9/10/2018

Utajiri wa Maisha

      Utajiri wa Maisha

Wang Jun Mkoa wa Shandong
Kwa miaka mingi tangu kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, mke wangu na mimi tumepitia hili pamoja chini ya ukandamizaji wa joka kubwa jekundu. Katika wakati huu, ingawa nimekuwa na udhaifu, maumivu, na machozi, nahisi kwamba nimenufaika pakubwa kutoka kwa uzoefu wa ukandamizaji huu. Uzoefu huu mchungu haujanifanya tu kuona kwa dhahiri asili mbovu ya kupinga maendeleo, na sura mbaya ya joka kubwa jekundu, lakini pia nimetambua asili yangu mwenyewe ya upotovu. Pia umeniruhusu kupata uzoefu wa Uweza wa Mungu na hekima. Kwa kweli nimepitia na kutambua umuhimu halisi wa Mungu kutumia joka kubwa jekundu kama foili[a], ambao kwao imani yangu katika kumfuata Mungu imekuwa imara zaidi na zaidi.
Baada ya kuikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho, kwa sababu ya kuinuliwa na baraka za Mungu, mke wangu na mimi tulitimiza wajibu wetu kwa kutoa ukarimu nyumbani mwetu. Wakati huo, kulikuwa na ndugu wa kiume na wa kike walioishi nasi kila siku na watu mara kwa mara waliingia na kutoka. Kwa hiyo, tulikuwa tunajulikana kiasi katika eneo hilo kwa kumwamini Mungu. Katika majira ya baridi ya mwaka wa 2003, unyanyasaji wa joka kubwa jekundu ukawa mgumu zaidi na zaidi. Siku moja, kiongozi wetu akatuambia: "Polisi wanawaangalia kwa makini. Hamuwezi kukaa hapa tena—mnapaswa kubeba vitu vyenu na kwenda nje kutekeleza wajibu wenu." Kama nimekabiliwa na utaratibu huu wa dakika ya mwisho, nilishtuka. Nilifikiri: Nyumba hii ya paa la matofali niliyofanya kazi ngumu sana kuijenga, ambayo tumeiishi kwa chini ya mwaka mmoja—siko tayari kuiacha hivyo tu! Ewe Mungu, kama unaweza tu kutuacha tuishi hapa kwa miaka michache kabla ya tulazimike kuondoka, hilo lingekuwa jambo zuri. Kuishi mahali pengine hakufai kama hapa, hakufai kama kuishi nyumbani. Lakini mara tu nilipofikiri juu ya ukandamizaji wa joka kubwa jekundu, bado niliamua kuwa baada ya kuiuza nyumba, tulipaswa kuondoka nyumbani ili kutimiza wajibu wetu. Nilipokuwa tu nikitazama pande zote za nyumba yetu iliyokuwa imejengwa karibuni, nilihisi wimbi la huzuni na maumivu. Kwa kweli sikuweza kuvumilia kutengana nayo; nilihisi kuwa kuiuza wakati huo kulikuwa kwa kusikitisha sana. Nilipokuwa tu nikiwaza juu ya mafanikio na hasara ya mwili na sikuweza kuamua, nikasikia maneno ya Mungu yakivuma katika masikio yangu: “Ibrahimu alimtoa Isaka. Nini ambacho mmetoa? Ayubu ilitoa kila kitu. Nini ambacho mmetoa? Watu wengi sana wameyatoa maisha yao, wakafa, wakamwaga damu yao ili kutafuta njia ya kweli. Je, mmelipa gharama hiyo? Kwa kulinganisha, hamna sifa zinazostahili hata kidogo kufurahia neema hiyo kubwa …” (“Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalichoma kiini cha moyo wangu kama upanga wenye ukali pande mbili. Nilihisi aibu ya kustaajabisha. Ilikuwa kweli! Ili kuridhisha matakwa ya Mungu, Ibrahimu alikuwa tayari kubeba maumivu makubwa kutengana na kile alichokipenda, kumfanya mwanawe wa pekee awe sadaka ya kuteketezwa kwa Mungu. Wakati Shetani na Mungu walikuwa na mapatano ya kupinga, ingawa Ayubu alipoteza mali yake yote na watoto wake kumi, alikuwa bado anaweza kulisifu na kulitukuza jina la Yehova. Hata mwishowe wakati alipopitia mateso ya kuwa ameachwa na marafiki na familia zake na kufikwa na ugonjwa, bado aliona heri angelaani siku ya kuzaliwa kwake kuliko kumlaumu Mungu. Alifanya ushuhuda wenye nguvu na wa kushangaza kwa ajili ya Mungu na Shetani alipata ushinde kamili na wa kufedhehesha. Pia kulikuwa na watakatifu na manabii kotekote katika enzi—ili kutekeleza mapenzi ya Mungu, baadhi yao waliacha ujana wao na ndoa zao, baadhi yao waliacha familia zao na jamaa na utajiri wa dunia. Wengine hata walijitolea uhai wao wenyewe na kumwaga damu yao kwa ajili ya kazi ya Mungu. … Lakini nikijiangalia mwenyewe, ingawa nilifurahia neema adimu ya wokovu ambayo vizazi vya watakatifu havikufurahia na maneno mazuri ya maisha yaliyokirimiwa na Mungu, nilikuwa nimeacha nini kwa ajili ya Mungu? Ni nini nimetoa kwa ajili ya Mungu? Kanisa lilinitaka niondoke nyumbani kwangu kwa sababu ya ukandamizwaji na ukimbizwaji wa joka kubwa jekundu, ili nisiingie katika mifumbato yake na kupatwa na mateso yalo ya kikatili. Huu ulikuwa upendo mkubwa wa Mungu na ulinzi kwetu, lakini sikujua mazuri na mabaya, wala sikujali kuhusu nia za kweli za Mungu. Hata sikufikiria usalama wangu mwenyewe, nilifikiri tu kuhusu hamu yangu ya nyumba mpya ya matofali na raha za mwili. Sikuwa na nia ya kutii mpango wa Mungu—nilikuwa nimejaa uroho sana, na nilijali zaidi kuhusu fedha kuliko maisha yenyewe! Leo, sikuwa radhi kuiacha nyumba yangu nyuma hata kwa ajili ya usalama wangu. Kama nilipaswa kuyaacha maslahi yangu mwenyewe kama sadaka kwa Mungu, au kama nilipaswa kujitolea maisha yangu au kumwaga damu yangu kwa ajili ya kazi ya Mungu, mtu kama mimi—mtu wa akili duni, mwenye ubinafsi na wa kustahili dharau anayependa fedha kama maisha yenyewe—angewezaje kuwa radhi kutoa sadaka hii kwa ajili ya Mungu? Si ningekimbia tu muda mrefu kabla ya wakati huo? Nilijifikiria mara nyingi nikiongea kwa kujigamba, nikisema: Niko radhi kufuata mfano wa Petro na kuwa mtangulizi kwa kumpenda Mungu. Niko radhi kuacha kila kitu, kutumia kila kitu bila kuzingatia manufaa yangu binafsi, hasara yangu au faida. Ninataka tu kumridhisha Mungu. Lakini wakati nimekabiliwa na hali halisi, hapakuwa na sehemu yoyote yangu ambayo ilikuwa inamzingatia Mungu. Nilifikiri tu juu ya maslahi yangu mwenyewe ya mara moja, na kwa kweli nilijaribu kujadiliana na Mungu kwa ajili ya raha za mwili. Kisha, nikajiuliza: Inaweza kuwa kwamba huu ndio upendo ninaopaswa kuurudisha kwa Mungu? Mungu amesema: “Ukipenda, basi unajinyima bila kusononeka, unavumilia hali ngumu, na unaambatana na Mimi. Ungeacha vitu vyako vyote kwa sababu Yangu…. La sivyo, basi upendo wako si upendo hata kidogo, bali ni uongo na usaliti! Upendo wako ni upendo wa aina gani? Je, ni upendo wa kweli? Je, ni wa uongo? Umejinyima kiasi gani? Umejitolea kiasi gani? Je, Nimepata upendo kiasi gani kutoka kwako? Je, unajua? Moyo wenu umejaa maovu, usaliti na uongo” (“Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilikula kiapo mbele ya Mungu lakini sikukiheshimu. Si huku ni kujaribu kumhadaa Mungu, kumdanganya Yeye? Nilipofikiria jambo hilo, sikuweza kujizuia kunyenyekea mbele Yake na kuomba: "Ewe Mwenyezi Mungu, daima nilikuwa naamini kwamba nilikuwa tayari kuwa mwenyeji wa idadi yoyote ya ndugu wa kiume na wa kike bila kulalamika juu ya shida zozote, na kwamba haya yalikuwa ni maonyesho ya upendo wangu Kwako. Lakini ni sasa tu ambapo nimebaini ufunuo juu ya ukweli kwamba ninaouita upendo visivyofaa ulikuwa ni wa masharti na kwa kuchagua. Yote yalikuwa yakitegemezwa kwa kile nilichotaka, na niliyapata tu katika mazingira ya raha. Lakini Uliponihitaji kuvumilia shida za kimwili na kutia hatarini maslahi yangu mwenyewe, 'upendo wangu' ulipotea tu. Kutoka kwa hilo niliona kwamba kwa kweli sikukupenda Wewe na kwamba kabisa sikuwa nikitekeleza wajibu wangu kwa madeni yangu kwa ukweli na ilikuwa hata kidogo zaidi kuulipia Upendo wako, lakini ilikuwa ni kutumia gharama ndogo niliyolipa kwa kuibadilisha na baraka nyingi. Kwa hakika mimi ni mfuata upepo kabisa, mimi ni mtu mwenye ubinafsi na mwenye akili finyu wa kustahili dharau. Mimi sifai kabisa kuishi mbele Yako, na hata sifai zaidi kupokea kila kitu Unachotoa katika maisha yangu! Ewe Mungu, mimi siko tayari tena kukudanganya Wewe na kuasi dhidi Yako, ili kukuumiza Wewe. Niko tayari kuweka nadhiri yangu, kuweka kando faida yangu mwenyewe, na kutii mipango Yako na utaratibu Wako."
Baada ya hayo, niliweka nguvu zangu katika kuuza ile nyumba mpya, na nikanunua fleti ya vyumba viwili katika eneo geni. Ingawa haikulingana na nyumba yetu ya zamani, kulikuwa na simu na mfumo wa kupasha chumba joto, na usafiri ulikuwa wa kufaa. Niliifurahia sana, na tukaanza tena wajibu wetu wa kuwa wenyeji. Kufumba na kufumbua ilikuwa majira ya kuchipua ya mwaka wa 2004 na polisi wa Chama cha Kikomunisti mara nyingine tena walikuwa wanatushuku. Wakawatuma wapelelezi wawili waliojifanya kuwa wapiga ramli kupata habari fulani. Kwa sababu ya kupata nuru na uongozi kutoka kwa Mungu, tuliitambua hila yao, na tukitegemea hekima kutoka kwa Mungu, tuliwafukuza. Kanisa lilipoambiwa juu ya hili, wajibu wetu ulisitishwa. Walitufanya kutafuta kazi fulani ili kuyalinda mazingira yetu. Kutoka wakati huo kwendelea, tuliwasiliana na ndugu zetu wa kiume na wa kike kwa nadra sana. Miezi sita ilipita na hali ya mahali palepale ikawa yenye fadhaa zaidi. Siku moja tulipokea taarifa kwa ghafla kutoka kwa kanisa ikisema kwamba Yuda fulani alikuwa ametusaliti na kwamba tulihitaji kuhama kwa haraka iwezekanavyo ili kuepuka kuanguka mikononi mwa joka kubwa jekundu. Kama tumekabiliwa na utaratibu huu kutoka kwa nyumba ya Mungu, wakati huu nilichagua kutii, na chuki kwa joka kubwa jekundu ilizaliwa moyoni mwangu. Nilifikiria kuhusu siku za nyuma nilipokuwa nimesikia maneno ya joka kubwa jekundu yakitangaza: "Wananchi wana uhuru wa dini, na haki zao halali na maslahi yao yamelindwa," na nikaona makanisa yakijengwa kila mahali. Nililihusudu na kulipenda jambo hilo; nilihisi kuwa nilikuwa nimeshinda mioyo ya watu. Lakini leo, kama nimekabiliwa na ukweli, hatimaye kwa kweli niliona kwa dhahiri sura mbaya ya joka kubwa jekundu, nilitambua njama zake, na nilijua kuwa matangazo yake na vitendo vyake vya juujuu vyote vilikuwa uongo na udanganyifu, vyote kujifanya. Zote zilikuwa njia zenye kustahili dharau, hila chafu za kuwavuruga na kuwapofusha watu. Lilikuwa ovu na katili, janja na danganyifu, la kurudi nyuma, dhidi ya Mungu, na la kupinga maendeleo kabisa. Lilikuwa ni pepo ambalo liliwala watu na kuleta madhara kwao! Mungu mwenye mwili alikuja duniani ili kuuokoa uumbaji Wake, wanadamu. Hili lilikuwa jambo lililokuwa njema na sahihi; lilikuwa jambo kubwa sana, la furaha, lakini joka kubwa jekundu halingemruhusu Mungu miongoni mwa wanadamu, halingewaruhusu watu kumwabudu Mungu na kutembea njia sahihi katika maisha yao. Lilifanya kila kitu lilichoweza kumwinda Kristo kwa wayowayo, kwa ukatili liliwatesa wateule wa Mungu, na kujaribu kuivuruga na kuiangamiza kazi ya Mungu. Lilijaribu kumfukuza Mungu, kuwaangamiza wateule wa Mungu, na kuiangamiza kazi Yake katika siku za mwisho. Kwa kweli lilikuwa la kupinga maendeleo lisilovumilika na Mbinguni! Wakati huo huo maneno haya ya Mungu yalinijia tu akilini mwangu: “Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi! … Kwa nini kuweka kikwazo hicho kisichopenyeka katika kazi ya Mungu? Kwa nini utumie hila mbalimbali kuwadanganya watu wa Mungu? Uhuru wa kweli na haki na matakwa halali vipo wapi? Usawa uko wapi? Faraja iko wapi? Wema upo wapi? Kwa nini kutumia mbinu za hila kuwadanganya watu wa Mungu? Kwa nini kutumia nguvu kukandamiza ujio wa Mungu? Kwa nini asimruhusu Mungu kuzunguka katika dunia ambayo Ameiumba? Kwa nini kumbana Mungu hadi Anakosa sehemu ya kupumzisha kichwa Chake?” (“Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kupitia maneno Yake niliweza kuona kwa dhahiri sura mbaya ya joka kubwa jekundu, kuona kwa dhahiri ukweli wa upinzani wake na mateso ya Mungu pamoja na madhara yalo na vizuizi vya watu. Niliwaza kuhusu ni ndugu wangapi wa kiume na wa kike ambao, chini ya ukandamizaji na ukimbizaji walo, hawakuweza kurudi nyumbani na waliishi maisha ya wazururaji, ya wasio na makazi. Niliwaza kuhusu jinsi ndugu wengi wa kiume na wa kike walikuwa wamepitia uharibifu wa mateso yalo ya kinyama, jinsi ndugu wengi wa kiume na wa kike walikuwa wamefungwa gerezani kwa mashtaka ya uongo na kupita siku nyingi za giza, wakiishi maisha katika gereza la chini ya ardhi yasiyostahili mbwa au nguruwe, kwa sababu tu walimwamini Mungu na kutekeleza wajibu wao. Niliwaza pia kuhusu ni ndugu wangapi wa kiume na wa kike ambao hawakuwa na uhuru kamwe chini ya upelelezi walo; hawakuwa na njia ya kutekeleza wajibu wao na hawakuweza kuishi maisha ya kawaida kanisani. Leo, sisi kumwamini Mungu na kutoa ukarimu ilikuwa tu ni kutekeleza wajibu wetu kama viumbe. Tulikuwa tunatekeleza majukumu yetu, na kabisa hatukuwa tumevunja sheria au kanuni za joka kubwa jekundu, lakini bado tulikuwa wenye uelekeo wa shutuma na udhalimu usio na msingi. Tuliweza tu kujiondoa na kwenda mahali pengine tena ili kutimiza wajibu wetu. Licha ya haya, polisi hawakupumzika katika ukimbizaji wao kwetu, lakini kwa kweli walijificha kwa kujifanya wapiga ramli ili kutafuta habari, wakifikiri kuwa wangeweza kupata ushahidi wa kutunasia na kututesa. Joka kubwa jekundu kwa kweli ni bovu kupita kiasi, danganyifu, lenye kustahili dharau, na katili! Kwa kufikiria hilo, nilihisi uchungu mkubwa zaidi wa haki na nilikuwa na chuki kubwa kwa joka kubwa jekundu. Shukrani iwe kwa Mungu! Ilikuwa ni kazi na maneno ya Mungu ya vitendo yaliyoondoa kabisa barakoa za joka kubwa jekundu na kufichua kikamilifu ubaya wa unafiki walo na sura ya heshima. Hili hatimaye lilifungua macho yangu ambayo yalikuwa yamepofushwa. Roho yangu iliamshwa, na nikaona uwazi wa ukweli ambao joka kubwa jekundu hujengea jina lake kwa kuudanganya umma na ukweli wa udanganyifu walo na uharibifu. Kwa hiyo nilikuwa na ujasiri na azimio la kulitelekeza kabisa, kulikataa. Aidha, nikilinganishwa na uovu wenye kustahili dharau na uchafu wa giza wa joka kubwa jekundu, nilipata ufahamu hata mkubwa zaidi wa haki ya Mungu, utakatifu, mwanga, na wema. Niliona wokovu Wake mkuu na utunzaji wa sisi wanadamu waovu; niliona kwamba bila kujali jinsi mazingira yalivyokuwa makali, bila kujali ni aina gani ya upinzani na ukandamizaji uliokuwepo kutoka kwa joka kubwa jekundu, Mungu hajawahi kuuacha wokovu Wake kwetu. Yeye bado anavumilia mateso yote ili kufanya kazi Anayopaswa kufanya. Katika ulimwengu huu mchafu, muovu, tunaweza tu kumtegemea Mungu—Yeye ndiye upendo wetu mkuu mno na wokovu wetu mkuu mno ambako tuna shauku ya maisha ya kufuatilia ukweli, na kumfuata Kristo. Shukrani ziwe kwa Mungu kwa kuniandalia karamu ya aina hiyo ili kuila, kwamba katikati ya taabu ninaweza kupata utambuzi na ufahamu. Kuanzia sasa kwendelea, ninaapa kwa maisha yangu kwamba nitafanya sitisho kamili na joka kubwa jekundu. Nitakuwa adui walo wa jadi. Bila kujali ni namna gani lilo hunitesa au kunifuatilia, sitatishwa na udhalimu walo. Nitamfuata tu Mungu kwa karibu, kutegemea uongozi Wake, kupenya ukandamizaji wa nguvu zote za giza, na kutimiza wajibu wangu ili kufidia neema ya wokovu wa Mungu.
Kwa sababu ya hali zisizopendeza ambazo hazikuturuhusu kukaa huko kwa muda mrefu, tulikurupuka mara nyingine tena ili kuhamia sehemu nyingine geni. Baada ya kuwasili, dada mmoja kutoka kwa nyumba ya Mungu akasema kuwa hili lilikuwa eneo la wachache wa kabila la hapo na kwamba joka kubwa jekundu halikuwa kali sana hapo. Mazingira yalikubalika hasa. Lakini moyo wangu haukuhisi starehe. Nikajiwazia: huu sasa ndio utawala wa joka kubwa jekundu na ni kama kwamba mawingu meusi yanajongelea juu ya jiji. Halitaturuhusu tumwamini Mungu kwa amani. Kwa hakika, tulipokuwa huko kwa muda wa siku 20 tu, wapelelezi wa joka kubwa jekundu walifika nyumbani kwetu wakisingizia kukusanya ada ya usafi na kuanza kutafuta watu ndani na nje ya nyumba yetu, wakimwuliza mke wangu kwa ukali alikotoka, mahali ambako yake yalikuwa yamesajiliwa, na kwa nini alikuwa amekuja hapa. Mmoja wao akamwuliza kama mumewe alifanana jinsi fulani. Akasema "Ndiyo," na mara tu waliposikia hilo waliangaliana. Ni hapo tu mke wangu alipotambua kwamba walijua jinsi nilivyofanana bila ya kuuona uso wangu. Ni lazima ilikuwa ni Yuda ambaye alinisaliti, ambaye hata alikuwa amewaelezea mfano wangu. Baada ya kuondoka walienda nyumbani kwa majirani nyuma yetu tu. Ni hapo tu tulipofahamu kuwa majirani zetu walikuwa wakifanya kazi nao na walikuwa wakitufuatia. Mara moja tukaripoti hili kwa kanisa. Baada ya muda mfupi, dada mmoja kutoka kwa kanisa alituandikia barua iliyosema: "Polisi wa mahali hapo wamewasiliana na polisi kutoka makazi yenu ya kudumu. Wana nia ya kuwazuia wale wenu ambao mmesalitiwa. Wanataka kwanza kuchunguza hali kwa ziara zisizotangazwa ili kuwafahamu, na wakati utakapokuwa sawa watawakamata nyote. Hali yenu ni ya hatari, mnapaswa kurudi kwa makazi yenu ya kudumu ya Shandong na kujificha. Shikeni njia haraka—mapema iwezekanavyo—mkikawia huenda msiweze kuondoka!" Baada ya kuona barua hii, hatukuthubutu kuipuuza. Tuliamua kuondoka siku iliyofuata. Usiku huo, nilikuwa nikigaagaa na kupinduka na kamwe sikuweza kulala. Sikuwa tu na ghadhabu sana kwa mateso ya hasira ya joka kubwa jekundu, lakini pia nilihisi kuchanganyikiwa na kutofarijika juu ya njia iliyo mbele. Oo! Mwanzoni nilidhani kwamba kumwamini Mungu ilikuwa rahisi, kwamba yote niliyoyahitaji kufanya ni kumkubali Mungu kwa maneno yangu, kumwamini Yeye ndani ya moyo wangu, na kufanya yote iliyowezekana kutimiza wajibu wangu na ningepokea sifa za Mungu. Sikuwahi kufikiria kamwe kwamba njia hii ingekuwa ngumu zaidi jinsi nilivyozidi kuitembea. Nilipokuwa tu nahisi wasiwasi na kusikitika kwa sababu ya safari yangu ngumu ya kumwamini Mungu, maneno Yake yalinipatia nuru: “Watu hawachukulii imani kwa kwa kuwa kuamini Mungu ni jambo geni, jambo lisilo la kawaida sana kwao. Kwa njia hii, hawafikii mahitaji ya Mungu. Kwa maneno mengine, ikiwa watu hawamjui Mungu, hawajui kazi Yake, basi hawafai kwa matumizi na Mungu, na zaidi ya hayo hawawezi kutimiza hamu ya Mungu. 'Imani katika Mungu' inamaanisha kuamini kuwa kuna Mungu; hii ndiyo dhana rahisi zaidi ya imani katika Mungu. Zaidi ya hayo, kuamini kuwa kuna Mungu si sawa na kuamini katika Mungu kwa ukweli; bali, ni hali ya imani sahili ikiwa na vipengee vya uzito vya kidini. Imani ya kweli katika Mungu ina maana kupitia maneno na kazi ya Mungu kwa msingi wa imani kuwa Mungu ndiye mkuu juu ya vitu vyote. Kwa hivyo mtakuwa huru kutokana na tabia yenu ya upotovu, mtatimiza hamu ya Mungu, na mtapata kumjua Mungu. Ni kwa kupitia safari ya aina hii tu ndio mnaweza kusemekana kuwa mnaamini katika Mungu” (kutoka kwa Dibaji wa Neno Laonekana katika Mwili). Niliketi kimya, nikijaribu kuelewa maana ya maneno Yake. Ndani, kwa polepole nilichangamka: Ndio, ni kweli kwamba imani ya kweli katika Mungu inamaanisha kupata maneno na kazi Yake kwa kutegemeza imani kwamba Yeye ana ukuu juu ya vitu vyote, hivyo tunaweza kuachiliwa huru kutoka kwa tabia zetu potovu, tutimize shauku ya Mungu, na tuje kumjua. Ni kwa njia ya safari kama hiyo tu tunapoweza kusemwa kuwa tunamwamini Mungu. Bila shaka haikuwa rahisi kama nilivyoamini, kwamba nilihitaji tu kumkiri Yeye kwa maneno yangu, kwendelea kuwa na mikutano na wengine, kula na kunywa maneno ya Mungu, na kutimiza wajibu wangu. Aina hii ya imani yangu ilikuwa tu imani isiyo dhahiri ya kidini na haikuwa na asili ya imani katika Mungu. Hata kama ningefuata hadi mwisho, singeweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu, wala singeweza kupata sifa Zake. Nilimfikiria Petro; katika imani yake kwa Mungu, alisisitiza kulichukua neno la Mungu katika maisha yake ya kila siku ili kupata uzoefu wake. Bila kujali kilichotokea, alikuwa akitafuta kuyaridhisha mapenzi ya Mungu na matakwa Yake. Kama ilikuwa hukumu na kuadibu, majaribu na usafishwaji, au shida na mateso pamoja na nidhamu, daima aliweza kulikubali na kulitii. Kutoka hapo, alitafuta ukweli, akafuatilia elimu yake mwenyewe na elimu ya Mungu. Ukimbizaji wake wa miaka mingi haukusababisha tu mabadiliko katika tabia yake mwenyewe, lakini pia alikuja kuwa na maarifa zaidi juu ya Mungu kuliko mtu mwingine yeyote kwa enzi zote. Imani ya Petro ilikuwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu, na ilikuwa ndiyo ya juu kabisa. Lakini nilikuwa na mtazamo sahili mno juu ya kumwamini Mungu. Nilidhani kwamba nilihitaji tu kwendelea kuwa na mikutano na wengine, kula na kunywa maneno ya Mungu, na kutimiza wajibu wangu na ningeweza kupokea sifa Zake. Kuna tofauti gani kati ya mawazo yangu na ya wale wasioamini na watu wa dini? Mwishowe, si yote bado yangekuwa ni bure? Ni hapo tu nilipotambua kwamba miaka yangu yote ya kumwamini Mungu ilikuwa imejawa na mchafuko. Sikujua hata ni nini maana ya kumwamini Mungu. Kama haingekuwa ni ufunuo wa Mungu wa vitendo na uongozi na upataji nuru wa maneno Yake, ningekuwa bado nikimfuata Mungu huku nikiishi katika dhana zangu na mawazo yangu. Bado singekuwa nimeona kwamba mimi kwa hakika ni muumini wa dini ambaye hufuata tu njia yake mwenyewe. Sikuweza kujizuia kuhisi hofu kidogo wakati huo. Nilitambua kwamba kama ningeendelea na njia hii ya kuchanganyikiwa ya kumfuata Mungu bila kuzingatia kupata uzoefu wa kazi Yake, au kuzingatia kufuatilia ukweli au mabadiliko katika tabia, hatimaye bila shaka ningeangamizwa na Mungu. Nilipoona hali zangu zenye hatari, mara moja nilimwomba Mungu: "Ewe Mungu! Asante kwa ufunuo Wako na nuru Yako ambavyo vimenisaidia kuelewa ukweli na kutambua makosa katika imani yangu kwa Mungu. Ewe Mungu! Niko tayari kufuata mfano wa vitendo vya Petro, kufuatilia njia aliyoichukua. Kwa kuwa nimechagua njia hii sasa, niko tayari kwenda mbele kwa ujasiri bila kujali jinsi njia hii ilivyo danganyifu au ni hatari ngapi zilizojificha mbele yangu. Niko tayari kuwa na ridhaa ya kuteseka, kutii usanifu Wako na mipango, na kwa kweli kupitia maneno Yako na kufanya kazi kulingana na matakwa Yako kwangu ili niweze kuwa kiumbe Wako ambaye anakwamini Wewe kwa kweli na anayekuabudu Wewe." Nilihisi utulivu sana baada ya kuomba na nilikuwa na ujasiri wa kupata uzoefu wa kazi ya Mungu.
Siku iliyofuata, tulipanda garimoshi kwenda Shandong. Baada ya kujificha kwa muda katika makazi yetu ya kudumu ya Shandong pamoja na vipingamizi vichache, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, hatimaye tuliweza kuwasiliana na kanisa, na tulianza tena maisha yetu ya kanisa. Lakini joka kubwa jekundu halikuwa limelegea katika mateso yalo kwetu. Bila kujali ni wapi tulikwenda, daima tulikuwa na uelekeo wa masharti na vikwazo vyake. Polisi walikuja mara kwa mara kukagua vibali vya makazi—wakati mwingine wangekuja mara mbili kwa siku na kusisitiza kabisa kwamba tujisajili kwa vibali vya makazi vya muda mfupi, vinginevyo wangetufukuza. Hivyo, kuhama nyumba kukawa kitu cha kawaida kwetu. Baadaye, tulihamia katika fleti kubwa ya vyumba vingi ambamo mtoto wa kiume wa ndugu mmoja mzee kanisani alikodesha mahali, hivyo huyu ndugu alitukaribisha huko. Lakini huko sio tu kuwa tulihitaji kujiandikisha kwa kibali cha makazi cha muda mfupi, lakini tulihitajika kuwa na kibali cha kuingia na kutoka ama sivyo hatungeweza kuja na kwenda, sembuse kuweza kuingia. Ilibidi tujifiche ndani ya nyumba na hatukuweza kwenda nje. Hata hivyo, polisi bado hawakukata tamaa. Bado wao mara kwa mara waliingia nyumba hadi nyumba wakifanya ukaguzi. Kutoka kwa hili tuliona kuwa katika nchi hii ya udikteta, isiyo na dini iliyoongozwa na chama kikanamungu, imani katika Mungu ilikandamizwa na kudhulumiwa kila mara. Hili kwa hakika lilisababisha chuki ya kimya kimya. Hasa wakati wa Olimpiki ya mwaka wa 2008 hali ilikuwa yenye fadhaa sana, ya kuchukiza sana. Joka kubwa jekundu liliweka mitego na polisi walikuwa wakilinda kila mahali. Hata hivyo, ilikuwa katika hali hizi tulipoona ukuu wa Mungu, hekima, na matendo Yake ya ajabu, kwamba ilikuwa Mungu ndiye aliazimia kila kitu. Kila wakati maafisa walipotaka kufanya ukaguzi, kwa mpango wa Mungu mtu aliyelinda lango kuu angekuja kumwambia ndugu yetu mzee ili tuweze kujipanga haraka na kujificha mapema. Kulikuwa na wakati mmoja ambapo polisi walifanya ukaguzi wa ghafla wakati tulipokuwa katikati ya mkutano. Tulisikia mbwa nje wakibweka kama wazimu. Watu waliofanya uchunguzi walikuwa wameingia kwa nguvu ndani ya uga wakisingizia kuangalia mita za umeme; walikuwa wakizunguka kila mahali, wakiangalia kwa makini, wakitafuta, wakihoji, na wakimwogofya ndugu yetu mzee, ambaye alitumia hekima kutoka kwa Mungu kuwafanya waondoke. Sote tulihofia baada ya wao kuondoka. Kwa bahati sote tulikuwa tumejificha mapema—kama wangetupata ama kupata vitabu vya maneno ya Mungu, matokeo hayangefikirika. Wakati tu kulikuwa na hofu ikilimatia moyoni wangu, maneno haya ya Mungu yalivuma masikioni mwangu: "Usikubali udhibiti wa mtu yeyote, jambo au kitu; alimuradi linapatana na mapenzi Yangu basi lifanye kwa mujibu wa maneno Yangu. Usiogope, kwa kuwa mikono Yangu hukusaidia, na kwa hakika Nitakukinga dhidi ya watu wote wabaya" ("Tamko la Ishirini na Nane" katika Neno Laonekana katika Mwili). "Tenda kwa ujasiri! Kuwa na ujasiri na ujivunie! Usiogope—Mimi, baba yako, niko hapa kukusaidia na hutateseka; unahitaji tu kuomba na kusali zaidi mbele Yangu, na nitakukirimu ujasiri wote. Kutoka kwa nje, wale walio na mamlaka wanaonekana kuwa waovu, lakini huhitaji kuogopa—hiyo ni kwa sababu una imani kidogo. Alimuradi unaweza kujenga imani yako, hakuna kitu kitakachokuwa kigumu mno. Rukia kwa furaha hadi uridhikekwa kuridhika! Kila kitu ki chini ya miguu yako, na kila kitu ki ndani ya ufahamu Wangu. Yawe ni mafanikio au maangamizo, si yote ina uelekeo wa neno ndogo mno kutoka Kwangu?" ("Tamko la Sabini na Tano" katika Neno Laonekana katika Mwili). Niliona aibu baada ya kusoma maneno ya Mungu. Ulikuwa ni ukweli. Si watu wote, matukio, na mambo katika dunia hii ndani ya madhumuni na mipango ya Mungu? Si vyote pinduka, kufanyika upya, kubadilika, na kutoweka kulingana na mawazo Yake? Joka kubwa jekundu pia ni kiumbe katika mikono ya Mungu. Bila kujali jinsi lilivyo kali, haliwezi kuepuka utawala Wake. Akitaka kuliangamiza, si Yeye angesema neno moja tu? Mungu hajaliangamiza, lakini Ameliruhusu ukatili wake kwa muda. Hili ni kutupa imani na ujasiri, na ni kutuwezesha kujua hekima ya Mungu, kudura, na matendo ya ajabu kupitia uzoefu wetu. Pia ni kuturuhusu kutambua vizuri, asili ovu, ya kupinga maendeleo na vilevile sura mbaya ya joka kubwa jekundu katika ukandamizaji wake, ili tuweze kulichukia, kulikataa, kulisaliti, na kulilaani kwa dhati. Chini ya mwongozo na uongozi wa maneno ya Mungu, sio tu kuwa sikuwa mwepesi kutishwa na mwenye kuogofywa tena, lakini nilijaa shukrani kwa Mungu. Nilikuwa tayari kuwa mtiifu katika mazingira haya na kushindana na joka kubwa jekundu, kuyakubali mafunzo ya Mungu mwenyewe na ukamilifu, kutafuta kuelewa na kupata zaidi katika ukweli. Miezi michache iliyofuata, polisi wa mahali palepale wangefanya ziara za ghafla mara mbili au tatu kila mwezi, hivyo hatukuweza kujiandaa kwa ziara zao. Lakini ilikuwa ni chini ya hali hizi za kuogofya ambapo tuliweza kuepuka mtazamo wao mara kwa mara chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu. Kulikuwa na kuponea chupuchupu daima, na mambo daima yalikuwa sawa kwa shida. Baada ya uzoefu huu, sikuweza kujizuia kuhisi shukrani ya kweli na sifa kwa Mungu ndani ya moyo wangu. Niliwaza: "Ee Mwenyezi Mungu! Wewe kwa hakika ni Bwana wa ulimwengu anayesimamia vitu vyote. Matendo Yako ya ajabu yako kila mahali na kwa njia ya uzoefu wangu halisi sijapata tu ladha ya kudura Yako na hekima, lakini nimeona kwamba Wewe ni msaidizi wangu mkuu mno, Wewe ni kimbilio langu na nimeona kuwa joka kubwa jekundu si kitu ila tishio la bure tu. Unapoliangalia kutoka nje ni la vita vya kishenzi na dhalimu mno, lakini wakati linapokabiliwa na Wewe, ni dhaifu sana na halina nguvu—haliwezi kuhimili pigo moja. Linaweza tu kuzingatia kwa utiifu kazi Zako na usanifu Wako. Kwa kadri nina imani ninaweza kuzishinda nguvu zote za giza. Ewe Mungu! Ingawa sasa niko katika nchi hii iliyodhibitiwa na pepo, sitakuwa chini ya vikwazo vya mtu yeyote, tukio, au kitu. Nitainuka tu kutoka kwa ukandamizaji wa giza, nisimame kutoka mahali hapa pa uchafu ili kutenda kama ushahidi wa ushindi Wako."
Chini ya hali ya kuogofya ya kufuatiliwa na joka kubwa jekundu, nilikuwa na uzoefu mkubwa kwamba ni maneno ya Mwenyezi Mungu yakiniongoza kupitia majaribu baada ya majaribu, na kunisaidia kushinda mara kwa mara katika majaribio ya Shetani. Ilikuwa ni neema kubwa na ulinzi wa Mungu vilivyonileta hapa leo. Nifikiri nyuma juu ya barabara niliyoichukua, nimepitia ukandamizwaji na ukimbizwaji wa joka kubwa jekundu, nimeshindwa kurudi nyumbani na kuhamishwa, nimeishi maisha ya mzururaji, na sijakuwa na "kiota chenye joto" kama watu wa dunia hii walivyo wala sijaweza kuwa mchangamfu kama wao wala kuongoza maisha ya burudani. Na kwa sababu ya ukandamizwaji wa joka kubwa jekundu, moyo wangu umepata mateso makubwa na maumivu. Hata hivyo, kwa kuwa nimepitia hali hizi za uchungu, nimepata utajiri wa maisha ambao hakuna mtu kwa enzi zote amepata. Kwa kupitia udhalimu wa joka kubwa jekundu, nilitambua nafsi yangu mwenyewe ya ubinafsi na ya kustahili dharau. Niliona kwamba kwa hakika sikumwamini au kumpenda Mungu. Kupitia uzoefu wangu wa ukandamizaji kutoka kwa joka kubwa jekundu, nilitambua asili yake ya udanganyifu, ya kustahili dharau na ya uovu. Katika hali hiyo nilikuwa na ufahamu zaidi juu ya asili ya haki ya Mungu, uaminifu, mwanga, na wema. Kupitia uzoefu huo wa ukandamizaji na joka kubwa jekundu nilikuja kuitambua imani yangu isiyo dhahiri na isiyo ya hakika na nilielewa maana ya kweli na thamani ya kumwamini Mungu. Kupitia ukandamizaji huo nilipata ufahamu mkubwa zaidi wa hekima ya Mungu na ukuu na matendo Yake ya ajabu, na nikaelewa asili ya ukatili, ya uovu na ya kupinga maendeleo ya joka kubwa jekundu ambayo ina chuki kwa Mungu. Niliona kwa dhahiri jinsi linavyowapotosha watu, kuwadanganya, na kuwadhuru. Kutoka kwa hayo nilikuza chuki kubwa kwalo, na nilikuwa tayari kutegemea maneno ya Mungu ili kutupa tabia potovu ya Shetani, kuweza kulikataa kabisa joka kubwa jekundu, kuishi kama mtu halisi na kuuridhisha moyo wa Mungu. Ilikuwa kazi ya Mungu ya vitendo ambayo imeniruhusu binafsi kuonja karamu hiyo ya fahari ya maisha. Haikuamsha tu moyo wangu ambao ulikuwa umepofushwa kwa muda mrefu na joka kubwa jekundu, lakini iliniruhusu kupata utajiri mwingi mkubwa sana wa maisha, na kabla ya sijalijua nilikuwa nimeingia kwa njia sahihi ya kumwamini Mungu. Ninatoa shukrani za dhati na sifa kwa Mwenyezi Mungu!
Tanbihi:
a. foili: Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kivilinganisha.

kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
 Kujua zaidi: Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni