6/14/2018

Umeme wa Mashariki | Ambua Barakoa, na Uanze Maisha Upya

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu

Umeme wa Mashariki | Ambua Barakoa, na Uanze Maisha Upya

Chen Dan    Mkoa wa Hunan
Mwishoni mwa mwaka jana, kwa sababu sikuweza kuzindua kazi ya injili katika eneo langu, familia ya Mungu ilimhamisha ndugu mmoja wa kiume kutoka eneo jingine ili kuchukua kazi yangu. Kabla ya haya sikuwa nimearifiwa, bali nilisikia kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutoka kwa dada mmoja niliyekuwa mbia naye. Nilifadhaika sana. Nilishuku kwamba mtu aliyekuwa madarakani hakuwa ameniarifu kwa kuhofia kwamba singekubali kuiacha nafasi yangu na ningeshindana. Kwa sababu hiyo, nilikuwa na dhana mbaya ya dada aliyekuwa madarakani. Baadaye, dada huyo alikutana nami na kuniuliza juu ya jinsi nilivyohisi kuhusu kubadilishwa kwangu—mwanzoni nilitaka kuzungumza mawazo yangu, lakini nilihofia kwamba angepata picha mbaya kunihusu na kufikiri nilikuwa nikitafuta kazi kwake. Hivyo badala yake, kwa sauti legevu ilivyowezekana nilisema, "Sio shida, sikuweza kufanya kazi jenzi hivyo ni jambo la maana ningeweza kubadilishwa. Sina mawazo yoyote hasa juu ya jambo hilo, wajibu wowote familia ya Mungu itakaonipa kutimiza nitatii." Kwa njia hii nilificha nafsi yangu ya kweli huku nikionyesha masimulizi ya uongo juu yangu kwa huyo dada. Baadaye, nilitumwa na familia ya Mungu kuwa mfanyakazi. Katika mkutano wetu wa kwanza wa wafanyakazi wenza, kiongozi wetu mpya aliyehamishwa aliweka wazi hali yake. Msemo mmoja hasa ambao alitumia, "kupoteza umaarufu wote na sifa" ulinipiga kwa nguvu nyingi sana: Ilikuwa ni kana kwamba alikuwa anaongea juu yangu. Nilikuwa nimeketi hapo nikihisi kufadhaika na kuhuzunika—niliweza kuhisi machozi yakichemka machoni mwangu, lakini niliyaziba kabisa nikiogopa kwamba wengine wangeona. Nilitaka kujiweka wazi, lakini pia niliogopa kuwa wafanyakazi wenzangu wangenidunisha. Kuepuka aibu, nilificha tena hali yangu ya kweli, bila kuwaacha wengine kuona kiwango ambacho nilikuwa nimesafishwa tayari. Hata nililazimisha tabasamu kuonyesha kila mtu jinsi hali yangu ilivyokuwa ya kawaida. Hivyo tu, nilileta hali yangu hasi kazini, na licha ya ukweli kwamba sikuthubutu kuzembea na nilifanya kazi kila siku tangu mapambazuko hadi magharibi, ilionekana kuwa nilivyofanya kazi kwa bidii ndivyo nilivyozidi kukosa ufanisi na kila aina ya matatizo iliibuka. Kazi ya injili ilikuwa ikifikia kikomo cha polepole na mkurugenzi wa mstari wa kwanza na baadhi ya wanachama wake walikuwa wamekamatwa na polisi wa CCP. Nikiwa nimekabiliana na yote haya, nilihisi nilikuwa nakaribia kuzirai na nilifikiri tu juu ya kubadilishwa kwangu kulikokaribia. Hata hivyo, nilikataa kujiweka wazi, na kujifanya kuwa na nguvu na imara mbele ya ndugu zangu wa kiume na wa kike.
Siku moja wakati wa ukuzaji wa kiroho nilisikia kifungu kifuatacho kutoka kwa ushirika wa Kristo, “Wakati wanazungumza na ndugu zao, watu wengine wanahofia sana wao kugundua ugumu ndani ya mioyo yao. Wanaogopa kwamba ndugu watakuwa na kitu cha kusema kuwahusu ama kuwadharau. Wanapoongea, watu daima wanaweza kuhisi uchu wao, kwamba kwa kweli wanamtaka Mungu, na kweli wako makini kuweka ukweli katika vitendo lakini kwa kweli, katika mioyo yao wako dhaifu sana, na baridi kabisa. Wanajifanya kuwa wenye nguvu, na hakuna anayeweza kugundua. Huu pia ni udanganyifu. Kwa ujumla, bila kujali kile unachofanya—iwe katika maisha, kumtumikia Mungu, ama kutekeleza wajibu wako—ukionyesha uso usio wa kweli kwa watu na kuutumia kuwadanganya, kuwafanya kukuheshimu ama kutokudharau, basi unakuwa mdanganyifu!” (“Ili Kuwa Mwaminifu, Unapaswa Kujiweka Wazi kwa” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Baada ya kusikia kifungu hiki nilipigwa na bumbuazi kabisa. Hukumu ya Kristo ilinichapa hadi kwa kina cha asili yangu. Nilipopima vitendo vyangu mwenyewe dhidi ya maneno haya, ilionekana kuwa nilikuwa tu mtu mdanganyifu ambaye Mungu alimnenea, mnafiki wa kweli. Ili kumpa kiongozi na wafanyakazi wenzangu picha kwamba nilikuwa mtu ambaye alikuwa tayari kuachilia hadhi na kufuata mipango ambayo familia ya Mungu iliniandalia, nilijificha kwa uangalifu na kuufunika ukweli, nikisalimisha kazi ya familia ya Mungu na maisha ya ndugu wa kiume na wa kike bila kuwaza tena. Sikuwa tayari hata kidogo kuwafichulia jinsi hali yangu na mwenendo wangu vilivyokwisha kuwa hasi baada ya kubadilishwa, hivyo tangu niliponyang'anywa cheo changu cha uongozi na kupewa kazi kama mfanyakazi, nilijifanya kuwa imara na shupavu ingawa nilihisi hasi na dhaifu ndani. Nilikuwa nikiishi katika udanganyifu wa Shetani. Nilikuwa nikiishi katika kutokuelewana na usaliti kwa Mungu. Hata hivyo, nilikuwa bado siko tayari kujiweka wazi na kutafuta ukweli ili kutatua tabia yangu potovu. Jinsi nilivyokuwa mdanganyifu, jinsi nilivyojitia mwapuza! Hata hivyo, bila kujali jinsi nilivyojificha na kuficha hisia zangu za kweli vizuri, sikuweza kuutoroka uchunguzi wa Mungu. Roho Mtakatifu alitumia udhaifu wangu katika kazi kufichua kila kitu. Sikuwa tayari kwa vyoyote kuachilia hadhi yangu, lakini badala yake nilifanya kila lililowezekana ili kuepuka aibu na kuhifadhi hadhi yangu kwa kuonyesha picha ya uongo ili kuwachanganya na kuwakanganya ndugu zangu wa kiume na wa kike. Ningewezaje kutojua kwamba, kwa kufanya hivyo, sio tu kwamba ningejinasa, lakini pia ningesababisha madhara makubwa kwa kazi ya familia ya Mungu? Ni hatari iliyokuwaje kuichezea kazi ya familia ya Mungu na maisha yangu mwenyewe!
Wakati huu, sikuweza kuzuia kujiuliza: Kwa nini daima mimi huonyesha picha yangu ya uongo kwa wengine? Si ni kwa sababu asili yangu ya uongo huniamuru daima kuepuka aibu na kulinda hadhi yangu? Kupitia kupata nuru kwa Roho Mtakatifu, nilikuja kutambua jinsi sumu ya Shetani ilivyochoma ndani yangu. Misemo, “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake” na “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo" tayari ilikuwa imekita mizizi kwa kina sana katika roho yangu kiasi kwamba vitendo vyangu vyote vilikuwa vimeathiriwa sana na kupangwa nayo. Nilifikiria nyuma jinsi hili lilikuwa limedhihirika katika siku za nyuma: Ni mara ngapi nilikuwa nimetenda kinyume na kanuni ya ukweli katika kutimiza wajibu wangu, kuficha uhalisi wa hali ili kuepuka aibu na kwa hofu kwamba, kama ningetoa maoni yangu ya dhati, wengine wangenikosoa? Ni mara ngapi nilisababisha madhara makali kwa maisha yangu kwa sababu, licha ya kuwa na utambuzi wa huzuni kwamba hali yangu ilikuwa katika hali mbaya na kujua kwamba nilipaswa kujiweka wazi katika ushirikiano na wengine, nilichagua badala yake kuteseka kimya kimya badala ya kujieka wazi na kutafuta njia ya mwanga kwa hofu kwamba ningeangaliwa kwa dharau? Kimsingi, wakati wowote ambapo heshima yangu na sifa zilikuwa kwa hatari kubwa, ningejificha kwa udanganyifu na kuonyesha picha ya uwongo ili kumchanganya Mungu na kuwakanganya wengine. Hata Mungu alipotaka kuniokoa kwa njia ya ufunuo mwingi, asili yangu ya udanganyifu bado iliamuru nijenge picha ya uongo, nimhadae Mungu na kuwakanganya wengine. Ni vipi, kwa njia hii, Mungu angeweza kufanya kazi kupitia mimi? Kama ningeendelea kwa njia hii, ningekujaje kupata wokovu? Haya yote yangekosaje kusababisha ghadhabu ya Mungu? Kama nimeshikwa na woga, nilisujudia mbele ya Mungu: Mwenyezi Mungu, sistahili kusimama mbele Yako! Asili yangu ya udanganyifu imesababisha madhara makubwa kwa kazi ya familia ya Mungu, lakini Wewe hujanishughulikia kulingana na makosa yangu na hata Umenipa fursa ya kurekebisha. Siulizi, sasa, kwamba univumilie au kwamba wengine waniheshimu, nauliza tu kwamba kuadibu Kwako na hukumu vikae nami daima. Kupitia kuadibu Kwako na hukumu niruhusu nione tabia Yako ya haki na nipate ufahamu mkamilifu zaidi wa asili yangu ya udanganyifu, ili niweze kuacha kujificha kwangu na kuishi kwa uaminifu.
Baadaye, nilisoma kifungu kifuatacho cha maneno ya Mungu: “Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu mioyo yenu; kutomdanganya katu katika chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kufunika ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kutia mchanga wa macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinafanywa ili tu mweze kujipendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu. … Kama wewe unao siri nyingi usiotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye kwake wokovu hutaweza kupatikana na ambaye hataweza kuibuka kutoka kwa giza kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ndiwe unayeishi mara nyingi katika mwangaza” (“Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kutoka kwa maneno ya Mungu, niliona kwamba wale ambao hawataki kushirikiana siri zao na kuweka wazi matatizo yao ili kutafuta ukweli ni wadanganyifu. Kwa sababu Mungu huwachukia na kuwakirihi wadanganyifu, watu wasio na uaminifu hawana kazi ya Roho Mtakatifu ndani yao na bila kujali ni miaka mingapi wametenda imani katika Mungu, hawatapata kamwe wokovu Wake na hatimaye wataondoshwa. Kwa sababu ya kupata nuru ya neno la Mungu, niliweza kutambua kwamba sababu yangu kushindwa katika huduma kwa Mungu ni kutokana na asili yangu ya udanganyifu. Sikutaka kamwe kumpa Mungu moyo wangu, kujiweka wazi mbele ya Mungu au ndugu zangu wa kiume na wa kike ili kupokea kuadibu na hukumu za Mungu ili kujitakasa. Kutokana na hayo, nilikuwa nikiishi katika hali isiyofaa, nilikuwa nimepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na nilikuwa nimetumbukia katika giza. Kama ningekuwa nimewasiliana kwa karibu kuhusu hali yangu halisi wakati wa ushirika na dada aliyekuwa na madaraka, bila shaka angekuwa amewasiliana kwa karibu nami na hali yangu ingekuwa imeboreka mara moja. Kama ningekuwa nimejiweka wazi daima tu, uhusiano wangu na Mungu ungekuwa wa kawaida na singekuwa nimeficha dhuluma dhidi yake au kusababisha madhara makubwa jinsi hiyo kwa kazi ya familia ya Mungu. Ninamshukuru Mungu kwa kunifichulia tabia Yake ya haki. Kwa njia ya neno la Mungu nilifichuliwa na kuhukumiwa na hivyo nilikuja kutambua hali yangu ya udanganyifu na sababu ya msingi ya kushindwa kwangu. Ufunuo na hukumu ya Mungu pia vilinionyesha njia ya kutenda: Bila kujali ni matatizo mangapi yanayonikabili, au uhafifu wa hali yangu, ni kwa kujiweka wazi tu na kutumia ukweli kufikia utatuzi na kulifuata neno la Mungu nitakapopata kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwa kufumua tu kujificha kwangu na kutenda kwa uaminifu nitakapopata wokovu wa Mungu.
Katika maneno ya Mungu nilipata tumaini na moyo wangu ulisisimuliwa kwa kina. Ingawa vitendo vyangu vilikuwa vyenye kumuumiza Mungu kwa kina, Yeye hakuniacha kamwe, lakini daima alikuwepo kwa utulivu Akifanya wokovu Wake. Nyuma ya kile kilichoonekana kama kuadibu na hukumu bila huruma, nadhari ya Mungu yenye ari iko wazi kabisa. Kwa hakika nilipitia kile kinachomaanishwa na, "upendo mkubwa kama ule unavyoonyeshwa katika uongozi wa baba kwa mwanawe." Asili ya Mungu haiko tu katika uaminifu, bali pia katika urembo na uzuri. Yote Anayotangaza ni ukweli na yanapaswa kuthaminiwa na wanadamu wote, kwa sababu hakuna mwanachama wa wanadamu wapotovu aliye na asili hii ya Mungu. Ijapokuwa asili yangu ya kweli ni ya udanganyifu na ya kustahili dharau na kila kitu ambacho nimefanya kimekwenda kinyume na ukweli, naapa kurudi kwa Mungu na kufanya kila liwezekanalo ili kutafuta ukweli, kutafuta mabadiliko katika tabia yangu na kamwe kutojificha kwa sababu ya kulinda hadhi yangu isiyo na thamani na heshima. Katika siku zijazo, bila kujali ni matatizo ya aina gani au mazingira mabaya ninayokabiliana nayo, ninaapa kujiweka wazi na wengine katika kutafuta ukweli na kuishi kwa uaminifu ili kuufariji moyo wa Mungu!

kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

     Kujua zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni