10/02/2019

1. Mungu amekuwa mwili nchini China katika siku za mwisho; ni msingi gani upo kwa jambo hili katika unabii wa Biblia na katika maneno ya Mungu?


XIII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Uhimu wa Mungu Kuwa Mwili Nchini China Katika Siku za Mwisho

1. Mungu amekuwa mwili nchini China katika siku za mwisho; ni msingi gani upo kwa jambo hili katika unabii wa Biblia na katika maneno ya Mungu?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Kwa kuwa kuanzia kuchomoka kwa jua hadi hata kutua kwake jina langu litakuwa kubwa miongoni mwa Mataifa” (Malaki 1:11).
Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia” (Mathayo 24:27).
Maneno Husika ya Mungu:
Katika maeneo mengi, Mungu Alitabiri kupata kundi la washindi katika nchi ya Sinim. Ni upande wa Mashariki mwa ulimwengu ambapo washindi wanapatikana, hivyo nchi ambapo Mungu kupata mwili mara ya pili Atatua bila shaka ni nchi ya Sinim, mahali ambapo joka jekundu linaishi. Hapo Mungu Atawapata warithi wa joka kuu jekundu na litashindwa na kuaibishwa.
kutoka katika “Kazi na Kuingia (6)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Unabii ulisema kuwa jina la Yehova lingekuwa kubwa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi na kuwa jina la Yehova lingeenezwa kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi—mbona ulisema hivi? Iwapo Mungu angekuwa Mungu wa Waisraeli tu, basi Angefanya kazi tu Israeli. Zaidi ya hayo, Asingepanua kazi hii, na Asingefanya huu unabii. Kwa sababu Alifanya huu unabii, Angehitaji kuipanua kazi Yake hadi mataifa yasiyo ya Kiyahudi na hadi kila taifa na mahali. Kwa sababu Alisema hili, basi Angefanya hivyo. Huu ndio mpango Wake, kwani Yeye ndiye Bwana aliyeumba mbingu na dunia na vitu vyote, na Mungu wa viumbe vyote. Bila kujali iwapo Anafanya kazi na Waisraeli ama katika Yudea nzima, kazi Anayoifanya ni kazi ya ulimwengu mzima na kazi ya binadamu wote. Kazi Anayoifanya leo katika taifa la joka kubwa jekundu—katika taifa lisilo la Kiyahudi—bado ni kazi ya binadamu wote. Israeli inaweza kuwa kituo cha kazi Yake duniani; vivyo hivyo, Uchina pia inaweza kuwa kituo cha kazi Yake miongoni mwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Je, sasa Hajatimiza unabii kwamba “jina la Yehova litakuwa kubwa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi”?
kutoka katika “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika siku za mwisho, Mungu anapata mwili katika taifa lisilo la Kiyahudi la joka kubwa jekundu; Ametimiza kazi ya Mungu kama Mungu wa viumbe wote; Amekamilisha kazi Yake yote ya usimamizi, na Atamaliza sehemu kuu ya kazi Yake kwa taifa la joka kubwa jekundu.
kutoka katika “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ninapopita katika mbingu na nchi mpya tu ndipo Ninachukua sehemu nyingine ya utukufu Wangu na kuifichua kwanza katika nchi ya Kanaani, Nikisababisha nuru kuiangazia dunia nzima, iliyozama katika giza totoro la usiku, ili kuruhusu dunia nzima kuja kwa nuru hiyo. Wacha watu wote duniani kote waje kupata nguvu kutoka kwa nuru, kuruhusu utukufu Wangu uongezeke na kuonekana upya kwa kila taifa. Wacha binadamu wote utambue kwamba Nilikuja zamani katika ulimwengu wa wanadamu na Nilileta utukufu Wangu kutoka Israeli hadi Mashariki zamani; kwani utukufu Wangu unang’aa kutoka Mashariki, ambako uliletwa kutoka Enzi ya Neema hadi leo. Lakini Nilitokea Israeli na kutoka huko Nikawasili Mashariki. Wakati nuru ya Mashariki inapong’aa polepole tu ndipo giza kote duniani litaanza kugeuka na kuwa nuru, na hapo tu ndipo mwanadamu atatambua kwamba Nilishatoka Israeli zamani na Nimeanza kuchomoza upya Mashariki. Niliwahi kushuka Israeli na baadaye Niliondoka kutoka huko, Siwezi tena kuzaliwa Israeli kwa mara nyingine, kwa kuwa kazi Yangu inauongoza ulimwengu mzima na, zaidi ya hilo, umeme unamulika moja kwa moja kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Hii ndiyo sababu Nimeshuka Mashariki na kuwaletea watu wa Mashariki Kanaani. Ningependa kuwaleta watu kutoka dunia nzima waje katika nchi ya Kanaani, na kwa hiyo Naendelea kutoa maneno Yangu katika nchi ya Kanaani ili kuudhibiti ulimwengu mzima. Kwa wakati huu, hakuna nuru katika dunia nzima isipokuwa katika Kanaani, na watu wote wamehatarishwa na njaa na baridi. Niliipa Israeli utukufu Wangu kisha Nikauchukua na baadaye Nikawaleta Waisraeli Mashariki, na vilevile binadamu wote Mashariki. Nimewaleta wote kwenye nuru ili waweze kuungana tena nayo, na kushirikiana na nuru, na wasilazimike kuitafuta tena. Nitawaacha wote wanaotafuta waione nuru tena na kuuona utukufu Niliokuwa nao katika Israeli; Nitawaacha waone kwamba tayari Nimeshuka juu ya wingu jeupe miongoni mwa wanadamu, kuwaacha waone mawingu mengi meupe na vishada vingi vya matunda, na, zaidi ya hayo, Nitawaacha wamwone Yehova Mungu wa Israeli. Nitawaacha waone Mkuu wa Wayahudi, Masihi aliyengojewa kwa hamu, na kuonekana kamili kwa Mimi niliyeteswa na wafalme kotekote katika enzi. Nitafanya kazi katika ulimwengu mzima na Nitatekeleza kazi kubwa, Nikifichua utukufu Wangu wote na matendo Yangu yote kwa mwanadamu katika siku za mwisho. Nitaonyesha uso Wangu uliojaa utukufu kwa wale ambao wameningoja kwa miaka mingi, kwa wale ambao wametamani kuniona Nikija juu ya wingu jeupe, kwa Israeli ambayo imengoja Nionekane kwa mara nyingine, na kwa wanadamu wote wanaonitesa, ili wote wajue kwamba Niliuchukua utukufu Wangu zamani na kuuleta Mashariki, Ili usiwe katika Uyahudi tena. Kwani siku za mwisho tayari zimewadia!
Kotekote katika ulimwengu Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, yakiyatingisha mataifa yote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo imewaleta watu katika wakati wa sasa. Nitawasababisha watu wote kushindwa na sauti Yangu, kuingia katika mkondo huu, na kunyenyekea mbele Yangu, kwa maana Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote zamani na Nikautoa upya Mashariki. Ni nani asiyetamani kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuona kupendeza Kwangu? Ni nani hangetaka kuja kwenye nuru? Ni nani hangeuona utajiri wa Kanaani? Ni nani hangoji kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mwenyezi Mkuu? Sauti Yangu itaenea kotekote duniani; Ningependa, kuwazungumzia maneno mengi zaidi wateule wangu, Nikiwatazama. Kama radi yenye nguvu inayotingisha milima na mito, Nanena maneno Yangu kwa ulimwengu wote na kwa wanadamu. Hivyo maneno yaliyo kinywani Mwangu yamekuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi maneno Yangu kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni kiasi kwamba mwanadamu huchukia kuyaacha na pia huyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote mwanadamu huyafurahia. Kama mtoto mchanga aliyezaliwa hivi karibuni, wanadamu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu. Kwa sauti Yangu, nitawaleta wanadamu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia rasmi katika jamii ya wanadamu ili waje kuniabudu. Kwa utukufu Ninaoutoa na maneno yaliyo kinywani Mwangu, Nitawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye “Mlima wa Mizeituni” wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari Nimekuwa duniani kwa muda mrefu, sio kama Mwana wa Wayahudi tena lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwani Nimeshafufuka kitambo, na Nimeondoka miongoni mwa wanadamu, na kisha Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu Nikiwa na utukufu. Mimi ndiye Niliyeabudiwa enzi nyingi kabla ya wakati huu, na pia Mimi ni “mtoto mchanga” Aliyeachwa na Israeli enzi nyingi kabla ya wakati huu. Zaidi ya hayo, Mimi ndiye Mwenyezi Mungu mwenye utukufu wote wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, wasikie sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vilevile madhumuni ya usimamizi Wangu. Hebu kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na watu wote wawe chini Yangu!
kutoka katika “Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni” katika Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni