Nyimbo za kusifu | 237. Kile Vijana Hawana Budi Kufuatilia
I
Macho yanayochukiza na udanganyifu
sivyo wanavyofaa kuvimiliki vijana.
Njia za kuogofya na haribifu
sizo wanazofaa kuzitenda vijana.
Wanafaa kuwa na malengo,
kwa shauku wajitahidi kuendelea,
sio kukata tamaa juu ya matarajio yao,
wadumishe imani katika maisha, katika wakati ujao.
Vijana wanafaa kuwa na azma ya utambuzi,
wakitafuta haki na ukweli.
Fuatilieni mambo yote mazuri,
pateni ukweli wa mambo ya hakika.
Wajibikeni juu ya maisha.
Lazima msichukulie hili kwa mzaha.
Lazima msichukulie hili kwa mzaha.
II
Vijana wanapaswa kushikilia katika njia ya ukweli,
hivyo wajitolee maisha yao kwa ajili ya Mungu.
Hawapaswi kukosa ukweli,
wala kuhifadhi uongo, uovu.
Wanapaswa kuchukua msimamo sahihi.
Hawapaswi kuzurura wakisonga tu.
Wanapaswa kuthubutu kujitolea,
kupigania haki na ukweli.
Vijana wanafaa kuwa na azma ya utambuzi,
wakitafuta haki na ukweli.
Fuatilieni mambo yote mazuri,
pateni ukweli wa mambo ya hakika.
Wajibikeni juu ya maisha.
Lazima msichukulie hili kwa mzaha.
Lazima msichukulie hili kwa mzaha.
III
Vijana hawapaswi kukubali kushindwa
na ukandamizaji wa nguvu za giza.
Wanapaswa kuwa na ujasiri
kubadilisha maana ya maisha yao.
Vijana hawapaswi kujisalimisha
kwa taabu,
wanapaswa kuwa makini na wazi,
kuwasamehe waumini wenzao.
Vijana wanafaa kuwa na azma ya utambuzi,
wakitafuta haki na ukweli.
Fuatilieni mambo yote mazuri,
pateni ukweli wa mambo ya hakika.
Wajibikeni juu ya maisha.
Lazima msichukulie hili kwa mzaha.
Lazima msichukulie hili kwa mzaha.
kutoka kwa "Maneno kwa Vijana na Wazee" katika Neno Laonekana katika Mwili
Sikiliza zaidi: nyimbo za kuabudu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni