12/18/2018

Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili"

 Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili"


    1. Katika Enzi ya Neema, Yohana alimwandalia Yesu njia. Hangeweza kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ila alitimiza tu kazi ya mwanadamu. Ingawa Yohana alikuwa mtangulizi wa Bwana; hangeweza kumwakilisha Mungu; alikuwa tu binadamu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu. Kufuatia ubatizo wa Yesu, "Roho Mtakatifu alimshukia Yeye kwa mfano wa njiwa." Kisha Akaanza kazi Yake, hivyo, Alianza kufanya huduma ya Kristo. Hiyo ndiyo maana Alichukua utambulisho wa Mungu, kwa sababu Alitoka Kwa Mungu. Haijalishi jinsi imani Yake ilivyokuwa kabla ya hii—labda wakati mwingine ilikuwa dhaifu, au wakati mwingine ilikuwa na nguvu—hayo ndiyo yalikuwa maisha Yake ya kawaida ya binadamu kabla Afanye huduma Yake. Baada ya kubatizwa (kuteuliwa), mara moja Alikuwa na nguvu na utukufu wa Mungu pamoja Naye, na hivyo Akaanza Kufanya huduma Yake. Angetenda ishara na maajabu, Atende miujiza, Alikuwa na nguvu na mamlaka, kwani Alifanya kazi kwa niaba ya Mungu Mwenyewe; Alifanya kazi ya Roho badala Yake na kuonyesha sauti ya Roho Mtakatifu; kwa hivyo Alikuwa Mungu Mwenyewe. Hili halina pingamizi. Yohana alitumiwa na Roho Mtakatifu. Hangemwakilisha Mungu, na hakungekuwa na uwezekano wa yeye kumwakilisha Mungu. Kama angetaka kufanya hivyo, Roho Mtakatifu hangelikubali, kwani hangeweza kufanya kazi ambayo Mungu Mwenyewe alinuia kukamilisha. Labda kulikuwa na mengi ndani yake yaliyokuwa ya mapenzi ya mwanadamu, ama kuna kitu uacha maadili ndani yake; hakuna hali yoyote ambapo angemwakilisha Mungu moja kwa moja. Makosa Yake na mambo yasiyo sahihi yalimwakilisha yeye pekee, lakini kazi Yake ilikuwa uwakilishi wa Roho Mtakatifu. Ilhali, huwezi kusema kuwa yeye mzima alimwakilisha Mungu. Je upotovu na kuwa kwake na makosa kungemwakilisha Mungu pia? Kuwa na makosa katika kumwakilisha mwanadamu ni kawaida, lakini kama alikuwa na upotovu katika kumwakilisha Mungu, basi si hiyo ingekuwa kutomheshimu Mungu? Je hilo halingekuwa kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu? Roho Mtakatifu hawezi kumruhusu mwanadamu asimame mahali pa Mungu anavyotaka, hata kama anasifiwa na wengine. Kama yeye si Mungu, basi hataweza kubaki akiwa amesimama mwishowe. Roho Mtakatifu hamkubali mwanadamu amwakilishe Mungu vile mwanadamu atakavyo! Kwa mfano, Roho Mtakatifu alimshuhudia Yohana na pia kumtambulisha kuwa mmoja wa wale watakaomwandalia Yesu njia, lakini kazi iliyofanywa ndani Yake na Roho Mtakatifu ilikuwa imepimwa vizuri. Kilichotakiwa kwa Yohana ilikuwa awe mtayarisha njia wa Yesu tu, kumtayarishia Yesu njia. Hiyo ni kusema, Roho Mtakatifu Aliiunga mkono kazi yake katika kutengeneza njia na kumruhusu afanye kazi ya aina hiyo pekee, hakuna mwingine. Yohana alimwakilisha Eliya, na alimwakilisha nabii aliyetengeneza njia. Hili liliungwa mkono na Roho Mtakatifu; bora kazi yake iwe kutengeneza njia, Roho Mtakatifu aliiunga mkono. Hata hivyo, kama angeweka madai kwamba yeye ni Mungu Mwenyewe na amekuja kumaliza kazi ya ukombozi, Roho Mtakatifu lazima amwadhibu. Haijalishi ukuu wa kazi ya Yohana, na ingawa iliungwa mkono na Roho Mtakatifu, kazi Yake ilibaki katika mipaka. Ni ukweli hakika kuwa kazi yake iliungwa mkono na Roho Mtakatifu, lakini nguvu aliyopewa katika wakati huo iliwekewa mipaka tu katika kutengeneza njia. Hangeweza, hata kidogo, kufanya kazi nyingine, kwani alikuwa tu Yohana aliyetengeneza njia, ila si Yesu. Kwa hivyo ushuhuda wa Roho Mtakatifu ni muhimu, lakini kazi ambayo mwanadamu anaruhusiwa kufanya na Roho Mtakatifu ni muhimu zaidi.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(1)" kwa Neno Laonekana katika Mwili


     2. Kuna wengine ambao wamepagawa na roho wachafu na wanalia kwa kusisitiza wakisema, "Mimi ni Mungu!" Lakini mwishowe, hawawezi wakasimama, kwani wanafanya kazi kwa niaba ya kiumbe asiyefaa. Wanawakilisha Shetani na Roho Mtakatifu hajali kuwahusu hata kidogo. Hata ujiinue vipi, ama kwa nguvu kivipi, wewe bado ni kiumbe aliyeumbwa na wewe unamilikiwa na Shetani. Mimi sipigi mayowe Nikisema, "Mimi ni Mungu, Mimi ni Mwana Mpendwa wa Mungu!" Lakini kazi Nifanyayo ni ya Mungu. Kuna haja Nipige mayowe? Hakuna haja ya kujiinua. Mungu hufanya kazi Yake Mwenyewe na hahitaji mwanadamu kumpa ruhusa ama cheo kubwa, na kazi Yake inatosha kuwakilisha utambulisho Wake na cheo. Kabla ya ubatizo Wake, si Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe? Je, Yeye hakuwa mwili wa Mungu? Hakika haiwezi kusemekana kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu baada ya kushuhudiwa? Je, hakukuwa na mwanadamu jina lake Yesu kitambo kabla Aanze kazi Yake? Huwezi kuleta njia mpya ama kumwakilisha Roho. Huwezi kueleza kazi ya Roho ama maneno Anenayo. Huwezi kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ama ile ya Roho. Huwezi kuelezea hekima, ajabu na mambo ya Mungu yasiyoeleweka, ama tabia yote ambayo Mungu humwadibu mwanadamu kupitia kwayo. Kwa hivyo madai yako ya kila mara ya kusema kuwa wewe ni Mungu hayajalishi; unalo tu jina lakini huna dutu. Mungu Mwenyewe Amekuja, lakini hakuna anayemtambua, ilhali Anaendelea na kazi Yake na Anafanya hivyo kwa uwakilishi wa Roho. Haijalishi unamwita mwanadamu ama Mungu, Bwana ama Kristo, ama umwite dada, yote ni sawa. Lakini kazi Afanyayo ni ile ya Roho na Anawakilisha kazi ya Mungu Mwenyewe. Hajali ni jina gani mwanadamu anamwita. Je, jina hilo linaweza kuamua kazi Yake? Bila kujali unachomwita, kutoka kwa mtazamo wa Mungu, Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu; Anawakilisha Roho na amekubaliwa na Yeye. Huwezi kutengeneza njia ya enzi mpya, na huwezi kuhitimisha enzi nzee na huwezi kukaribisha enzi mpya ama kufanya kazi mpya. Kwa hivyo, huwezi kuitwa Mungu!


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(1)" kwa Neno Laonekana katika Mwili


   3. Hata mwanadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu hawezi kumwakilisha Mungu Mwenyewe. Na mwanadamu huyu hawezi tu kumwakilisha Mungu bali pia kazi yake haiwezi kumwakilisha Mungu moja kwa moja. Hivyo ni kusema uzoefu wa mwanadamu hauwezi kuwekwa moja kwa moja katika usimamizi wa Mungu, na hauwezi kuwakilisha usimamizi wa Mungu. Kazi yote ambayo Mungu Mwenyewe hufanya ni kazi Anayolenga Kufanya katika mpango Wake wa usimamizi na inahusiana na usimamizi mkuu. Kazi ifanywayo na mwanadamu (mwanadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu) hukidhi uzoefu wake binafsi. Anapata njia mpya ya uzoefu mbali na ile iliyotembelewa na wale waliomtangulia na anawaongoza ndugu zake chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Kinachotolewa na watu hawa ni uzoefu wao ama maandishi ya kiroho ya watu wa kiroho. Ingawa wanatumiwa na Roho Mtakatifu, kazi ya watu kama hao haina uhusiano na kazi ya usimamizi mkuu katika mpango wa miaka elfu sita. Wamesimamishwa na Roho Mtakatifu katika wakati tofauti kuongoza watu katika mkondo wa Roho Mtakatifu hadi wakamilishe kazi yao ama maisha yao yafike mwisho. Kazi wanayofanya ni kutayarisha njia ifaayo kwa ajili ya Mungu Mwenyewe ama kuendeleza kitu kimoja kwa usimamizi wa Mungu Mwenyewe katika dunia. Watu hao hawawezi kufanya kazi kuu katika usimamizi Wake, na hawawezi kufungua njia mpya, ama kumaliza kazi yote ya Mungu kutoka enzi ya kitambo. Kwa hivyo, kazi wafanyayo inawakilisha kiumbe aliyeumbwa pekee akifanya kazi Yake na hawezi kuwakilisha Mungu Mwenyewe Akifanya huduma Yake. Hii ni kwa sababu kazi wanayofanya haifanani na ile inayofanywa na Mungu Mwenyewe. Kazi ya kukaribisha enzi mpya haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba ya Mungu. Haiwezi kufanywa na mwingine ila Mungu Mwenyewe. Kazi yote inayofanywa na mwanadamu ni kufanya wajibu wake kama mmoja wa viumbe na inafanywa akiguswa au kupewa nuru na Roho Mtakatifu. Uongozi ambao watu hao hupeana ni jinsi ya kuzoea katika kila siku ya maisha ya mwanadamu na jinsi mwanadamu anapaswa kutenda kwa maelewano na mapenzi ya Mungu. Kazi ya mwanadamu haihusishi usimamizi wa Mungu ama kuwakilisha kazi ya Roho. … Kwa hivyo, kwa sababu kazi ya wanadamu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu si sawa na kazi ifanywayo na Mungu Mwenyewe, utambulisho wao na wanayefanya kazi kwa niaba yake ni tofauti. Hii ni kwa sababu kazi ambayo Roho Mtakatifu Analenga Kufanya ni tofauti, na hapo kutoa utambulisho tofauti na hadhi kwa wale wote wafanyao kazi. Wanadamu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu wanaweza kufanya kazi mpya na wanaweza kutoa kazi iliyofanywa katika enzi iliyopita, lakini kazi yao haiwezi kueleza tabia na mapenzi ya Mungu kwa enzi mpya. Wanafanya kazi ili kuondoa kazi ya enzi iliyopita tu, sio kufanya kazi mpya kuwakilisha moja kwa moja tabia ya Mungu Mwenyewe. Hivyo, haijalishi matendo mangapi yaliyopitwa na wakati wanakomesha ama matendo mapya wanaanzisha, bado wanawakilisha mwanadamu na viumbe vilivyoumbwa. Mungu Mwenyewe Akifanya kazi, hata hivyo, Hatangazi wazi kukomeshwa kwa matendo ya enzi ya zamani au kutangaza moja kwa moja kuanzishwa kwa enzi mpya. Yeye hufanya kazi Yake moja kwa moja na kwa njia ya moja kwa moja. Yeye hufanya kazi Anayolenga kufanya moja kwa moja; hivyo, yeye hueleza moja kwa moja kazi Aliyoleta, Anafanya kazi Yake moja kwa moja Alivyolenga hapo awali, Akieleza uwepo Wake na tabia Yake. Mwanadamu anavyoona, tabia Yake na kazi Yake pia hazifanani na zile ya kitambo. Hata hivyo, kutoka kwa mtazamo wa Mungu Mwenyewe, huu ni uendelezo na ujenzi zaidi wa kazi Yake. Mungu Mwenyewe Akifanya kazi, Anaeleza neno Lake na Analeta kazi mpya moja kwa moja. Tofauti ni, mwanadamu akifanya kazi, ni kwa ukombozi na kusoma, ama ni kwa maendeleo ya maarifa na mpangilio wa mazoezi iliyojengwa juu ya msingi wa kazi za wengine. Hiyo ni kusema, umuhimu wa kazi inayofanywa na mwanadamu ni ya kuweka mkataba na "kutembea njia za kitambo kwa vitu mpya." Hii inamanisha kuwa hata njia ambayo inatembelewa na watu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu imejengwa juu ya yale yalifunguliwa na Mungu Mwenyewe. Kwa hivyo mwanadamu ni baada ya yote mwanadamu, na Mungu ni Mungu.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(1)" kwa Neno Laonekana katika Mwili


      4. Yohana alizaliwa kwa ahadi, na jina lake kupewa na malaika. Katika wakati huo wengine walitaka kumpa jina la baba yake Zakaria, lakini mama yake alinena akisema, "Mtoto huyu hawezi kuitwa kwa jina hilo. Anapaswa kuitwa Yohana." Haya yote yalielekezwa na Roho Mtakatifu. Basi mbona Yohana hakuitwa Mungu? Jina la Yesu pia lilikuwa uelekezi wa Roho Mtakatifu, na Alizaliwa wa Roho Mtakatifu, na kwa ahadi ya Roho Mtakatifu. Yesu Alikuwa Mungu, Kristo, na Mwana wa mtu. Kazi ya Yohana ilikuwa kuu pia, lakini mbona hakuitwa Mungu? Ni nini tofauti kati ya kazi iliyofanywa na Yesu na ile iliyofanywa na Yohana? Je, sababu pekee ni kwa kuwa Yohana ndiye aliyetengeneza njia ya Yesu? Au ni kwa sababu ilikuwa imepangwa na Mungu? Ingawa Yohana alisema kuwa, "Ninyi tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni uko karibu," na kuhubiri pia injili ya ufalme wa mbinguni, kazi yake haikuwa yenye kina na ilijumuisha tu mwanzo. Kinyume, Yesu Alikaribisha enzi mpya na kuikamilisha enzi ya kitambo, lakini pia Alitimiza sheria ya Agano la Kale pia. Kazi Aliyofanya ni kubwa kuliko ile ya Yohana, na Alikuja kuwakomboa wanadamu wote—Alifanya hatua hii ya kazi. Yohana alitayarisha tu njia. Ingawa kazi yake ilikuwa kubwa, maneno yake mengi, na wale wafuasi waliomfuata wengi, kazi yake haikufanya kitu kingine ila kuletea mwanadamu mwanzo mpya. Mwanadamu hakupokea maisha, njia, ama ukweli wa ndani kutoka kwake, na hawakupata kupitia kwake uelewa wa mapenzi ya Mungu. Yohana alikuwa nabii mkuu (Eliya) aliyeanza msingi mpya wa kazi ya Yesu na kutayarisha aliyeteuliwa; alikuwa mtangulizi wa Enzi ya Neema. Mambo kama haya hayawezi kutambuliwa kirahisi kwa kuchunguza kuonekana kwao kwa kawaida. Hasa sana, Yohana alifanya kazi kubwa; zaidi ya hayo, alizaliwa kutoka kwa ahadi ya Roho Mtakatifu, na kazi yake ikashikiliwa na Roho Mtakatifu. Hivyo, kutofautisha kati ya utambulisho wao inaweza kufanywa tu kupitia kazi yao, kwa kuwa sura tu ya nje ya mwanadamu haiwezi kuonyesha dutu yake, na mwanadamu hawezi kuhakikisha ushuhuda wa kweli wa Roho Mtakatifu. Kazi iliyofanywa na Yohana na ile iliyofanywa na Yesu si sawa na ilikuwa ya asili tofauti. Hii ndiyo inafaa kuonyesha kama yeye ni Mungu ama sio Mungu. Kazi ya Yesu ilikuwa kuanza, kuendelea, kuhitimisha na kukamilisha. Kila moja ya hatua hizi zilichukuliwa na Yesu, ilhali kazi ya Yohana haikuwa zaidi ya kuanzisha. Hapo mwanzo, Yesu Alieneza injili na kuhubiri njia ya kutubu, na Akaendelea mpaka kumbatiza mwanadamu, kuponya magonjwa, na kukemea mapepo. Mwishowe, Alimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi na kukamilisha kazi Yake ya enzi yote. Alimhubiria mwanadamu na kueneza injili ya ufalme wa mbinguni katika sehemu zote. Hii ilikuwa sawa na Yohana, tofauti ikiwa kwamba Yesu Alikaribisha enzi mpya na kuleta Enzi ya Neema kwa mwanadamu. Kutoka kwa Mdomo Wake lilitoka neno jinsi mwanadamu anavyopaswa kutenda na njia mwanadamu anayopaswa kufuata Enzi ya Neema, na mwishowe, Akamaliza kazi ya Wokovu. Kazi kama hiyo haingeweza kutekelezwa na Yohana. Kwa hivyo, ni Yesu ndiye Aliyefanya Kazi Ya Mungu Mwenyewe, na ni Yeye ndiye Mungu Mwenyewe na Anamwakilisha Mungu moja kwa moja.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(1)" kwa Neno Laonekana katika Mwili


     5. Iwapo hutambui kwamba hatua ya kazi siku hii ni ile ya Mungu Mwenyewe, ni kwa sababu huna maono. Hata hivyo, huwezi kukataa hatua hii ya kazi; kukosa kwako kuitambua hakumaanishi kuwa Roho Mtakatifu hafanyi kazi ama ya kwamba kazi Yake si sawa. Wengine hata hulinganisha kazi ya wakati huu dhidi ya ile ya Yesu katika Biblia, na kutumia tofauti zilizopo kati ya kazi hizi kukataa hatua hii ya kazi. Je haya si matendo ya aliyepofushwa? Yote yaliyoandikwa katika Biblia ni machache na hayawezi kuwakilisha kazi yote ya Mungu. Injili Nne zina chini ya sura mia moja zote pamoja ambamo mliandikwa mambo yale yaliotendeka yanayohesabika, kwa mfano Yesu Akilaani mti wa mkuyu, Petro akimkana Bwana mara tatu, Yesu Akiwaonekania wanafunzi Wake baada ya kusulubiwa na ufufuo Wake, Akifunza kuhusu kufunga, kufunza kuhusu maombi, kufunza kuhusu talaka, kuzaliwa na kizazi cha Yesu, uteuzi wa Yesu wa wanafunzi, na mengine mengi. Hata hivyo, mwanadamu anayathamini kama hazina, hata kuthibitisha kazi ya leo kulingana nayo. Hata wanaamini kuwa Yesu Alitenda kiasi tu katika muda baada ya kuzaliwa Kwake. Ni kana kwamba wanaamini kuwa Mungu anaweza kufanya hayo tu, kwamba hakuna kazi nyingine. Je huu si upumbavu?


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(1)" kwa Neno Laonekana katika Mwili


    6. Watu huamini kuwa Mungu mwenye Mwili lakini haishi jinsi mwanadamu anavyoishi; wanaamini kuwa ni msafi hata hawezi kusugua meno Yake ama kuosha uso Wake, kwani ni mtu mtakatifu. Je hizi kikamilifu si dhana ya mwanadamu? Biblia haina rekodi yoyote kuhusu maisha ya Yesu kama mwanadamu, kazi Yake pekee, lakini hili halithibitishi kuwa hakuwa na ubinadamu wa kawaida ama hakuishi maisha ya mwanadamu wa kawaida kabla ya umri wa miaka thelathini. Alianza kazi Yake rasmi Akiwa na miaka 29, lakini huwezi kukana maisha Yake yote kama mwanadamu kabla ya umri huo. Biblia iliacha hatua hiyo katika maandishi Yake; kwani yalikuwa maisha Yake kama mwanadamu wa kawaida na si hatua ya kazi Yake takatifu, hakukuwa na haja ya maneno hayo kuandikwa chini. Kwani kabla ya ubatizo wa Yesu, Roho Mtakatifu hakufanya kazi Yake moja kwa moja, lakini akadumisha maisha Yake kama mwanadamu wa kawaida tu hadi siku ambayo Yesu Alikuwa Anapaswa kuanza huduma Yake. Ingawa Alikuwa Mungu katika mwili, Alipitia mchakato wa kukomaa kama jinsi mwanadamu wa kawaida afanyavyo. Hatua hii iliwachwa nje ya Biblia, kwani haingeleta usaidizi mkubwa kwa kukuwa kwa maisha ya mwanadamu. Kabla ya ubatizo Wake ulikuwa wakati ambapo hakujulikana, na wala Hakutenda ishara na miujiza. Baada tu ya ubatizo wa Yesu ndipo Alipoanza kazi ya ukombozi wa mwanadamu, kazi iliyokuwa imejaa neema, ukweli, na upendo na huruma. Mwanzo wa kazi hii ndio ulikuwa pia mwanzo wa Enzi ya Neema; kwa sababu hii, matukio haya yaliandikwa chini na kupitishwa kwa vizazi mpaka wakati huu. … Kabla ya Yesu kufanya huduma Yake, ama isemwavyo katika Biblia, kabla ya Roho kushuka juu Yake, Yesu Alikuwa mwanadamu wa kawaida na bila kuwa na chochote kisicho cha kawaida. Roho Mtakatifu Aliposhuka, hiyo ni, Alipoanza kazi ya huduma Yake, Alijazwa na vitu vya kimiujiza. Kwa njia hii, mwanadamu anaanza kuamini kwamba mwili wa Mungu hauna ubinadamu wa kawaida na aidha anafikiri kimakosa kwamba Mungu mwenye mwili hana ubinadamu. Hakika, kazi na yale yote anayoyaona mwanadamu katika dunia hii kumhusu Mungu si ya kawaida. Uonacho na macho yako na usikiayo na masikio yako yote sio ya kawaida, kwani kazi Yake na maneno Yake hayaeleweki na kufikiwa na mwanadamu. Kitu cha kimbingu kikiletwa duniani, itakuwa vipi kiwe kitu cha kawaida? Mafumbo ya ufalme wa mbinguni yanapoletwa duniani, mafumbo yasiyoweza kufikiriwa na kueleweka na mwanadamu, ambayo ni ya ajabu na yenye hekima—yote si yasiyo ya kawaida? Hata hivyo, unapaswa kujua kuwa, haijalishi jinsi kisicho cha kawaida, mambo yote yanatekelezwa katika ubinadamu Wake wa kawaida. Mwili wa Mungu umejaa ubinadamu, la sivyo, haungekuwa Mwili wa Mungu katika mwili.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(1)" kwa Neno Laonekana katika Mwili


     7. Kazi ya Roho wa Mungu katika mwili pia inaongozwa na kanuni zake. Ni wakati tu Anapojitayarisha na ubinadamu wa kawaida ndipo Anapoweza kufanya kazi na kumwongoza Baba. Hapo tu ndipo Angeanza kazi Yake. Utotoni Mwake, Yesu hangeelewa mengi ya yale yaliyotendeka katika wakati wa kale, na ni kwa kuuliza waalimu tu ndipo Alipata kuelewa. Iwapo Angeanza kazi Yake pindi Alipojua kuzungumza, Angewezaje kutofanya makosa yoyote? Mungu Angewezaje kufanya makosa? Kwa hivyo, ilikuwa tu baada ya kuweza ndipo Alianza kazi Yake; Hakufanya kazi yoyote hadi Alipokuwa na uwezo wa kuyatekeleza. Akiwa na miaka 29, Yesu Alikuwa Amekomaa vya kutosha na ubinadamu Wake kutosha kutekeleza kazi Aliyopaswa kutekeleza. Ilikuwa hapo tu ndipo Roho Mtakatifu, Aliyekuwa Amejificha kwa miaka thelathini, Alianza kujionyesha, na Roho wa Mungu Akaanza kirasmi kufanya kazi ndani Yake. Katika wakati huo, Yohana alikuwa ametenda kazi kwa miaka saba kwa kutayarisha njia Yake, na baada ya kumaliza kazi Yake, Yohana alitupwa gerezani. Mzigo wote basi ukamwangukia Yesu. Kama Angetekeleza kazi hii Akiwa na miaka 21 ama 22, Alipokuwa bado hana ubinadamu wa kutosha na Ameingia tu utu uzima, Akiwa bado haelewi mambo mengi, hangeweza kuchukua udhibiti. Katika wakati huo, Yohana alikuwa ameshafanya kazi yake kwa muda kabla Yesu kuanza kazi Yake katika miaka Yake ya katikati. Katika miaka hiyo, ubinadamu Wake wa kawaida ulikuwa unatosha kufanya kazi Aliyopaswa kufanya.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(1)" kwa Neno Laonekana katika Mwili


      8. Kazi ya Mungu mwenye mwili katika mwili na kanuni nyingi. Kuna mengi ambayo mwanadamu haelewi, ilhali mwanadamu anatumia mara kwa mara fikira zake kuipima au kuwa na matarajio mengi kutoka Kwake. Hata wakati huu kunao wengi wasiofahamu kabisa kuwa maarifa yao ni ya fikira zao tu. Haijalishi enzi ama mahali ambapo Mungu anapata mwili, kanuni za kazi Yake katika mwili Wake hazibadiliki. Hawezi kuwa Mwili kisha Avuke mwili kwa kufanya kazi; zaidi, hawezi kuwa mwili kisha Akose kufanya kazi katika mwili wa kawaida wa binadamu. Vinginevyo, umuhimu wa Mungu kupata mwili utapotea na kuwa bure, na Neno kuwa mwili itakuwa haina maana. Zaidi ya hayo, Baba tu Aliye mbinguni (Roho) Anajua kuhusu Mungu katika mwili wa Mungu, na sio mwingine, sio hata mwili Mwenyewe ama wajumbe wa mbinguni. Hivyo, kazi ya Mungu katika mwili ni ya kawaida zaidi na bora kueleza Neno kuwa mwili; mwili unamaanisha mwanadamu wa kawaida.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(1)" kwa Neno Laonekana katika Mwili


       9. Wengine wanaweza kushangaa, mbona enzi ikaribishwe na Mungu Mwenyewe? Kiumbe kilichoumbwa hakiwezi kusimama kwa niaba Yake? Nyote mnafahamu kuwa Mungu Anakuwa mwili hasa kwa ajili ya kuikaribisha enzi mpya, na, kwa hakika, Anapoikaribisha enzi mpya, Atakuwa Ameikamilisha enzi ya kale wakati uo huo. Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho; ni Yeye Mwenyewe ndiye Anayeanzisha kazi Yake na hivyo lazima iwe ni Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani na huishinda dunia. Kila wakati Yeye Mwenyewe Anapofanya kazi miongoni mwa mwanadamu, ni mwanzo wa mapigano mapya. Bila mwanzo wa kazi mpya, kwa kawaida hakutakuwa na kikomo kwa enzi ya kale. Na bila kikomo kwa enzi ya kale ina maana kuwa vita na Shetani havijafika mwisho. Ni kama tu Mungu Mwenyewe Anakuja miongoni mwa mwanadamu na kutenda kazi mpya ndipo mwanadamu atakapoweza kujitoa kutoka katika umiliki wa Shetani na kupata maisha na mwanzo mpya. Vinginevyo, mwanadamu ataishi milele katika wakati wa kale na milele kuishi katika ushawishi wa kale wa Shetani. Katika kila enzi inayoongozwa na Mungu, sehemu ya mwanadamu huwekwa huru, na hivyo, mwanadamu huendelea na kazi ya Mungu kuelekea enzi mpya. Ushindi wa Mungu ni ushindi kwa wale ambao humfuata Yeye. Kama binadamu wa kuumbwa angepewa usukani wa kutimiza enzi, basi iwe kutoka kwa mtazamo wa mwanadamu ama Shetani, hii ni kama kupinga au kusaliti Mungu, na hivyo kazi ya mwanadamu ingegeuka kuwa chombo kwa Shetani. Mwanadamu anapotii na kumfuata Mungu katika enzi iliyokaribishwa na Mungu Mwenyewe tu ndipo Shetani angeshawishiwa kabisa, kwani hiyo ndiyo kazi ya kiumbe aliyeumbwa. Kwa hivyo Nasema kuwa mnafaa tu kufuata na kutii, na hakuna kingine kitakachoulizwa kutoka kwenu. Hiyo ndiyo maana ya kusema kila mmoja kuendeleza kazi na kufanya kazi Yake. Mungu hufanya kazi Yake Mwenyewe na Yeye hahitaji mwanadamu kufanya kazi Yake kwa niaba Yake, na wala hajishughulishi katika kazi ya viumbe. Mwanadamu anafanya kazi yake na haingilii kati kazi ya Mungu, na huo ndio utii wa kweli na ushahidi kuwa Shetani ameshindwa. Baada ya Mungu Mwenyewe kukaribisha enzi mpya, Yeye Mwenyewe hafanyi kazi tena kati ya mwanadamu. Ni wakati huo tu ndipo mwanadamu anaingia rasmi katika enzi mpya kufanya kazi yake na kutekeleza misheni yake kama kiumbe aliyeumbwa. Hivyo ndivyo zilivyo kanuni za kazi zisizowezwa kukiukwa na yeyote. Kufanya kazi katika njia hii pekee ndio yenye busara. Kazi ya Mungu hufanywa na Mungu Mwenyewe. Ni Yeye ndiye Anayeweka kazi katika mwendo, na pia Yeye ndiye Anayemaliza. Ni Yeye ndiye hupanga kazi, na pia Yeye ndiye Anayesimamia, na zaidi ya hayo, ni Yeye ndiye Anayeleta kazi kuzaa matunda. Ni ilivyoandikwa katika Biblia, "Mimi ndiye Mwanzo na Mwisho: Mimi ndiye Mpanzi na Mvunaji." Hayo yote yanahusiana na usimamizi wa kazi Yake yanayofanywa na mkono Wake. Yeye ndiye Mtawala wa mpango wa miaka elfu sita; hakuna anayeweza kufanya kazi Yake kwa niaba Yake ama kuleta kazi Yake hadi mwisho, kwani Yeye ndiye Aliye katika uongozi wa yote. Kwa kuwa Aliumba dunia, Ataongoza ulimwengu mzima kuishi katika nuru Yake, na Atamaliza enzi yote na kuleta mpango Wake wote kwa mafanikio!


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (1)" kwa Neno Laonekana katika Mwili


    10. Katika wakati ambapo Yesu Alifanya kazi Uyahudi, Aliifanya wazi, lakini sasa, Nazungumza na Kufanya kazi kati yenu kwa siri. Wasioamini hawana ufahamu wowote. Kazi Yangu kati yenu imetengwa kutoka kwa nyingine. Maneno haya, kuadibu huku na hukumu hii, vinajulikana tu kwako na sio mwingine. Kazi hii yote inatendeka kati yenu na kuonekana tu kwenu; hakuna yeyote asiyeamini anayefahamu haya, kwani muda haujafika. Wanadamu hao wako karibu kufanywa wakamilifu baada ya kuvumilia adibu, lakini wale walio nje hawajui lolote juu yake. Kazi hii imefichwa sana! Kwao, Mungu mwenye mwili ni siri, lakini kwa wale walio katika mkondo, Anaweza kuchukuliwa kuwa wazi. Ingawa kwa Mungu yote ni wazi, yote yanakuwa wazi na yote yanaachiliwa, haya tu ni ya ukweli kwa wale wanaomwamini, na hakuna kitu kinachofanywa kujulikana kwa wale wasioamini Kazi inayofanywa hapa imetengwa kwa ushurutisho ili kuwazuia wasijue. Wakipata kujua, kinachowangojea ni shutuma na mateso. Hawataamini. Kufanya kazi katika taifa la joka kuu jekundu, mahali palipo nyuma zaidi, sio kazi rahisi. Kama kazi hii ingewekwa wazi na kujulikana, basi ingekuwa vigumu kuendelea. Hatua hii ya kazi haiwezi kuendelea katika sehemu hii. Wangestahimili vipi kama kazi hii ingeendelezwa kwa uwazi? Hii haingeleta hata hatari kubwa zaidi? Kama kazi hii haingefichwa, na badala Yake kuendelea kama wakati wa Yesu Alivyowaponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa njia ya kustaajabisha, basi si ingekuwa tayari "imeshanyakuliwa" na ibilisi? Je, wangestahimili uwepo wa Mungu? Kama sasa ningeingia kwenye kumbi kuwahadhiria wanadamu, je, si ningekuwa nimeshapasuliwa katika vipande kitambo? Na ikiwa hivyo, kazi Yangu itawezaje kuendelea kufanyika? Sababu ambayo ishara na miujiza haitendeki wazi wazi ni kwa ajili ya kujificha. Kwa hivyo kazi Yangu haiwezi kuonekana, kujulikana wala kugunduliwa na wasioamini. Iwapo hatua hii ya Kazi ingefanyika kwa njia sawa na kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, haingekuwa thabiti sana. Kwa hivyo, kazi hii kufichwa namna hii ni ya manufaa kwenu na kwa kazi yote. Wakati kazi ya Mungu duniani inafika kikomo, kumaanisha, wakati kazi hii katika siri inakamilika, hatua hii ya kazi italipuka na kuwa wazi. Watu wote watajua kwamba kuna kundi la washindi ndani ya taifa la Uchina; kila mwanadamu atafahamu kuwa Mungu katika mwili yuko Uchina na kwamba kazi Yake imefika kikomo. Hapo tu ndipo kutampambazukia mwanadamu: Ni kwa nini taifa la Uchina halijaonyesha kudhoofika wala kuporomoka? Inaonekana kuwa Mungu anaendeleza kazi Yake binafsi katika taifa la China na amefanya kuwa kamilifu kundi la watu na kuwafanya washindi.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (2)" katika Neno Laonekana Katika Mwili


      11. Mungu mwenye mwili Anajidhihirisha mwenyewe kwa watu kadhaa wanaomfuata Anapofanya kazi Yeye binafsi, na sio kwa viumbe wote. Alijifanya mwili ili Akamilishe hatua ya kazi Yake, na sio ili amwonyeshe mwanadamu mfano Wake. Hata hivyo, kazi Yake lazima ifanywe na Yeye binafsi, kwa hivyo inalazimu Afanye kazi hiyo katika mwili. Kazi hii inapokamilika, Ataondoka duniani; Hawezi kusalia duniani kwa muda mrefu kwa hofu ya kuzuia kazi inayokuja. Anachokionyesha kwa halaiki ni tabia Yake ya haki na matendo Yake yote, na sio umbo la mwili Wake wakati Amejifanya mwili mara mbili, kwa maana mfano wa Mungu unaweza tu kuonyeshwa kupitia kwa tabia Yake, na si kubadilishwa na mfano wa mwili Wake wa nyama. Mfano wa mwili Wake wa nyama huonyeshwa kwa watu wachache tu, kwa wale wanaomfuata Anapofanya kazi katika mwili. Hiyo ndio maana kazi inayofanywa wakati huu inafanywa kwa siri. Ni kama tu vile Yesu alivyojionyeshwa kwa Wayahudi pekee yao Alipofanya kazi Yake, na hakujionyesha hadharani kwa mataifa mengine. Hivyo, pindi Alipomaliza kazi Yake, Aliondoka miongoni mwa wanadamu na hakukawia; kwa wakati uliofuata Hakujionyesha kwa nafsi Yake kwa mwanadamu, bali kazi iliendeshwa moja kwa moja na Roho Mtakatifu. Mara tu kazi ya Mungu katika mwili inapokamilika, Anaondoka katika dunia ya mwanadamu, na kamwe Hafanyi tena kazi sawa na ile Aliyofanya Akiwa katika mwili. Kazi inayofuata hufanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja. Wakati huu, mwanadamu hawezi kuona mfano Wa Mungu katika mwili; Yeye Hajionyeshi wazi kwa mwanadamu hata kidogo, na daima Anabaki mafichoni. Muda wa kazi ya Mungu mwenye mwili ni mchache, ambayo lazima ifanywe katika Enzi bayana, muda, taifa na kati ya watu bayana. Kazi kama hiyo inawakilisha tu kazi ya wakati wa Mungu katika mwili, na inalenga enzi fulani, ikiwakilisha kazi ya Roho wa Mungu katika enzi moja hasa, na sio ujumla wa kazi Yake. Kwa hivyo, umbo la Mungu mwenye mwili halitaonyeshwa kwa kila mwanadamu. Kinachoonyeshwa kwa halaiki ni uhaki wa Mungu na tabia Yake kwa ukamilifu, na wala sio mfano Wake Alipokuwa mwili mara mbili. Sio sura inayoonyeshwa kwa mwanadamu, wala mifano yote miwili ikijumlishwa. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba mwili wa Mungu uondoke duniani baada ya kukamilisha kazi Anayohitajika kufanya, kwa kuwa Anakuja tu kufanya kazi Anayopaswa kufanya, na sio kuwaonyesha wanadamu mfano wa umbo Lake. Ingawa umuhimu wa kuingia katika mwili umeshatimizwa na Mungu mara mbili Akijifanya mwili na nyama, bado hatajionyesha wazi kwa taifa ambalo halijawahi kumwona mbeleni.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (2)" katika Neno Laonekana Katika Mwili


   12. Mnapaswa kujua kwamba kazi ya Mungu katika mwili inafaa kufungua enzi mpya. Kazi hii ni ya muda wa miaka michache tu, na Hawezi kukamilisha kazi yote ya Roho wa Mungu. Hii ni sawia na vile umbo la Yesu kama Myahudi linaweza tu kuwakilisha mfano wa Mungu alivyofanya kazi katika Yudea, na Angefanya tu kazi ya msalabani. Wakati ambao Yesu Alikuwa katika mwili, Hangefanya kazi ya kutamatisha enzi au kumwangamiza mwanadamu. Kwa hivyo, baada ya kusulubiwa na kukamilisha kazi Yake, Alipaa juu na daima Akajificha kutoka kwa mwanadamu. Kutoka wakati huo kuendelea, wale waumini wa mataifa waliweza tu kuiona picha Yake ambayo walibandika kwenye kuta zao, na sio udhihirisho wa Bwana Yesu. Picha hii imechorwa na mwanadamu tu, na si mfano ambao Mungu Mwenyewe Alimwonyesha mwanadamu. Mungu Hatajionyesha kwa halaiki wazi wazi katika mfano ambao Yeye Alikuwa nao mara mbili Akiwa katika mwili. Kazi Anayofanya miongoni mwa wanadamu ni kuwaruhusu kuelewa tabia Yake. Haya yote yanafanyika kwa kumpitisha mwanadamu katika kazi za enzi tofauti, na vile vile tabia ambazo Ameziweka wazi na kazi ambayo Amefanya, na bali si kupitia kwa udhihirisho wa Yesu. Hiyo ni kusema, umbo la Mungu halionyeshwi kwa mwanadamu kupitia katika mfano wa Mungu mwenye mwili, lakini ni kwa kupitia katika kazi iliyotekelezwa na Mungu mwenye mwili wa sura na umbo; na kupitia katika kazi Yake, mfano Wake unaonekana na tabia Yake inajulikana. Huu ndio umuhimu wa kazi Angependa kufanya katika mwili.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (2)" katika Neno Laonekana Katika Mwili


    13. Wakati kazi ya Alipokuwa mwili mara mbili inakamilika, Anaanza kuonyesha tabia Yake ya haki katika mataifa, Akiruhusu halaiki ione mfano wa umbo Lake. Anapenda kudhihirisha tabia Yake, na kupitia katika hili Aweke wazi tamati za aina tofauti ya wanadamu, hapo kuifikisha mwishokabisa enzi nzee. Kazi Yake katika mwili haitendeki katika sehemu pana (kama vile Yesu Alivyofanya kazi katika sehemu ya Yuda peke Yake, na leo hii Ninafanya kazi miongoni mwenu pekee) kwa sababu kazi Yake katika mwili ina mipaka na kingo. Anafanya tu kazi ya muda mchache katika mfano wa kawaida na mwili wa kawaida, badala ya kufanya kazi ya milele kupitia kwa Mungu mwenye mwili, ama kufanya kazi ya kuwaonekania watu wote wa mataifa. Kazi hii katika mwili lazima izuiliwe katika mawanda (kama vile kufanya kazi katika Yuda ama kati Yenu), kisha kupanua kazi iliyofanyika katika mipaka hii. Bila shaka, kazi ya upanuzi huu huendeshwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja na haiwezi kuwa kazi ya mwili Wake wa nyama. Kwa maana kazi katika mwili iko na mipaka na haiwezi kuenea katika pembe zote za ulimwengu. Hauwezi kuyatekeleza haya. Kupitia kwa kazi katika mwili, Roho Wake hutekeleza kazi inayofuatia. Kwa hivyo, kazi inayofanywa katika mwili ni ya utayarisho inayotekelezwa ndani ya mipaka; Roho Wake kisha Anaendeleza kazi hii, na kuipanua.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (2)" katika Neno Laonekana Katika Mwili


   14. Mungu huja tu katika dunia hii kufanya kazi ya kuongoza enzi; kufungua enzi mpya na kutamatisha enzi ya zamani. Hajakuja kuishi kulingana na maisha ya mwanadamu wa kawaida kwa kikamilifu, kupitia Mwenyewe raha na machungu ya maisha kama mwanadamu, au kumfanya mtu fulani mkamilifu kwa mkono Wake au kumtazama binafsi mtu Fulani anavyokua. Hii sio kazi Yake; kazi Yake ni kufunua tu enzi mpya na kutamatisha enzi iliyotangulia. Hiyo ina maana, Atafungua enzi mpya, akamilishe iliyotangulia, amshinde shetani kwa kufanya kazi Yake Yeye binafsi. Kila mara Anapotekeleza kazi Yeye Mwenyewe, ni kana kwamba Anakanyaga mguu wake katika uwanja wa vita Katika mwili, kwanza Anaishinda dunia kisha Anatawala juu ya Shetani; Anachukua utukufu wote na kufungua pazia kwa kazi ya enzi yote elfu mbili, na kuwapa binadamu wote duniani njia ya kweli ya kufuata, na maisha ya amani na furaha. Hata hivyo, Mungu Hawezi kuishi na mwanadamu duniani kwa muda mrefu, kwa maana Mungu ni Mungu, ni si kama mwanadamu kamwe. Hawezi kuishi urefu wa maisha ya mwanadamu wa kawaida, hiyo ina maana, Hawezi kuishi duniani kama mwanadamu ambaye si wa kawaida, kwa maana Yuko na sehemu ndogo ya uanadamu wa kawaida wa wanadamu wa kawaida kumuwezesha kuishi vile. Kwa maneno mengine, Mungu Anawezaje kuanzisha familia na kukuza watoto duniani? Je, si hii itakuwa ni aibu? Yeye anao uanadamu wa kawaida tu kwa minajili ya kutekeleza kazi Yake kwa njia ya kawaida, na sio kumwezesha Yeye kuanzisha familia kama mwanadamu wa kawaida. Hisia Zake za kawaida, mawazo ya kawaida, na kula kwa kawaida na mavazi ya mwili Wake yanatosha kuthibitisha kuwa Yuko na uanadamu wa kawaida; Hakuna haja Yake kuanzisha familia ndio athibitishe kwamba Yeye kweli yuko na uanadamu wa kawaida. Hiyo haina maana hata kidogo! Mungu Anakuja duniani, kumaanisha Neno linageuka kuwa mwili; Kwa urahisi Anamruhusu mwanadamu kulielewa neno Lake na kuliona neno Lake, hiyo ni, kumruhusu mwanadamu kuona kazi inayotekelezwa na mwili. Nia Yake sio kwamba wanadamu wauchukue mwili Wake kwa njia Fulani, bali kwamba mwanadamu awe mtiifu mpaka mwisho, kumaanisha, aweze kutii maneno yote yanayotoka katika kinywa Chake, na kunyenyekea na kukubali kazi yote Anayofanya. Yeye Anafanya kazi katika mwili tu, sio kumfanya mwanadamu kwa kujua aabudu ukuu na utukufu wa mwili Wake. Anamwonyesha tu mwanadamu hekima ya kazi Yake na mamlaka yote Aliyo nayo. Kwa hivyo, ingawa Anao uanadamu wa kipekee, Hafanyi matangazo yoyote, na Anatilia tu maanani kazi ambayo Anapaswa kufanya. Mnapaswa kujua ni kwa nini Mungu Alijifanya mwili ilhali hajigambi wala kushuhudia juu ya ubinadamu Wake wa kawaida, na badala Yake Anatekeleza tu kazi ambayo Angependa kufanya. Hii ndio sababu mnaona tu uwepo wa uungu katika Mungu mwenye mwili, kwa sababu Hatangazi kuwa Kwake katika mwili ndio mwanadamu aige. Wakati tu mwanadamu anamwongoza mwanadamu ndipo anapozungumzia kuhusu kile alicho kama binadamu, ndivyo apate heshima na utii wao vyema zaidi na hivyo kufanikisha uongozi wa wengine. Kinyume na hilo, Mungu huwashinda watu kupitia katika kazi Yake pekee (hiyo ni, kazi isiyoweza kufanywa na mwanadamu). Hamshawishi mwanadamu au kuwafanya wanadamu wote wamwabudu, bali Anaweka tu katika mwanadamu hisia za uchaji Kwake au kumfanya mwanadamu aweze kujua kuhusu kutowezekana kwa kumchunguza Yeye. Hakuna haja ya Mungu kumpendeza mwanadamu. Kile anachohitaji ni kuwa wewe umheshimu na kumwabudu mara tu unaposhuhudia tabia Yake.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (2)" katika Neno Laonekana Katika Mwili


     15. Kazi ya Mungu mwenye mwili ni tofauti na ile ya wale wanaotumiwa na Roho Mtakatifu. Mungu anapofanya kazi Yake duniani, Yeye anajali kutimilika kwa huduma Yake pekee Yake. Na kwa mambo mengine yasiyohusiana na huduma Yake, Yeye kimatendo hajishughulishi hata kidogo, hata kwa kiwango cha kuzipa mgongo shughuli hizo. Yeye hufanya tu kazi Anayopaswa kufanya, na hajishughulishi na kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya. Kazi Anayofanya ni ile tu inahusiana na enzi Aliyomo na huduma Anayopaswa kukamilisha, kana kwamba mambo mengine yote si jukumu Lake. Yeye hajijazi na maarifa ya kawaida kuhusu jinsi ya kuishi kama mwanadamu, na Hajifunzi mahusiano ya jamii au mambo yoyote ambayo mwanadamu anaelewa. Hajishughulishi kamwe na mambo ambayo mwanadamu anapaswa kujua na Anafanya tu kitu ambacho ni jukumu Lake. Kwa hivyo, mwanadamu anavyoona, Mungu mwenye mwili ni mwenye upungufu katika mambo mengi mno, hata kwa kiasi kwamba Anavipa mgongo vingi ambavyo mwanadamu anapaswa kuwa navyo, na kwamba hana ufahamu wa mambo kama hayo. Mambo kama ufahamu wa maisha ya kawaida, na vile vile kanuni za tabia na kuhusiana na wengine, huonekana kuwa hazina uhusiano Kwake. Hata hivyo, huwezi kuona kutoka kwa Mungu mwenye mwili tabia zozote zisizo za kawaida. Hiyo ni kusema, Uanadamu Wake unadumisha maisha Yake kama mwanadamu wa kawaida na fikira za kawaida za ubongo Wake, na kumpa uwezo wa kutofautisha kati ya mazuri na mabaya. Hata hivyo, Hajajazwa na kingine chochote, yote ambayo ni ya wanadamu (walioumbwa) pekee. Mungu anapata mwili ili kukamilisha huduma Yake pekee. Kazi Yake inaelekezwa kwa enzi nzima na sio kwa mtu binafsi au mahali fulani. Kazi Yake inaelekezwa kwa ulimwengu mzima. Huu ndio mwelekeo wa kazi Yake na kanuni Anayofuata katika kazi Yake. Hii haiwezi kubadilishwa na yeyote, na mwanadamu hawezi kuhusika kwa sehemu yoyote.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (3)" katika Neno Laonekana Katika Mwili


      16. Mungu anakuja tu duniani kukamilisha kazi Yake, na kwa hivyo Kazi Yake duniani ni ya muda mfupi. Haji duniani na nia ya Roho wa Mungu kukuza mwili Wake kuwa mkuu wa kipekee wa kanisa. Mungu anapokuja duniani, ni Neno ambalo kugeuka kuwa mwili; mwanadamu, hata hivyo, hajui kuhusu kazi Yake na kwa nguvu anaona Yeye kuwa sababu ya mambo. Lakini nyote mnapaswa kufahamu kuwa Mungu ni Neno lililogeuka kuwa mwili, na sio mwili uliokuzwa na Roho wa Mungu ili kusimamia nafasi ya Mungu kwa ufupi. Mungu Mwenyewe hakuzwi, ila ni Neno kugeuka mwili, na leo hii Anatekeleza kazi Yake kirasmi miongoni mwenu.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (3)" katika Neno Laonekana Katika Mwili


    17. Mungu hugeuka mwili ili tu Aiongoze enzi na Aanzishe kazi mpya. Lazima muelewe hoja hii. Hii ni tofauti kabisa na kazi ya mwanadamu, na mawili haya hayawezi kuzungumzwa kwa pamoja. Mwanadamu anahitaji muda mrefu wa kukuzwa na kufanywa mkamilifu kabla mwanadamu aweze kutumiwa kutekeleza kazi, na uanadamu wa hali ya juu unahitajika. Mwanadamu hapaswi kudumisha hali yake ya uanadamu wa kawaida tu, bali pia mwanadamu zaidi ya hapo lazima aelewe kanuni nyingi na sheria za tabia kabla ya mengine, na zaidi ya hayo lazima ajifunze zaidi kuhusu hekima na maadili ya mwanadamu. Haya ndiyo mwanadamu lazima kujengwa nayo. Hata hivyo, hivi sivyo ilivo na Mungu mwenye mwili, kwa maana kazi Yake haimwakilishi mwanadamu na wala si ya binadamu; bali ni dhihirisho la moja kwa moja la hali Yake na utekelezi wa moja kwa moja wa kazi Anayopaswa kufanya. (Kwa kawaida, kazi Yake hufanyika wakati inapaswa kufanyika, na sio tu wakati wowote kiholela. Badala Yake, kazi Yake hufanyika wakati ambapo ni wakati wa kukamilisha huduma Yake). Yeye hajihusishi katika maisha ya mwanadamu wala katika kazi ya mwanadamu, hiyo inamaanisha, uanadamu Wake haujengwi na yoyote kati ya haya (lakini hili haliathiri kazi Yake). Anatimiza huduma Yake tu ikiwa wakati umewadia wa kufanya hivyo; haijalishi hali Aliyomo, Yeye huendelea mbele na kazi Anayopaswa kufanya. Haijalishi mwanadamu anajua nini kumhusu, au maoni ya mwanadamu kumhusu, kazi Yake haiathiriki. Hii ni kama tu vile Yesu Alivyofanya kazi Yake; hakuna Aliyejua Yeye ni nani, lakini Aliendelea tu mbele na kazi Yake. Mambo haya hayakumuathiri katika utendaji wa kazi Yake Aliyopaswa kufanya. Kwa hivyo, Hakukiri au kutangaza kuwa Yeye ni nani, na Yeye Alimfanya mwanadamu Amfuate tu. Kwa kawaida, huu haukuwa tu uvumilivu wa Mungu; ilikuwa ni njia ambayo Yesu Anafanya kazi katika mwili. Angeweza tu kufanya kazi kwa namna hii, kwani mwanadamu hangeweza kumtambua Yesu kwa jicho la kawaida. Na hata kama mwanadamu angeweza, mwanadamu hangeweza kusaidia katika kazi Yake. Zaidi ya hayo, hakugeuka mwili ili mwanadamu apate kujua mwili huu Wake; ilikuwa ni kwa ajili ya kufanya kazi Yake na kukamilisha huduma Yake. Kwa sababu hii, hakutilia maanani hali ya kufanya Ajulikane. Alipokamilisha kazi Aliyopaswa kufanya, utambulisho Wake na hadhi Yake vilijulikana wazi kwa mwanadamu. Mungu mwenye mwili hukaa kimya na hafanyi matangazo yoyote. Yeye hajishughulishi na mwanadamu au vile mwanadamu anaendelea katika kumfuata, na yeye husonga tu mbele katika kutimiza huduma Yake na kufanya kazi Anayopaswa kufanya. Hakuna Anayeweza kusimama mbele ya njia ya kazi Yake. Wakati muda unawadia wa kazi Yake kukamilika, ni muhimu kazi hiyo ikamilike na kufikishwa kikomo. Hakuna anayeweza kusema vinginevyo. Baada tu ya Yeye kuondoka kutoka kwa mwanadamu baada ya kukamilisha kazi Yake ndipo mwanadamu ataelewa kazi Anayofanya, ingawa hataifahamu kikamilifu. Na itachukua muda mrefu ndipo mwanadamu aelewe nia Yake Alipofanya kazi hiyo mara ya kwanza. Kwa maneno mengine, kazi ya enzi ambapo Mungu anageuka mwili imegawanywa katika sehemu mbili. Sehemu moja ni kupitia katika kazi na maneno ya Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Pindi tu huduma ya mwili Wake imetimika kikamilifu, sehemu nyingine ya kazi inatakiwa kutekelezwa na Roho Mtakatifu; basi utakuwa wakati wa mwanadamu kutimiza wajibu wake, kwa maana Mungu ameshafungua njia tayari, na lazima itembelewe na mwanadamu mwenyewe. Hiyo ni kusema, Mungu anageuka kuwa mwili ili kutekeleza sehemu moja ya kazi Yake, na inaendelezwa kwa urithi na Roho Mtakatifu na vile vile wale watu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu. Kwa hivyo mwanadamu anapaswa kujua kazi ya msingi inayopaswa kutekelezwa na Mungu mwenye mwili katika hatua hii ya kazi. Mwanadamu lazima aelewe hasa umuhimu wa Mungu kugeuka kuwa mwili na kazi Anayopaswa kufanya, badala ya kumuuliza Mungu ni nini kinachotakiwa kwa mwanadamu. Haya ni makosa ya mwanadamu, na vile vile fikira, na zaidi ya hayo, ni kutotii kwake.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (3)" katika Neno Laonekana Katika Mwili


    18. Mungu anakuwa mwili bila nia ya kumfanya mwanadamu apate kuujua mwili Wake, ama kukubali mwanadamu kutofautisha tofauti kati ya mwili wa Mungu mwenye mwili na ule wa mwanadamu; Mungu hapati mwili ili kufunza mwanadamu uwezo wa utambuzi, na zaidi nia ya mwanadamu kumwabudu Mungu mwenye mwili, ambayo kupitia kwayo atapata utukufu mkuu. Hakuna kati ya haya yaliyo mapenzi ya Mungu ya awali ya Mungu kuwa mwili. Mungu hawi mwili ili kulaani mwanadamu, kufichua mwanadamu akipenda, ama kufanya vitu kuwa vigumu kwa mwanadamu. Hakuna kati ya hayo lililo penzi la awali la Mungu. Kila wakati ambapo Mungu anakuwa mwili, ni kazi isiyo na budi. Ni kwa ajili ya kazi Yake kuu na usimamizi Wake mkuu ndio maana Anafanya hivyo, na si kwa sababu ambazo mwanadamu anafikiria. Mungu anakuja tu duniani Anavyohitajika na kazi Yake, na kila wakati ikiwa lazima. Haji duniani Akiwa na nia ya kuzurura, ila kutekeleza kazi ambayo Anapaswa kufanya. Mbona basi Ajipatie kazi hii ngumu na kujiweka katika hatari kubwa kufanya kazi hii? Mungu anakuwa mwili tu inapobidi, na kila wakati ikiwa na umuhimu wa kipekee. Kama ingekuwa tu kwa sababu ya kumfanya mwanadamu amuangalie na kufungua macho yao, basi kwa uhakika kabisa, hangekuja kati ya wanadamu kwa kubembeleza. Anakuja duniani kwa usimamizi Wake na kazi Yake kuu, na kuwa na uwezo wa kutwaa wanadamu zaidi. Anakuja kuwakilisha enzi na kumshinda Shetani, na ni katika mwili ndimo Anakuja kumshinda Shetani. Zaidi, Anakuja kuwaongoza binadamu wote katika maisha yao. Haya yote yanahusu uongozi Wake, na yanahusu kazi ya ulimwengu wote. Mungu angekuwa mwili ili tu kumruhusu mwanadamu kuja kuujua mwili Wake na kuyafungua macho ya mwanadamu, basi mbona Hangesafiri kwa kila taifa? Je hili sio jambo la wepesi zaidi? Lakini hakufanya hivyo, badala yake, Akachagua mahali palipofaa pa kuishi na kuanza kazi Aliyopaswa kufanya. Mwili huu pekee ni wa umuhimu mkuu. Anawakilisha enzi nzima, na Anatekeleza kazi ya enzi nzima; Analeta enzi ya zamani kufika tamati na kuikaribisha mpya. Haya yote ni mambo muhimu yanayohusu usimamizi wa Mungu, na ni umuhimu wa hatua ya kazi iliyotekelezwa na Mungu kuja duniani.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (3)" katika Neno Laonekana Katika Mwili


     19. Kazi ya kila enzi huanzishwa na Mungu Mwenyewe, lakini unapaswa kujua kwamba licha ya kazi yoyote ya Mungu, Yeye haji kuanzisha muungano au kufanya mikutano yoyote halisi au kuanzisha makundi ya aina yoyote kwa ajili yenu. Yeye huja tu kufanya kazi Anayopaswa kufanya. Kazi Yake haizuiliwi na mwanadamu yeyote. Yeye hufanya kazi Yake vile Anavyopenda; haijalishi kile mwanadamu anajua au kufikiri, Yeye hutilia maanani katika kutekeleza kazi Yake. Tangu kuumbwa kwa dunia, kumekuwa na hatua tatu za kazi; kutoka kwa Yehova mpaka kwa Yesu, na kutoka kwa Enzi ya Sheria mpaka kwa Enzi ya Neema, Mungu hajawahi kuitisha mkutano halisi kwa mwanadamu, wala hajawahi kuwakusanya wanadamu wote pamoja kufanya mkutano halisi wa ulimwengu ili kupanua kazi Yake. Yeye hufanya tu kazi ya mwanzo wa enzi nzima wakati muda na wakati na mahali uko sawa, na kupitia kwa hili Anaikaribisha enzi ili kuwaongoza wanadamu katika maisha yao. Mikutano halisi ni mikutano ya wanadamu; kuwakusanya watu pamoja kusherehekea siku kuu katika kazi za mwanadamu. Mungu hasherehekei siku kuu na, zaidi ya hayo, Anachukizwa nazo; Yeye haitishi mikutano halisi na zaidi ya hayo Anachukizwa nayo. Sasa lazima uelewe ni nini hasa kazi ya Mungu mwenye mwili!


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (3)" katika Neno Laonekana Katika Mwili


     20. Tabia yote ya Mungu imefichuliwa katika mpango wote wa uongozi wa miaka elfu sita. Haikufichuliwa tu katika Enzi ya Neema, ni katika Enzi ya Sheria tu, na zaidi ya hayo, ni katika wakati huu wa siku za mwisho. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inawakilisha hukumu, gadhabu na kuadibu. Kazi ifanywayo katika siku za mwisho haiwezi kuwekwa mbadala wa kazi ya Enzi ya Sheria ama ile ya Enzi ya Neema. Ingawa, hatua zote tatu zinaungana kuwa kitu kimoja na yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kawaida, utekelezaji wa kazi hizi umegawanyishwa katika enzi tofauti. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inaleta kila kitu mpaka tamati; ile iliyofanywa katika Enzi ya Sheria ni ya mwanzo; na ile iliyofanywa katika Enzi ya Neema ni ya ukombozi. Na kuhusu maono ya kazi katika mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita, hakuna anayeweza kupata ufahamu au kuelewa. Maono kama hayo yamebaki kuwa mafumbo kila wakati. Katika siku za mwisho, kazi ya neno pekee inafanyika ili kuukaribisha Wakati wa Ufalme lakini haiwakilishi enzi zile zingine. Siku za mwisho sio zaidi ya siku za mwisho na sio zaidi ya Enzi ya Ufalme, ambayo haiwakilishi Enzi ya Neema au Enzi ya Sheria. Siku za mwisho ni wakati ambapo kazi zote ndani ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita inafichuliwa kwenu. Mafumbo kama hayo hayawezi kufichuliwa na mwanadamu yeyote. Haijalishi mwanadamu ana maarifa makubwa ya Biblia vipi, yanabaki tu kuwa maneno na si kitu zaidi, kwani mwanadamu haelewi kiini cha Biblia. Mwanadamu anaposoma Biblia, anaweza kupokea baadhi ya ukweli, kueleza baadhi ya maneno ama kuchunguza vifungu maarufu na nukuu, lakini hatawahi kuwa na uwezo wa kunasua maana iliyoko katika maneno hayo, kwani yote aonayo mwanadamu ni maneno yaliyokufa pekee, sio matendo ya kazi ya Yehova na Yesu, na mwanadamu hawezi kufumbu mafumbo ya kazi ya aina hiyo. Kwa hivyo, fumbo la mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ni fumbo kuu, iliyofichwa zaidi na isiyosahawishika kwa mwanadamu. Hakuna anayeweza kuelewa moja kwa moja mapenzi ya Mungu, ama, Yeye Mwenyewe Aeleze na kumfungulia mwanadamu, vinginevyo, yatabaki kuwa mafumbo milele kwa mwanadamu na kubaki mafumbo yaliyofungwa milele. Usiwajali wale walio katika ulimwengu wa kidini; kama hamngeambiwa leo, pia nyinyi hamngeweza kuelewa.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili


      21. Kazi katika siku za mwisho ni hatua ya mwisho kati ya hizo tatu. Ni kazi ya enzi nyingine mpya na haiwakilishi kazi ya usimamizi mzima. Mpango wa miaka elfu sita umegawawa katika hatua tatu za kazi. Hakuna hatua moja pekee itakayowakilisha kazi ya enzi hizo tatu ila inaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya yote. Jina Yehova haliwezi kuwakilisha tabia yote ya Mungu. Ukweli kuwa Alitekeleza kazi katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kuwa Mungu Anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria. Yehova alitengeneza sheria kwa mwanadamu na kutoa amri, Akimuuliza mwanadamu ajenge hekalu na madhabahu; kazi Aliyofanya inawakilisha tu Enzi ya Sheria. Kazi Alioyoifanya haidhibitishi kuwa Mungu ni Mungu Anayemwamuru mwanadamu kufuata sheria, Mungu Aliye hekaluni, ama Mungu Aliye mbele ya madhabahu. Haya hayawezi kusemwa. Kazi chini ya sheria inaweza tu kuwakilisha enzi moja. Kwa hivyo, kama Mungu Alifanya kazi katika Enzi ya Sheria pekee, mwanadamu angemfafanua Mungu na kusema, "Mungu ni Mungu Aliye hekaluni. Ili kumtumikia Mungu, lazima tuvae mavazi ya kikuhani na tuingie hekaluni." Iwapo kazi katika Enzi ya Neema haingetekelezwa na Enzi ya Sheria ingeendelea mpaka wakati huu wa sasa, mwanadamu hangefahamu kuwa Mungu pia ni mwenye huruma na upendo. Iwapo kazi katika Enzi ya Sheria haingefanywa, na kwamba tu ile ya Enzi ya Neema ndiyo iliyofanywa, mwanadamu angefahamu tu kwamba Mungu Anakomboa mwanadamu na kumsamehe dhambi zake. Wangefahamu tu kuwa Yeye ni mtakatifu na asiye na hatia, kwamba Anaweza kujitoa kafara na kusulubishwa kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu angejua tu kuhusu haya na asiwe na ufahamu wa mambo mengine yoyote. Kwa hivyo kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu. Enzi ya Sheria inawakilisha vipengelele vingine, Enzi ya Neema vipengele vingine na enzi hii vipengele vingine. Tabia ya Mungu inaweza tu kuonekana kwa mchanganyiko wa hatua zote tatu. Ni wakati tu mwanadamu anajua hatua hizi tatu ndipo anaweza kuipokea kikamilifu. Hakuna hatua kati ya hizo tatu ambayo inaweza kuachwa. Utaiona tu tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake mara tu utakapozijua hatua hizi tatu za kazi. Mungu kukamilisha kazi yake katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kwamba Yeye ni Mungu chini ya sheria, na kukamilika kwa kazi Yake ya ukombozi haionyeshi kuwa Mungu Atamkomboa mwanadamu milele. Hizi zote ni hitimisho zilizofanywa na mwanadamu kuhusu jambo hilo. Enzi ya Neema imefika mwisho, lakini huwezi kusema kuwa Mungu ni wa msalaba tu na kuwa msalaba unawakilisha wokovu wa Mungu. Ukifanya hivyo, basi utakuwa unamfasili Mungu. Katika hatua hii, Mungu Anafanya zaidi kazi ya Neno, lakini huwezi kusema kuwa Mungu hajawahi kuwa Mwenye huruma kwa mwanadamu na kwamba yote Aliyoleta ni kuadibu na hukumu. Kazi katika siku za mwisho inaonyesha wazi kazi ya Yehova na ile ya Yesu na mafumbo yote yasioeleweka na mwanadamu. Hii inafanywa ili kuonyesha hatima na mwisho wa binadamu na kukamilisha kazi yote ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Hatua hii ya kazi katika siku za mwisho huleta kila kitu kufika mwisho. Mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu lazima yaelezwe ili kumpa mwanadamu ufahamu na kuweza kuelewa kwa kina katika mioyo yao. Hapo tu ndipo wanadamu wataweza kugawanywa kulinga na aina zao. Baada tu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilishwa ndipo mwanadamu atapata kuelewa tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake, kwani usimamizi Wake utakuwa umefika mwisho.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili


     22. Kazi yote iliyofanyika katika mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita imefika mwisho sasa. Ni baada tu ya kazi hii kubainika wazi kwa mwanadamu na kutekelezwa miongoni mwa wanadamu ndipo watakapofahamu tabia Yake na mali Yake na uwepo. Kazi za enzi hizi zitakapokamilika, mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu yatakuwa yamebainika, ukweli wote ambao haukuwa unaeleweka utawekwa wazi, na mwanadamu atakuwa ameambiwa njia na hatima ya baadaye. Hii ndio kazi yote inayopaswa kufanyika katika hatua hii.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili


    23. Kinachohitajika kutoka kwa mwanadamu wakati huu sio kama ilivyokuwa kitambo na zaidi sio kama kilichohitajika kutoka kwake katika Enzi ya Sheria. Na ni kipi kilichoulizwa kwa mwanadamu chini ya Sheria kazi ilipofanya Israeli? Hawakuulizwa cochote zaidi ya kuiheshimu Sabato na Sheria za Yehova. Lakini si hivyo katika wakati huu. Siku ya Sabato, mwanadamu anafanya kazi, hukusanyika na kuomba kama kawaida, na hakuna vizuizi vinavyowekwa. Wale katika Enzi ya Neema ilibidi wabatizwe; sio hilo tu, pia walitarajiwa kufunga, kuvunja mkate, kunywa divai, kufunika vichwa vyao na kuosha miguu yao. Sasa, sheria hizi zimefutwa na mahitaji makuu yanaulizwa kutoka kwa mwanadamu, kwani kazi ya Mungu inaendelea kuimarika na kuingia kwa mwanadamu kunafika kiwango cha juu. Zamani, Yesu Aliweka mikono Yake juu ya mwanadamu na kuomba, lakini sasa kwamba kila kitu kimesemwa, kuwekelea mikono kuna maana gani? Maneno pekee yanaweza kupata matokeo. Alipowekelea mikono Yake juu ya mwanadamu hapo awali, ilikuwa ni kwa ajili ya kumbariki na kumponya mwanadamu. Hivyo ndivyo Roho Mtakatifu Alivyofanya kazi wakati huo, lakini sio hivyo wakati huu. Wakati huu, Roho Mtakatifu Anatumia maneno katika kazi Yake ili kupata matokeo. Ameyafanya maneno Yake wazi kwenu, na mnapaswa tu kuyaweka katika matendo. Maneno Yake ni mapenzi Yake na yanaonyesha kazi Atakayofanya. Kupitia kwa maneno Yake, utaweza kuelewa mapenzi Yake na yale ambayo Anauliza upate. Unayaweka tu maneno Yake katika matendo moja kwa moja bila haja ya kuwekelea mikono. Wengine wanaweza kusema, "Wekelea mikono Yako juu yangu! Wekelea mikono yako juu yangu ili niweze kupokea baraka zako na kushiriki kwako." Haya yote ni mazoezi yaliyopitwa na wakati na na ambayo yanakataliwa katika wakati huu, kwani enzi zimebadilika. Roho Mtakatifu Anafanya kazi kulingana na enzi, sio tu katika mapenzi Yake ama kulingana na masharti. Enzi zimebadilika, na enzi mpya lazima ilete kazi mpya. Huu ni ukweli wa kila hatua ya kazi, na hivyo kazi Yake haiwezi kurudiwa. Katika Enzi ya Neema, Yesu Alifanya nyingi ya kazi hiyo, kama kuponya magonjwa, kukemea mapepo, kuwekelea mikono Yake juu ya wanadamu, na kumbariki mwanadamu. Hata hivyo, kuendelea kufanya hivyo hakutasaidia chochote katika wakati huu. Roho Mtakatifu Alifanya kazi hivyo katika huo wakati, kwani ilikuwa Enzi ya Neema, na mwanadamu alipewa neema ya kutosha ili afurahie. Mwanadamu hakuhitajika kulipa gharama yoyote na angepokea neema mradi tu angekuwa na imani. Kila mtu alitendewa kwa neema kubwa. Sasa, enzi imebadilika, na kazi ya Mungu imeendelea zaidi; kupitia kuadibu na hukumu Yake, uasi wa mwanadamu na vitu vichafu katika mwanadamu vitatupiliwa mbali. Jinsi ilivyokuwa hatua ya wokovu, ilimbidi Mungu kufanya kazi hiyo, Akimwonyesha mwanadamu neema ya kutosha ili mwanadamu afurahie, ili Amkomboe mwanadamu kutoka kwa dhambi, na kwa neema amsamehe mwanadamu dhambi zake. Hatua hii inafanywa ili kubaini kukoseka kwa usawa katika mwanadamu kupitia kuadibu, hukumu, kupigwa na maneno, na vile vile nidhamu na ufunuo wa maneno, ili baadaye waweze kuokolewa. Hii ni kazi ya undani zaidi kuliko ukombozi. Katika Enzi ya Neema, mwanadamu alifurahia neema ya kutosha na amezoea neema hii, kwa hivyo sio ya kufurahiwa na mwanadamu tena. Kazi kama hii imepitwa na wakati sasa na haitafanyika tena. Sasa, mwanadamu anaokolewa kupitia hukumu ya neno. Baada ya mwanadamu kuhukumiwa, kuadibiwa na kusafishwa, tabia yake basi inabadilika. Je sio kwa sababu ya maneno ambayo Nimenena? Kila hatua ya kazi inafanywa kulingana na maendeleo ya binadamu wote na kwa enzi. Kazi yote ina umuhimu wake; inafanywa kwa ajili ya wokovu wa mwisho, ili binadamu awe na hatima nzuri baadaye, na kwa mwanadamu kugawanywa kulingana na aina Yake mwishowe.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili


     24. Kazi katika siku za mwisho ni kunena maneno. Mabadiliko makuu yanaweza kusababishwa kwa watu kupitia katika maneno hayo. Mabadiliko yanayosababishwa sasa kwa watu hawa kwa sababu ya kukubali maneno haya ni makubwa kuliko yale ya watu katika Enzi ya Neema kwa kukubali ishara na maajabu hayo. Kwani, katika Enzi ya Neema, mapepo yaliondoka kutoka kwa mwanadamu kwa kuwekewa mikono na maombi, lakini tabia potovu ndani ya mwanadamu ilibaki. Mwanadamu aliponywa magonjwa na kusamehewa dhambi zake, lakini kazi ya jinsi tabia potovu za kishetani katika mwanadamu haikutupiliwa mbali na bado iko ndani yake. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini haimaanishi kuwa mwanadamu hana dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia potovu za zamani za kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili. Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwena Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na uonekano wa kiungu; kama mwanadamu angeishi katika huo msingi, alichukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, hii ina maana kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia ya kuielekea tabia iliyobadilika; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii inamfanya mwanadamu kuwa safi kupitia neno ili kumpatia mwanadamu njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendeleaa na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupuwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili


    25. Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguzwa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Na kama sio Mungu kuvalia umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, mwanadamu hawangeweza kupokea wokovu huu. Kwani mwanadamu hawezi kumkaribia kwa njia yoyote ile, zaidi kama jinsi hakuna anayeweza kukaribia wingu la Yehova. Ni kwa kuwa mwanadamu wa kuumbwa tu, hivyo ni kusema, kuliweka neno Lake katika mwili Atakaogeukana kuwa, ndio ataweza kulifanya neno yeye Mwenyewe ndani ya wale wote wanaomfuata. Hapo ndipo mwanadamu ataskia mwenyewe neno Lake, kuona neno Lake, na kupokea neno Lake, kisha kupitia hili aokolewe kamili. Kama Mungu hangegeuka na kupata mwili, hakuna mwanadamu mwenye mwili ambaye angepokea wokovu huo mkuu, wala hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye angeokolewa. Kama Roho wa Mungu angefanya kazi moja kwa moja kati ya mwanadamu, mwanadamu angepigwa ama kubebwa kabisa kama mfungwa na Shetani kwani mwanadamu hawezi kushirikiana na Mungu.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili


     26. Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho. Ni mpaka siku za mwisho tu ambapo Mungu Ametakasa binadamu kikamilifu kwa kufanya kazi ya hukumu na kuadibu mwanadamu kwa kuwa muasi, ndipo Mungu atakamilisha kazi Yake ya wokovu na kupumzika. Kwa hivyo, katika hatua tatu za kazi, ni mara mbili tu ndipo Mungu Alikuwa mwili ili kufanya kazi Yake kati ya mwanadamu Mwenyewe. Hiyo ni kwa sababu moja tu kati ya hatua tatu za kazi ni kuwaongoza wanadamu katika maisha yao, ihali zingine mbili ni kazi ya wokovu. Mungu Anapokuwa mwili tu ndipo Atakapoishi pamoja na mwanadamu, kuzoea mateso ya dunia, na kuishi katika mwili wa kawaida. Katika hali hii tu ndipo Ataweza kumpatia mwanadamu wa uumbaji Wake neon la matendo wanalohitaji. Mwanadamu anapokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sio moja kwa moja kutoka kwa maombi yao kwenda mbinguni. Kwani mwanadamu ni mwenye mwili; mwanadamu hawezi kuona Roho wa Mungu na pia kutoweza kumkaribia. Kile tu mwanadamu anaweza kushiriki na mwili wa Mungu; kupitia Yeye tu ndipo mwanadamu ataweza kuelewa maneno yote, na ukweli wote, na kupokea wokovu kamili. Kupatikana kwa mwili mara ya pili kunatosha kumaliza dhambi za mwanadamu na kumtakasa mwanadamu. Hivyo, kupatikana kwa mwili mara ya pili kutafikisha tamati kazi yote ya Mungu mwenye mwili na kukamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili. Baada ya hapo, kazi ya Mungu mwenye mwili itakuwa imefika mwisho kabisa. Baada ya kupata mwili mara ya pili, hatakuwa mwili tena kwa kazi Yake. Kwani usimamizi Wake wote utakuwa umefika mwisho. Katika siku za mwisho, mwili Wake utakuwa umepata watu Wake teule kabisa, na yote mwanadamu katika siku za mwisho watakuwa wamegawanywa kulingana na aina yao. Hatafanya kazi ya wokovu tena, wala Hatarudi kuwa mwili ili kutekeleza kazi yoyote.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili


      27. Katika kazi ya siku za mwisho, neno ni kubwa zaidi ya udhihirisho wa ishara na maajabu, na mamlaka ya neno yanashinda yale ya ishara na maajabu. Neno linaweka wazi tabia zote potovu katika moyo wa mwanadamu. Huwezi kutambua kivyako wewe mwenyewe. Yatakapofunuliwa kwako kupitia kwa neno, utakuja kujua mwenyewe; hutaweza kuyakataa, na na utashawishika kikamilifu. Je haya si mamlaka ya neno? Haya ndiyo matokeo yanayopatikana kwa kazi ya wakati huu ya neno. Kwa hivyo, mwanadamu hawezi kuokolewa kikamilifu kutoka kwa dhambi zake kwa kuponya magonjwa na kukemea mapepo na hawezi kufanywa mkamilifu kabisa kwa udhihirisho wa ishara na maajabu. Mamlaka ya kuponya na kukemea mapepo yanapatia mwanadamu neema tu, lakini mwili wa mwanadamu bado ni wa Shetani na tabia potovu za kishetani zitabaki ndani ya mwanadamu. Kwa maneno mengine, yale ambayo hayajatakaswa bado ni ya dhambi na uchafu. Ni baada tu ya mwanadamu kufanywa safi kupitia kwa maneno ndipo atakapotwaliwa na Mungu na kutakaswa. Lingine lisipofanywa ila kukemea mapepo katika mwanadamu na kumkomboa, huko ni kumshika tu kutoka kwa mikono ya Shetani na kumrudisha kwa Mungu. Hata hivyo, hajafanywa msafi ama kubadilishwa na Mungu, anabaki mpotovu. Ndani ya mwanadamu bado kuna uchafu, pingamizi na uasi; mwanadamu amerudi tu kwa Mungu kupitia kwa ukombozi, lakini mwanadamu hana maarifa kumhusu na bado anamkataa na kumsaliti Mungu. Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuutupa nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa. Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivyo, hata kama sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. … unaingia ndani zaidi kuliko dhambi, ulipandwa na Shetani na umekita mizizi ndani zaidi ya mwanadamu. Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" katika Mwili Neno Laonekana


      28. Kile ambacho mwanadamu amepata sasa—kimo cha mwanadamu leo, maarifa yao, upendo, uaminifu, utiifu, na pia kuona kwao—ni matokeo yanayopatikana kupitia hukumu kwa neno. Kwamba unaweza kuwa na uaminifu na kubaki umesimama mpaka siku hii ipatikane kwa kupita neno. Hivi sasa mwanadamu anaona kuwa kazi ya Mungu kupata mwili ni ya ajabu kweli. Kuna mengi ambayo hayawezi kupatikana na mwanadamu; ni mafumbo na maajabu. Kwa hivyo, wengi wamejiwasilisha. Wengine hawajawahi kujiwasilisha kwa mwanadamu yeyote kutoka siku za kuzaliwa kwao, ilhali wanapoyaona maneno ya Mungu siku hii, wanajiwasilisha kikamilifu bila kujua wamefanya vile, na hawajaribu kuchunguza au kusema chochote kingine. Mwanadamu ameanguka chini ya neno na chini ya hukumu kupitia kwa neno. Kama Roho wa Mungu angemwongelesha mwanadamu moja kwa moja, wote wangejiwasilisha kwa sauti hiyo, na kuanguka chini bila maneno ya ufunuo, vile Paulo alivyoanguka chini kukiwa na nuru alipokuwa akisafiri kwenda Damasko. Mungu angeendelea kufanya kazi kwa njia hii, mwanadamu hangeweza kutambua upotovu wake kupitia kwa hukumu katika neno na kupata wokovu. Ni kwa kupata mwili pekee ndiyo Ataweza kuwasilisha maneno Yake Mwenyewe kwa masikio ya wale wote ambao wana masikio waweze kuyasikia maneno Yake na kupokea kazi Yake ya hukumu kupitia kwa neno. Hayo tu ndio matokeo yanayopokewa na neno Lake, badala ya kutokea kwa Roho ikimtisha mwanadamu kuwasilisha. Ni kupitia tu kwa kazi ya vitendo na ya ajabu ndio tabia ya mwanadamu, iliyofichika ndani zaidi kwa enzi nyingi, ifichuliwe kabisa ili mwanadamu aitambue na kuibadilisha. Hili ndiyo kazi ya vitendo ya Mungu mwenye mwili wa Mungu; Ananena na kutekeleza hukumu juu ya mwanadamu kupitia kwa neno. Haya ndiyo mamlaka ya Mungu mwenye mwili na umuhimu wa Mungu kupata mwili. Inafanyika kuonyesha mamlaka ya Mungu mwenye mwili, matokeo yanayopatikana na kazi ya neno, na kwamba Roho Amekuja kwa mwili; Anaonyesha mamlaka Yake kupitia hukumu juu ya mwanadamu kwa neno. Ingawa mwili Wake ni hali ya nje ya mwanadamu wa kawaida, ni matokeo ambayo neno Lake linapokea ndiyo yanamwonyesha mwanadamu kuwa Amejaa mamlaka, kwama ni Mungu Mwenyewe na kwamba maneno Yake ni uelezo wa Mungu Mwenyewe. Hii inaonyesha wanadamu wote kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe, Mungu Mwenyewe Aliyekuwa mwili, na kwamba Hawezi kukosewa na yeyote. Hakuna anayeweza kuepuka hukumu Yake kupitia kwa neno, na hakuna nguvu ya giza inayoweza kutamalaki juu ya mamlaka Yake.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili


     29. Anakuwa mwili kwani mwili pia unaweza kuwa na mamlaka, na Anaweza kutekeleza kazi kati ya wanadamu katika halii ya njia halisi, inayoonekana na kuguswa na mwanadamu. Kazi kama hii ni ya ukweli kuliko kazi ingine yoyote ifanywayo moja kwa moja na Roho wa Mungu Aliye na mamlaka yote, na matokeo Yake ni dhahiri pia. Hii ni kwa sababu mwili Wake unaweza kuongea na kufanya kazi kwa njia halisi; hali ya nje ya mwili Wake haina mamlaka yoyote na inaweza kukaribiwa na mwanadamu. Dutu Yake inabeba mamlaka, lakini mamlaka Yake hayaonekani kwa yeyote. Anaponena na kufanya kazi, mwanadamu hana uwezo wa kutambua uwepo wa mamlaka Yake; hili ni nzuri kwa kazi Yake hata zaidi. Na kazi yote kama hiyo inaweza kupata matokeo. Ingawa hakuna mwanadamu anayefahamu kuwa Anayo mamlaka ama kuona kuwa hawezi kukosewa ama kuona hasira Yake, kupitia mamlaka Yake yaliyofichika na hasira na hotuba ya uma, Anapata matokeo yaliyotarajiwa ya neno Lake. Kwa maneno mengine, kupitia kwa tani ya sauti Yake, ukali wa hotuba Yake, na hekima ya maneno Yake, mwanadamu anashawishika kabisa. Kwa njia hii, mwanadamu anawasilisha kwa neno la Mungu mwenye mwili wa Mungu, ambaye anaonekana kutokuwa na mamlaka, hivyo kufikia lengo Lake la wokovu kwa mwanadamu. Huu ndio umuhimu mwingine wa kuingia Kwake katika mwili: kuongea na ukweli zaidi na kukubali ukweli wa neno Lake kuwa na athari juu ya mwanadamu ili kushuhudia nguvu ya neno la Mungu. Kwa hivyo kazi hii, isipofanywa kupitia kupata mwili, haitakuwa na matokeo hata kidogo na haitaweza kuokoa watenda dhambi kikamilifu. Mungu Asipokuwa mwili, Atabaki kama Roho bila kuonekana au kuguswa na mwanadamu. Mwanadamu ni kiumbe wa mwili, na mwanadamu na Mungu ni wa dunia mbili tofauti na ni tofauti kwa asili. Roho wa Mungu hana uuwiano na mwili wa mwanadamu, na hakuna uhusiano unaoweza kuwepo kati yao; pia, mwanadamu hawezi kuwa roho. Hivyo, Roho wa Mungu lazima ageuke mmoja wa viumbe na kufanya kazi yake ya asili. Mungu anaweza kujipandisha mahali pa juu zaidi na pia aweze kunyenyekea na kuwa mwanadamu aliyeumbwa, kufanya kazi na kuishi kati ya wanadamu, laikini mwanadamu hawezi kupanda juu na kuwa roho na pia kuteremka chini. Kwa hivyo, Mungu lazima awe mwili ili atekeleze kazi Yake. Kama ilivyokuwa wakati wa kuingia katika mwili mara ya kwanza, mwili wa Mungu mwenye mwili pekee ndio unaoweza kumkomboa mwanadamu kupitia kusulubiwa, ilhali hakuna uwezo wa Roho wa Mungu kusulubiwa kama sadaka ya dhambi kwa mwanadamu. Mungu Angekuwa mwili moja kwa moja ili kuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu, lakini mwanadamu hangepanda mbinguni moja kwa moja kuchukua sadaka ambayo Mungu alikuwa amewaandalia. Hivyo, lazima Mungu asafiri kwenda na kurudi kati ya mbingu na nchi, badala ya kumwacha mwanadamu apande mbinguni kuchukua wokovu huu, kwani mwanadamu alikuwa ameanguka na hangepanda mbinguni, ama hata kupata sadaka ya dhambi. Kwa hivyo, ilikuwa lazima kwa Yesu kuja kati ya wanadamu na binafsi kufanya kazi ambayo mwanadamu hangeweza kukamilisha. Kila wakati ambapo Mungu aligeuka kuwa mwili, ilikuwa lazima kabisa Afanye hivyo. Iwapo hatua yoyote ingetekelezwa moja kwa moja na Roho wa Mungu, Hangevumilia ukosefu wa hadhi unaoambatana na kupata mwili.


kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili


      30. Katika hatua hii ya mwisho ya kazi, matokeo yanapatikana kupitia kwa neno. Kupitia kwa neno, mwanadamu anaelewa mafumbo mengi na kazi ya Mungu katika vizazi vilivyopita; kupitia kwa neno, mwanadamu anapewa nuru na Roho Mtakatifu; kupitia kwa neno, mwanadamu anapata kuelewa mafumbo ambayo hayajawahi kuelezwa na vizazi vilivyopita, na pia kazi za manabii na, mitume wa enzi zilizopita, na kanuni ambazo walitumua kufanya kazi; kupitia kwa neno, mwanadamu anatambua tabia ya Mungu Mwenyewe, na pia uasi na pingamizi ya mwanadamu, na kujua dutu yao. Kupitia kwa hatua hizi za kazi na maneno yote yaliyonenwa, mwanadamu anatambua kazi ya Roho Mtakatifu, kazi ya mwili wa Mungu, na zaidi ya hayo, tabia Yake yote. Maarifa yako ya kazi ya usimamizi wa Mungu wa kupita miaka elfu sita ulitwaliwa kupitia kwa neno. Je, maarifa yako hayakuwa ya fikira zako za awali na mafanikio kwa kuyaweka kando pia yalipatikana kupitia neno? Katika hatua ya awali, Yesu Alifanya ishara na maajabu, lakini sio hivyo katika hatua hii. Je si kuelewa kwako kwa nini Hafanyi hivyo pia kulipatikana kupitia neno? Kwa hivyo, maneno yanenwayo katika hatua hii, yanashinda kazi iliyofanywa na mitume na manabii wa vizazi vilivyopita. Hata unabii uliotabiriwa na manabii haungeweza kupata matokeo haya. Manabii waliongelea unabii pekee, ya kile kitakachotendeka hapo baadaye, lakini sio kazi ambayo Mungu angefanya katika wakati huo. Hawakuongea kuongoza mwanadamu katika maisha yao, kuhifadhi ukweli juu ya mwanadamu ama kumfichulia mwanadamu mafumbo, ama hata kutawaza maisha. Kwa maneno yaliyonenwa katika hatua hii, kuna unabii na ukweli, lakini hasa yanafanya kazi ya kutawaza maisha juu ya mwanadamu. Maneno ya wakati huu sio kama unabii wa manabii. Hii ni hatua ya kazi isioya unabii ila ya maisha ya mwanadamu, kubadili tabia ya maisha ya mwanadamu. Hatua ya kwanza ilikuwa kazi ya Yehova kutengeneza njia ya mwanadamu kuabudu Mungu duniani. Ilikuwa kazi ya kuanzisha kutafuta chanzo cha kazi duniani. Wakati huo, Yehova aliwafunza Waisraeli kuiheshimu Sabato, kuwaheshimu wazazi wao na kuishi kwa amani na wengine. Kwa kuwa wanadamu wa wakati huo hawakuwa wanaelewa kiini cha mwanadamu, wala hawakuelewa wanavyopaswa kuishi duniani, ilikuwa lazima Kwake katika hatua ya kwanza ya kazi kuwaongoza wanadamu katika maisha yao. Yote yale Yehova aliwazungumzia hayakuwa yamewahi kujulikana kwa binadamu ama kuwa katika umiliki wao. Wakati huo, manabii wengi walisimamishwa kuongelea unabii, yote kutengenezwa chini ya uongozi wa Yehova. Hii ilikuwa sehemu ya kazi hiyo. Katika hatua ya kwanza, Mungu hakuwa mwili, hivyo Alizungumza na makabila yote na mataifa kupitia kwa manabii. Yesu alipofanya kazi Yake katika huo wakati, Hakuzungumza sana kama wakati huu wa leo. Kazi hii ya neno katika siku za mwisho haijafanyika katika enzi na vizazi vilivyopita. Ingawa Isaya, Danieli na Yohana walitabiri utabiri mwingi, unabii huo ulikuwa tofauti kabisa na maneno yazungumzwayo sasa. Walichoongelea ulikuwa unabii pekee, lakini maneno ya sasa sio unabii. Iwapo Ningebadilisha Ninayoongea sasa yawe unabii, je mngeweza kuyaelewa? Iwapo ningezungumzia mambo ya usoni, maneno ya baada ya mimi kuondoka, utawezaje kupata kuelewa? Kazi ya neno haikuwahi kufanyika wakati wa Yesu ama Enzi ya Sheria. Labda wengine wanaweza kusema, "Je Yehova hakuzungumza maneno pia katika wakati wa kazi Yake? Juu yaa kuponya magonjwa, kukemea mapepo na kufanya ishara na maajabu, je Yesu hakuzungumza katika wakati huo?" Kuna tofauti katika vile maneno yananenwa. Ni nini ndiyo ilikuwa dutu ya maneno yaliyonenwa na Yehova? Alikuwa tu anawaongoza wanadamu katika maisha yao duniani, ambayo hayakuwa yanahusiana na mambo ya kiroho katika maisha. Ni kwa nini inasemekana kuwa maneno ya Yehova yalitangazwa katika sehemu zote? Neno "kutangazwa" linamaanisha kutoa maelezo kamili na maelezo ya moja kwa moja. Hakupa mwanadamu maisha; ila, Alimchukua mwanadamu kwa mkono na kumfunza jinsi ya kumheshimu sana. Hakukuwa na mafumbo. Kazi ya Yehova katika Israeli haikuwa kushughulika na ama kumwadhibu mwanadamu ama kutoa hukumu na kuadibu; ilikuwa kuongoza. Yehova alimwambia Musa awaeleze watu Wake wakusanye mana jangwani. Kila asubuhi kabla ya jua kuchomoza, walikuwa wakusanye mana, iliyotosha tu kuliwa siku hiyo. Mana haingewekwa hadi siku inayofuata, kwani ingeoza. Hakuwafunza wanadamu kufichua asili zao, na Hakufichua mawazo yao na fikira. Hakuwabadilisha wanadamu ila tu aliwaongoza katika maisha yao. Katika wakati huo, mwanadamu alikuwa kama mtoto; mwanadamu hakuelewa chochote na angefanya hatua za kuelekezwa; kwa hivyo, Yehova aliamuru tu sheria kuongoza watu. Iwapo unataka kueneza injili ili wale wote wanaotafuta kwa moyo wa kweli wapate maarifa ya kazi inayofanywa katika siku hii na kushawishika kabisa, basi lazima uielewe hadithi ya ndani, dutu na umuhimu wa kazi iliyofanywa katika kila hatua. Kwa kusikia ushirika wako, wataelewa kazi ya Yehova na kazi ya Yesu na, zaidi ya hayo, kazi yote inayofanywa wakati huu, na vilevile uhusiano na tofauti kati ya hatua hizo tatu za kazi, ili kwamba, baada ya wao kisikiza, wataona kuwa hakuna hatua yoyote kati ya hizo tatu inahitilafiana na nyingine. Kwa hakika, yote yamefanywa na Roho mmoja. Ingawa Walitekeleza kazi tofauti katika enzi tofauti na kuzungumza meneno yasiofanana, kanuni ambazo Walifuata katika kazi hizi zilikuwa sawa. Haya ndiyo maono makuu zaidi ambayo watu wote wanapaswa kuelewa.

kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni