Sura ya 56. Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?
Mwenyezi Mungu alisema, Upendo wa Mungu, ambaye alikuwa mwili, unajidhihirisha wapi kwa binadamu? Baada ya kupitia uzoefu wa kazi hatua kwa hatua, mnaweza kuona kwamba Mungu anapozungumza katika kila hatua ya kazi, anatumia ruwaza fulani, anazungumza unabii fulani, na anaonyesha ukweli fulani na tabia ya Mungu, na watu wote wana mijibizo. Mijibizo yao ni nini? Hawajinyenyekeshi kwa Mungu, hususan hawachukui hatua ya kutafuta ukweli, au hawapo radhi kukubali kazi ya Mungu. Wote wana mitazamo hasi na wabishi, na wanakanganyikiwa, wanakataa na hawakubali.
Hata hivyo, toka mwanzo, Mungu hajabadilisha namna Anavyofanya kazi Yake, upendo Wake kwa binadamu haubadiliki. Bila kujali mtazamo wa watu, bila kujali kama wanakataa au wanakubali shingo upande, au wanabadilika kidogo, upendo wa Mungu haubadiliki. Kazi Yake haijawahi kuvurugwa katika hatua yoyote ile. Hiki ni kipengele kimojawapo ambapo upendo Wake unadhihirishwa. Aidha, baada ya kila hatua ya kazi kukamilika, bila kujali namna ambavyo watu wanajidhihirisha, upendo wa Mungu kwa watu haubadiliki. Siku zote Anafanya kazi na siku zote Anawaokoa watu. Katika hatua inayofuata Anapokuwa anafanya kazi Yake, maneno Yake ya hukumu na ufunuo yatakuwa ya kina, wazi zaidi, na kuelekezwa zaidi katika hali ya sasa ya watu. Anazungumza maneno fulani kuwaruhusu watu waweze kumuelewa na kumfahamu Yeye vizuri zaidi, na hususan ili kwamba waweze kuelewa mapenzi Yake na waweze kupata mapenzi Yake. Watu wataona kwamba Mungu bado Anawapenda binadamu. Bila kujali kama mijibizo ya watu siku zote kuwa ni hasi au inampinga Mungu, watu siku zote watakuwa na aina hii ya mijibizo katika kila hatua ya kazi. Hata hivyo, Mungu siku zote huzungumza na hufanya kazi, na Mungu kamwe hajawahi kubadili upendo Wake kwa binadamu. Kwa hiyo, kazi yote ya Mungu kwa binadamu ni upendo. Baadhi ya watu husema: "Kama yote ni upendo, basi kwa nini Anahukumu na kumwadibu mwanadamu? Kwa nini inaonekana ni chuki kwa watu? Hata anawajaribu watu na kuwaacha wafe!" Ni kweli, Mungu ana upendo tu kwa watu! Mungu huurudi na kuuhukumu uasi wa watu ili kuwafanya watu waelewe ukweli na kuwafanya watubu na kuanza upya, na kuwafanywa watu waielewe tabia ya Mungu, na hivyo kuwafanya watu kumheshimu Mungu na kujinyenyekesha Kwake. Baadhi ya watu akili zao zipo katika hali ya kupinga, lakini Mungu hakati tamaa hata kidogo katika kuwaokoa watu; hii huhitaji kiwango kikubwa cha upendo, sio? Wakati wa kipindi cha wafanya huduma, watu wengi wapo katika hali ya uhasi na maumivu kiasi kwamba wanalia na kuhangaika kwa kiasi ambacho wanaomboleza na kulalama kwa sauti, wakijiuliza wanawezaje kuwa wafanya huduma katika shida nyingi kiasi hicho. Kwa kweli hawako radhi! Hauko radhi na huelewi, lakini Mungu anakuelewa. Je, huu si upendo? Upendo Wake unajumuisha ufahamu wa watu, kuwaongoza watu wote, na uelewa wa kina wa watu. Upendo Wake haukanganywi, si wa kujifanya, si mtupu, bali ni wa kweli. Anauona upungufu na ujinga wako na Ana huruma juu yako, Anakupenda na siku zote Anakuamsha kihisia. Bila kujali kama upo tayari au haupo radhi kuwa mfanya huduma, siku zote Anazungumza na kukupatia miezi kadhaa ya utakasaji ili kufunua ufisadi wako na kukufanya uifahamu hali yako ya fedheha. Je, kunakuwa na upendo wakati wa kipindi hiki cha miezi mitatu? Kama Hakuwa na upendo, basi Angekupuuza; kwa kutazama mwenendo wako wa mambo wakati wa kipindi cha wanfanya huduma, Angekuwa amekusukumilia mbali mapema. Je, hauko radhi kuwa mfanya huduma? Hutoteswa na Mungu, lakini unarukaruka kwa furaha pale unapopata baraka. Ikiwa Mungu alikuwa na chuki pekee badala ya upendo, basi watu wangeangamizwa kwa sababu ya mijibizo yao miovu. Miezi mitatu ya utakasaji si muda mrefu. Kwa nini Nasema sio muda mrefu? Kwa sababu hiki ni kiasi tu cha muda ambao watu wanaweza kuvumilia. Kama ingekuwa kwa muda mrefu kidogo, basi wasingeweza kuvumilia. Ingawa siku zote wanaimba, wanakutana pamoja, na kushiriki, wanafurahia tu mambo hayo na hakika wasingeweza kuendelea kusimama; kwa hiyo, wanabadilishwa kuwa watu wa Mungu mapema Hii pia inahitaji upendo; Mungu anatumia moyo Wake na upendo kuwabadilisha watu na kuwashikilia watu. Huu pia ni udhihirishaji wa upendo. Unaweza kuona upendo wa Mungu katika kipindi cha muda huu; hachelewi hata kwa siku moja au mwezi mmoja. Siku itakapofika ambapo Atapaswa kuzungumza, basi huzungumza bila kuchelewa. Kama Angechelewa miezi mingine michache, basi hatua kwa hatua baadhi ya watu wangeondoka. Huku ni kufanya kazi kulingana na hali halisi za watu. Hachelewi kabisa au kupoteza muda, Anamzingatia kila mtu kwa umahususi. Kwa kuwa Anawaokoa watu, Anawajibika hadi mwisho. Lakini baadhi ya watu hawayaishi matarajio, wanateleza na kuanguka chini. Kabla ya watu hawajaondoka, Roho Mtakatifu kwa umahususi anawasukuma na kuwasihi wabaki. Baadhi ya watu kwa kweli wamebembelezwa kubaki lakini hawakubaki. Mungu kwa kweli anawapenda watu sana, lakini watu hawamruhusu Mungu kuwapenda. Ikiwa Mungu hawezi kuwapenda watu wanaojiondoa, basi itabadilika kuwa chuki, na Anaweza kumpuuza kabisa mtu wa aina hiyo. Kwa kuzingatia hatua na kiwango cha muda wa kazi, urefu wa hatua, kiasi cha maneno yaliyosemwa katika hatua, toni ya sauti, mbinu zilizotumika katika hatua, na ukweli unaoambatana nayo kukufanya uelewe, yote hujumuisha mawazo Yake makuu na tafakari na mpangilio na upangaji sahihi. Siku zote Anatumia hekima Yake kuwaongoza binadamu, kuwakimu, kuwahudumia, na kuwakuza kidogokidogo na kuwaleta katika siku hii. Kila mtu ambaye amepitia mambo haya sasa ana kiasi fulani cha ufahamu; hata kama Siijadili, watu wengi wanaweza; watu wanaweka mchakato wa hatua kwa hatua katika kumbukumbu zao. Hakuna maneno ya kuelezea upendo uliopo katika hili. Mungu anawapenda watu sana lakini watu hawataupitia upendo huo kwa kina; upendo huu ni wa kina sana na haiwezekani kuuelezea vizuri kwa maneno; haiwezekani kuuelezea kwa mtazamao wa wakati. Kwa mtazamo wa wakati, tunaweza kuona ni jinsi gani upendo Wake kwa binadamu ni wa kina sana; Anatoa uangalifu mkubwa kwa mambo madogomadogo na haruhusu muda kusonga hata kidogo. Anahofia kwamba ikiwa muda utasonga sana watu watajiondoa na kumwacha. Upendo Wake unawashikilia watu kwa nguvu na haukati tamaa kabisa. Aidha, kuna hatua za kurudi na hukumu pia ambazo Mungu Anazifahamu. Ikiwa kungekuwa na mbinu nyingine zaidi, watu wangehisi kwamba Mungu alikuwa Anawahadaa na kuwachezea. Vimo vya watu havijafikia kiwango na ni rahisi sana kwao kujitoa. Kwa hiyo, baada ya miezi mitatu ya utakasaji, Mungu alizungumza tena na kuwafanya wafanya huduma kuwa watu Wake na kila mtu alifurahi. Watu walitikiswa kihisia kiasi kwamba wakaangua kilio na wakaona kwamba hekima ya Mungu ni nzuri sana. "Wakati huo wote nilidhani nilikuwa mfanya huduma kweli, nilidhani sina hatima, na kwamba hii ilimaanisha kwamba Mungu hatutaki na tumekwisha kabisa." Wakati huo kama Ningesema kwamba nisingewaruhusu kufa, hakuna ambaye angeamini; mngedhani kwamba Mungu tayari amesema hivyo na kwamba ilikuwa ni kweli kabisa. Baada ya miezi mitatu, Nilizungumza kifungu kingine cha maneno na kuhitimisha hukumu ya wafanya huduma. Ingawa asili za watu zimepotoka, wakati mwingine watu wanakuwa hawana hatia hasa kama mtoto mdogo. Kwa nini inasemwa kwamba watu siku zote ni watoto wachanga mbele ya Mungu? Kila tendo wanalofanya ni kama la mtoto mchanga; watu wanawaangalia wengine kana kwamba wote wamepotoka na kuoza, lakini katika macho ya Mungu, watu siku zote ni watoto wachanga, wanyofu na wasio na hatia; kwa hiyo Mungu hawachukulii watu kama maadui, badala yake Anawaangalia kama walengwa Wake wa wokovu na upendo. Kwa hiyo upendo wa Mungu kwa watu si kama ambavyo watu wanafikiria, ambayo ni kusema tu mambo mazuri na heri. Wakati huu, kuna maneno fulani katika kazi ya Mungu ambayo kwa kweli hayakidhi matarajio ya watu, hadi kufikia hatua ya kuvunja mioyo ya watu na kuwasababishia maumivu. Baadhi ya maneno ya hukumu ni kama yanawachora na kuwakaripia watu, lakini kwa kweli yote yana muktadha wa kweli na yapo sambamba na uhakika na ukweli. Hayajaongezwa chumvi. Mungu anazungumza kulingana na dutu ya watu iliyopotoka na kwa kuwa watu watapitia uzoefu kwa kipindi fulani, basi wataelewa. Kusudi la Mungu kusema mambo haya ni kuwabadilisha na kuwaokoa watu. Ni kwa kuzungumza tu kwa namna hii ndiyo Anaweza kupata matokeo mazuri kabisa. Unapaswa kuona kwamba nia njema ya Mungu ni kwa ajili ya kuwaokoa watu na kila kitu kilichomo ndani yake ni upendo wa Mungu. Bila kujali kama unauangalia kwa mtazamo wa hekima katika kazi ya Mungu, kwa mtazamo wa hatua na ruwaza katika kazi ya Mungu, au kwa mtazamo wa wakaa wa kazi au mipangilio na mipango Yake sahihi—chote kilichomo ndani yake ni upendo Wake. Kwa mfano, watu wote wana upendo kwa wana na mabinti zao na ili kuwaruhusu watoto wao kutembea katika njia sahihi, wote wanaweka jitihada kubwa. Wanapogundua udhaifu wa watoto wao, wanahofia kwamba ikiwa watazungumza kwa sauti laini, watoto wao hawatasikia na hawataweza kubadilika, na wanahofia kwamba ikiwa watazungumza kwa ukali sana, wataumiza staha ya watoto wao na watoto wao hawataweza kuvumilia. Kwa hiyo, hii yote inafanyika chini ya ushawishi wa upendo na kiwango kikubwa cha jitihada kinatumika. Nyinyi ambao ni wana na mabinti mtakuwa mmeshawahi kupata upendo wa wazazi wenu. Sio tu upole na kujali ndio upendo, lakini hata zaidi, kuadibu sana ni upendo. Mungu yupo chini ya ushawishi wa upendo kwa binadamu na chini ya sharti la mwanzo la upendo. Kwa hiyo, Anafanya kwa kadri ya uwezo Wake wote kuwaokoa wanadamu waliopotoka. Hashughuliki nao kwa kutimiza wajibu tu, badala yake anafanya mipango sahihi, kulingana na hatua. Kwa kuzingatia wakati, eneo, toni ya sauti, mbinu ya kuzungumza, na kiwango cha jitihada kilichowekwa..., mnaweza kusema kwamba yote hii inafunua upendo Wake, na inaelezea vizuri kabisa kwamba upendo Wake kwa binadamu hauna mipaka na haupimiki. Na watu wengi wanasema maneno ya uasi wanapokuwa katikati ya kujaribiwa kwa mfanya huduma na wanatoa malalamiko. Lakini Mungu hagombanigombani juu ya mambo haya, na hakika hawaadhibu watu kwa hili. Kwa sababu Anawapenda watu, Anasamehe kila kitu. Ikiwa Angekuwa na chuki tu badala ya upendo, basi Angeweza kuwahukumu watu mapema kabisa. Kwa kuwa Mungu ana upendo, Hagombanigombani, bali Anavumilia, na Anaweza kuona shida za watu. Hii kabisa ni kufanya kila kitu chini ya ushawishi wa upendo. Mungu tu ndiye anawaelewa watu, wewe hata hujielewi. Hiyo si sahihi? Tafakari kuhusu hilo kwa makini, baadhi ya watu wanalalamika kuhusu hiki na kile; watu wanasababisha shida bila sababu, wanaishi kwenye baraka lakini hawahisi baraka. Hakuna Anayejua ni maumivu kiasi gani Mungu ambaye Alishuka duniani kutoka mbinguni atalazimika kuteseka kiasi gani. Mungu alikuwa mtu, Yeye ni mkuu sana na Aliweza kuwa mdogo hivyo, wa hali ya chini na Aliteswa hivyo. Ni maumivu kiasi gani Aliyopitia! Chukua mfano kutoka duniani: Mtawala mzuri huwapenda watu wake kama tu watoto wake, na ili kuelewa shida na mateso ya watu, yeye binafsi anatoka na kwenda kushuhudia. Kulinagana na nafasi yake, hapaswi kuteseka na maumivu haya, lakini ili kuondoa maumivu ya watu, anawatembelea kwa siri akiwa katika mavazi ya kawaida. Anakwenda miongoni mwa watu na kushuhudia na kuyaelewa maumivu ya watu kama mtu wa kawaida. Kulingana na nafasi yake, kujishusha hadhi kwenye hadhi ya mtu wa kawaida ni jambo la unyenyekevu; anapaswa kuishi kama mtu wa kawaida na watu hawaijui hadhi yake, na kwa kweli wanamchukulia kama mtu wa kawaida. Kuna hatari nyingi miongoni mwa watu, na kimsingi wanamchukulia kwa namna tofauti, na huanza kupata shida na mateso ya watu; huteseka kwa maumivu ambayo watu wanawayapata; analazimika kuwa mwangalifu na makini kila mahali. Anafanya hivi kwa ajili gani? Kuna lengo moja tu linalomsukuma. Mungu anaweza kufanya kazi kwa namna hii leo kwa sababu mpango Wake wa usimamizi umefikia kiwango hiki. Anawapenda binadamu hivyo Anawaokoa binadamu, Anaweza kufanya hili kwa sababu Anasukumwa na upendo na yupo ndani ya viunga vya upendo. Mungu alikuwa mwili na Aliteseka kwa mateso makubwa ili kuliokoa kundi hili la binadamu walioharibika. Hii kwa kutosheleza kabisa inathibitisha kwamba upendo Wake ni mkubwa sana. Kuna ushauri, faraja, tumaini, uvumilivu, na ustahimilivu katika maneno ambayo Mungu huzungumza, hata zaidi, kuna hukumu, adibu, laana, kufichuliwa hadharani, ahadi za kuvutia, n.k. katika maneno Yake. Bila kujali mbinu, yote hii imetawaliwa na upendo. Hii ni dutu ya kazi Yake, sio? Nyinyi nyote kwa sasa mna kiasi fulani cha uelewa, lakini sio wa kina kiasi hicho. Angalau mnaweza kuwa na kiasi fulani cha ufahamu, na baada ya kuwa na uzoefu wa miaka mitatu hadi mitano, mtaweza kuhisi kwamba upendo huu ni wa kina sana na ni mkubwa sana. Haiwezekani kutumia meneno ya binadamu kuelezea. Ikiwa watu hawana upendo, wanawezaje kurudisha upendo wa Mungu? Hata kama uliyatoa maisha yako kwa Mungu, usingeweza kumlipa. Baada ya nyinyi kupitia uzoefu wa mika mitatu hadi mitano, na kutafakari juu ya mafunuo na tabia zenu za sasa, mtakuwa na majuto kupita kiasi na mtapiga magoti chini na kusujudu vichwa vyenu kwenye ardhi. Kwa nini watu wengi wanafuatilia kwa karibu? Kwa nini watu wengi wamekuwa na shauku kubwa hivi? Wana uelewa wa upendo wa Mungu, na wanaona kwamba kazi ya Mungu ni kuwaokoa watu. Fikiria kuhusu hilo, je, kazi ya Mungu sio sahihi hususan kwa kuzingatia muda? Kiungo kimoja hufuata kiungo kingine bila kuchelewa hata kidogo. Kwa nini Hachelewi? Bado ni kwa ajili ya binadamu. Hayupo radhi kutoa sadaka au kupoteza roho hata moja. Watu hawajali kuhusu majaliwa yao wenyewe, kwa hiyo, ni nani katika dunia hii anakupenda sana? Hujipendi, hujui kutunza maisha yako mwenyewe, na hujui yana thamani kiasi gani. Ni Mungu Ndiye Anayewapenda sana binadamu. Ni Mungu pekee ndiye Anayewapenda sana binadamu. Watu wanaweza kuwa bado hawajaliona hili, wakidhani kwamba wanajipenda. Kwa kweli, ni upendo gani ambao watu wanao wao kwa wao? Ni upendo wa Mungu tu ndio upendo wa kweli; taratibu utaelewa upendo wa kweli ukoje. Ikiwa Mungu hangekuwa mwili na kufanya kazi na kuwaongoza watu uso kwa uso, ikiwa Hangekutana na watu na kuishi na watu wakati wote, basi kuuelewa upendo wa Mungu kwa kweli kisingekuwa kitu rahisi kwa watu kufanya.
Watu na Mungu kimsingi hawafanani na wanaishi katika dola mbili tofauti. Watu hawawezi kuielewa lugha ya Mungu, na zaidi hawawezi kuyaelewa mawazo ya Mungu. Ni Mungu pekee ndiye Anayewaelewa watu na haiwezekani kwa watu kumwelewa Mungu. Mungu ni lazima Awe mwili na Afanane na mwanadamu (kufanana kwa umbo la nje). Mungu anavumilia mateso na maumivu mengi ili kuwaokoa binadamu na kuwafanya watu kuielewa na kuifahamu kazi ya Mungu. Kwa nini Mungu siku zote Anawaokoa watu na hajawahi kukata tamaa? Hii si kwa sababu ya upendo Wake kwa watu? Anamwona binadamu akiharibiwa na Shetani na Hawezi kuvumilia kuacha au kukata tamaa. Kwa hivyo kuna mpango wa usimamizi. Ikiwa Angewaharibu binadamu Akipatwa na hasira kama watu walivyodhani, basi kusingekuwa na haja ya kuwaokoa watu waziwazi kwa namna Afanyavyo sasa. Na kwa kuwa Alikuwa mwili na Akateseka kwa maumivu, upendo Wake umedhihirishwa, upendo Wake unavumbuliwa kidogokidogo na watu na unafahamika kwa watu wote. Kama isingekuwa kwa kufanya kazi namna hii sasa, na ikiwa watu wangejua tu kwamba kuna Mungu mbinguni na kwamba Anawapenda binadamu, basi hili litakuwa ni fundisho tu, na watu kamwe wasingeweza kuuona upendo wa Mungu. Ni kwa Mungu tu kuwa mwili na kufanya kazi ndipo watu wanaweza kuwa na uelewa wa kweli juu Yake ambao si wa kufikirika au mtupu na wala sio maneno matupu, lakini badala yake ni ufahamu ambao ni wa kweli. Hii ni kwa sababu upendo ambao Mungu anawapatia watu ni wa manufaa yanayoonekana, kazi hii inaweza kufanywa tu kwa kuwa mwili na haiwezi kuchukuliwa nafasi na Roho Mtakatifu. Ni upendo mkubwa kiasi gani ambao Yesu aliwapa watu? Alihudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu waliopotoka kwa kusulubiwa, Alikuja kukamilisha kazi ya ukombozi kwa ajili ya binadamu, hadi aliposulubiwa. Upendo huu hauna mipaka na kazi ambayo Mungu ameifanya ni ya muhimu sana. Kuna watu ambao wana dhana kuhusu Mungu kuwa mwili. Ni dhana gani hizi walizonazo? Bila Mungu kuwa mwili, imani ya watu kwa Mungu ingekuwa ni mfumo tupu na wakati wa mwisho wangeangamizwa. Upendo wa Mungu kwa binadamu hasa umedhihirishwa katika kazi Yake wakati akiwa katika mwili, Yeye binafsi Akiwaokoa watu, Akizungumza uso kwa uso na watu, na kuishi miongoni mwa watu bila kuwa mbali nao hata kwa hatua moja, bila kujifanya, lakini akifanya kweli. Huwaokoa watu kwa kiasi kwamba Aliweza kuwa mwili na kupita miaka mingi ya maumivu pamoja na watu duniani, yote hii ni kwa sababu ya upendo Wake na huruma kwa binadamu. Upendo wa Mungu kwa binadamu hauna masharti au matakwa. Anapata nini kutoka kwa binadamu? Watu hawamchangamkii Mungu. Nani anaweza kumchukulia Mungu kama Mungu? Watu hata hawampatii Mungu faraja, hata leo hii Mungu hajapokea upendo wa kweli kutoka kwa watu. Mungu Anatoa bila ubinafsi na Anakimu bila ubinafsi, lakini watu bado hawaridhiki na wanaendelea kuomba neema bila kukoma. Watu ni wagumu sana kushughulika nao na ni wasumbufu sana! Hata hivyo, siku moja siku itafika ambapo kazi ya Mungu itapata matokeo na idadi kubwa ya watu watatoa shukrani za kweli kutoka mioyoni mwao. Watu ambao wamepitia uzoefu wa miaka mingi wanaweza kuelewa kipengele hiki. Ingawa watu ni wazito, hata hivyo sio maroboti; si vitu visivyokuwa na uhai. Watu ambao hawajawahi kuwa na uzoefu na kazi ya Mungu wanaweza wasieweze kutambua mambo haya; wanakubali kwa kusema kwamba ukweli huu ni sahihi, lakini hawana uelewa wa kina sana.
Mungu alikuwa mwili na Amefanya kazi kwa miaka kadhaa na Amesema mambo yasiyoweza kuhesabika. Mungu anaanza kwa kutoa hukumu ya wafanya huduma, na baadaye Husema unabii na Huanza kazi ya hukumu na kurudi, kisha Hutumia kifo kuwatakasa watu. Baada ya hapo, Huwaongoza watu katika njia sahihi ya kumwamini Mungu, Akizungumza na kuwapatia watu ukweli wote na kupambana na dhana mbalimbali za mwanadamu. Baadaye, Humpatia mwandamu tumaini dogo kumruhusu kuona kuna tumaini mbele yake; yaani, Mungu na watu wanaingia katika mwisho mzuri wa safari kwa pamoja. Ingawa kazi hii inafanywa kulingana na mipango ya Mungu, yote inafanywa kulingana na mahitaji ya binadamu. Haifanywi kiholela na Yeye; Hutumia hekima Yake kufanya kazi yote hii. Kwa kuwa ana upendo, Anaweza kutumia hekima na kwa bidii kushughulika na watu hawa walioharibika. Hachezi na watu hata kidogo. Hebu angalia toni ya sauti na namna ya kutamka maneno katika maneno ya Mungu; wakati fulani inawapatia watu majaribu, wakati fulani meneno Yake huwafanya watu kutahayari, wakati fulani huwapatia watu maneno ambayo huwaokoa na hufanya wawe watulivu. Kwa kweli Anawafikiria sana na kuwajali watu. Ingawa watu ni viumbe wa Mungu, na wote wamepata uharibifu kutoka kwa Shetani, na ingawa watu hawana thamani, ni wazururaji, na asili zao ziko namna hii, Hashughuliki na watu kulingana na hulka zao, na Hashughuliki nao kulingana na adhabu ambayo wangestahili kuipata. Ingawa maneno Yake ni makali, siku zote Anashughulika na watu kwa ustahimilivu, uvumilivu, na huruma. Tafakari hili kwa taratibu na kwa makini! Ikiwa Mungu hakushughulika na watu kwa uvumilivu, huruma na neema, je, Angeweza kusema mambo haya yote ili kuwaokoa watu? Kwa nini Hakuwahukumu watu moja kwa moja? Watu ni wapumbavu sana na wajinga, watu hawana upendo katika dutu yao, na hawajui upendo ni nini, na hawajui kwa nini Mungu hufanya kazi namna hii. Watu wanapokuwa hawauoni upendo wa Mungu, basi wanahisi: Mungu hufanya kazi hii vizuri sana, ni faida kwa binadamu na inaweza kuwabadilisha watu. Hata hivyo, hakuna mtu hata mmoja ambaye huhisi kwamba Mungu Amefanya kazi Yake vizuri sana, kwa umuhimu mkubwa sana, na kwamba upendo Wake kwa binadamu ni wa kina sana, na kwamba kwa kweli hajawahi kushughulika na watu kama uchafu usioweza kuvumilika. Watu hawajawahi kumchukulia Mungu kama Mungu, lakini Mungu amewachukulia watu kama watu. Sivyo ilivyo? Mungu husema kwamba nyinyi ni wanyama, lakini Hajawahi kiwachukulia nyinyi kama wanyama. Ikiwa Angewachukulia kama wanyama, basi kwa nini Awapatie ukweli? Angekuwa Anakuokoa kwa ajili ya nini? Baadhi ya watu wanahisi wamekosewa sana na wanasema: "Mungu Alisema mimi ni mzururaji, nimeaibika sana siwezi kuendelea kuishi." Kwa kweli watu hawaelewi mapenzi ya Mungu. Mtu anaweza kusema kwamba unaweza kupitia uzoefu wa hekima na makusudi mema ya kazi ya Mungu katika maisha yako yote lakini hutaweza kuyaelewa kwa kina sana. Bila kujali kama uzoefu wako ni wa kina au la almradi mwishoni unaelewa na unajua kidogo, basi hiyo inatosha. Mungu anawaomba watu kuuelewa ukweli na kujikita katika kubadilisha tabia zao, ili polepole kuingia kwa kina katika kujitoa kwao na kujinyenyekeza vilevile katika upendo walio nao kwa Mungu katika mioyo yao. Watu wanapojitolea mhanga kidogo na kupata shida kidogo, basi wanafikiri kwamba michango yao ni mikubwa sana mbele ya Mungu, na kwamba wana ukuu. Wanapofanya mchango wao mdogo, wanakoga ukuu wao, na kama hawataji michango yao, basi hawahisi wapo imara au wametulia. Je, watu wana upendo? Watu wana upendo gani? Je, Mungu hupokea upendo wa kweli wa watu? Je, Mungu si mwenye kustahili upendo wa watu?
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni