Kwa kuwa watu humpuuza mwanadamu Niliye na huyapuuza matendo Yangu, wanafikiri kuwa hivi ni vitu ambavyo hufanywa na wanadamu. Lakini mbona hufikiri: Je, watu wanaweza kutimiza yale Ninayoyatenda? Watu hawanijui kwa kiwango hiki, hawayaelewi maneno Yangu. Wanadamu waovu, waliopotoka! Je, Nitakumeza lini? Je, Nitakuzika katika ziwa la moto wa jehanamu lini? Je, ni mara ngapi Nimefukuzwa kutoka katika kundi lenu, watu wamenitukana, kunidhihaki na kuniharibia jina mara ngapi, na watu wamenihukumu waziwazi na kuniasi mara ngapi? Wanadamu vipofu! Je, hamjui kuwa ninyi ni konzi la matope mikononi Mwangu tu? Je, hamjui kuwa ninyi ni vitu vya uumbaji Wangu. Sasa, ghadhabu Yangu inaachiliwa na hakuna mtu ambaye anaweza kujikinga dhidi yake. Anaweza tu kuomba huruma tena na tena. Lakini kwa kuwa kazi Yangu imepiga hatua hadi kiwango hiki, hakuna anayeweza kuibadilisha. Wale ambao wameumbwa lazima warudi kwenye matope. Si kwamba Mimi ni mdhalimu, lakini kwamba ninyi ni wapotovu sana, wakatili sana, na ni kwa sababu mmekamatwa na Shetani na kuwa ala zake. Mimi ndimi Mungu mtakatifu Mwenyewe, Siwezi kuchafuliwa, na Siwezi kumiliki hekalu najisi. Kuanzia sasa kuendelea, ghadhabu Yangu iliyo kali sana (kali zaidi kuliko hasira) itaanza kumwagwa juu ya mataifa na watu wote, na itaanza kuwaadibu watu wote duni sana ambao hutoka Kwangu ila hawanijui Mimi. Ninawachukia wanadamu mno, na Sitakuwa na huruma tena, ila Nitashusha kwa wingi laana Zangu zote. Bila shaka hakutakuwa na huruma wala upendo, kila kitu kitateketezwa mpaka kikose kuwepo, na ufalme Wangu pekee ndio utasalia, ili kwamba watu Wangu watanisifu katika Nyumba Yangu, kunipa utukufu, na kunichangamsha milele (hii ndiyo kazi ya watu Wangu). Mkono Wangu utaanza kuwaadibu rasmi wale walio nje na ndani ya nyumba Yangu. Hakuna mwovu yeyote atakayeweza kuepuka mshiko Wangu na hukumu. Kila mtu lazima apite majaribu haya na kuniabudu Mimi. Huu ni uadhama Wangu, na zaidi ya hayo, ni amri ya utawala ambayo Ninawatangazia waovu. Hakuna mtu anayeweza kumwokoa yeyote mwingine. Wanaweza tu kuwachunga wao wenyewe, lakini bila kujali wanalofanya, hawataweza kuepuka mkono Wangu wa kuadibu. Sababu ya kuwa imesemekana kwamba amri Zangu za utawala ni kali imefichuliwa hapa. Huu ni ukweli ambao kila mtu anaweza kuuona kwa macho yake.
Ninapoanza kupata hasira, pepo wote, wakubwa na wadogo, watatoroka kwa vurumai, wakiwa na hofu kuu kuwa mkono Wangu utawaua. Lakini hakuna mtu yeyote anayeweza kuepuka kutoka mikononi Mwangu. Mimi hushikilia vifaa vyote vya mateso, mkono Wangu huvithibiti vyote, kila kitu kiko katika mshiko Wangu, na hakuna mtu anayeweza kujikomboa. Hii ni hekima Yangu. Nilipokuja katika eneo la binadamu, Nilikuwa nimekwisha kumaliza aina zote za kazi ya matayarisho, Nikiweka msingi wa kuanzisha kazi Yangu miongoni mwa wanadamu (kwa sababu Mimi ndimi Mungu mwenye hekima, na Mimi hushughulikia kile kinachopasa kufanywa na kile ambacho hakipasi kufanywa vizuri). Baada ya kila kitu kupangwa vizuri, Nilipata mwili na Nikaja katika eneo la mwanadamu, lakini hakuna mtu aliyenitambua. Kando na hao Niliowapa nuru, wana wote wa uasi hunifanyia kiburi, hunifedhehesha, na kunidharau. Lakini mwishowe, Nitawafanya kuwa na adabu na watiifu. Ingawa kwa watu inaonekana kuwa Sifanyi mengi, kazi Yangu kubwa tayari imetamatishwa. (Watu wote humtii kikamilifu mwanadamu Niliye katika neno na moyo. Hii ndiyo ishara.) Leo, Ninainuka na kuadibu aina zote za roho mbaya zinazoniasi. Bila kujali zimenifuata kwa muda gani, lazima ziondoke katika upande Wangu. Simtaki yeyote ambaye ananipinga (ni wale wanaokosa ufahamu wa kiroho, wale ambao wamepagawa na roho mbaya kwa muda, na wale wasionijua). Simtaki hata mmoja wao! Wote wataondolewa, na kuwa wana wa kuangamia kabisa! Baada ya kunifanyia huduma leo, lazima wote waondoke! Msibaki katika nyumba Yangu, msiwe watovu wa nidhamu wala wa kutofanya kazi tu. Wale walio wa Shetani wote ni wana wa ibilisi, na wataangamia milele. Wale wote wanaonikaidi wataondoka upande Wangu kimya, hivyo mwendo wa kazi Yangu utakuwa wa kutozuiwa zaidi bila madakizo zaidi. Vitu vyote vitafanywa kwa amri Yangu, bila vikwazo vyovyote wala mapingamizi yoyote. Vyote vitaanguka machoni Pangu na kuharibiwa katika uteketezaji Wangu. Hili linaonyesha uweza Wangu, hekima Yangu kamili (haya yanatendeka katika wazaliwa Wangu wa kwanza). Hili litaongeza utukufu mkubwa zaidi kwa jina Langu, na kuongeza utukufu mkuu Kwangu. Kutoka kwa kile Ninachofanya na kutoka kwa toni ya sauti Yangu, ninyi nyote mnaona kuwa Nimemaliza kazi Yangu katika nyumba Yangu kikamilifu na Nimeanza kuyageukia mataifa yasiyo ya Uyahudi. Ninaanza kazi Yangu hapo na kutekeleza hatua inayofuata ya kazi Yangu.
Maneno Yangu mengi hayalingani na dhana zenu, lakini wana Wangu, msiondoke. Kwamba hayalingani na dhana za binadamu haimaanishi kuwa si sauti Yangu. Ni hasa kwa sababu ya hili kwamba inaweza kuthibitishwa kuwa ni sauti Yangu. Kama ingelingana na dhana za binadamu, basi hiyo ingekuwa kazi ya roho mbaya. Hivyo, lazima mtie bidii zaidi katika maneno Yangu, mfanye Ninayoyafanya, na kupenda Ninachokipenda. Hii enzi ya mwisho pia ni enzi ambapo maafa yote hutokea tena, na hata zaidi enzi ambapo Ninafichua tabia Zangu zote. Mabaragumu Yangu yote matakatifu yatakapoanza kupigwa, watu kwa kweli wataogopa, na kisha hakuna atakayethubutu kufanya maovu, lakini badala yake watasujudu mbele Yangu, wakitambua vyema hekima Yangu na uweza Wangu. Mimi, hata hivyo, ndimi Mungu Mwenyewe mwenye hekima! Je, ni nani awezaye kunikanusha? Na ni nani anayethubutu kuinuka kunipinga? Ni nani anayethubutu kutokubali hekima Yangu? Je, nani anayethubutu kutojua uweza Wangu? Roho Wangu anapofanya kazi kubwa kila mahali, watu wote hujua uweza Wangu, lakini lengo Langu bado halijafikiwa. Nataka watu waone uweza Wangu kwa sababu ya ghadhabu Yangu, waone hekima Yangu, na waone utukufu wa nafsi Yangu. (Haya yote ni katika wazaliwa wa kwanza, bila makosa yoyote. Kando nao, hakuna anayeweza kuwa sehemu ya nafsi Yangu; hili limeamuriwa na Mimi.) Katika nyumba Yangu, kuna mafumbo yasiyokuwa na mwisho ambayo watu hawawezi kuyaelewa. Ninapozungumza, watu husema kuwa Sina huruma kabisa, wao husema kuwa watu wengi mno tayari hunipenda kwa kiwango fulani, lakini kwa nini Nasema kuwa wao ni wa ukoo wa joka kuu jekundu? Na kwa nini Nitawaacha mmoja baada ya mwingine? Je, si ni vema kuwa na watu wengi zaidi katika nyumba Yangu? Lakini bado Natenda hivi. Hakuwezi kuwa na mmoja zaidi wala mmoja chache kuliko nambari Niliyoamua kabla. (Hii ni amri Yangu ya utawala. Haiwezi tu kutobadilishwa na watu, lakini hata Mimi mwenyewe Siwezi kuibadilisha, kwa kuwa Siwezi kushindwa mbele ya Shetani. Haya yametosha kuonyesha hekima Yangu na uadhama Wangu. Mimi ndimi Mungu mmoja Mwenyewe. Ni ukweli tu kwamba watu huinama mbele Yangu; Sishindwi mbele ya watu.) Hii hasa ndiyo hoja ambayo humuaibisha Shetani zaidi. Watu wote ambao Nimewachagua ni wanyenyekevu, watiifu, ni wasikivu na waaminifu, na wanaweza kunihudumia kwa unyenyekevu na katika mashaka. (Shetani alitaka kutumia hili kunifedhehesha, lakini Nilimpigana.) Tabia Yangu inaweza kuonekana kutoka kwa watu hawa. Wakati ambapo Nimerudi baada ya ushindi vitani, Nitawatia mafuta wazaliwa Wangu wa kwanza ili wawe wafalme katika Ufalme Wangu, na ni wakati huo tu ambapo Nitaanza kupumzika, kwa kuwa wazaliwa Wangu wa kwanza watakuwa wafalme pamoja Nami. Wazaliwa Wangu wa kwanza huniwakilisha Mimi, na hunionyesha Mimi. Katika unyenyekevu wao na huduma yao isiyo wazi, wao hunitii, katika uaminifu wao hutekeleza maneno Yangu, katika uaminifu wao huyasema yale Ninayoyasema, na katika unyenyekevu wao huleta utukufu kwa jina Langu (bila ufidhuli au ukatili, bali kwa uadhama na ghadhabu). Wazaliwa Wangu wa kwanza! Ni wakati wa kuhukumu ulimwengu wa dunia! Ninawapa baraka, Ninawapa mamlaka, na Ninawatuza baraka! Kila kitu kimekwisha kutimizwa, na vyote vinathibitiwa nanyi, kupangwa nanyi, kwa kuwa Mimi ni Baba yenu, Mimi ndimi mnara wenu ulio dhabiti, Mimi ndimi kimbilio lenu, Mimi ndimi usaidizi wenu, na hata zaidi Mimi ndimi Yule mwenye Uweza wako, na Mimi ni kila kitu chako! Kila kitu kiko mikononi Mwangu, na kila kitu pia kiko mikononi mwenu. Si leo tu, lakini pia jana, na hata kesho! Je, hii haifai kuadhimishwa? Je, haifai shangwe yenu? Ninyi nyote, kubalini fungu mnalostahili kutoka Kwangu. Ninakupa kila kitu changu, na Sihifadhi hata kipande kimoja, kwa sababu mali Yangu yote ni yenu, na utajiri Wangu uko juu yenu. Hii ndiyo sababu Nilisema “vyema sana” baada ya kuwaumba.
Je, mnajua yule anayeelekeza kile mnachofanya, kufikiria, na kusema leo? Na kila kitu mnachofanya ni cha nini? Ninawauliza, mnahudhuria vipi karamu ya ndoa ya Mwanakondoo? Je, ni leo? Ama ni wakati ujao? Je, karamu ya ndoa ya Mwanakondoo ni nini? Hamjui, siyo? Basi Ninawaelezea: Nilipokuja katika eneo la binadamu, Nilikuwa nimeandaa aina zote za watu, mambo, na vitu ili kuhudumia mtu Niliye leo. Sasa kwa kuwa kila kitu kimekamilika, Ninawatupa pembeni watendaji huduma. Je, hili linahusiana vipi na karamu ya ndoa? Watu hawa wanaponihudumia, yaani, Ninapofanywa kuwa Mwanakondoo, Ninaonja ladha ya karamu ya ndoa. Hivyo ni kusema kuwa, uchungu wote Nilioupitia, vitu vyote ambavyo Nimefanya, vitu vyote ambavyo Nimesema, kila mtu Niliyepatana naye, na kila ambacho Nimekifanya katika wakati Wangu miongoni mwa wanadamu vimekuwa karamu ya ndoa. Baada ya mwanadamu Niliye kupakwa mafuta, mlinifuata (wakati huu Nilikuwa Mwanakondoo), hivyo chini ya uongozi Wangu, mmezipitia aina zote za uchungu, maafa, kuachwa na kutukanwa na dunia, kuachwa na familia, na mnaishi katika baraka Zangu. Haya yote ni karamu ya ndoa ya Mwanakondoo. Mimi hutumia karamu ya ndoa kwa sababu yote Niliyowaelekeza katika kufanya ni kwa ajili ya kuwapata. Lakini haya yote ni sehemu ya karamu. Katika siku zijazo, mtu aweza pia kusema leo, kila kitu mnachofurahia, kila kitu mnachopata, na nguvu ya kifalme mnayoshiriki pamoja nami, yote ni karamu. Upendo Wangu huja kwa wale wote wanaonipenda. Wale Ninaowapenda watasalia hadi milele, hawataondolewa asilani, watakuwa katika upendo Wangu daima. Ni milele!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Sura ya 109
Kujua zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni