5. Ni zipi tofauti muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na hao watu ambao hutumiwa na Mungu?
Aya za Biblia za Kurejelea:
"Mimi nawabatiza na maji ili mtubu. Lakini yule ajaye baada ya mimi ni mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye sistahili kuvichukua viatu vyake. Atawabatiza na Roho Mtakatifu, na moto" (MT 3:11).
Maneno Husika ya Mungu:
Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe. …
… Yote yanayomuasi Mungu yanatoka kwa Shetani; Shetani ni chanzo cha ubaya na uovu wote. Sababu kwamba mwanadamu anayo sifa sawa na ile ya Shetani ni kwa sababu mwanadamu amelagaiwa na kufinyangwa Shetani. Kristo hajawahi kupotoshwa na Shetani, hivyo Anazo tu tabia za Mungu na hakuna hata moja ya Shetani.
kutoka kwa "Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa sababu ni mwanadamu mwenye kiini cha Mungu, Yuko juu ya wanadamu wote walioumbwa, juu ya mwanadamu yeyote anayeweza kutekeleza kazi ya Mungu. Kwa hivyo, miongoni mwa wale wote walio na umbo la binadamu kama Lake, miongoni mwa wale wote walio na ubinadamu, Yeye pekee ndiye Mungu mwenye mwili Mwenyewe—wengine wote ni wanadamu walioumbwa. Japokuwa wote wana ubinadamu, wanadamu walioumbwa si chochote zaidi ya wanadamu, ilhali Mungu mwenye mwili ni tofauti: katika mwili Wake, si tu kwamba ana ubinadamu ila pia muhimu zaidi Ana uungu.
kutoka kwa "Kiini cha Mwili Ulio na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Uungu wa Kristo ni zaidi ya wanadamu wote, kwa hivyo Yeye Anayo mamlaka ya juu ya viumbe vyote vilivyoumbwa. Mamlaka haya ni uungu Wake, yaani, nafsi na tabia ya Mungu Mwenyewe, ambayo huamua utambulisho Wake.
kutoka kwa "Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa kuwa Mungu ni mtakatifu na safi, na halisi na wa kweli, mwili Wake unatoka kwa Roho. Hili ni wazi, na bila shaka. Sio tu kuweza kushuhudia kwa Mungu Mwenyewe, bali pia kuweza kutekeleza kabisa mapenzi ya Mungu: huu ni upande mmoja wa dutu ya Mungu. Kwamba mwili unatoka kwa Roho na sura kuna maana kwamba mwili ambao Roho anajivisha ni tofauti kimsingi na mwili wa mwanadamu, na tofauti hii hasa iko ndani ya roho zao.
kutoka kwa "Ufafanuzi wa Tamko la Tisa" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu ni mwili wa Mungu mwenyewe. Roho wa Mungu ni mkubwa, Yeye ni mwenyezi, mtakatifu, na mwenye haki—na vilevile ndivyo ambavyo mwili Wake ulivyo pia mkubwa, wenye uwezo, mtakatifu, na wenye haki. Mwili kama huo unaweza kufanya tu kile ambacho ni chenye haki na manufaa kwa mwanadamu, kile ambacho ni kitakatifu, chenye utukufu, na uweza, na hakiwezi kukifanya chochote ambacho kinakiuka ukweli au uadilifu na haki, isitoshe hata kile ambacho kinaasi dhidi ya Roho wa Mungu. Roho wa Mungu ni mtakatifu, na hivyo basi mwili Wake hauwezi kuharibiwa na Shetani; mwili Wake una kiini tofauti na ule mwili wa mwanadamu. Kwani ni mwanadamu, wala si Mungu, ambaye anaharibiwa na Shetani, na mwili wa Mungu usingeweza kuharibiwa na Shetani. Kwa hivyo, licha ya ukweli kwamba mwanadamu na Kristo wanakaa mahala pamoja, ni mwanadamu tu ndiye ambaye anatawaliwa, anatumiwa, na kutegwa na Shetani. Kinyume cha hayo, Kristo daima hapenyezwi na uovu wa Shetani, kwa kuwa Shetani hataweza kamwe kupaa hadi mahala pa aliye juu zaidi, na hataweza kumkaribia Mungu. Leo, nyote mnapaswa kuelewa kuwa ni mwanadamu tu, aliyepotoshwa na Shetani, ambaye ananisaliti, na kwamba daima tatizo hili halitakuwa linamhusu Kristo.
kutoka kwa "Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa sababu wanadamu ni, kwa hakika, binadamu, na wanaweza tu kuangalia kila kitu kutoka kwa mtazamo na kutoka katika kimo cha mtu. Hata hivyo, Mungu mwenye mwili ni tofauti kabisa na mtu aliyepotoka. Bila kujali ni vipi ambavyo mwili wa Mungu mwenye mwili ulivyo wa kawaida, ulivyo kama wengine, ulivyo wa chini, au hata namna ambavyo watu wanamdharau Yeye, fikira Zake na mwelekeo Wake kwa wanadamu ni mambo ambayo hakuna binadamu angeweza kufuatisha na wala hakuna binadamu angeweza kuiga. Siku zote Atawaangalia wanadamu kutoka kwa mtazamo wa uungu, kutoka katika kimo cha madaraka Yake kama Muumba. Siku zote Atawaona wanadamu kupitia katika kiini na akili ya Mungu. Hawezi kabisa kuwaona wanadamu kutoka katika kimo cha mtu wa kawaida na kutoka kwa mtazamo wa mtu aliyepotoka. Wakati watu wanapowaangalia wanadamu, wanawaangalia kwa mtazamo wa binadamu, na wanatumia mambo kama vile maarifa ya mwanadamu na masharti na nadharia za wanadamu kama kipimo. Hali hii imo ndani ya mawanda ya kile ambacho watu wanaweza kuona kwa macho yao; ni ndani ya upana ambao watu waliopotoka wanaweza kutimiza. Wakati Mungu anapowatazama wanadamu, Anawatazama kwa macho ya kiungu, na Anatumia kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho kama kipimo. Mawanda haya yanajumuisha mambo ambayo watu hawawezi kuona, na hapo ndipo Mungu mwenye mwili na wanadamu waliopotoka walivyo tofauti kabisa. Tofauti hii inaamuliwa na viini tofauti vya wanadamu na vya Mungu na ndivyo vinavyoamua utambulisho na nafasi zao pamoja na mtazamo na kimo ambacho wanaona mambo.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III" katika Neno Laonekana katika Mwili
Yeye ambaye Anafanya kazi katika Uungu Anawakilisha Mungu, ilhali wale wanaofanya kazi katika ubinadamu ni wanadamu wanaotumiwa na Mungu. Yaani, Mungu katika mwili ana utofauti halisi na wanadamu wanaotumiwa na Mungu. Mungu mwenye mwili Anaweza kufanya kazi ya Uungu, lakini wanadamu wanaotumiwa na Mungu hawawezi. Mwanzoni mwa kila enzi, Roho wa Mungu anaongea binafsi kuzindua enzi mpya na kuleta mwanadamu kwenye mwanzo mpya. Wakati Yeye Atamaliza mazungumzo Yake, itaashiria kwamba kazi ya Mungu katika Uungu imekamilika. Baada ya hapo, wanadamu wote hufuata mwongozo wa wale hutumiwa na Mungu kuingia katika uzoefu wa maisha.
kutoka kwa "Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Japo Mungu mwenye mwili Ana akili ya mwanadamu wa kawaida, kazi Yake haijatiwa doa na mawazo ya kibinadamu; Anafanya kazi katika kibinadamu na akili ya kawaida chini ya masharti ya awali kuwa atakuwa na ubinadamu na akili ya kawaida, na si na mawazo ya kawaida ya kibinadamu. Haijalishi mawazo ya mwili Wake ni bora kiasi gani, kazi Yake haionyeshi alama ya mantiki au kufikiria. Kwa maneno mengine, kazi Yake haiwazwi na akili ya mwili Wake, ila ni onyesho la moja kwa moja la kazi ya uungu katika ubinadamu Wake. Kazi yake yote ni huduma Anayostahili kutimiza, na haiwazwi hata chembe kwa akili Zake. Kwa mfano, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kusulubishwa hayakuwa mazao ya akili Zake za kibinadamu, yasingeweza kutimizwa na mwanadamu yeyote mwenye akili za kibinadamu. Vivyo hivyo, kazi ya ushindi ya leo ni huduma ambayo ni sharti itekelezwe na Mungu mwenye mwili, lakini si kazi ya mapenzi ya mwanadamu, ni kazi ambayo uungu Wake unapaswa kufanya, kazi ambayo hakuna mwanadamu wa mwili anaiweza.
kutoka kwa "Kiini cha Mwili Ulio na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Tangu mwanzo, wanadamu ambao Mungu Ametumia wote wana mawazo ya kawaida na fikra. Wao wote wanajua jinsi ya kujiendesha na kushughulikia mambo ya maisha. Wanashikilia itikadi za kawaida za binadamu na kuwa na vitu vyote ambavyo wanadamu wa kawaida wanapaswa kuwa navyo. Wengi wao wana vipaji vya pekee na werevu wa kiasili. Kwa kufanya kazi kupitia wanadamu hawa, Roho wa Mungu Anakusanya na kutumia vipaji vyao, ambavyo ni zawadi yao Aliyowapa Mungu. Ni Roho wa Mungu Ndiye Anayeleta vipaji vyao katika kazi, na kuwasababisha kutumia uwezo wao kumhudumia Mungu. Hata hivyo, kiini cha Mungu hakina itikadi na hakina fikira. Hakiungani na mawazo ya binadamu na hata kinakosa vitu ambavyo binadamu wa kawaida huwa navyo. Yaani, Mungu hata hafahamu vizuri kanuni za maadili ya binadamu. Hivi ndivyo ilivyo Mungu wa leo Anapokuja duniani. Kazi Yake na maneno Yake hayajachafuliwa na nia au fikira za binadamu, bali ni dhihirisho la moja kwa moja la Roho, na Anafanya kazi moja kwa moja kwa niaba ya Mungu. Hii ina maana Roho huja kufanya kazi, ambayo Haweki ndani mawazo ya mwanadamu hata kidogo. Yaani, Mungu katika mwili Anajumuisha Uungu moja kwa moja, Hana mawazo ya binadamu au itikadi, na Haelewi kanuni za maadili ya binadamu. Kama kungekuwa na kazi ya Uungu tu (kumaanisha iwapo ingekuwa Mungu mwenyewe pekee ndiye Anayefanya kazi hiyo), kazi ya Mungu haingeweza kufanyika duniani. Kwa hivyo Mungu Anapokuja duniani, lazima Awe na wanadamu wachache Anaowatumia kufanya kazi katika ubinadamu pamoja na kazi Yake katika Uungu. Kwa maneno mengine, Yeye Anatumia kazi ya mwanadamu ili kusaidia kazi Yake takatifu. La sivyo, mwanadamu hangeweza kuja katika mawasiliano ya moja kwa moja na kazi ya Mungu.
kutoka kwa "Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya wanadamu wanaotumiwa pia ni kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwamba tu kazi ya Mungu ni dhihirisho kamili la Roho Mtakatifu, na hakuna tofauti, ilhali kazi ya wanadamu wanaotumiwa inachanganyika na mambo mengi ya kibinadamu, na wala sio udhihirishaji wa moja kwa moja wa Roho Mtakatifu, wala udhihirishaji kamili. … Roho Mtakatifu anapofanya kazi kwa wanadamu wanaotumika, karama zao na tabia zao halisi zinatumiwa pia na wala haziachwi. Tabia zao halisi zinatumiwa zote kwa ajili ya kutoa huduma kwa kazi. Tunaweza kusema kuwa Anafanya kazi kwa kutumia sehemu zilizopo za wanadamu ili kupata matokeo yatendayo kazi. Kinyume chake, kazi inayofanyika katika mwili uliopatikana ni kumdhihirisha moja kwa moja Roho na wala haichanganywi na akili na mawazo ya mwanadamu, haifikiwi na karama za mwanadamu, uzoefu wa mwanadamu au hali ya ndani ya mwanadamu.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna anayeishi katika mwili anayeweza kumwakilisha Mungu kwa njia ya moja kwa moja isipokuwa kama yeye ni binadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo, hata tabia ya mtu kama huyo na kile anachoishi kwa kudhihirishwa chote hakiwezi kuchukuliwa kwamba kinamwakilisha Mungu kabisa; inaweza kusemekana tu kwamba kile anachoishi kwa kudhihirishwa kinatawaliwa na Roho Mtakatifu. Tabia ya mtu kama huyo haiwezi kumwakilisha Mungu.
…………
… Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwakilishi tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu, ilhali tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu. Kazi ambayo Mungu hufanya ndani yao ni kule tu kufanya kazi na pamoja na kupanua kile ambacho tayari kimo ndani yao. Wawe ni manabii kutoka kwenye enzi zilizopita au binadamu wanaotumiwa na Mungu, hakuna yeyote anayeweza kumwakilisha Mungu kwa njia ya moja kwa moja. … binadamu yeyote aliye na asili ya dhambi hawezi kumwakilisha Mungu, na kwamba dhambi ya binadamu inamwakilisha Shetani. Hiyo ni kusema kwamba dhambi haimwakilishi Mungu na Mungu hana dhambi. Hata kazi inayofanywa ndani ya binadamu na Roho Mtakatifu inaweza tu kuchukuliwa kuwa imetawaliwa na Roho Mtakatifu na haiwezi kusemwa kwamba ilifanywa na binadamu kwa niaba ya Mungu. Kwa kadri ambavyo binadamu anahusika, si dhambi yake wala tabia yake inamwakilisha Mungu.
kutoka kwa "Mtu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni