5/26/2018

Umeme wa Mashariki | Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

Umeme wa Mashariki | Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Wuzhi    Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong
Katika majira ya kuchipua ya mwaka wa 2006, nilinyang'anywa cheo changu kama kiongozi na nikarudishwa nilikotoka kwa sababu nilifikiriwa kuwa "bwana ndiyo" sana. Niliporejea mara ya kwanza, nilitumbukia ndani ya kikalibu cha mateso na maumivu makubwa. Sikuwahi kufikiri kwamba baada ya miaka mingi ya uongozi mambo yangeharibika kwa sababu ya kuwa "bwana ndiyo." Huu ulikuwa ndio mwisho kwangu, nilidhani, kila mtu aliyenijua angejua juu ya kushindwa kwangu na ningefanywa kama mfano mbaya katika kanisa. Ningewezaje kukabiliana na wengine baada ya haya yote? Jinsi nilivyozidi kufikiria, ndivyo nilivyozidi kuwa hasi, mpaka hatimaye nikapoteza imani ya kuendelea kutafuta ukweli. Hata hivyo, wakati nilifikiri juu ya sadaka zote na matumizi niliyoyatoa katika miaka hii michache iliyopita, sikuweza kushawishika kuondoka. Kama nikijimaliza kabisa na kukubali kushindwa, si jitihada zangu zote zitakuwa bure? Si watu watanidunisha hata zaidi? Siwezi kuruhusu hilo lifanyike! Ni lazima nijitetee na nisiwaache wengine waniangalie kwa dharau. Sasa, bila kujali ni jinsi gani ninavyopaswa kujitahidi, ni makosa mangapi yanayonipata, ni lazima nifanye haraka—siwezi kuondoka nusu njia! Almradi ninakumbuka mafundisho ya kushindwa na kuzingatia kutafuta ukweli, labda siku moja naweza kuwa kiongozi tena. Mawazo haya yakiwa katika kumbukumbu, uhasi wote na huzuni zilififia na nilihisi nguvu iliyofanywa upya katika ukimbizaji wangu.
Kutoka wakati huo kuendelea, nilifanya kazi saa nyingi kila siku, kwa bidii nikila na kunywa neno la Mungu ili kujiandaa na ukweli wakati nikitafakari na kufanya utambuzi katika makosa yangu ya zamani. Niliandika insha nyingi mno zikieleza uzoefu wangu wa maisha, pamoja na mahubiri. Muda mfupi baadaye, nilipoona kwamba mbili kati ya insha zangu zilikuwa zimechaguliwa, nilihisi imani hata zaidi katika ukimbizaji wangu. Nilijifikiria mwenyewe: Endelea tu kufanya kazi na hivi karibuni sana ndoto yangu itakuja kuwa. Kwa njia hiyo, niliendelea katika ukimbizaji wangu na nilihisi nimefarijiwa kuwa hali yangu ilikuwa imerudi kuwa takribani "ya kawaida".
Siku moja wakati wa kukuzwa kwa roho, nilivutiwa na kifungu fulani cha neno la Mungu: “Kama utajielewa, ni lazima uielewe hali yako ya kweli; jambo muhimu zaidi katika kuielewa hali yako mwenyewe ni kuwa na ufahamu juu ya fikira zako na mawazo yako. Katika kila kipindi cha muda, fikira za watu zimekuwa zikidhibitiwa na jambo moja kubwa; ikiwa unaweza kuzielewa fikira zako, unaweza kukielewa kitu kilicho nyuma yazo” (“Watu Ambao Daima Wana Mahitaji kwa Mungu Ndio wa Mwisho Kuwa Tayari Kusikia Hoja” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nikiwaza juu ya neno la Mungu, ghafla niligeuza swali kwangu mwenyewe: Ni nini kinachotawala mawazo yangu sasa? Ni nini kilicho ndani ya mawazo yangu yote? Nilianza kutafakari kwa uangalifu juu ya mchakato wangu wa mawazo na, kwa uongozi wa Mungu, nilikuja kutambua kuwa tangu nilipobadilishwa, mawazo yangu yalikuwa yametawaliwa na tamaa ya kwamba "ni lazima nipate tena kwa juhudi sifa yangu ya zamani na hadhi yangu na nijitetee. Siwezi kuendelea kuangaliwa kwa dharau na wengine." Wazo hili lilikuwa kama nguzo ya kiroho, likiniruhusu kustahimili katika kikalibu cha kukata tamaa kwangu na kunipa msukumo wa kufuatilia lengo langu. Nikiwa na wazo hili katika kumbukumbu, nilikuwa nimebakia "thabiti na asiyekubali kushindwa" chini ya mfululizo wa daima wa "matusi na aibu." Wakati huu, nilitambua kwamba ukimbizaji wangu ulikuwa mchafu, uliojaa tamaa na usiokuwa mzuri hata chembe.
Nikifikiria nyuma, naona kwamba Mungu alikuwa amenifichua ili kuniruhusu kutafakari juu yangu mwenyewe na kuelewa asili yangu mwenyewe ya kishetani ili niweze kuwa na msingi dhabiti na wazi katika ukimbizaji wangu wa ukweli, kutupa uovu na dhambi na kupokea wokovu wa Mungu. Hata hivyo, kwa hakika sikumshukuru Mungu kwa zawadi Yake ya wokovu, wala kujichukia mwenyewe kwa maovu niliyoyafanya. Aidha, sikujilaumu au kuhisi kujuta kwa ajili ya kushindwa kufikia matarajio ya matumaini ya Mungu. Badala yake, nikiendeshwa na asili ya kiburi kwamba "ni lazima nishinde kwa vyovyote," Nilijiingiza katika upangaji wa njama hii, nikifikiria tu siku ambapo ningepanda ngazi tena, kuteuliwa tena kama kiongozi, na kurejesha sifa ambayo nilikuwa nimeiharibu kabisa. Kwa ufanisi, nilikuwa na matumaini ya kujenga upya mfano wa kishetani wangu mwenyewe kwa wengine kuupenda na kuuabudu. Kwa hakika, nilikuwa na tama kubwa—kubwa sana kiasi kwamba nilikuwa radhi kupigana ngumi na Mungu mpaka mwisho kabisa. Nilikuwa na kiburi kupita kiasi na sikuwa na uchaji hata kidogo au kumuogopa Mungu ndani ya moyo wangu. Kutafakari nyuma juu ya hali yangu ya zamani, woga ulinijaa. Singewahi kufikiri kwamba tamaa kama hiyo isiyowezekana ilisababisha mawazo yangu. Si ajabu kwamba Mungu alisema, “ikiwa unaweza kuzielewa fikira zako, unaweza kukielewa kitu kilicho nyuma yazo.” Kweli. Katika siku za nyuma, niliona mawazo yangu kuwa dhana za muda mfupi tu na kamwe sikuchukua muda kuyachambua na kuyaelewa. Ni sasa tu ninapoelewa kwamba kuyafahamu mawazo ya mtu na kuyachambua kikamilifu mambo yaliyoshikiliwa ndani ya moyo wa mtu ni muhimu sana kwa kuelewa asili ya ndani ya mtu!
Asante Mungu kwa kunurishwa huku, ambako kumeniinua kutoka kwa upofu. Kama sivyo, ningekuwa bado ningehadaiwa na udanganyifu wangu mwenyewe—nikiinuka mbele na tamaa pofu kwelekea kwa mauti yangu ya karibu sana. Ni gutuko lililoje la kushangaza! Katika mchakato huo, nilitambua pia kwamba kwa kunibadilisha, Mungu alikuwa akinilinda na kunipa wokovu. Kwa mtu aliye na kiburi na lengo lenye jazba hivyo, kama singekuwa nimepitia kikalibu cha mateso cha kuadibu na hukumu ya Mungu, siku zote ningekuwa mpinga Kristo na kuyakaribisha mauti yangu mwenyewe. Ewe Mungu, ninaapa kuacha ukimbizaji wote usio sawa, kuacha majivuno na tamaa yangu na kuitii kila amri Yako. Nitafuatilia ukweli kwa bidii, kutimiza kila wajibu wangu na kuishi kama mtu halisi na wa kweli ili kuufariji moyo Wako.

kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Utukufu wote Uwe kwa Mwenyezi Mungu!

      Kujua zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni