Hawa watu wenye haki kama Nuhu, ambao wangeweza kumwabudu Mungu na kuepuka uovu, wamekoma kuwepo. Lakini bado Mungu ana fadhili kwa mwanadamu huyu, na Anamsamehe mwanadamu wakati huu wa enzi ya mwisho. Mungu anawatafuta wanaomtaka Yeye ajitokeze. Anawatafuta wale wanaoweza kuyasikia maneno Yake, wale ambao hawajasahau agizo Lake na wanatoa mioyo na miili yao Kwake. Anawatafuta wale walio watiifu kama watoto wachanga mbele Yake, na hawampingi. Kama hujazuiliwa na nguvu zozote katika ibada yako Kwake, basi Mungu atakutazama na neema, na kukupea baraka Zake. Kama wewe ni wa daraja la juu, wa sifa ya heshima, aliyemiliki maarifa mengi, mmiliki wa mali nyingi, na kuungwa mkono na watu wengi, lakini mambo haya hayakuzuii kuja mbele za Mungu kuukubali wito Wake na agizo Lake, kufanya kile Mungu anachokuambia ufanye, basi yote unayoyafanya yatakuwa yenye umuhimu zaidi duniani na yenye haki zaidi ya binadamu. Ukiukataa wito wa Mungu kwa sababu ya hadhi yako na malengo yako mwenyewe, yote utakayoyafanya yatalaaniwa na hata kudharauliwa na Mungu. Labda wewe ni rais, ama mwanasayansi, ama mchungaji, ama mzee, lakini bila kujali ukuu wa ofisi yako, ukitegemea maarifa yako na uwezo katika shughuli zako, basi daima utakuwa wa kushindwa na kamwe utanyimwa baraka za Mungu, kwa sababu Mungu hakubali chochote unachofanya, na Hakubali kwamba kazi yako ni yenye haki, wala kukubali kwamba unafanya kazi kwa msaada wa mwanadamu. Atasema yote unayofanya, ni ya kutumia maarifa na nguvu za mwanadamu kumvulia mwanadamu ulinzi wa Mungu na kumnyima baraka za Mungu. Atasema kuwa unamwongoza mwanadamu kuelekea gizani, kuelekea kifo, na kuelekea mwanzo wa kuwepo bila mipaka ambapo mwanadamu amempoteza Mungu na baraka Zake.
Kutoka wakati mwanadamu kwanza alikuwa na sayansi ya jamii, akili yake ilishughulishwa na sayansi na maarifa. Kisha sayansi na maarifa vikawa vyombo vya kutawala mwanadamu, na hapakuwa tena na nafasi ya kutosha kumwabudu Mungu, na hapakuwa tena na mazingira mazuri ya kumwabudu Mungu. Nafasi ya Mungu ikashuka hata chini zaidi moyoni mwa mwanadamu. Dunia moyoni mwa mwanadamu bila nafasi ya Mungu ni giza, tupu bila matumaini. Na hivyo kukatokea wanasayansi wa jamii, wataalamu wa historia na wanasiasa wengi kueleza nadharia ya sayansi ya jamii, nadharia ya mageuko ya binadamu, na nadharia nyingine zinazopinga ukweli kwamba Mungu alimuumba mwanadamu, kujaza moyo na akili ya mwanadamu. Na kwa njia hii, wanaoamini kwamba Mungu aliumba kila kitu wanakuwa wachache zaidi, na wale wanaoamini nadharia ya mageuko wanakuwa hata wengi kwa nambari. Watu zaidi wanachukulia rekodi za kazi ya Mungu na maneno Yake wakati wa enzi ya Agano la Kale kuwa hadithi na hekaya. Kwa mioyo yao, watu wanakuwa wasiojali heshima na ukubwa wa Mungu, kwa imani kwamba Mungu yupo na anatawala kila kitu. Kusalia kwa mwanadamu na majaliwa ya nchi na mataifa si muhimu kwao tena. Mwanadamu anaishi katika dunia tupu akijishughulisha tu na kula, kunywa, na ufuatiliaji wa furaha. … Watu wachache wanashughulika kutafuta Afanyapo Mungu kazi Yake leo, ama kutafuta jinsi Anavyoongoza na kupanga majaliwa ya mwanadamu. Na kwa njia hii, ustaarabu wa ubinadamu bila fahamu ukawa huwezi kukutana na matakwa ya mwanadamu hata zaidi, na hata kuna watu zaidi wanaohisi kwamba, kuishi kwa dunia kama hii, wanayo furaha ya chini kuliko watu walioenda. Hata watu wa nchi zilizokuwa na ustaarabu wa juu wanaeleza malalamiko haya. Kwani bila mwongozo wa Mungu, bila kujali jinsi viongozi na wanasosiolojia wanatafakari kuhifadhi ustaarabu wa binadamu, haina mafanikio. Hakuna anayeweza kujaza utupu kwa moyo wa mwanadamu, kwani hakuna anayeweza kuwa uhai wa mwanadamu, na hakuna nadharia ya kijamii inayoweza kumwokoa kutokana na utupu unaomtesa. Sayansi, maarifa, uhuru, demokrasia, wasaa wa mapumziko, faraja, haya yote ni mapumziko ya muda, Hata na mambo haya, mwanadamu hataepuka kufanya dhambi na kuomboleza udhalimu wa jamii. Mambo haya hayawezi kupunguza tamaa ya mwanadamu na hamu ya kuchunguza. Kwa sababu mwanadamu aliumbwa na Mungu na kafara na uchunguzi usio na sababu wa mwanadamu vitamwongoza tu kwa dhiki zaidi. Mwanadamu daima atakuwa katika hali ya hofu isiyoisha, hatajua jinsi ya kuukabili mustakabali wa wanadamu, ama jinsi ya kuikabili njia iliyo mbele. Mwanadamu atakuja hata kuogopa sayansi na elimu, na kuhofia hata zaidi utupu ulio ndani yake sana. Duniani humu, bila kujali kama unaishi katika nchi huru ama isiyo na haki za binadamu, huwezi kabisa kuponyoka majaliwa ya mwanadamu. Kama wewe ni kiongozi ama anayeongozwa, huwezi kabisa kuponyoka hamu ya kuchunguza majaliwa, siri na majaliwa ya mwanadamu. Chini ya hayo, huna uwezo wa kutoroka hisia ya utupu inayotatiza. Matukio kama haya, yaliyo kawaida kwa wanadamu wote, yanaitwa matukio ya kijamii na wanasosiolojia, lakini hakuna mtu mkubwa anayeweza kuja mbele kutatua shida kama hizi. Mwanadamu, hata hivyo, ni mwanadamu. Nafasi na maisha ya Mungu hayawezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Mwanadamu hahitaji tu jamii iliyo na haki, ambapo kila mtu analishwa vyema na ana uhuru na usawa, lakini wokovu wa Mungu na Yeye kuwapa uhai. Wakati tu mwanadamu atapokea wokovu wa Mungu na kupatiwa uhai na Yeye ndipo mahitaji, hamu ya kuchunguza, na utupu wa kiroho wa mwanadamu utaweza kutatuliwa. Iwapo watu wa nchi ama taifa hawawezi kupokea wokovu na utunzaji wa Mungu, basi nchi ama taifa kama hilo litatembelea njia inayoelekea uharibifuni, inayoelekea gizani, na litaangamizwa na Mungu.
Labda nchi yako inafanikiwa sasa, lakini ukiruhusu watu wako kupotea kutoka kwa Mungu, basi nchi yako itazidi kujipata bila baraka za Mungu. Ustaarabu wa nchi yako utazidi kukanyagiwa chini, na kabla ya muda mrefu watu watamwasi Mungu na kulaani Mbingu. Na hivyo, bila kujulikana kwa mwanadamu, majaliwa ya nchi yataletwa kwa uharibifu. Mungu ataziinua nchi zenye nguvu ili kukabiliana na nchi hizo zilizolaaniwa na Mungu, na anaweza hata kuzifuta kutoka uso wa dunia. Kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa kunategemea kama viongozi wao wanamwabudu Mungu, na kama wanawaongoza watu wao karibu na Mungu na kumwabudu. Lakini, kwa hii enzi ya mwisho, kwa sababu wale wanaomtafuta Mungu kwa kweli na kumwabudu wanazidi kuwa wachache, Mungu anaweka fadhili ya pekee juu ya nchi ambapo Ukristo ni dini ya serikali. Anazikusanya pamoja kuunda kambi ya haki kiasi ya dunia, wakati nchi zikanazo Mungu ama zile zisizomwabudu Mungu wa kweli zinakuwa wapinzani wa kambi ya haki. Kwa njia hii, Mungu hana tu mahali miongoni mwa wanadamu pa kufanyia kazi Yake, lakini pia Anapata nchi zinazoweza kutumia mamlaka ya haki, ili kulazimisha mipaka na vikwazo kwa nchi hizo zinazompinga Mungu. Lakini licha ya hayo, bado hakuna watu zaidi wanaokuja mbele kumwabudu Mungu, kwa sababu mwanadamu amepotea mbali sana kutoka Kwake, na Mungu hajakuwa kwa mawazo ya mwanadamu kwa muda mrefu. Kunabakia tu duniani nchi zinazotumia haki na kupinga udhalimu. Lakini hii ni mbali na matakwa ya Mungu, kwani hakuna kiongozi wa nchi yoyote atamruhusu Mungu kuongoza watu wake, na hakuna chama cha kisiasa kitakachokusanya pamoja watu wake kumwabudu Mungu; Mungu amepoteza mahala Pake halali kwa mioyo ya nchi zote, taifa, chama tawala, na hata kwa moyo wa kila mtu. Ingawa nguvu za haki ziko kwa dunia hii, utawala ambapo Mungu hana mahali kwa moyo wa mwanadamu ni dhaifu. Bila baraka ya Mungu, uwanja wa kisiasa utaanguka katika vurugu na wenye kuweza kudhuriwa na mashambulizi. Kwa mwanadamu, kuwa bila baraka ya Mungu ni kama kukosa mwanga wa jua. Bila kujali jinsi viongozi wanafanya mchango kwa watu wao kwa uangalifu, bila kujali idadi ya mikutano ya haki wanadamu wanafanya pamoja, hakuna kati ya hii itakayorejesha mambo ama kubadilisha majaliwa ya mwanadamu. Mwanadamu anaamini kuwa nchi ambapo watu wanalishwa na kuvalishwa nguo, ambapo watu wanaishi kwa amani, ni nchi nzuri, na iliyo na uongozi mzuri. Lakini Mungu hafikirii hivyo. Anaamini kuwa nchi ambapo hakuna mtu anayemwabudu ndiyo Atakayoiangamiza. Njia ya mwanadamu ya kufikiria ni tofauti kabisa na ya Mungu. Kwa hiyvo, kama mkuu wa nchi hamwabudu Mungu, basi majaliwa ya nchi hii itakuwa ya kutisha, na nchi haitakuwa na majaliwa.
Mungu hashiriki katika siasa za mwanadamu, lakini majaliwa ya nchi ama taifa inadhibitiwa na Mungu, Mungu anadhibiti dunia hii na ulimwengu mzima. Majaliwa ya mwanadamu na mpango wa Mungu yanashikamana kwa undani, na hakuna mwanadamu, nchi ama taifa limetolewa kwa mamlaka ya Mungu. Iwapo mwanadamu anatamani kujua majaliwa yake, basi lazima aje mbele ya Mungu. Mungu atawafanya wanaomfuata na kumwabudu kufanikiwa, na Atashusha na kuwaangamiza wale wanaompinga na kumkataa.
Kumbuka tukio katika Biblia ambapo Mungu aliangamiza Sodoma, na fikiria pia jinsi mke wa Loti alivyokuwa nguzo ya chumvi. Fikiria nyuma jinsi watu wa Ninawi walitubu dhambi zao kwa gunia na majivu, na kumbuka kilichofuata baada ya Wayahudi kumsulubisha Yesu miaka 2,000 iliyopita. Wayahudi walitolewa Israeli na kukimbilia nchi duniani kote. Wengi waliuwawa, na taifa lote la Kiyahudi lilikabiliwa na uharibifu wa kipekee. Walimsulubisha Mungu—wakafanya uhalifu wa kuchukiza—na kuchochea tabia ya Mungu. Walifanywa kulipa kwa ajili ya walichofanya, walifanywa kukubali matokeo ya vitendo vyao. Walimlaani Mungu, walimkataa Mungu, na hivyo walikuwa na majaliwa moja pekee: kuadhibiwa na Mungu. Haya ndiyo matokeo machungu na maafa ambayo viongozi wao waliletea nchi na taifa lao.
Leo, Mungu amerudi duniani kufanya kazi Yake. Atasimama kwanza kwa mkutano mkubwa wa viongozi madikteta: Uchina, ngome kali ya ukanaji Mungu. Mungu amepata kundi la watu kwa hekima na nguvu Zake. Wakati huu, Anawindwa na chama tawala cha Uchina kwa kila namna na kukabiliwa na mateso makubwa, bila mahala pa kupumzisha kichwa Chake na kutoweza kupata makazi. Licha ya haya, Mungu bado anaendelea kufanya kazi Aliyonuia kufanya: Anatamka sauti Yake na kueneza injili. Hakuna anayeweza kuelewa uweza wa Mungu. Uchina, nchi inayomchukulia Mungu kama adui, Mungu hajawahi kukoma kazi Yake. Badala yake, watu zaidi wamekubali kazi na neno Lake, kwani Mungu anafanya yote Awezayo kuokoa kila mshiriki wa ubinadamu. Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo. Nahimiza watu wa mataifa, nchi na hata viwanda vyote kusikiza sauti ya Mungu, kutazama kazi ya Mungu, kuzingatia majaliwa ya mwanadamu, hivyo kumfanya Mungu kuwa mtakatifu zaidi, wa heshima zaidi, wa juu zaidi na chombo cha pekee cha kuabudu miongoni mwa wanadamu, na kuruhusu wanadamu wote kuishi chini ya baraka za Mungu, kama tu ukoo wa Ibrahimu ulivyoishi chini ya ahadi ya Yehova, na kama tu Adamu na Hawa, walioumbwa awali na Mungu, walivyoishi kwa Bustani ya Edeni.
Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yanayotapakaa kwa nguvu. Hakuna anayeweza kumweka kizuizini, na hakuna anayeweza kusimamisha nyayo Zake. Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na kiu naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake. Wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makuu na adhabu inayostahili.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni