Mnapaswa kujua kuhusu hadithi ya ndani na uumbaji wa Biblia. Ufahamu huu haushikiliwi na wale ambao hawajakubali kazi mpya ya Mungu. Wao hawajui. Waelezee mambo haya ya kiini, na hawatakuwa pamoja nawe wenye kushikilia sana elimu ya vitabuni na sheria kuhusu Biblia. Wao huchunguza kwa uthabiti kile ambacho kimetabiriwa: Kauli hii imeshatimia? Kauli ile imeshatimia? Kukubali kwao injili ni kwa mujibu wa Biblia; wao huhubiri injili kulingana na Biblia. Wao huyategemea maneno ya Biblia kumwamini Mungu; bila Biblia, wao hawatamwamini Mungu. Hii ndiyo njia ambayo wao huishi, kuichunguza Biblia hivyo. Wakati ambapo wao huchunguza Biblia tena na kukuuliza wewe kuhusu ufafanuzi, unaweza kusema, “Kwanza, hebu tusithibitishe kila kauli. Badala yake, hebu tuangalie vile Roho Mtakatifu hufanya kazi. Hebu tulinganishe dhidi ya ukweli ili tuone kama njia tunayotembea inakubaliana na kazi ya Roho Mtakatifu, na tutumie kazi ya Roho Mtakatifu kuangalia kwa makini kama njia hiyo ni sahihi. Kuhusu kama kauli hii au kauli ile imeshatimia, sisi binadamu hatupaswi kuingilia. Ni bora kwetu badala yake kuzungumza kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu na kazi ya karibuni zaidi ambayo Mungu anafanya sasa. Biblia ina maneno ya Mungu yaliyonenwa na manabii na maneno yaliyoandikwa na wanadamu waliotumiwa na Mungu wakati huo; ni Mungu Mwenyewe tu ndiye anaweza kueleza maneno hayo, Roho Mtakatifu pekee ndiye anaweza kutambulisha maana ya maneno hayo, na Mungu Mwenyewe tu ndiye anaweza kuivunja mihuri saba na kukifungua kitabu. Wewe si Mungu, na wala Mimi si Mungu, kwa hiyo nani anathubutu kueleza kwa hiari maneno ya Mungu? Je, wewe unathubutu kueleza maneno hayo? Hata kama manabii Yeremia, Yohana na Eliya wangekuwa hapa, hawangethubutu, kwani wao si Mwanakondoo. Ni Mwanakondoo pekee ndiye anaweza kuivunja mihuri saba na kufungua kitabu, na hakuna mwingine awezaye kuyaeleza maneno Yake. Sithubutu kunyang’anya jina la Mungu, seuze kujaribu kuyaeleza maneno ya Mungu. Naweza tu kuwa yule ambaye humtii Mungu. Je, wewe ni Mungu? Hakuna viumbe wa Mungu ambao huthubutu kufungua kitabu au kuyafafanua maneno hayo, na hivyo Sithubutu kuyaeleza pia. Ni bora usijaribu kuyaeleza. Hakuna kati yetu atakayeeleza. Hebu tuzungumze kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu; hili ndilo mwanadamu anaweza kufanya. Najua machache kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, lakini kwa vile Sina uzoefu Wangu binafsi na kazi hiyo, Naweza tu kuizungumzia kwa kiasi kidogo. Kuhusu maneno yaliyonenwa na Isaya au Yesu wakati huo, Sitafanya ufafanuzi. Sijifunzi Biblia; badala yake, Mimi hufuata kazi ya sasa ya Mungu. Wewe kwa kweli unaichukulia Biblia kuwa kitabu kidogo, lakini siyo kweli kwamba kinaweza tu kufunguliwa na Mwanakondoo. Isipokuwa Mwanakondoo, nani mwingine anaweza kufanya hivyo? Wewe si Mwanakondoo, na wala Mimi sithubutu kudai kuwa Mungu Mwenyewe, kwa hiyo hebu tusichambue au kuichunguza Biblia. Bora kujadili kazi ambayo hufanywa na Roho Mtakatifu, yaani, kazi ya sasa ambayo hufanywa na Mungu Mwenyewe. Hebu tuangalie kanuni na kiini cha kazi ya Mungu, kisha tuyaangalie kwa makini dhidi ya hayo kuona kama njia tunayotembea siku hii ni ya kweli. Hebu tulinganishe na hili kama kiwango.” Kama ninyi huhubiri injili, hasa kwa wale walio katika ulimwengu wa kidini, lazima muelewe Biblia na muwe na ujuzi wa hadithi yake ya ndani, la sivyo, hutaweza kuhubiri injili. Mara tu unapopata utambuzi wa taswira kubwa, usiyachunguze maneno ya Biblia yaliyopitwa na wakati, na zungumza tu kuhusu kazi ya Mungu na ukweli wa maisha, kisha utaweza kuwapata wale wanaotafuta kwa roho ya kweli.
Mnafaa kuelewa kazi ya Yehova, sheria Alizoweka, na kanuni ambazo kwazo Aliyaongoza maisha ya mwanadamu, yaliyomo kwenye kazi Aliyofanya kwenye Enzi ya Sheria, kusudio lililomfanya Yeye kuweka wazi zile sheria, umuhimu wa kazi Yake katika Enzi ya Neema, na kazi anayofanya Mungu kwenye awamu hii ya mwisho. Hatua ya kwanza ni kazi ya Enzi ya Sheria, hatua ya pili ni kazi ya Enzi ya Neema, na hatua ya tatu ni kazi ya siku za mwisho. Lazima muelewe awamu hizi za kazi ya Mungu. Tangu mwanzo hadi mwisho, kuna hatua tatu kwa jumla. Ni nini kiini cha kila hatua ya kazi? Ni hatua ngapi hutekelezwa katika kazi ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita? Kila hatua hutekelezwa vipi, na kwa nini kila mojawapo hutekelezwa kwa njia hii? Haya yote ni maswali ya maana sana. Kazi ya kila enzi ni wakilishi. Yehova alitekeleza kazi gani? Mbona Alifanya hivyo? Mbona Aliitwa Yehova? Yesu alitekeleza kazi gani katika Enzi ya Neema, na Alifanyaje hivyo? Ni hali gani za tabia ya Mungu huwakilishwa na kila hatua ya kazi na kila enzi? Ni hali zipi za tabia Yake zilijitokeza katika Enzi ya Sheria? Na katika Enzi ya Neema? Na kisha katika enzi ya mwisho? Haya maswali halisi ni yale ambayo ni lazima myaelewe. Tabia yote ya Mungu imefichuliwa katika mpango wote wa uongozi wa miaka elfu sita. Haikufichuliwa tu katika Enzi ya Neema, ni katika Enzi ya Sheria tu, na zaidi ya hayo, ni katika wakati huu wa siku za mwisho. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inawakilisha hukumu, ghadhabu na kuadibu. Kazi ifanywayo katika siku za mwisho haiwezi kuwekwa mbadala wa kazi ya Enzi ya Sheria ama ile ya Enzi ya Neema. Ingawa, hatua zote tatu zinaungana kuwa kitu kimoja na yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kawaida, utekelezaji wa kazi hizi umegawanyishwa katika enzi tofauti. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inaleta kila kitu mpaka tamati; ile iliyofanywa katika Enzi ya Sheria ni ya mwanzo; na ile iliyofanywa katika Enzi ya Neema ni ya ukombozi. Na kuhusu maono ya kazi katika mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita, hakuna anayeweza kupata ufahamu au kuelewa. Maono kama hayo yamebaki kuwa mafumbo kila wakati. Katika siku za mwisho, kazi ya neno pekee inafanyika ili kuukaribisha Wakati wa Ufalme lakini haiwakilishi enzi zile zingine. Siku za mwisho sio zaidi ya siku za mwisho na sio zaidi ya Enzi ya Ufalme, ambayo haiwakilishi Enzi ya Neema au Enzi ya Sheria. Siku za mwisho ni wakati ambapo kazi zote ndani ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita inafichuliwa kwenu. Mafumbo kama hayo hayawezi kufichuliwa na mwanadamu yeyote. Haijalishi mwanadamu ana maarifa makubwa ya Biblia vipi, yanabaki tu kuwa maneno na si kitu zaidi, kwani mwanadamu haelewi kiini cha Biblia. Mwanadamu anaposoma Biblia, anaweza kupokea baadhi ya ukweli, kueleza baadhi ya maneno ama kuchunguza vifungu maarufu na nukuu, lakini hatawahi kuwa na uwezo wa kunasua maana iliyoko katika maneno hayo, kwani yote aonayo mwanadamu ni maneno yaliyokufa pekee, sio matendo ya kazi ya Yehova na Yesu, na mwanadamu hawezi kufumbua mafumbo ya kazi ya aina hiyo. Kwa hivyo, fumbo la mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ni fumbo kuu, iliyofichwa zaidi na isiyoshawishika kwa mwanadamu. Hakuna anayeweza kuelewa moja kwa moja mapenzi ya Mungu, ama, Yeye Mwenyewe Aeleze na kumfungulia mwanadamu, vinginevyo, yatabaki kuwa mafumbo milele kwa mwanadamu na kubaki mafumbo yaliyofungwa milele. Usiwajali wale walio katika ulimwengu wa kidini; kama hamngeambiwa leo, pia nyinyi hamngeweza kuelewa. Kazi hii ya miaka elfu sita ni ya fumbo zaidi kuliko unabii wote wa manabii. Ni fumbo kuu zaidi tangu uumbaji, na hakuna nabii wa awali ambaye amewahi kuweza kulielewa, kwani fumbo hili hufumbuliwa tu katika enzi ya mwisho na kamwe halijawahi kufichuliwa hapo awali. Mkielewa fumbo hili na muweze kulipokea kwa ukamilifu, wale watu wote wa kidini watashindwa kwa fumbo hili. Hili pekee ndilo kuu zaidi ya maono, lile ambalo mwanadamu hutamani sana kulielewa lakini pia lile ambalo si wazi zaidi kwake. Mlipokuwa katika Enzi ya Neema, hamkujua kazi ambayo ilifanywa na Yesu wala ile ambayo ilifanywa na Yehova. Watu hawakuelewa chochote kuhusu kwa nini Yehova alitangaza sheria, kwa nini Aliwaambia watu wazitii sheria au kwa nini ilikuwa lazima kwa hekalu kujengwa, na sembuse watu kuelewa kwa nini Waisraeli waliongozwa kutoka Misri hadi jangwani na kisha hadi Kanaani. Ni mpaka siku hii ndipo mambo haya yamefichuliwa.
Kazi katika siku za mwisho ni hatua ya mwisho kati ya hizo tatu. Ni kazi ya enzi nyingine mpya na haiwakilishi kazi ya usimamizi mzima. Mpango wa miaka elfu sita umegawa katika hatua tatu za kazi. Hakuna hatua moja pekee itakayowakilisha kazi ya enzi hizo tatu ila inaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya yote. Jina Yehova haliwezi kuwakilisha tabia yote ya Mungu. Ukweli kuwa Alitekeleza kazi katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kuwa Mungu Anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria. Yehova alitengeneza sheria kwa mwanadamu na kutoa amri, Akimuuliza mwanadamu ajenge hekalu na madhabahu; kazi Aliyofanya inawakilisha tu Enzi ya Sheria. Kazi Aliyoifanya haidhibitishi kuwa Mungu ni Mungu Anayemwamuru mwanadamu kufuata sheria, Mungu Aliye hekaluni, ama Mungu Aliye mbele ya madhabahu. Haya hayawezi kusemwa. Kazi chini ya sheria inaweza tu kuwakilisha enzi moja. Kwa hivyo, kama Mungu Alifanya kazi katika Enzi ya Sheria pekee, mwanadamu angemfafanua Mungu na kusema, “Mungu ni Mungu Aliye hekaluni. Ili kumtumikia Mungu, lazima tuvae mavazi ya kikuhani na tuingie hekaluni.” Iwapo kazi katika Enzi ya Neema haingetekelezwa na Enzi ya Sheria ingeendelea mpaka wakati huu wa sasa, mwanadamu hangefahamu kuwa Mungu pia ni mwenye huruma na upendo. Iwapo kazi katika Enzi ya Sheria haingefanywa, na badala yake kazi katika Enzi ya Neema pekee , basi yote ambayo mwanadamu angefahamu ni kwamba Mungu Anakomboa tu mwanadamu na kumsamehe dhambi zake. Wangefahamu tu kuwa Yeye ni mtakatifu na asiye na hatia, kwamba Anaweza kujitoa kafara na kusulubishwa kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu angejua tu kuhusu haya na asiwe na ufahamu wa mambo mengine yoyote. Kwa hivyo kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu. Enzi ya Sheria inawakilisha vipengele vingine, Enzi ya Neema vipengele vingine na enzi hii vipengele vingine. Tabia ya Mungu inaweza tu kuonekana kwa mchanganyiko wa hatua zote tatu. Ni wakati tu mwanadamu anajua hatua hizi tatu ndipo anaweza kuipokea kikamilifu. Hakuna hatua kati ya hizo tatu ambayo inaweza kuachwa. Utaiona tu tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake mara tu utakapozijua hatua hizi tatu za kazi. Ukweli kamba Mungu alikamilisha kazi yake katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kwamba Yeye ni Mungu chini ya sheria tu, na ukweli kamba alikamilisha kazi Yake ya ukombozi haimaanishi kuwa Mungu Atamkomboa mwanadamu milele. Hizi zote ni hitimisho zilizofanywa na mwanadamu kuhusu jambo hilo. Enzi ya Neema ikiwa imefika mwisho, huwezi basi kusema kuwa Mungu ni wa msalaba tu na kuwa msalaba pekee unawakilisha wokovu wa Mungu. Ukifanya hivyo, basi utakuwa unamfasili Mungu. Katika hatua hii, Mungu Anafanya zaidi kazi ya Neno, lakini huwezi kusema kuwa Mungu hajawahi kuwa Mwenye huruma kwa mwanadamu na kwamba yote Aliyoleta ni kuadibu na hukumu. Kazi katika siku za mwisho inaonyesha wazi kazi ya Yehova na ile ya Yesu na mafumbo yote yasioeleweka na mwanadamu. Hii inafanywa ili kuonyesha hatima na mwisho wa binadamu na kukamilisha kazi yote ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Hatua hii ya kazi katika siku za mwisho huleta kila kitu kufika mwisho. Mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu lazima yaelezwe ili kumpa mwanadamu ufahamu na kuweza kuelewa kwa kina katika mioyo yao. Hapo tu ndipo wanadamu wataweza kugawanywa kulinga na aina zao. Baada tu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilishwa ndipo mwanadamu atapata kuelewa tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake, kwani usimamizi Wake utakuwa umefika mwisho. Kwa kuwa mmeipitia kazi ya Mungu katika enzi ya mwisho, tabia ya Mungu ni gani? Je, wewe unathubutu kusema kwamba Mungu ni Mungu ambaye hunena maneno tu? Hungeweza kuthubutu kufanya uamuzi huu. Wengine husema kwamba Mungu ni Mungu ambaye hufumbua mafumbo, kwamba Mungu ni Mwanakondoo na Ambaye huvunja mihuri saba. Hakuna ambaye huthubutu kufanya uamuzi huu. Na kuna wengine ambao husema kwamba Mungu ni aliyepata mwili. Hili bado si sahihi. Wengine husema kwamba Mungu mwenye mwili hunena maneno tu na Hafanyi ishara na maajabu. Wala hungeweza kuthubutu kunena kwa njia hii, kwani Yesu alipata mwili na Alifanya ishara na maajabu, kwa hiyo wewe huthubutu kumfafanua Mungu kwa urahisi. Kazi yote iliyofanyika katika mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita imefika mwisho sasa. Ni baada tu ya kazi hii kubainika wazi kwa mwanadamu na kutekelezwa miongoni mwa wanadamu ndipo watakapofahamu tabia Yake na mali Yake na uwepo. Kazi za enzi hizi zitakapokamilika, mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu yatakuwa yamebainika, ukweli wote ambao haukuwa unaeleweka utawekwa wazi, na mwanadamu atakuwa ameambiwa njia na hatima ya baadaye. Hii ndio kazi yote inayopaswa kufanyika katika hatua hii. Ingawa njia ambayo mwanadamu hutembea leo pia ni njia ya msalaba na ya kuteseka, kile ambacho mwanadamu wa leo hutenda, hula, hunywa na hufurahia ni tofauti zaidi na yale ya mwanadamu aliyekuwa chini ya sheria na katika Enzi ya Neema. Kinachohitajika kutoka kwa mwanadamu wakati huu sio kama ilivyokuwa kitambo na zaidi sio kama kilichohitajika kutoka kwake katika Enzi ya Sheria. Na ni kipi kilichoulizwa kwa mwanadamu chini ya Sheria kazi ilipofanya Israeli? Hawakuulizwa chochote zaidi ya kuiheshimu Sabato na Sheria za Yehova. Lakini si hivyo katika wakati huu. Siku ya Sabato, mwanadamu anafanya kazi, hukusanyika na kuomba kama kawaida, na hakuna vizuizi vinavyowekwa. Wale katika Enzi ya Neema ilibidi wabatizwe, na pia zaidi walitarajiwa kufunga, kuvunja mkate, kunywa divai, kufunika vichwa vyao na kuwaoshea wengine miguu yao. Sasa, sheria hizi zimefutwa na mahitaji makuu yanaulizwa kutoka kwa mwanadamu, kwani kazi ya Mungu inaendelea kuimarika na kuingia kwa mwanadamu kunafika kiwango cha juu. Zamani, Yesu Aliweka mikono Yake juu ya mwanadamu na kuomba, lakini sasa kwamba kila kitu kimesemwa, kuwekelea mikono kuna maana gani? Maneno pekee yanaweza kupata matokeo. Alipowekelea mikono Yake juu ya mwanadamu hapo awali, ilikuwa ni kwa ajili ya kumbariki na kumponya mwanadamu. Hivyo ndivyo Roho Mtakatifu Alivyofanya kazi wakati huo, lakini sio hivyo wakati huu. Wakati huu, Roho Mtakatifu Anatumia maneno katika kazi Yake ili kupata matokeo. Ameyafanya maneno Yake wazi kwenu, na mnapaswa tu kuyaweka katika matendo. Maneno Yake ni mapenzi Yake na yanaonyesha kazi Atakayofanya. Kupitia kwa maneno Yake, utaweza kuelewa mapenzi Yake na yale ambayo Anauliza upate. Unayaweka tu maneno Yake katika matendo moja kwa moja bila haja ya kuwekelea mikono. Wengine wanaweza kusema, “Wekelea mikono Yako juu yangu! Wekelea mikono yako juu yangu ili niweze kupokea baraka zako na kushiriki kwako.” Haya yote ni mazoezi yaliyopitwa na wakati na ambayo yanakataliwa katika wakati huu, kwani enzi zimebadilika. Roho Mtakatifu Anafanya kazi kulingana na enzi, sio tu katika mapenzi Yake ama kulingana na masharti. Enzi zimebadilika, na enzi mpya lazima ilete kazi mpya. Huu ni ukweli wa kila hatua ya kazi, na hivyo kazi Yake haiwezi kurudiwa. Katika Enzi ya Neema, Yesu Alifanya nyingi ya kazi hiyo, kama kuponya magonjwa, kukemea mapepo, kuwekelea mikono Yake juu ya wanadamu, na kumbariki mwanadamu. Hata hivyo, kuendelea kufanya hivyo hakutasaidia chochote katika wakati huu. Roho Mtakatifu Alifanya kazi hivyo katika huo wakati, kwani ilikuwa Enzi ya Neema, na mwanadamu alipewa neema ya kutosha ili afurahie. Mwanadamu hakuhitajika kulipa gharama yoyote na angepokea neema mradi tu angekuwa na imani. Kila mtu alitendewa kwa neema kubwa. Sasa, enzi imebadilika, na kazi ya Mungu imeendelea zaidi; kupitia kuadibu na hukumu Yake, uasi wa mwanadamu na vitu vichafu katika mwanadamu vitatupiliwa mbali. Jinsi ilivyokuwa hatua ya wokovu, ilimbidi Mungu kufanya kazi hiyo, Akimwonyesha mwanadamu neema ya kutosha ili mwanadamu afurahie, ili Amkomboe mwanadamu kutoka kwa dhambi, na kwa neema amsamehe mwanadamu dhambi zake. Hatua hii ya sasa ni ya kufichua udhalimu ulio ndani ya mwanadamu kwa njia ya kuadibu, hukumu, kupigwa na maneno, na vile vile nidhamu na ufunuo wa maneno, ili baadaye binadamu waweze kuokolewa. Hii ni kazi ya undani zaidi kuliko ukombozi. Katika Enzi ya Neema, mwanadamu alifurahia neema ya kutosha na amezoea neema hii, kwa hivyo sio ya kufurahiwa na mwanadamu tena. Kazi kama hii imepitwa na wakati sasa na haitafanyika tena. Sasa, mwanadamu anaokolewa kupitia hukumu ya neno. Baada ya mwanadamu kuhukumiwa, kuadibiwa na kusafishwa, tabia yake basi inabadilika. Je sio kwa sababu ya maneno ambayo Nimenena? Kila hatua ya kazi inafanywa kulingana na maendeleo ya binadamu wote na kwa enzi. Kazi yote ina umuhimu wake; inafanywa kwa ajili ya wokovu wa mwisho, ili binadamu awe na hatima nzuri baadaye, na kwa mwanadamu kugawanywa kulingana na aina Yake mwishowe.
Kazi katika siku za mwisho ni kunena maneno. Mabadiliko makuu yanaweza kusababishwa kwa watu kupitia katika maneno hayo. Mabadiliko yanayosababishwa sasa kwa watu hawa kwa sababu ya kukubali maneno haya ni makubwa kuliko yale ya watu katika Enzi ya Neema kwa kukubali ishara na maajabu hayo. Kwani, katika Enzi ya Neema, mapepo yaliondoka kutoka kwa mwanadamu kwa kuwekewa mikono na maombi, lakini tabia potovu ndani ya mwanadamu ilibaki. Mwanadamu aliponywa magonjwa na kusamehewa dhambi zake, lakini kazi ya jinsi tabia potovu za kishetani katika mwanadamu haikutupiliwa mbali na bado iko ndani yake. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini haimaanishi kuwa mwanadamu hana dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia potovu za zamani za kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivyo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili. Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwema Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na kuonekana kwa kiungu; kama mwanadamu angeishi katika huo msingi, alichukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, hii ina maana kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia ya kuielekea tabia iliyobadilika; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii inamfanya mwanadamu kuwa safi kupitia neno ili kumpatia mwanadamu njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendelea na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.
Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguzwa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Na kama sio Mungu kuvalia umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, mwanadamu hawangeweza kupokea wokovu huu. Kwani mwanadamu hawezi kumkaribia kwa njia yoyote ile, zaidi kama jinsi hakuna anayeweza kukaribia wingu la Yehova. Ni kwa kuwa mwanadamu wa kuumbwa tu, hivyo ni kusema, kuliweka neno Lake katika mwili Atakaogeukana kuwa, ndio ataweza kulifanya neno yeye Mwenyewe ndani ya wale wote wanaomfuata. Hapo ndipo mwanadamu atasikia mwenyewe neno Lake, kuona neno Lake, na kupokea neno Lake, kisha kupitia hili aokolewe kamili. Kama Mungu hangegeuka na kupata mwili, hakuna mwanadamu mwenye mwili ambaye angepokea wokovu huo mkuu, wala hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye angeokolewa. Kama Roho wa Mungu angefanya kazi moja kwa moja kati ya mwanadamu, mwanadamu angepigwa ama kubebwa kabisa kama mfungwa na Shetani kwani mwanadamu hawezi kushirikiana na Mungu. Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho. Ni mpaka siku za mwisho tu ambapo Mungu Ametakasa binadamu kikamilifu kwa kufanya kazi ya hukumu na kuadibu mwanadamu kwa kuwa muasi, ndipo Mungu atakamilisha kazi Yake ya wokovu na kupumzika. Kwa hivyo, katika hatua tatu za kazi, ni mara mbili tu ndipo Mungu Alikuwa mwili ili kufanya kazi Yake kati ya mwanadamu Mwenyewe. Hiyo ni kwa sababu moja tu kati ya hatua tatu za kazi ni kuwaongoza wanadamu katika maisha yao, ilhali zingine mbili ni kazi ya wokovu. Mungu Anapokuwa mwili tu ndipo Atakapoishi pamoja na mwanadamu, kuzoea mateso ya dunia, na kuishi katika mwili wa kawaida. Katika hali hii tu ndipo Ataweza kumpatia mwanadamu wa uumbaji Wake neno la matendo wanalohitaji. Mwanadamu anapokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sio moja kwa moja kutoka kwa maombi yao kwenda mbinguni. Kwani mwanadamu ni mwenye mwili; mwanadamu hawezi kuona Roho wa Mungu na pia kutoweza kumkaribia. Kile tu mwanadamu anaweza kushiriki na mwili wa Mungu; kupitia Yeye tu ndipo mwanadamu ataweza kuelewa maneno yote, na ukweli wote, na kupokea wokovu kamili. Kupatikana kwa mwili mara ya pili kunatosha kumaliza dhambi za mwanadamu na kumtakasa mwanadamu. Hivyo, kupatikana kwa mwili mara ya pili kutafikisha tamati kazi yote ya Mungu mwenye mwili na kukamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili. Baada ya hapo, kazi ya Mungu mwenye mwili itakuwa imefika mwisho kabisa. Baada ya kupata mwili mara ya pili, hatakuwa mwili tena kwa kazi Yake. Kwani usimamizi Wake wote utakuwa umefika mwisho. Katika siku za mwisho, mwili Wake utakuwa umepata watu Wake teule kabisa, na yote mwanadamu katika siku za mwisho watakuwa wamegawanywa kulingana na aina yao. Hatafanya kazi ya wokovu tena, wala Hatarudi kuwa mwili ili kutekeleza kazi yoyote. Katika kazi ya siku za mwisho, neno ni kubwa zaidi ya udhihirisho wa ishara na maajabu, na mamlaka ya neno yanashinda yale ya ishara na maajabu. Neno linaweka wazi tabia zote potovu katika moyo wa mwanadamu. Huwezi kutambua binafsi wewe mwenyewe. Yatakapofunuliwa kwako kupitia kwa neno, utakuja kujua mwenyewe; hutaweza kuyakataa, na utashawishika kikamilifu. Je haya si mamlaka ya neno? Haya ndiyo matokeo yanayopatikana kwa kazi ya wakati huu ya neno. Kwa hivyo, mwanadamu hawezi kuokolewa kikamilifu kutoka kwa dhambi zake kwa kuponya magonjwa na kukemea mapepo na hawezi kufanywa mkamilifu kabisa kwa udhihirisho wa ishara na maajabu. Mamlaka ya kuponya na kukemea mapepo yanapatia mwanadamu neema tu, lakini mwili wa mwanadamu bado ni wa Shetani na tabia potovu za kishetani zitabaki ndani ya mwanadamu. Kwa maneno mengine, yale ambayo hayajatakaswa bado ni ya dhambi na uchafu. Ni baada tu ya mwanadamu kufanywa safi kupitia kwa maneno ndipo atakapotwaliwa na Mungu na kutakaswa. Wakati mapepo yalikemewa kutoka kwa mwanadamu na alikombolewa, hii ilimaanisha tu kwamba alipokonywa kutoka kwa mikono ya Shetani na kurudishwa kwa Mungu. Hata hivyo, hajafanywa msafi ama kubadilishwa na Mungu, anabaki mpotovu. Ndani ya mwanadamu bado kuna uchafu, pingamizi na uasi; mwanadamu amerudi tu kwa Mungu kupitia kwa ukombozi, lakini mwanadamu hana maarifa kumhusu na bado anamkataa na kumsaliti Mungu. Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuutupa nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa. Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivyo, hata kama sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. Kwa mfano, wakati ambapo watu walijua kwamba walitoka kwa Moabu, walitoa maneno ya malalamiko, hawakutafuta tena uzima, na wakawa baridi kabisa. Je, hili halionyeshi kwamba bado hawawezi kutii kwa ukamilifu kutawaliwa na Mungu? Je, hii siyo tabia ya kishetani ya upotovu kabisa? Ulipokuwa hupitii kuadibu, mikono yako iliinuliwa juu zaidi ya wengine wote, hata ile ya Yesu. Na ulilia kwa sauti kubwa: Kuwa mwana mpendwa wa Mungu! Kuwa mwandani wa Mungu! Ni heri tufe kuliko kumtii Shetani! Muasi Shetani wa zamani! Liasi joka kuu jekundu! Acha joka kuu jekundu lianguke kabisa kutoka mamlakani! Acha Mungu atufanye kamili! Vilio vyako vilikuwa vikubwa zaidi ya wengine. Lakini kisha zikaja nyakati za kuadibu na, mara tena, tabia ya upotovu ya watu ilifichuliwa. Kisha, vilio vyao vikakoma, na hawakuwa tena na azimio. Huu ni upotovu wa mwanadamu; unaingia ndani zaidi kuliko dhambi, ulipandwa na Shetani na umekita mizizi ndani zaidi ya mwanadamu. Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea. Mwanadamu alipiga kelele hivyo wakati uliopita kwa sababu mwanadamu hakuwa na ufahamu wa tabia yake potovu ya asili. Huo ndio uchafu ulio ndani ya mwanadamu. Kotekote katika kipindi kirefu hivyo cha hukumu na kuadibu, mwanadamu aliishi katika mazingira ya mvutano. Je, haya yote hayakutimizwa kupitia kwa neno? Wewe pia hukulia kwa sauti ya juu kabla ya majaribio ya watendaji huduma? Ingia katika ufalme! Wale wote ambao wanalikubali jina hili wataingia katika ufalme! Wote watashiriki Mungu! Wakati ambapo majaribio ya watendaji huduma yalikuja, hukulia tena. Mwanzoni, wote walilia, “Mungu! Popote Uniwekapo, nitatii kuongozwa na Wewe.” Baada ya kusoma maneno ya Mungu, “Nani atakuwa Paulo Wangu?” mwanadamu alisema, “Niko radhi!” Kisha akayaona maneno, “Na kuhusu imani ya Ayubu?” Kwa hiyo akasema, “Niko radhi kuichukua imani ya Ayubu. Mungu, tafadhali nijaribu!” Majaribio ya watendaji huduma yalipokuja, alizirai mara moja na nusura angekosa kusimama tena. Baada ya hilo, uchafu ndani ya moyo wa mwanadamu ulipungua polepole. Je, hili halikutimizwa kupitia kwa neno? Kwa hiyo, kile ambacho mmepitia wakati wa sasa ni matokeo ambayo hutimizwa kupitia kwa neno, hata makuu zaidi ya yale ambayo hutimizwa kupitia kwa Yesu kufanya ishara na maajabu. Utukufu wa Mungu na mamlaka ya Mungu Mwenyewe ambayo ninyi huona hayaonekani tu kupitia kwa usulubishaji, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo, lakini zaidi kupitia kwa hukumu Yake kwa neno. Hili hukuonyesha wewe kwamba sio tu ufanyaji wa ishara, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo ndiyo mamlaka na nguvu za Mungu, bali hukumu kwa neno unaweza kuwakilisha bora mamlaka ya Mungu na kufichua uweza Wake.
Kile ambacho mwanadamu amepata sasa—kimo cha mwanadamu leo, maarifa yao, upendo, uaminifu, utiifu, na pia kuona kwao—ni matokeo yanayopatikana kupitia hukumu kwa neno. Kwamba unaweza kuwa na uaminifu na kubaki umesimama mpaka siku hii ipatikane kwa kupita neno. Hivi sasa mwanadamu anaona kuwa kazi ya Mungu kupata mwili ni ya ajabu kweli. Kuna mengi ambayo hayawezi kupatikana na mwanadamu; ni mafumbo na maajabu. Kwa hivyo, wengi wamejiwasilisha. Wengine hawajawahi kujiwasilisha kwa mwanadamu yeyote kutoka siku za kuzaliwa kwao, ilhali wanapoyaona maneno ya Mungu siku hii, wanajiwasilisha kikamilifu bila kujua wamefanya vile, na hawajaribu kuchunguza au kusema chochote kingine. Binadamu wameanguka chini ya neno na wamesujudu chini ya hukumu kwa neno. Kama Roho wa Mungu angemwongelesha mwanadamu moja kwa moja, wote wangejiwasilisha kwa sauti hiyo, na kuanguka chini bila maneno ya ufunuo, vile Paulo alivyoanguka chini kukiwa na nuru alipokuwa akisafiri kwenda Damaski. Mungu angeendelea kufanya kazi kwa njia hii, mwanadamu hangeweza kutambua upotovu wake kupitia kwa hukumu katika neno na kupata wokovu. Ni kwa kupata mwili pekee ndiyo Ataweza kuwasilisha maneno Yake Mwenyewe kwa masikio ya wale wote ambao wana masikio waweze kuyasikia maneno Yake na kupokea kazi Yake ya hukumu kupitia kwa neno. Hayo tu ndio matokeo yanayopokewa na neno Lake, badala ya kutokea kwa Roho ikimtisha mwanadamu kuwasilisha. Ni kupitia tu kwa kazi ya vitendo na ya ajabu ndio tabia ya mwanadamu, iliyofichika ndani zaidi kwa enzi nyingi, ifichuliwe kabisa ili mwanadamu aitambue na kuibadilisha. Hili ndiyo kazi ya vitendo ya Mungu mwenye mwili wa Mungu; Ananena na kutekeleza hukumu juu ya mwanadamu kupitia kwa neno. Haya ndiyo mamlaka ya Mungu mwenye mwili na umuhimu wa Mungu kupata mwili. Inafanyika kuonyesha mamlaka ya Mungu mwenye mwili, matokeo yanayopatikana na kazi ya neno, na kwamba Roho Amekuja kwa mwili; Anaonyesha mamlaka Yake kupitia hukumu juu ya mwanadamu kwa neno. Ingawa mwili Wake ni hali ya nje ya mwanadamu wa kawaida, ni matokeo ambayo neno Lake linapokea ndiyo yanamwonyesha mwanadamu kuwa Amejaa mamlaka, kwama ni Mungu Mwenyewe na kwamba maneno Yake ni maonyesho ya Mungu Mwenyewe. Hii inaonyesha wanadamu wote kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe, Mungu Mwenyewe Aliyekuwa mwili, na kwamba Asikosewe na yeyote. Hakuna anayeweza kuepuka hukumu Yake kupitia kwa neno, na hakuna nguvu ya giza inayoweza kutamalaki juu ya mamlaka Yake. Mwanadamu anamtii Yeye kabisa kwa sababu Yeye ni Neno aliyepata mwili, kwa sababu ya mamlaka Yake, na kwa sababu ya hukumu Yake kwa neno. Kazi iliyoletwa na mwili Wake uliokuwa mwili ni mamlaka ambayo Anamiliki. Anakuwa mwili kwani mwili pia unaweza kuwa na mamlaka, na Anaweza kutekeleza kazi kati ya wanadamu katika halii ya njia halisi, inayoonekana na kuguswa na mwanadamu. Kazi kama hii ni ya ukweli kuliko kazi ingine yoyote ifanywayo moja kwa moja na Roho wa Mungu Aliye na mamlaka yote, na matokeo Yake ni dhahiri pia. Hii ni kwa sababu mwili Wake unaweza kuongea na kufanya kazi kwa njia halisi; hali ya nje ya mwili Wake haina mamlaka yoyote na inaweza kukaribiwa na mwanadamu. Dutu Yake inabeba mamlaka, lakini mamlaka Yake hayaonekani kwa yeyote. Anaponena na kufanya kazi, mwanadamu hana uwezo wa kutambua uwepo wa mamlaka Yake; hili ni nzuri kwa kazi Yake hata zaidi. Na kazi yote kama hiyo inaweza kupata matokeo. Ingawa hakuna mwanadamu anayefahamu kuwa Anayo mamlaka ama kuona kuwa Hastahili kukosewa ama kuona hasira Yake, kupitia mamlaka Yake yaliyofichika na hasira na hotuba ya uma, Anapata matokeo yaliyotarajiwa ya neno Lake. Kwa maneno mengine, kupitia kwa tani ya sauti Yake, ukali wa hotuba Yake, na hekima ya maneno Yake, mwanadamu anashawishika kabisa. Kwa njia hii, mwanadamu anawasilisha kwa neno la Mungu mwenye mwili wa Mungu, ambaye anaonekana kutokuwa na mamlaka, hivyo kufikia lengo Lake la wokovu kwa mwanadamu. Huu ndio umuhimu mwingine wa kuingia Kwake katika mwili: kuongea na ukweli zaidi na kukubali ukweli wa neno Lake kuwa na athari juu ya mwanadamu ili kushuhudia nguvu ya neno la Mungu. Kwa hivyo kazi hii, isipofanywa kupitia kupata mwili, haitakuwa na matokeo hata kidogo na haitaweza kuokoa watenda dhambi kikamilifu. Mungu Asipokuwa mwili, Atabaki kama Roho bila kuonekana au kuguswa na mwanadamu. Mwanadamu ni kiumbe wa mwili, na mwanadamu na Mungu ni wa dunia mbili tofauti na ni tofauti kwa asili. Roho wa Mungu hana uwiano na mwili wa mwanadamu, na hakuna uhusiano unaoweza kuwepo kati yao; pia, mwanadamu hawezi kuwa roho. Hivyo, Roho wa Mungu lazima ageuke mmoja wa viumbe na kufanya kazi yake ya asili. Mungu anaweza kujipandisha mahali pa juu zaidi na pia aweze kunyenyekea na kuwa mwanadamu aliyeumbwa, kufanya kazi na kuishi kati ya wanadamu, laikini mwanadamu hawezi kupanda juu na kuwa roho na pia kuteremka chini. Kwa hivyo, Mungu lazima awe mwili ili atekeleze kazi Yake. Kama ilivyokuwa wakati wa kuingia katika mwili mara ya kwanza, mwili wa Mungu mwenye mwili pekee ndio unaoweza kumkomboa mwanadamu kupitia kusulubiwa, ilhali hakuna uwezo wa Roho wa Mungu kusulubiwa kama sadaka ya dhambi kwa mwanadamu. Mungu Angekuwa mwili moja kwa moja ili kuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu, lakini mwanadamu hangepanda mbinguni moja kwa moja kuchukua sadaka ambayo Mungu alikuwa amewaandalia. Hivyo, lazima Mungu asafiri kwenda na kurudi kati ya mbingu na nchi, badala ya kumwacha mwanadamu apande mbinguni kuchukua wokovu huu, kwani mwanadamu alikuwa ameanguka na hangepanda mbinguni, ama hata kupata sadaka ya dhambi. Kwa hivyo, ilikuwa lazima kwa Yesu kuja kati ya wanadamu na binafsi kufanya kazi ambayo mwanadamu hangeweza kukamilisha. Kila wakati ambapo Mungu aligeuka kuwa mwili, ilikuwa lazima kabisa Afanye hivyo. Iwapo hatua yoyote ingetekelezwa moja kwa moja na Roho wa Mungu, Hangevumilia ukosefu wa hadhi unaoambatana na kupata mwili.
Katika hatua hii ya mwisho ya kazi, matokeo yanapatikana kupitia kwa neno. Kupitia kwa neno, mwanadamu anaelewa mafumbo mengi na kazi ya Mungu katika vizazi vilivyopita; kupitia kwa neno, mwanadamu anapewa nuru na Roho Mtakatifu; kupitia kwa neno, mwanadamu anapata kuelewa mafumbo ambayo hayajawahi kuelezwa na vizazi vilivyopita, na pia kazi za manabii na, mitume wa enzi zilizopita, na kanuni ambazo walitumia kufanya kazi; kupitia kwa neno, mwanadamu anatambua tabia ya Mungu Mwenyewe, na pia uasi na pingamizi ya mwanadamu, na kujua dutu yao. Kupitia kwa hatua hizi za kazi na maneno yote yaliyonenwa, mwanadamu anatambua kazi ya Roho Mtakatifu, kazi ya mwili wa Mungu, na zaidi ya hayo, tabia Yake yote. Maarifa yako ya kazi ya usimamizi wa Mungu wa kupita miaka elfu sita ulitwaliwa kupitia kwa neno. Je, maarifa yako hayakuwa ya fikira zako za awali na mafanikio kwa kuyaweka kando pia yalipatikana kupitia neno? Katika hatua ya awali, Yesu Alifanya ishara na maajabu, lakini sio hivyo katika hatua hii. Je si kuelewa kwako kwa nini Hafanyi hivyo pia kulipatikana kupitia neno? Kwa hivyo, maneno yanenwayo katika hatua hii, yanashinda kazi iliyofanywa na mitume na manabii wa vizazi vilivyopita. Hata unabii uliotabiriwa na manabii haungeweza kupata matokeo haya. Manabii waliongelea unabii pekee, ya kile kitakachotendeka hapo baadaye, lakini sio kazi ambayo Mungu angefanya katika wakati huo. Hawakuongea kuongoza mwanadamu katika maisha yao, kuhifadhi ukweli juu ya mwanadamu ama kumfichulia mwanadamu mafumbo, ama hata kutawaza maisha. Kwa maneno yaliyonenwa katika hatua hii, kuna unabii na ukweli, lakini hasa yanafanya kazi ya kutawaza maisha juu ya mwanadamu. Maneno ya wakati huu sio kama unabii wa manabii. Hii ni hatua ya kazi isiyo ya unabii ila ya maisha ya mwanadamu, kubadili tabia ya maisha ya mwanadamu. Hatua ya kwanza ilikuwa kazi ya Yehova kutengeneza njia ya mwanadamu kuabudu Mungu duniani. Ilikuwa kazi ya kuanzisha kutafuta chanzo cha kazi duniani. Wakati huo, Yehova aliwafunza Waisraeli kuiheshimu Sabato, kuwaheshimu wazazi wao na kuishi kwa amani na wengine. Hii ilikuwa kwa sababu wanadamu wa wakati huo hawakuwa wanaelewa kiini cha mwanadamu, wala hawakuelewa wanavyopaswa kuishi duniani. Ilikuwa lazima Kwake katika hatua ya kwanza ya kazi kuwaongoza wanadamu katika maisha yao. Yote yale Yehova aliwazungumzia hayakuwa yamewahi kujulikana kwa binadamu ama kuwa katika umiliki wao. Wakati huo, manabii wengi walisimamishwa kuongelea unabii, yote kutengenezwa chini ya uongozi wa Yehova. Hii ilikuwa sehemu ya kazi hiyo. Katika hatua ya kwanza, Mungu hakuwa mwili, hivyo Alizungumza na makabila yote na mataifa kupitia kwa manabii. Yesu alipofanya kazi Yake katika huo wakati, Hakuzungumza sana kama wakati huu wa leo. Kazi hii ya neno katika siku za mwisho haijafanyika katika enzi na vizazi vilivyopita. Ingawa Isaya, Danieli na Yohana walitabiri utabiri mwingi, unabii huo ulikuwa tofauti kabisa na maneno yazungumzwayo sasa. Walichoongelea ulikuwa unabii pekee, lakini maneno ya sasa sio unabii. Iwapo Ningebadilisha Ninayoongea sasa yawe unabii, je mngeweza kuyaelewa? Iwapo ningezungumzia mambo baada ya Mimi kuondoka, utawezaje kupata kuelewa? Kazi ya neno haikuwahi kufanyika wakati wa Yesu ama Enzi ya Sheria. Labda wengine wanaweza kusema, “Je Yehova hakuzungumza maneno pia katika wakati wa kazi Yake? Juu yaa kuponya magonjwa, kukemea mapepo na kufanya ishara na maajabu, je Yesu hakuzungumza katika wakati huo?” Kuna tofauti katika vile maneno yananenwa. Ni nini ndiyo ilikuwa dutu ya maneno yaliyonenwa na Yehova? Alikuwa tu anawaongoza wanadamu katika maisha yao duniani, ambayo hayakuwa yanahusiana na mambo ya kiroho katika maisha. Ni kwa nini inasemekana kuwa maneno ya Yehova yalitangazwa katika sehemu zote? Neno “kufundisha” linamaanisha kuwaambia waziwazi na kuamrisha moja kwa moja. Hakupa mwanadamu maisha; ila, Alimchukua mwanadamu kwa mkono na kumfunza jinsi ya kumheshimu sana. Hakukuwa na mafumbo. Kazi ya Yehova katika Israeli haikuwa kushughulika na ama kumwadhibu mwanadamu ama kutoa hukumu na kuadibu; ilikuwa kuongoza. Yehova alimwambia Musa awaeleze watu Wake wakusanye mana jangwani. Kila asubuhi kabla ya jua kuchomoza, walikuwa wakusanye mana, iliyotosha tu kuliwa siku hiyo. Mana haingewekwa hadi siku inayofuata, kwani ingeoza. Hakuwafunza wanadamu kufichua asili zao, na Hakufichua mawazo yao na fikira. Hakuwabadilisha wanadamu ila tu aliwaongoza katika maisha yao. Katika wakati huo, mwanadamu alikuwa kama mtoto; mwanadamu hakuelewa chochote na angefanya hatua za kuelekezwa; kwa hivyo, Yehova aliamuru tu sheria kuongoza watu.
Iwapo unataka kueneza injili ili wale wote wanaotafuta kwa moyo wa kweli wapate maarifa ya kazi inayofanywa katika siku hii na kushawishika kabisa, lazima uielewe hadithi ya ndani, dutu na umuhimu wa kazi iliyofanywa katika kila hatua. Kwa kusikia ushirika wako, wataelewa kazi ya Yehova na kazi ya Yesu na, zaidi ya hayo, kazi yote ya Mungu wa leo, na vilevile uhusiano na tofauti kati ya hatua hizo tatu za kazi, ili kwamba, baada ya wao kusikiza, wataona kuwa hakuna hatua yoyote kati ya hizo tatu inahitilafiana na nyingine. Kwa hakika, yote yamefanywa na Roho mmoja. Ingawa Wanafanya kazi katika enzi tofauti , maudhui ya kazi Wanayotekeleza ni tofauti, na maneno Wanayozungumza pia ni tafauti, kanuni ambazo Wanafanya kazi nazo ni sawa. Haya ndiyo maono makuu zaidi ambayo watu wote wanapaswa kuelewa.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni