Sasa mko kwenye hatua ya mwisho ya njia, na hii ni sehemu muhimu. Labda umevumilia mateso mengi kabisa, umefanya kazi nyingi, umetembea barabara nyingi, na umesikiliza mahubiri mengi, na haijakuwa rahisi kufika hadi sasa. Ikiwa huwezi kuvumilia mateso yaliyo mbele yako na kama unaendelea kama ulivyofanya zamani, basi huwezi kufanywa mkamilifu. Hii si ili kukutisha—huu ni ukweli. Baada ya Petro kupitia kazi ya Mungu kiasi fulani, alipata umaizi na ufahamu mwingi.
Pia alielewa kiasi fulani cha kanuni ya huduma, na baadaye aliweza kujitolea kikamilifu kwa kile ambacho Yesu alimwaminia. Usafishaji mkubwa alioupokea mara nyingi ulikuwa kwa sababu katika mambo aliyoyafanya, alihisi kwamba alikuwa na deni kubwa kwa Mungu na kwamba hangeweza kamwe kumfidia, na aligundua kuwa wanadamu wamepotoka sana, kwa hivyo alikuwa na dhamiri yenye hatia. Yesu alikuwa amemwambia mambo mengi na wakati huo alikuwa na ufahamu mdogo tu. Wakati mwingine bado alikuwa na upinzani na uasi. Baada ya Yesu kutundikwa msalabani, hatimaye alizinduka kidogo na alihisi hatia kubwa. Hatimaye ilifikia hatua ambapo alikuwa na hasira wakati ambapo alikuwa na wazo ambalo halikuwa sahihi. Alijua hali yake mwenyewe vizuri sana, na pia alijua vizuri utakatifu wa Bwana. Matokeo yake, moyo wa upendo kwa Bwana ulikua ndani yake hata zaidi, na alilenga katika maisha yake zaidi. Kwa sababu hiyo alipitia dhiki kubwa, na ingawa wakati mwingine ilikuwa kama kwamba alikuwa na ugonjwa mkubwa na hata alionekana kuchungulia kaburi, baada ya kusafishwa kwa njia hii mara nyingi, alikuwa na ufahamu zaidi wa nafsi yake, na kwa njia hii tu ndipo alipata upendo wa kweli kwa Bwana. Inaweza kusemwa kuwa maisha yake yote yaliishiwa katika usafishaji, na hata zaidi, yaliiishiwa katika kuadibiwa. Uzoefu wake ulikuwa tofauti na wa mtu mwingine yeyote, na upendo wake ulizidi ule wa mtu yeyote ambaye hajakamilishwa. Sababu yake kuchaguliwa kama mfano ni kwamba alipata uchungu zaidi maishani mwake na uzoefu wake ulifanikiwa zaidi. Ikiwa kweli mnaweza kutembea hatua ya mwisho ya njia kama vile Petro, basi hakuna kiumbe hata mmoja ambaye anaweza kuchukua baraka zenu.
Pia alielewa kiasi fulani cha kanuni ya huduma, na baadaye aliweza kujitolea kikamilifu kwa kile ambacho Yesu alimwaminia. Usafishaji mkubwa alioupokea mara nyingi ulikuwa kwa sababu katika mambo aliyoyafanya, alihisi kwamba alikuwa na deni kubwa kwa Mungu na kwamba hangeweza kamwe kumfidia, na aligundua kuwa wanadamu wamepotoka sana, kwa hivyo alikuwa na dhamiri yenye hatia. Yesu alikuwa amemwambia mambo mengi na wakati huo alikuwa na ufahamu mdogo tu. Wakati mwingine bado alikuwa na upinzani na uasi. Baada ya Yesu kutundikwa msalabani, hatimaye alizinduka kidogo na alihisi hatia kubwa. Hatimaye ilifikia hatua ambapo alikuwa na hasira wakati ambapo alikuwa na wazo ambalo halikuwa sahihi. Alijua hali yake mwenyewe vizuri sana, na pia alijua vizuri utakatifu wa Bwana. Matokeo yake, moyo wa upendo kwa Bwana ulikua ndani yake hata zaidi, na alilenga katika maisha yake zaidi. Kwa sababu hiyo alipitia dhiki kubwa, na ingawa wakati mwingine ilikuwa kama kwamba alikuwa na ugonjwa mkubwa na hata alionekana kuchungulia kaburi, baada ya kusafishwa kwa njia hii mara nyingi, alikuwa na ufahamu zaidi wa nafsi yake, na kwa njia hii tu ndipo alipata upendo wa kweli kwa Bwana. Inaweza kusemwa kuwa maisha yake yote yaliishiwa katika usafishaji, na hata zaidi, yaliiishiwa katika kuadibiwa. Uzoefu wake ulikuwa tofauti na wa mtu mwingine yeyote, na upendo wake ulizidi ule wa mtu yeyote ambaye hajakamilishwa. Sababu yake kuchaguliwa kama mfano ni kwamba alipata uchungu zaidi maishani mwake na uzoefu wake ulifanikiwa zaidi. Ikiwa kweli mnaweza kutembea hatua ya mwisho ya njia kama vile Petro, basi hakuna kiumbe hata mmoja ambaye anaweza kuchukua baraka zenu.
Petro alikuwa mtu mwenye dhamiri—alikuwa wa aina hiyo ya ubinadamu. Alipokuwa akimfuata Yesu mara ya kwanza, hakuwa na budi ila kuwa na mawazo mengi ya upinzani na uasi. Lakini wakati alipokuwa akimfuata Yesu hakuyachukulia mambo haya kwa uzito, na aliamini kuwa watu wanapaswa kuwa hivyo, na kwa hivyo mwanzoni hakuhisi na hatia yoyote, wala hakushughulikiwa. Yesu hakuwa makini juu ya mjibizo aliokuwa nao, wala Hakuyafikiria. Aliendelea tu na kazi Aliyopaswa kufanya. Hakuwahi kubagua Petro au ndugu zake. Unaweza kusema: "Inawezekana kwamba Yesu hakujua kuhusu mawazo haya waliyoyaonyesha?" La hasha! Ilikuwa kwa sababu Yeye alimfahamu Petro kweli—inaweza kusemwa kwamba Alikuwa na ufahamu mkubwa juu yake—hivi kwamba Hakuchukua hatua yoyote dhidi ya Petro. Aliwachukia wanadamu lakini pia Aliwahurumia. Je, si kuna watu wengi kati yenu sasa ambao wana upinzani kama vile Paulo, na walio na mawazo mengi kama vile Petro alivyokuwa nayo kwa Bwana Yesu wakati huo? Ninawaambieni, ingekuwa bora zaidi kwenu kutoamini sana katika hisia zenu za tatu. Kuhisi kwako hakuaminiki na kuliharibiwa kabisa na upotovu wa Shetani muda mrefu uliopita. Je, unadhani kuhisi kwako kuko kamili kabisa? Paulo alimpinga Bwana Yesu mara nyingi lakini Yesu hakuwa na majibu yoyote. Je, inawezekana kwamba Yesu alikuwa na uwezo wa kutibu wagonjwa na kuwatoa pepo, lakini hakuweza kumfukuza "pepo" ndani ya Paulo? Kwa nini baada tu ya Yesu kufufuliwa na kupaa mbinguni, wakati huo huo Paulo aliendelea kuwakamata wanafunzi wa Yesu bila sababu, ndipo hatimaye Yesu alimtokea njiani kwenda Dameski, na kumwandama? Inaweza kuwa kwamba Bwana Yesu alionyesha hisia polepole sana? Au je, ilikuwa kwa sababu Hakuwa na mamlaka yoyote katika mwili? Je, unafikiri kwamba unapokuwa mharibifu na mpinzani sirini, Sijui? Je, unadhani kuwa makombo ya nuru ya Roho Mtakatifu ambayo unayo inaweza kutumiwa kunipinga Mimi? Petro alipokua mchanga, alipata mawazo mengi kwa Yesu, kwa nini hakuwa na hatia? Hivi sasa, watu wengi wanafanya mambo bila lawama, na hata wanapoambiwa wazi kwamba kufanya hivyo sio sahihi, hawasikilizi. Je, si hii kabisa ni kwa sababu ya uasi wa mwanadamu? Nimesema mengi sasa, lakini bado unakosa hata chembe ya utambuzi wa dhamiri, kwa hivyo utawezaje kuwa na uwezo wa kutembea hatua ya mwisho ya njia hadi mwisho wake? Je, huhisi kwamba hili ni suala kubwa sana?
Baada ya watu kushindwa wanaweza kutii mpango wa Mungu; wanaweza kutegemea imani yao na mapenzi yao kumpenda Mungu kumfuata. Kwa hivyo, hatua ya mwisho ya njia inaweza kutembewa vipi? Katika siku zako za kupitia shida unapaswa kuvumilia shida zote, na lazima uwe tayari kuteseka; ni katika njia hii tu ndiyo unaweza kuchukua hatua hii ya njia vizuri. Je, unafikiri kuwa ni rahisi kuchukua hatua hii ya njia? Mnapaswa kujua kazi ambayo mnapaswa kutimiza, lazima muongeze ubora wenu wa tabia na kujizatiti kwa ukweli wa kutosha. Hii sio kazi ya siku moja au mbili—si rahisi kama unavyofikiri! Kuitembea hatua ya mwisho ya njia inategemea aina ya imani na ambayo utakuwa nayo kweli. Labda huwezi kuona Roho Mtakatifu akifanya kazi ndani yako, au labda huna uwezo wa kugundua kazi ya Roho Mtakatifu kanisani, kwa hivyo unakuwa bila rajua na unavunjika moyo, na unajaa kukata tamaa katika njia iliyo mbele. Hasa, hao waliokuwa wapiganaji wa zamani wote wameanguka—je, si haya yote ni pigo kwako? Unapaswa kuona vipi mambo haya? Je, una imani au la? Je, unaelewa kikamilifu kazi ya leo, au la? Mambo haya yanaweza kuamua kama una uwezo wa kutembea hatua ya mwisho ya njia vizuri.
Kwa nini inasemekana kwamba sasa mko kwenye hatua ya mwisho ya njia? Ni kwa sababu mnaelewa kila kitu mnachopaswa kuelewa, na Nimewaambia kila kitu ambacho watu wanapaswa kufanikisha. Nimewaambia pia kuhusu kila kitu mlichoaminiwa nacho. Kwa hivyo, mnayotembea sasa ni sehemu ya mwisho ya njia inayoongozwa na Mimi. Ninahitaji tu kuwa muwe na uwezo wa kuishi kwa kujitegemea, kwamba bila kujali ni lini utakuwa na barabara ya kuchukua, uongeze ubora wa tabia yako kama kawaida, uyasome maneno ya Mungu vizuri, na uwe na maisha ya kibinadamu yanayostahili. Sasa Ninakuongoza uishi kwa njia hii, lakini siku zijazo Sitafanya hivyo tena. Je, utaweza bado kuishi hivi? Je, utaweza kuendelea? Huu ndio ulikuwa uzoefu wa Petro. Yesu alipokuwa akimwongoza, hakuwa na ufahamu; alikuwa daima asiyejali kama mtoto, na hakutilia maanani mambo aliyoyafanya. Baada tu ya Yesu kuondoka ndipo alianza maisha yake ya kibinadamu yaliyofaa. Maisha yake yenye maana yalianza tu baada ya Yesu kuondoka. Ingawa yeye alikuwa na urazini fulani wa kawaida wa mwanadamu na kile ambacho mtu wa kawaida anapaswa kuwa nacho, uzoefu wake wa kweli na matendo ulianza tu upya Yesu alipoondoka. Je, mambo yako vipi kwenu wakati huu? Sasa Ninawaongoza kwa njia hii na mnafikiri kuwa ni nzuri. Hakuna mazingira na majaribio ambayo hukufikia, lakini kwa njia hii hakuna njia ya kuona aina ya kimo ulicho nacho hasa, wala hakuna njia yoyote ya kuona kama kweli wewe ni mtu anayefuatilia ukweli. Unasema kwa mdomo wako kwamba unaelewa kiini chako mwenyewe, lakini haya ni maneno matupu. Baadaye, wakati ukweli unakujia, wakati huo tu ndipo ufahamu wako utathibitishwa. Hata ingawa sasa una aina hii ya ufahamu: “Ninaelewa kwamba mwili wangu umepotoka sana, na asili ya mwili wa watu ni kumwasi na kumpinga Mungu. Kuwa na uwezo wa kupokea hukumu ya Mungu na kuadibiwa yote ni kuinuliwa Naye. Nimeelewa hayo sasa, na niko tayari kuulipiza upendo wa Mungu”, ambayo ni rahisi kusema, baadaye wakati dhiki, majaribio, na mateso vitakapokujia, haitakuwa rahisi kuvipitia. Mnafuata njia hii kila siku, lakini bado hamwezi kuendelea na uzoefu wenu. Ingekuwa vibaya hata zaidi kama Ningewaachilia na Nisipowatilia maanani; watu wengi wataanguka chini na kuwa nguzo ya chumvi, ishara ya aibu. Haya yote yanawezekana sana. Je, huna mahangaiko au wasiwasi kuhusu hili? Petro alipitia aina hiyo ya mazingira na uzoefu wa aina hiyo ya mateso, lakini bado alisimama imara. Kama mazingira hayo yangeletwa kwako, je, ungeweza kusimama imara? Mambo ambayo Yesu alisema na kazi Aliyofanya wakati Alipokuwa duniani vilimpa Petro msingi, na ilikuwa katika msingi huu ndipo alitembea njia yake ya baadaye. Je, mnaweza kufikia kiwango hicho? Njia ambazo umetembea awali na ukweli ulioelewa—je, zinaweza kuwa msingi wako wa kusimama imara katika siku zijazo? Je, zinaweza kuwa maono yako ya kusimama imara baadaye? Nitawaambia ukweli—mtu anaweza kusema kwamba kile watu wanachokielewa sasa yote ni mafundisho ya dini. Hii ni kwa sababu kile wanachokielewa siyo mambo yote ambayo wameyapitia. Kwamba umeweza kuendelea mpaka sasa ni kwa sababu ya uongozi wa mwanga mpya. Sio kwamba kimo chako kimefikia kiwango fulani, lakini imekuwa ni maneno Yangu ambayo yamekuongoza hadi leo; sio kwamba una imani kubwa, lakini kwa sababu ya hekima ya maneno Yangu, hukuwa na budi ila kunifuata mpaka sasa. Ikiwa singezungumza sasa, Singetoa sauti Yangu, hungeweza kusonga na ungeacha kwenda mbele mara moja. Je, hiki sio kimo chenu halisi? Hamjui mtaingia ndani kutoka kwa vipengele gani na katika vipengele gani kufidia kile mnachokosa. Hamna ufahamu jinsi ya kuishi maisha ya kibinadamu yenye maana, jinsi ya kulipiza upendo wa Mungu, au kuwa na ushuhuda wenye nguvu na mkubwa sana. Hamwezi kufikia mambo haya kabisa! Ninyi ni wavivu na wajinga! Yote mnayoweza kufanya ni kuegemea kwa kitu kingine, na kile mnachotegemea ni mwanga mpya, na Yule aliye mbele akiwaongoza. Kwamba umeweza kuendelea mpaka leo imetegemea kabisa nuru mpya na matamko ya hivi karibuni. Ninyi sio kama Petro, ambaye alikuwa stadi wa kufuatilia njia ya kweli, au kama Ayubu, ambaye aliweza kumwabudu Yehova kwa uaminifu na kuamini kwamba Yeye alikuwa Mungu bila kujali jinsi Yehova alivyomjaribu, na kama Alimbariki au la. Je, unaweza kufanya hivyo? Umeshindwaje? Kipengele kimoja ni hukumu, kuadibiwa, na laana, na kipengele kingine ni mafumbo ambayo yanakushinda. Ninyi nyote ni kama punda. Ikiwa Ninachosema sio cha kifahari vya kutosha, ikiwa hakuna mafumbo yoyote, basi hamwezi kushindwa. Ikiwa angekuwa ni mtu anayehubiri na daima alihubiri kuhusu vitu vile vile kwa muda, ingechukua chini ya muda wa miaka miwili kwa ninyi nyote kukimbia, na msingeweza kuendelea. Hamjui jinsi ya kwenda ndani zaidi, wala hamwelewi jinsi ya kufuata ukweli au njia ya uzima. Yote mnayoelewa ni kupokea kitu ambacho ni riwaya, kama vile kusikiliza mafumbo au maono, au kusikiliza jinsi Mungu alivyokuwa akifanya kazi, au kusikiliza uzoefu wa Petro, au historia ya kusulubiwa kwa Yesu ... Mko tayari kusikiliza mambo haya tu, na kadiri mnavyozidi kuyasikiliza ndivyo manavyozidi kupata nguvu. Mnayasikiliza haya yote ili kuondoa huzuni zenu na uchoshi! Maisha yenu yanahimiliwa kabisa na mambo haya ya riwaya. Je, mnafikiri kwamba mmefika hapa leo kwa ajili ya imani yenu wenyewe? Je, hivi si vimo vidogo, vya kusikitisha ambavyo mnavyo? Uaminifu wenu u wapi? Ubinadamu wenu uko wapi? Je, mna uhai wa binadamu? Je, ni vipengele vingapi ambavyo mnavyo kwa ajili ya kufanywa wakamilifu? Je, Ninavyosema si ukweli? Ninazungumza na kufanya kazi kwa njia hii lakini bado hamwezi kutilia maanani. Wakati mnapofuata, pia mnatazama. Daima mnaendelea kuonekana kutojali, na daima mnaongozwa kwa kushurtishwa. Hivi ndivyo nyote mmendelea. Imekuwa kabisa kuadibiwa, usafisho, na kurudi ambavyo vimewaongoza hadi leo. Laiti mahubiri fulani juu ya uingiaji wa maisha yangehubiriwa, je, si nyote mngeteleza zamani? Kila mmoja wenu ni mwenye majivuno zaidi kuliko wa pili; kwa kweli, mmejaa chuki pekee! Umeelewa baadhi ya mafumbo, na umeelewa mambo ambayo watu hawajapata kuelewa hapo awali, kwa hivyo umefikia hata sasa kwa shida. Hamna sababu ya kutofuata, kwa hivyo mmefanya tu kujidhibiti na kwenda pamoja na mtiririko. Hii ni matokeo tu ambayo yamepatikana kwa njia ya maneno Yangu, lakini hakika sio si kwa uwezo wenu wenyewe. Huna kitu cha kujisifu kuhusu. Kwa hivyo, katika hatua hii ya kazi umesababishwa kwa siku ya sasa kwa njia ya maneno. Vinginevyo, ni nani kati ya watu hawa ambaye angeweza kutii? Nani angeweza kufika hadi leo? Kuanzia mwanzoni mlitaka kuondoka kwa nafasi ya kwanza ipatikanayo, lakini hamkuthubutu; hamkuwa na ujasiri. Hadi leo, mmekuwa mkifuata shingo upande.
Ilikuwa tu baada ya Yesu kutundikwa msalabani na kuondoka ndipo Petro alianza kwenda mwendo wake mwenyewe, akaanza kutembea njia ambayo ilimpasa; alianza kujiandaa tu baada ya kuona mapungufu yake na kasoro zake. Aliona kwamba alikuwa na upendo mdogo mno na radhi yake ya kuteseka hayakuwa ya kutosha, kwamba hakuwa na umaizi wowote, na kwamba urazini wake ulikosa. Aliona kwamba kulikuwa na vitu vingi ndani yake ambavyo havikukubaliana na mapenzi ya Yesu, na kwamba kulikuwa na vitu vingi ambavyo viliasi na kupinga na vingi vilivyochanganyika na mapenzi ya kibinadamu. Ilikuwa tu baada ya hapo ndiyo alipata kuingia katika kila kipengele. Yesu alipokuwa akimwongoza, Alifunua hali yake na Petro aliikubali na kutoa ahadi, lakini hakuwa na ufahamu wa kweli hadi baada ya hapo. Hiyo ilikuwa kwa sababu wakati huo, hakuwa na uzoefu wowote, na hakujua kimo chake mwenyewe kabisa. Hiyo ni kusema, sasa Ninatumia maneno ili kuwaongoza, na haiwezekani kuwafanya wakamilifu kwa muda mfupi, na mtaweza tu kuelewa na kujua ukweli. Hii ni kwa sababu kuwashinda na kuwafanya muamini mioyoni mwenu ndiyo kazi ya sasa, na baada tu ya watu kushindwa ndipo baadhi yao watafanywa kuwa wakamilifu. Sasa hivi maono hayo na ukweli huo unaoelewa vinajenga msingi wa uzoefu wako wa baadaye; katika dhiki ya baadaye nyote mtapata uzoefu wa vitendo wa maneno haya. Baadaye, wakati majaribio yanakujia na unakabiliwa na dhiki, utafikiria maneno unayosema leo: Bila kujali shida, majaribio, au maumivu makubwa ninayokutana nayo, ni lazima nimkidhi Mungu. Fikiria juu ya uzoefu wa Petro, na fikiria juu ya ule wa Ayubu—utaamshwa na maneno ya leo. Ni kwa njia hii tu ndiyo imani yako itatiwa nguvu. Wakati huo, Petro alisema kuwa hakustahili kupokea hukumu wala kuadibiwa na Mungu, na wakati huo pia utakuwa radhi watu wote waone tabia ya haki ya Mungu kupitia kwako. Utakuwa tayari kukubali hukumu Yake na kuadibu, na hukumu Yake, kuadibu, na laana vitakuwa faraja kwako. Hivi sasa, huwezi tu kujiandaa kwa ukweli. Licha ya kuwa utashindwa kusimama imara katika siku zijazo, pia huenda usiwe na uwezo wa kupitia kazi ya sasa. Kwa njia hii, je, si utakuwa kitu cha kuondolewa na kuadibiwa? Hivi sasa hakujakuwa na ukweli wowote uliokujia, na Nimekupa katika vipengele ambavyo unakosa; Ninasema kutoka kila kipengele. Hakika hamjavumilia mateso mengi; mnachukua tu kinachopatikana, hamjalipa aina yoyote ya gharama, na hata zaidi hamna uzoefu wenu halisi na utambuzi. Kwa hiyo, mnayoelewa sio vimo vyenu vya kweli. Mna mipaka katika kuelewa, maarifa, na kuona, lakini hamjavuna mavuno mengi. Ikiwa Sikuwatilia maanani lakini kuwaruhusu kuwa na uzoefu katika nyumba zenu wenyewe, mngekuwa mmetoroka tena kwenye ulimwengu mkuu zamani. Njia ambayo mtataitembea siku zijazo itakuwa ya mateso, na ukitembea hatua ya sasa ya mwisho wa njia vizuri, utakapopatwa na dhiki kuu baadaye, utakuwa na ushuhuda. Unaelewa umuhimu wa maisha ya kibinadamu, na wewe uko kwenye njia sahihi ya maisha ya kibinadamu, na katika siku zijazo, bila kujali jinsi Mungu anavyokutendea, utatii miundo Yake bila malalamiko yoyote au chaguo, na hutakuwa na matakwa kwa Mungu. Kwa njia hii, utakuwa na thamani. Hivi sasa hujapitia taabu, hivyo unaweza kutii chochote. Unasema kwamba vyvovyote akuongozavyo Mungu ni vizuri, na kwamba utatii miundo Yake yote! Mungu akikulaani au kukuadibu, utakuwa tayari kumkidhi. Baada ya kusema hivyo, unachosema sasa hakileti taswira ya kimo chako. Unachotaka kufanya sasa hakiwezi kuonyesha kwamba una uwezo wa kufuata mpaka mwisho. Dhiki kuu zitakapokujia au unapopatwa na mateso au kulazimishwa, au majaribio makubwa, hutaweza kuyasema maneno hayo. Ikiwa unaweza kuwa na ufahamu wa aina hiyo kisha usimame imara, hiki tu ndicho kitakuwa kimo chako. Petro alikuwa vipi wakati huo? Alisema: “Bwana, nitatoa maisha yangu kuwa kafara kwa ajili Yako. Ikiwa ungependa nife, nitafa!” Hivyo ndivyo alivyoomba wakati huo pia, na pia alisema: "Hata kama wengine hawakupendi, lazima nikupende mpaka mwisho. Nitakufuata wakati wote.” Hivyo ndivyo alivyosema wakati huo, lakini mara tu majaribio yalipomjia, akaanguka na kulia. Nyote mnajua kwamba Petro alimkana Bwana mara tatu, siyo? Kuna watu wengi ambao watalia na kuonyesha udhaifu wa wanadamu wakati ambapo majaribio yatawajia. Wewe si bwana wako mwenyewe. Katika hili, huwezi kujidhibiti. Labda leo unafanya vizuri sana, lakini ni kwa sababu una mazingira mazuri. Ikiwa hilo lingebadilika kesho, ungeonyesha woga wako na kutoweza kwako, na ungeonyesha pia ungeleta hizaya na kutostahili kwako. "Ujasiri" wako ungekuwa umeshuka muda mrefu uliopita, na wakati mwingine hata ungeshindwa na kutelekeza. Hii inaonyesha kwamba kile ulichokielewa wakati huo sio kimo chako halisi. Mtu lazima aangalie kimo halisi cha mtu ili aone kama anampenda Mungu kweli, kama anaweza kutii mpango wa Mungu, na kama wanaweza kutia nguvu zao zote katika kufikia kile ambacho Mungu anataka na kusalia kujitoa kwa Mungu na kutoa kile kilicho bora zaidi kwa Mungu, hata ikiwa inamaanisha kutoa maisha yao wenyewe.
Lazima ukumbuke kwamba maneno haya yamezungumzwa sasa: Baadaye, utapata shida kubwa na mateso makubwa! Kufanywa mkamilifu sio kawaida au rahisi. Kwa kiwango kidogo sana lazima uwe na imani ya Ayubu au labda hata imani kubwa kuliko yake. Unapaswa kujua kwamba majaribio haya yatakuwa makubwa kuliko majaribio ya Ayubu, na kwamba bado unapaswa kupitia kuadibiwa kwa muda mrefu. Je, hili ni jambo rahisi? Ikiwa ubora wa tabia yako hauwezi kuboreshwa, uwezo wako wa kuelewa umepungukiwa, na unajua kidogo sana, basi wakati huo hutakuwa na ushuhuda wowote, lakini utakuwa kama utani, kitu cha kuchezewa na Shetani. Ikiwa huwezi kushikilia maono sasa, basi huna msingi wowote, na utaondolewa siku zijazo! Kila sehemu ya barabara si rahisi kutembea, kwa hiyo usichukulie hili kwa urahisi. Chunguza hili kwa uangalifu sasa na kufanya maandalizi ya jinsi ya kutembea hatua ya mwisho ya njia hii. Hii ndiyo njia ambayo inapaswa kuchukuliwa siku zijazo na watu wote wanapaswa kuichukua. Huwezi kuruhusu ufahamu huu wa sasa uingie katika sikio moja na kutokea kwa lingine, wala usifikiri kwamba kile Ninachosema kwako ni kupoteza pumzi. Siku itakuja wakati ambapo utayatumia vizuri—maneno hayawezi kusemwa bure. Huu ndio wakati wa kujitayarisha; ni wakati wa kuandaa njia ya siku zijazo. Unapaswa kuandaa njia ambayo unapaswa kutembea baadaye; unapaswa kuwa na hangaiko na wasiwasi juu ya jinsi utakavyoweza kusimama imara baadaye na kujiandaa vizuri kwa njia yako ya baadaye. Usiwe mlafi na mvivu! Lazima ufanye kabisa kila kitu unachoweza kutumia vizuri muda wako ili kupata kila kitu unachohitaji. Ninakupa kila kitu ili uweze kuelewa. Mmeona na macho yenu kwamba katika chini ya miaka mitatu, Nimesema mambo mengi na kufanya kazi nyingi. Kipengele kimoja cha kufanya kazi kwa njia hii ni kwa sababu watu wana mapungufu sana, na jambo lingine ni kwa sababu muda ni mfupi sana na hakuwezi kuwa na kuchelewa zaidi. Kulingana na vile unayofikiria, ni polepole sana, kwa hiyo Nitaaandama nawe kwa muda gani? Ikiwa ungependa Niandamane nawe hadi Nitakapokuwa mzee na mwenye muvi, hilo halitawezekana! Watu kuwa wazi kabisa ndani yao wenyewe lazima kupatikane, na kisha wanaweza kushuhudia, na kutumiwa. Je, hiyo sio polepole sana? Kwa kupitia dhiki kubwa, ufahamu wa kweli ndani ya watu wote utafikiwa. Hii ni hatua ya kazi. Mara tu ukifahamu kikamilifu maono yaliyoshirikishwa leo na ufanikiwe kuwa na kimo halisi, dhiki zozote utakazopitia wakati ujao hazitakushinda—utaweza kuzihimili. Wakati Nimekamilisha hatua hii ya mwisho ya kazi na Nimekwisha kumaliza kuyatamka maneno ya mwisho, watu wa baadaye watahitaji kutembea njia yao wenyewe. Hii itatimiza maneno yaliyotangulia: Roho Mtakatifu ana agizo kwa kila mtu mmoja, na kazi ya kufanywa na kila mmoja. Katika siku zijazo, kila mtu atatembea njia ambayo wanapaswa kuchukua, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Nani atakayeweza kumtunza nani anapokuwa akipitia mateso? Kila mtu ana mateso yake mwenyewe, na kila mmoja ame na kimo chake mwenyewe. Hakuna kimo cha mtu sawa na mtu mwingine. Waume hawatawachunga wake zao na wazazi hawatawachunga watoto wao; hakuna mtu atakayeweza kumchunga mtu mwingine yeyote. Sio kama sasa—utunzaji na usaidizi wa pande mbili bado unawezekana. Hiyo itakuwa wakati wa kufichua kila aina ya mtu. Yaani, wakati ambapo Mungu anampiga mchungaji, kondoo wa kundi litatawanyika, na wakati huo hamtakuwa na kiongozi yeyote wa kweli. Watu watagawanyika—haitakuwa kama sasa, ambapo mnaweza kukusanyika pamoja kama kutaniko. Baadaye, wale ambao hawana kazi ya Roho Mtakatifu wataonyesha maumbo yao ya kweli. Wanaume watawasaliti wake zao, wake watawasaliti waume zao, watoto watawasaliti wazazi wao, wazazi watawatesa watoto wao—moyo wa binadamu hauwezi kutabiriwa! Yote ambayo yanaweza kufanywa ni mtu kushikilia kile anacho, na kutembea hatu ya mwisho ya njia vizuri. Hivi sasa hamuoni haya kwa uwazi na nyote mu wasioona mbali. Kufanikiwa katika kupitia hatua hii ya kazi sio jambo rahisi.
Wakati wa dhiki hautakuwa wa muda mrefu sana—hautakuwa hata mwaka. Ikiwa ingekuwa ingedumu kwa mwaka ingechelewesha hatua ya pili ya kazi, na kimo cha watu hakitoshi. Kama ingekuwa muda mrefu sana hawangeweza kuhimili—vimo vyao vina mapungufu yake. Baada ya kazi Yangu kukamilika, hatua inayofuata itakuwa kwa watu kutembea katika njia wanayopaswa. Kila mtu lazima aelewe njia anayopaswa kutembea—hii ni njia ya mateso na mchakato wa kuteseka, na pia ni njia ya kusafisha radhi yako ya kumpenda Mungu. Unapaswa kuingia katika ukweli gani, ni ukweli gani unapaswa kujiandaa nao, unavyopaswa kujifunza, na unapaswa kuingia kutoka kwa kipengele kipi—unapaswa kuelewa mambo yote haya. Lazima ujizatiti sasa. Ukisubiri mpaka dhiki zikujie, muda utakuwa umekwisha kuchelewa. Kila mtu lazima awe na mzigo kwa ajili ya maisha yake mwenyewe; daima usisubiri maonyo ya wengine au kwao kuinua masikio yako na kuzungumza nawe. Nimesema mengi sana lakini bado hujui ni ukweli gani unapaswa kuingia katika au kujiandaa mwenyewe nayo. Hii inaonyesha kwamba hujatia juhudi katika kusoma maneno ya Mungu. Huubebi mzigo wowote kwa ajili ya maisha yako kabisa—je, hilo linawezaje kuwa sawa? Huna uwazi juu ya kile unachopaswa kuingia katika, huelewi kile unachopaswa kuelewa, na wewe hujali kabisa kuhusu njia unayopaswa kuchukua—je, si wewe tu ni kipande kidogo sana cha mabaki ya meli yanayoelea majini? Je, wewe una maana gani? Mnachofanya sasa ni kujenga na kutengeneza njia zenu wenyewe. Lazima ujue kile ambacho watu wanapaswa kufikia na kiwango cha mahitaji ya Mungu kwa wanadamu. Lazima uwe na ufahamu ufuatao: Bila kujali chochote, ingawa mimi ni mpotovu sana, ni lazima nifidie mapungufu haya mbele ya Mungu. Wakati ambapo Mungu hakuwa ameniambia, sikuelewa, lakini sasa kwa kuwa Ameniambia, kwa kuwa nimeelewa lazima niharakishe kufidia, kuishi maisha ya ubinadamu wa kawaida, na kuishi kwa kudhihiriasha mfano ambao unaweza kuyakidhi mapenzi ya Mungu. Hata kama siwezi kufikia kile Petro alichofanya, angalau ni lazima niishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na kwa njia hii naweza kukidhi moyo wa Mungu.
Hatua ya mwisho ya njia hii inatoka sasa hadi mwisho wa dhiki ya baadaye. Hatua hii ya njia utakuwa wakati ambapo vimo halisi vya watu vitafunuliwa na kama wana imani ya kweli au la. Kwa kuwa hatua hii ya njia itakuwa ngumu zaidi kuliko yoyote ambayo ilipitiwa katika siku za nyuma, na itakuwa barabara iliyojaa mawe kuliko hapo awali, inaitwa "hatua ya mwisho ya njia.” Ukweli ni kwamba si sehemu ya mwisho ya barabara; hii ni kwa sababu baada ya kupata dhiki, utapitia kazi ya kupanua injili na kutakuwa na sehemu ya watu ambao watapitia kazi ya kutumiwa Kwa hivyo "hatua ya mwisho ya njia" huzungumzwa tu kwa kutaja dhiki ya kusafisha watu na mazingira magumu. Katika sehemu hiyo ya barabara katika siku za nyuma, ni Mimi Mwenyewe ndiye Niliyekuwa Nikikuongoza katika safari yako ya furaha, Nikikuchukua kwa mkono kukufundisha na Kukulisha kinywa—kwa—kinywa. Ingawa umepitia kuadhabiwa na hukumu mara nyingi, vimekuwa mapigo madogo kwako yaliyorudiwa rudiwa tu. Kwa kweli hiyo imesababisha mtazamo wako juu ya imani katika Mungu kubadilika kabisa kidogo; imesababisha pia tabia yako kuwa imara kidogo, na kukuruhusu kuwa na ufahamu mdogo Kwangu. Lakini Ninasema hili, kwa kutembea katika sehemu hiyo ya njia, gharama au jitihada zilizolipwa na watu ni ndogo sana—ni Mimi niliyekuongoza hadi leo. Hii ni kwa sababu Mimi sikuhitaji kufanya chochote na mahitaji Yangu kwako si ya juu kamwe—Ninakuruhusu tu wewe kuchukua kile kiinachopatikana. Katika kipindi hiki Nimeyakidhi mahitaji yenu bila kukoma, na Sijawahi kamwe kuwa na madai yasiyofaa. Mmepitia kuadibiwa mara kwa mara lakini bado hamjafikia mahitaji Yangu ya awali. Mnarudi nyuma na huvunjika moyo, lakini Sizingatii hili kwa sababu huu sasa ni wakati wa kazi Yangu binafsi na Sichukulii kwa uzito kujitolea kwako kwa ajili Yangu. Lakini katika njia kutoka hapa kuendelea, Sitafanya kazi tena au kuzungumza, na wakati huo Sitawafanya tena kuendelea katika mtindo kama usiovutia. Nitawawezesha kuwa na masomo maridhawa ya kujifunza, na Sitawaruhusu kuchukua kile kinachopatikana. Vimo halisi mlivyonavyo leo lazima vifunuliwe. Ikiwa jitihada zenu za miaka mingi zimekuwa za matunda au la itaonekana katika jinsi mnavyotembea hatua ya mwisho ya njia. Katika siku za nyuma, mlifikiri kuwa kumwamini Mungu kulikuwa rahisi sana, na hiyo ilikuwa kwa sababu Mungu hakuwa makini na wewe. Na vipi sasa? Je, mnafikiri kuwa kumwamini Mungu ni rahisi? Je, bado mnahisi kuwa kuamini katika Mungu ni furaha na bila mawazo kama watoto wanaocheza mitaani? Ni kweli kwamba wewe ni kondoo, hata hivyo, lazima uwe na uwezo wa kutembea njia ambayo unapaswa kutembea ili kulipa neema ya Mungu, na kumpata kabisa Mungu unayeamini. Msijichezee wenyewe—msijipumbaze! Ikiwa unaweza kufaulu katika hatua hii ya njia, utakuwa na uwezo wa kuona hali isiyokuwa ya kawaida, ya ajabu ya kazi Yangu ya injili ikienea katika ulimwengu wote, na utakuwa na bahati nzuri ya kuwa mwandani Wangu wa karibu, na kutekeleza sehemu yako katika kupanua Kazi Yangu katika ulimwengu wote. Wakati huo, utafurahia sana kutembea njia ambayo unapaswa kutembea. Siku zijazo zitakuwa na uchangamfu usio na mwisho, lakini jambo la msingi sasa ni kutembea hatua ya mwisho wa njia vizuri. Lazima utafute, na uandae jinsi ya kufanya hili. Hili ndilo unalopaswa kufanya hivi sasa—hili ni suala la haraka sasa!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni