2/25/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda


Hatua ya kazi ya watenda-huduma ni hatua ya kwanza ya kazi ya ushindi; kwa sasa hii ni hatua ya pili ya kazi ya ushindi. Kwa nini ukamilifu unajadiliwa katika kazi ya ushindi? Ni kuujenga msingi kwa ajili ya siku za baadaye—kwa sasa hii ni hatua ya mwisho katika kazi ya kushinda, na baada ya hii, kazi ya kuwakamilisha watu itaanza rasmi wakati watakuwa wanapitia dhiki kuu. Jambo la msingi sasa ni ushindi; hata hivyo, hii pia ni hatua ya kwanza ya kukamilisha, kukamilisha ufahamu na utii wa watu, ambayo kwa kweli bado yanajenga msingi wa kazi ya kushinda. Kama unataka kukamilishwa, lazima uwe na uwezo wa kusimama imara katikati ya mateso ya siku za baadaye na uziweke nguvu zako zote katika kupanua hatua yenye kufuata ya kazi. Huku ni kukamilishwa, na huo ndio wakati ambao watu watakuwa wamepatwa na Mungu kabisa. Kile kinachojadiliwa hivi sasa ni kushindwa, ambako pia ni kukamilishwa; hata hivyo, kile kinachofanywa sasa ni msingi wa kukamilishwa katika siku za baadaye. Ili kufanywa mkamilifu, lazima watu wapitie mashaka, na lazima wayapitie juu ya msingi wa kushindwa. Kama watu hawana msingi huu wa sasa, kama hawajashindwa kikamilifu, basi itakuwa vigumu kwao kusimama hadi hatua inayofuata. Kushindwa tu si kufikia lengo la mwisho—ni kushuhudia kwa Mungu tu mbele ya Shetani. Kukamilishwa ni lengo la mwisho, na kama bado hujakamilishwa, basi utahesabiwa kama asiyefaa. Wanapokabiliwa na mashaka katika siku za baadaye, ndipo tu kimo halisi cha watu kitaonekana, yaani, usafi halisi wa upendo wako kwa Mungu utaonekana. Sasa, watu wote husema: “Haidhuru kile Mungu anachofanya sisi tutatii, nasi tuko tayari kuwa foili, kuchochea ukuu wa Mungu, tabia ya Mungu. Haidhuru kama Anaifadhili neema Yake juu yetu au la ama kama Anatulaani au Anatuhukumu, tutatoa shukrani Kwake.” Wewe kusema hili sasa ni ufahamu kiasi tu, lakini kama linaweza kutumika kwa hali halisi linategemea kama ufahamu wako kweli ni wa kweli. Kwamba watu sasa wameona na kueleweka mambo haya ni mafanikio ya kazi ya ushindi; kama unaweza kukamilishwa au la itaonekana hasa wakati mashaka yanakuja juu yako. Wakati huo itaonekana kama una upendo wa kweli kwa Mungu katika moyo wako au la, na kama kweli unao upendo safi kwa ajili Yake, utasema: “Sisi ni foili tu; sisi ni viumbe katika mikono ya Mungu.” Na wakati unapoieneza injili kwa mataifa mengine, utasema: “Mimi ni mtendaji-huduma tu na ni kwa sababu ya tabia zetu potovu ndiyo Mungu alinena sana kiasi kwamba tumeiona tabia Yake ya haki. Kama Mungu hangesema mambo hayo hatungeweza kumwona Yeye, hatungeweza kuionja hekima Yake, na hatungeweza kuupata wokovu mkuu mno, baraka kubwa mno. ”Kama kweli unayo maoni hayo, basi unafanya vizuri. Sasa umesema mambo mengi bila kufikiri na daima unasema wito kwa sauti kubwa: "Sisi ni foili na watenda-huduma; tuko tayari kushindwa na kuwa mashahidi wakubwa sana wa Mungu…” Huwezi tu kupaaza sauti na umalize bila kulifikiria tena, na uthibitishe kwamba wewe ni mtu mwenye kimo. Lazima uwe na ufahamu wa kweli, na ufahamu wako unapaswa kujaribiwa.

Tafakari uzoefu katika kipindi hiki cha wakati na uangalie tena mambo haya ambayo Nimeyasema, kisha uyalinganishe kile unachofanya. Ni kweli kabisa kwamba wewe ni foili kabisa! Ni kiwango gani cha ufahamu ulicho nacho sasa? Mawazo yako, fikra, tabia, maneno na matendo yako, kila kitu ambacho unaishi kwa kudhihirisha—si yot tu ni foili kwa haki na utakatifu wa Mungu? Si kila kitu ambacho kinafunuliwa kiko katika maneno ya sasa ya Mungu kuhusu tabia potovu ya wanadamu? Tabia ya Mungu yenye haki na utakatifu vinaonyesha kupitia mawazo yako na nia zako, na kupitia kwa yale unayoyafunua. Yeye, pia Akiishi katika nchi ya uchafu, hajatiwa waa na uchafu hata kidogo. Anaishi katika dunia ile ile chafu kama wewe, lakini Anamiliki mantiki na umaizi; Anachukia uchafu. Wewe mwenyewe huwezi kuona mambo machafu katika maneno na matendo yako mwenyewe lakini Yeye Anaweza—Anaweza kukuonyesha. Mambo hayo yako ya zamani—ukosefu wako wa kukuza, umaizi, na hisia, maisha yako ya kuelekea nyuma—yote yamefunuliwa kupitia kwa kufichua Kwake kwa mambo hayo sasa. Mungu Amekuja duniani kufanya kazi kwa namna hii, ili watu wauone utakatifu Wake na tabia Yake ya haki. Anakuhukumu na Kukuadibu na Kukufanya ujielewe. Wakati mwingine asili yako yenye pepo mbaya huonekana na Anaweza kukuonyesha. Anakijua kiini cha wanadamu sana. Anaishi kama wewe unavyoishi, Anakula chakula sawa na wewe, Anaishi katika aina ya nyumba kama wewe, lakini Anajua mengi zaidi kukuliko. Lakini kile Anachochukia hasa ni maisha ya filosofia ya watu na upotovu na udanganyifu wao. Anavichukia vitu hivi na Yeye hana nia ya kuvitambua. Yeye hasa anachukia maathiriano ya kimwili ya watu. Ingawa Haelewi kabisa baadhi ya maarifa ya jumla ya maathiriano wa binadamu, Anafahamu kikamilifu wakati ambapo watu wanafichua baadhi ya tabia zao potovu. Katika kazi Yake, Ananena na kuwafundisha watu kupitia mambo haya ndani yao, na kupitia haya Yeye huwahukumu watu na kufichua tabia yake yenye haki na takatifu. Hivi ndivyo watu wanakuwa foili kwa ajili ya kazi Yake. Ni Mungu mwenye mwili tu ambaye Anaweza kufichua kila aina ya tabia potovu za mwanadamu na nyuso zote mbaya za Shetani. Yeye hakuadhibu, Angeweza tu kukufanya wewe uwe foili kwa utakatifu wa Mungu. Huwezi kusimama imara mwenyewe kwa sababu wewe ni mchafu sana. Anaongea kupitia mambo yale ambayo watu wanadhihirisha na Yeye huyafunua ili watu waweze wajue jinsi Mungu ni mtakatifu. Hataacha uchafu hata kidogo ndani ya binadamu, sio hata wazo dogo zaidi chafu katika mioyo yao au maneno na matendo ambayo si sambamba na mapenzi Yake. Kupitia kwa maneno Yake, hakuna uchafu na hakuna kitu ndani ya mtu kitabaki—vyote vitawekwa wazi. Ni hapo tu ndipo utakapoona ya kwamba Yeye kweli yuko tofauti na watu. Anachukizwa kabisa na uchafu hata kidogo zaidi katika wanadamu. Wakati mwingine watu hata hawaelewi, na wanasema: “Kwa nini Wewe una hasira kila mara? Mungu, kwa nini Huujali udhaifu wa wanadamu? Kwa nini Huna msamaha kidogo kwa wanadamu? Kwa nini Hujali hisia za mwanadamu? Unajua jinsi watu walivyo wapotovu, hivyo kwa nini bado Unawatendea watu kwa njia hii?” Anachukizwa na dhambi; Anachukia dhambi. Yeye anachukizwa hasa na uasi wowote unaoweza kuwa ndani yako. Wakati ambapo unafichua tabia ya uasi Anachukizwa kupita kadiri. Ni kwa kupitia mambo haya ambapo tabia Yake na asili vinaweza kuonyeshwa. Unaipolinganisha na wewe mwenyewe, utaona kwamba ingawa Anakula chakula sawa, Anavaa mavazi sawa, na Ana starehe sawa na watu, ingawa Anaishi kandokando na pamoja na watu, Yeye si sawa. Je, hii si maana halisi ya kuwa foili? Ni kupitia mambo haya kwa watu ndiyo maana nguvu kuu ya Mungu inaonekana kwa urahisi sana; ni giza ambalo huchochea kuwepo kwa mwanga wa thamani.

Bila shaka Yeye hawatumii ninyi kwa makusudi kama foili, lakini wakati ambapo kazi hii inaonyesha matokeo, inaonyesha uasi wa wanadamu kama foili kwa ajili ya tabia ya Mungu yenye haki. Ni kwa sababu mmetenda kama foili ndiyo maana mna nafasi ya kujua maonyesho asili ya tabia ya Mungu yenye haki. Ni kwa sababu ya uasi wenu ndiyo maana mmepatwa na hukumu na kuadibu mara kwa mara; lakini pia ni kwa sababu ya uasi wenu ndiyo manaa mmetenda kama foili na mmepata neema kubwa sana ambayo Mungu amewakirimu. Ni uasi wenu ambao ni foili kwa uenyezi na hekima ya Mungu, na ni kwa sababu yake ndipo mmepata wokovu mkuu mno, baraka kubwa mno. Ingawa mmepokea hukumu Yangu mara kwa mara, pia mmepata wokovu mkuu ambao wale waliokuwa mbele yenu hawakuwahi kuupata. Kazi hii ni yenye maana ya ajabu sana kwenu. “Foili” hii kwa kweli ni yenye thamani sana kwenu—ni kwa sababu ya kutenda kama foili ndipo mmepata wokovu na neema. Je, si kuwa aina hii ya foili ya thamani sana? Je, si ni ya maana sana? Ni kwa sababu mnaishi katika ulimwengu sawa na Mungu, kwa sababu mnaishi naye katika nchi chafu ndipo mmekuwa foili Wake na mmepata wokovu wa ajabu sana. Kama Hangekuwa mwili, nani angekuwa na huruma kwenu, na nani angewatunza ninyi watu duni? Nani angewajali ninyi? Kama Mungu mwenye mwili hangekuwa anafanya kazi miongoni mwenu, ni wakati gani ambapo mngeweza kuupata wokovu huu ambao hakuna mtu yeyote amewahi kuupata awali? Kama Nisingekuwa mwili Niwajali na kuzihukumu dhambi zenu, si mgekuwa mmeanguka Kuzimuni muda mrefu uliopita? Kama Nisingekuwa mwili kujinyenyekeza miongoni mwenu, mngekuwa na haki gani kuwa foili kwa tabia ya Mungu yenye haki? Je, hamtendi kama foili kwa sababu Nimekuwa mwili kati yenu ili kwamba muweze kuupata wokovu mkuu mno? Si hiyo kabisa ni kwa sababu Nilikuwa mwili? Kama isingekuwa kwa ajili ya Mungu mwenye mwili akiishi miongoni mwenu, je, mngeweza kugundua kwamba mnaishi katika kuzimu duniani, vibaya zaidi kuliko nguruwe au mbwa? Je, si hukumu na kuadibu ambako mmepata kumekuwa kwa sababu ninyi ni foili kwa ajili ya kazi Yangu katika mwili? Kazi ya kuwa foili inafaa sana kwenu kwa kuwa mmeupata wokovu wa hukumu ya Mungu kwa sababu ya hii. Je, hamhisi kuwa ni baraka ya maisha yenu kuweza kutenda kama foili wenye sifa? Yote ambayo mmeyafanya ni kazi ya kuwa foili, lakini mmepata wokovu ambao hamjawahi kuupata au kufikiri kabla. Kuwa foili ni wajibu wenu sasa, na baraka za milele mtakazozifurahia wakati ujao zitakuwa zawadi mnayostahili. Wokovu mnaoupata si ufahamu wa mara moja au maarifa leo, lakini ni baraka zaidi, mwendelezo wa milele wa maisha. Ingawa ni kupitia kuwa foili ndiyo mnashindwa, mnapaswa kujua kwamba wokovu huu, baraka hii ni kuwapata ninyi kabisa; ni ushindi na pia ili kuwaokoa bora zaidi. Kuwa foili ni ukweli, lakini ni kwa sababu ya uasi wenu ndiyo ninyi ni foili na mmepata baraka ambazo hakuna aliyewahi kuzipata. Leo, mnaona na kusikia, na kesho mtapata, na mtapokea baraka kubwa hata zaidi. Hivyo si kuwa aina hii ya foili jambo muhimu sana? Ni kupitia kwa foili ya tabia zenu za uasi ndiyo kazi ya sasa ya kushinda huzaa matunda, ambayo ni, kilele cha kuadibu na hukumu ya pili ni kuufanya uchafu na uasi wenu kuwa foili ili muweze kuiona tabia ya haki ya Mungu. Wakati mtakapokuwa watiifu kwa mara nyingine tena katika kuadibu na hukumu ya pili, tabia Yake yenye haki yote itafunuliwa wazi kwenu. Hiyo ni, wakati ambapo kukubali kwenu kazi ya ushindi kumefika mwisho utakuwa wakati ambapo mmetimiza wajibu wenu wa kuwa foili. Si kuamua jambo kuwahusu bila kujali kuwajua, lakini ni kuikamilisha kazi ya kwanza ya kushinda kupitia kwa wajibu wenu kama watenda-huduma, ikifichua tabia yenye haki ya Mungu, isiyokosewa. Kupitia kwa kutenda kwenu kama foili, kupitia kwa uasi wenu kama foili, matunda ya kazi ya pili ya ushindi yamepatikana. Tabia Yake yenye haki ambayo haikuwa imefunuliwa kwenu kikamilifu mara ya kwanza sasa imefunguliwa yote juu yenu ili muweze kuiona tabia Yake yote yenye haki, muone yote ambayo Yeye aliye, ambayo ni ya hekima ya kazi Yake, ajabu, na utakatifu na usafi. Matunda haya ya kazi Yake yamefanikishwa kupitia kwa vipindi tofauti vya ushindi pamoja na hatua mbalimbali za hukumu. Kadri hukumu Yake inavyofikia kilele chake, ndivyo Yeye anavyoweza kufichua tabia za uasi za watu na ndivyo Yeye anaweza kufikia matokeo ya ushindi. Tabia Yake yote ya haki imedhihirishwa kutoka miongoni mwa aina hii ya kazi ya kushinda. Kazi ya ushindi imetengwa katika hatua mbili ambazo zinatekelezwa katika nyakati tofauti na ziko katika viwango mbalimbali. Na bila shaka matokeo yanayopatikana pia ni tofauti; ambayo ni, kiwango cha utii wa watu kinakuwa cha kina zaidi na zaidi. Tangu wakati huu kuendelea hatimaye itawezekana kuwaleta watu kwenye njia sahihi ya kukamilishwa. Baada ya kazi yote ya ushindi kukamilika (wakati ambapo hukumu ya pili imepata matokeo yake ya mwisho) hatimaye Mungu hatawahukumu wanadamu tena, lakini atawataka waingie katika njia sahihi ya kupitia maisha. Hii ni kwa sababu hukumu inawakilisha ushindi, na aina ya ushindi ni hukumu na kuadibu.

Ni kwa Mungu kuwa mwili tu katika mahali palipo nyuma mno kimaendeleo na pachafu mno ndiyo Yeye anaweza kudhihirisha ukamilifu wote wa tabia Yake takatifu na yenye haki. Na kupitia kwa nini ndiyo tabia Yake yenye haki inadhihirishwa? Kupitia kwa hukumu ya dhambi za watu, hukumu ya Shetani, karaha kuelekea dhambi, na chuki kwa maadui Zake ambao wanaasi dhidi Yake na kumpinga Yeye. Kile ambacho Nasema leo ni kuhukumu dhambi za watu na maovu yao; ni kulaani uasi wa watu. Udanganyifu na upotovu wao, na maneno na matendo yao, mambo yote ambayo hayako sambamba na mapenzi Yake yatapitia hukumu, na uasi wa watu unaamuliwa kuwa wenye dhambi. Ananena kulingana na kanuni za hukumu, naye anadhihirisha tabia Yake yenye haki kwa kuhukumu maovu yao, kulaani uasi wao, na kufichua nyuso zao zote mbaya. Utakatifu unawakilisha tabia Yake ya haki; utakatifu Wake kwa kweli ni tabia Yake ya haki. Msingi wa maneno Yangu leo ni kuzungumza, kuhukumu, na kufanya kazi ya ushindi kutokana na tabia zenu potovu. Hii pekee ni kazi halisi, na hii pekee ndiyo inaweza kabisa kuufanya utakatifu wa Mungu uonekane kwa urahisi sana. Kama hukuwa na tabia potovu hata kidogo, Mungu hangekuhukumu, pia hungeweza kuiona tabia Yake ya haki. Kwa kuwa una tabia potovu, Mungu hatakuachilia. Ni kupitia kwa hili ndiyo utakatifu wake unafunuliwa. Kama uchafu na uasi wa watu ni mkubwa mno na Aliuona lakini hakusema neno na wala Hakukuhumu wala kukuadibu kwa maovu yako, ingeonyesha kuwa Yeye hakuwa Mungu hata kidogo kwa sababu Yeye hangechukia dhambi, lakini angekuwa tu mchafu kama wanadamu walivyo. Hukumu Yangu kwako leo ni kwa sababu ya uchafu wako; kuadibu Kwangu kwako leo ni kwa sababu ya upotovu na uasi wako. Si kwa ajili ya kupata mamlaka na ufahari kati yenu wala kuwadhulumu kimakusudi, lakini ni kwa sababu ninyi mnaoishi katika nchi ya uchafu mmepakwa matope na uchafu mwingi sana. Mmepoteza tu uadilifu wenu, ubinadamu wenu, na hamko tofauti na nguruwe wanaoishi katika maeneo maovu mno. Ni kwa sababu ya mambo haya ndani yenu ndiyo mnahukumiwa na kwamba hasira Yake imepatiliziwa juu yenu. Ni kwa sababu ya hukumu hizi ndiyo mmeweza kuona kwamba Mungu ni Mungu mwenye haki, kwamba Mungu ni Mungu mtakatifu. Ni kwa sababu ya utakatifu na haki yake ndiyo Amewahukumu kuwapatilizia hasira Zake juu yenu. Kwa sababu Yeye anaweza kudhihirisha tabia yake ya haki anapotazama uasi wa wanadamu, na kwa sababu Anaweza kudhihirisha utakatifu Wake anapotazama uchafu wa wanadamu, hii inatosha kuonyesha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mtakatifu na bila doa, lakini pia Anaishi katika nchi ya uchafu. Kama Yeye angekuwa mtu Anayejitia matope pamoja na watu na kama Asingekuwa na dalili zozote za utakatifu au tabia ya haki, Asingekuwa na sifa kuhukumu uovu wa wanadamu au kuwa hakimu wa wanadamu. Kama mwanadamu angemhukumu mwanadamu, isingekuwa kama kuzaba kofi uso wake wenyewe? Mtu anawezaje kuwa na haki ya kuhukumu aina sawa ya mtu, ambaye ni mchafu tu kama yeye? Yule tu ambaye anaweza kuwahukumu wanadamu wote wachafu ni Mungu mtakatifu Mwenyewe, na mwanadamu angewezaje kuzihukumu dhambi za mwanadamu? Mwanadamu angewezaje kuona dhambi za mwanadamu, na angewezaje kuwa na sifa zinazostahili kumshutumu mwanadamu? Kama Mungu hangekuwa na haki ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, basi Angewezaje kuwa Mungu mwenye haki mwenyewe? Wakati ambapo tabia potovu za watu zinadhihirishwa, Yeye ananena kuwahukumu, na ni wakati huo tu ndipo wanaweza kuona kwamba Yeye ni mtakatifu. Hukumu, kuadibiwa, na mfichuo wa dhambi za wanadamu—hakuna mtu mmoja au kitu kinaweza kuepuka hukumu hii. Yote ambayo ni machafu yanahukumiwa na Yeye. Ni kwa kupitia hili tu ndiyo tabia Yake inasemekana kuwa yenye haki. Vinginevyo, inawezaje kusemwa kwamba ninyi mnastahili kuitwa foili?

Kazi iliyofanywa katika Israeli ni tofauti kabisa na kazi ya leo. Yehova aliyaongoza maisha yao lakini hakuwahukumu wala kuwaadibu almradi inavyofanyika sasa kwa sababu wakati huo, watu walielewa kidogo mno kuhusu mambo ya dunia na walikuwa na tabia chache potovu. Wakati huo, Waisraeli walikuwa wanyenyekevu kwa Yehova katika kila namna. Wakati Alipowaamuru kujenga madhabahu wangeharakisha kufanya hivyo, na Alipowaamuru kuvaa mavazi ya makuhani wangetii. Wakati huo Yehova alikuwa tu kama mchungaji wao akiliongoza kundi la kondoo duniani, na kondoo wote walifuata mahali mchungaji aliwaongoza kula nyasi katika malisho. Yehova Aliyaongoza maisha yao; Alikuwa mwongozo kwa ajili ya chakula chao, mavazi, malazi, na usafiri. Huo haukuwa wakati wa kufichua tabia ya Mungu kwa sababu watu wa wakati huo walikuwa watoto wachanga, na kisha kulikuwa na watu wachache sana ambao walikuwa waasi au wapinzani, nao hawakuwa wametiwa matope mno. Hivyo hawangeweza kuwa foili kwa ajili ya tabia ya Mungu. Utakatifu wa Mungu unafichuliwa kwa watu katika nchi ya uchafu. Na sasa ni uchafu unaofichuliwa na watu katika nchi ya uchafu ambao Mungu huuhukumu. Kwa njia hii, kile Alicho kinaonyeshwa chote katika hukumu Yake. Na kwa nini Yeye huhukumu? Ni kwa sababu Anachukizwa na dhambi, na hivyo Yeye ana uwezo wa kutoa maneno ya hukumu. Kama Yeye hangechukizwa na uasi wa mwanadamu, Angekuwa mwenye ghadhabu sana? Kama hakungekuwa na maudhi, hakuna chuki ndani Yake, ikiwa watu ni waasi lakini hakuwajali, hiyo ingeonyesha kwamba Yeye alikuwa mchafu tu kama wachafu kama wanadamu. Sababu amabyo Yeye ana uwezo wa kuhukumu na kuwaadibu wanadamu ni kwamba Anakuchukizwa na uchafu. Kila kitu ambacho Anachukizwa nacho ni kile Yeye mwenyewe hamiliki. Kama Yeye pia angekuwa na upinzani na uasi ndani ya nafsi Yake, hangechukizwa na watu wapinzani na waasi. Kama Kazi Yake katika siku za mwisho ingekuwa bado inafanywa katika Israeli haingekuwa na umuhimu hata kidogo. Kwa nini kazi ya siku za mwisho inafanywa nchini China, mahali penye giza sana, iliyo nyuma zaidi kimaendeleo? Ni kufichua utakatifu na haki ya Mungu. Kwa ufupi, jinsi mahali palivyo penye giza zaidi ndipo panapoweza kutoa mwanga bora kwa utakatifu Wake. Ukweli ni kwamba kufanya yote haya ni kwa ajili ya kazi ya Mungu. Mnajua tu sasa kwamba Mungu aliye mbinguni ameshuka duniani na anasimama katikati yenu, na Amepewa umuhimu dhidi ya uchafu na uasi wenu, ili muanze kuwa na ufahamu wa Mungu—je, si hili linatia moyo pakubwa? Ukweli ni kwamba ninyi ni kundi la watu nchini China ambao mmechaguliwa, na kwa sababu watu hawa wamechaguliwa na wamefurahia neema ya Mungu, na kwa sababu watu hawa hawafai kufurahia neema Yake nyingi, inaonyesha kwamba yote haya yanatia moyo pakubwa kwenu. Mungu Amejidhihirisha na tabia Yake yote takatifu kwenu, na Ametawaza yote hayo juu yenu, Akiwaruhusu kufurahia baraka tele. Hamjaonja tu tabia Yake yenye haki, lakini la muhimu zaidi, mmeonja wokovu Wake pamoja na ukombozi Wake na upendo usio na kikomo, ili ninyi, wachafu zaidi ya watu wote, mmepokea neema kuu mno—si huku ni kubarikiwa? Je, si huku ni kutiwa moyo na Mungu? Ninyi ni wa hadhi ya chini sana na hamkufaa baraka kuu kama hii, lakini Mungu alikuwa na nia ya kukutia moyo. Je, huoni aibu? Kama huwezi kutimiza wajibu wako, mwishowe utajionea aibu kabisa. Utajiadibu. Kwa sasa Yeye hakuchapi wala kukuadhibu; mwili yako uko salama salimini, lakini mwishowe maneno Yake yatakuletea aibu kwako mwenyewe. Hadi sasa Sijawahi kumwadibu mtu yeyote hadharani. Nimenena kwa ukali, lakini Nimekuwaje kuwaelekea watu? Nimekuwa mwenye faraja, Nimewahimiza, na pia Nimewaonya. Hii haijakuwa kwa lengo lingine zaidi ila kuwaokoa. Inawezekana kuwa kwamba hamueilewi nia Yangu kwa kweli? Ninaposema hivi nyote mnapaswa kuelewa na mnapaswa kutiwa moyo kwa maneno haya. Kunao wengi ambao hatimaye wameelewa hili sasa: Je, baraka hii si kutenda kama kama foili? Je, si kuwa foili jambo lenye baraka kuliko mambo yote? Mwishowe, mtaeneza injili ifuatayo: “Sisi ni foili wa mfano hasa. Watawauliza: “Ni nini maana ya kuwa na foili wa mfano hasa?” Na kisha mtasema: “Sisi ambao tunaikamilisha kazi ya Mungu na kutumika kama foili kwa nguvu za Mungu—ni kupitia kwa uasi wetu ndiyo tunatumika kama foili kwa ajili ya tabia Yake yote yenye haki. Sisi ni vyombo vya huduma na viungo kwa kazi ya mwisho ya Mungu—sisi ni vifaa. “Wanaposikia hivyo, watavutiwa sana. Kisha mtasema: “Sisi pia ni vielelezo na mifano kwa ajili ya kuikamilisha kazi ya ulimwengu mzima, na kuwashinda wanadamu wote. Bila kujali kama ninyi ni watakatifu au wachafu, tumebarikiwa zaidi kuwaliko, kwa sababu tumemwona Mungu. Nguvu ya Mungu imechochewa kupitia nafasi Yake kutushinda sisi, na ni kwa sababu ya uchafu wetu ndipo tabia yake yenye haki imechochewa. Je, mna uwezo wa hilo? Hamna haki! Hii kabisa ni sisi kutiwa moyo na Yeye! Ingawa sisi si wenye kiburi, tuna fahari ya kumtukuza Mungu kwa sababu hakuna mtu mwingine yeyote anaweza kushuhudia ahadi hiyo kubwa mno, na hakuna mtu mwingine yeyote anaweza kufurahia baraka kubwa kama hiyo. Ni ajabu kwamba watu wachafu jinsi hii kweli wanaweza kufanya kazi ya foili katika usimamizi wa Mungu, na kwa kweli tunashukuru zaidi ya maneno yanavyoweza kueleza. Watauliza: “Kwa hiyo basi, kielelezo na mfano ni nini?” Nanyi mtasema: “Sisi ni waasi zaidi miongoni mwa wanadamu wote pamoja na kuwa wachafu mno. Sisi ni wale walio wapotovu kwa undani zaidi na Shetani na wenye maendeleo kidogo mno na binadamu duni kabisa ambao ni wa mwili. Sisi ni wa mfano hasa wenye taswira ya kutumiwa na Shetani. Sasa tumechaguliwa na Mungu kuwa wale ambao wameshindwa kwanza kati ya wanadamu. Tumeiona tabia ya Mungu yenye haki, tumeirithi ahadi Yake, na Yeye atawashinda watu zaidi kupitia kwetu. Hii ndiyo sababu sisi ni vielelezo na mifano kwa wale ambao wameshindwa kati ya wanadamu.” Huu ni ushuhuda wenu bora kabisa, na huu ni uzoefu wenu bora kabisa.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni