12/18/2017

Sura ya 21. Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu

Wale wanaomwamini Mungu wanaweza wote kuongea kuhusu mafundisho, wakisema kwamba maoni yetu juu ya imani katika Mungu lazima yawe safi, kwamba tunapaswa kumtii Mungu, kumpenda Mungu, na kutimiza wajibu wetu kwa uaminifu, kwamba hatupaswi kuasi dhidi ya Mungu na kwamba lazima tujielewe. Ingawa wameyanena mambo haya mara nyingi, hawayaelewi. Bado hakuna ufahamu halisi ya maana ya kweli katika ukweli huu. Unayaelewa tu maneno juu juu, lakini si maana ya kiroho au maudhui ya ndani ya maneno. Hivyo basi, nyinyi hamna ukweli ndani ya mioyo yenu. Mnaweza kuwa na ufahamu kidogo, lakini ni mwepesi mno. Kwa wale ambao wamemwamini Mungu kwa muda mrefu na ambao wana uzoefu fulani, wanaelewa katika mioyo yao baadhi ya mambo ya rahisi, ilhali hawawezi kuonyesha au kutumia ufahamu wao. Kwa wale ambao ni wapya kwa kanisa, wanaweza tu kusema baadhi ya mafundisho na kuhubiri injili, lakini hawauelewi ukweli hata kidogo. Wale kati yenu ambao ni wasomi na waliostaarabika pia hawauelewi ukweli; usifikiri ufahamu wako wa mafundisho au maana halisi kuwa ufahamu wa ukweli. Baadhi ya wale ambao wamemwamini Mungu kwa muda mrefu, ambao wana ubora mzuri wa tabia na wanaelewa roho kwa kiasi kizuri, wanaweza kuwa na uzoefu kidogo wa ukweli, lakini bado hawawezi kusema kwamba wao wanauelewa. Unapoongea kuhusu ufahamu, kati ya sentensi kumi unazonena labda mbili zina ufahamu wa kweli. Mengine ya unayoyasema ni ya mafundisho, lakini wewe unahisi kana kwamba sasa unaweza kufaulu—unaweza kuhubiri kwa uthabiti kwa siku moja au siku kadhaa bila kujali mahali ambapo unaenda, daima ukiwa na kitu cha kusema na kutoacha kamwe. Wakati umemaliza, unataka kuyapanga katika kitabu, kunakili na kukisambaza, kubuni “tawasifu ya mtu mashuhuri” ambao, baada ya kutolewa, ungewaruhusu watu kula na kunywa maneno haya na ambao ungeleta manufaa kwa wote. Watu hawawezi kuuelewa ukweli kabisa, katika hali bora zaidi kuelewa maana halisi. Wakati wao wamejitayarisha kwa kiasi fulani, kwa sababu wao ni werevu na wana kumbukumbu nzuri, kwa sababu mara nyingi wao huzungumza kuhusu kazi ya Mungu, umuhimu wa kupata mwili, siri ya kupata mwili, na mbinu na hatua za kazi ya Mungu, wanahisi kwamba wao wenyewe wanaumiliki ukweli, kwamba wao wamejawa nao. Huu ni upumbavu sana! Linadhibitisha kwamba hakuna hata mmoja kati yao anayeuelewa ukweli. Sasa watu wanaelewa baadhi ya mafundisho, hawajielewi, seuze kuwa na akili yoyote. Kwa kuelewa baadhi ya mafundisho wanahisi kwamba wanaumiliki ukweli, kwamba wao si wasio na thamani sana, na wanasimama kwa majivuno, wakifikiri: “Nimesoma neno la Mungu mara nyingi. Maneno mengine nayakumbuka kwa usahihi na nimeyachora moyoni mwangu. Popote niendapo, nikianza kuongea ninaweza kuendelea kwa siku nyingi, na ninaweza kuongea kwa utaratibu na ukamilifu kuhusu kifungu chochote cha maneno ya Mungu.” Kwa kweli, huelewi chochote. Mbona yasemekana kwamba huelewi? Kipengele kimoja ni kwamba nyinyi hamuwezi kutatua matatizo, hamuwezi kupata chanzo chake, wala hamuwezi kufahamu asili yake. Kipengele kingine ni kwamba, bila kujali shida au suala ni nini, maarifa yenu kulihusu ni ya kipumbavu na tata, na hamwezi kuyaunganisha na ukweli.
Kuhusu mtazamo wa imani wa mtu katika Mungu—jinsi watu wanavyomwamini Mungu, kile kinachoweza kuitwa “imani,” ni mtu wa aina gani anayeweza kuitwa “mwamini,” ni mtu wa aina gani aliye na Mungu ndani ya moyo wake, jinsi ya kueleza maneno “imani katika Mungu,” jinsi ya kuuelewa ukweli huu, aina gani ya msimamo huonyesha kwamba mtazamo wa mtu wa imani katika Mungu ni sahihi, aina gani ya msimamo huonyesha kwamba mtazamo wa mtu waimani katika Mungu si sahihi, na jinsi watu wanafaa kumwamini Mungu—je, nyinyi mshawahi kufikiri mambo haya? Nyinyi nyote mnaonekana kuwa majitu wa ukweli. Je, umewahi kufikiri kipi kinajumuisha imani? Ni mambo gani katika maisha yako ya kila siku ni maonyesho ya kutoamini, ni maonyesho gani yanafanywa na wale waumini wanaomiliki imani halisi, ni maonyesho gani yanayofanywa na wale ambao hawaamini, na katika mambo ambayo wewe hukutana nayo katika maisha yako ya kila siku, ni gani kati yake ambayo yanahusiana na imani katika Mungu na ni gani kati yake ambayo hayahusiani kabisa na imani katika Mungu–je, mnaweza kuzungumza kuhusu mambo haya kwa dhahiri? Je, kweli unaelewa maana ya imani katika Mungu? Je, wewe unaelewa ni mtu wa aina gani ana imani halisi, au mtu wa aina gani ni muumini halisi? Viumbe vyote vinaamini katika Mungu–Je, unaelewa maana ya hili? Hili linahusisha maono juu ya imani katika Mungu. Watu wengine husema: “Imani katika Mungu ni jambo zuri na ni njia sahihi. Imani katika Mungu ni bora kuliko biashara yoyote au kazi. Imani katika Mungu ni jambo kubwa kabisa katika maisha ya mwanadamu. Kutimiza wajibu wa mtu kwa ajili ya Mungu huku ukimwamini Mungu ni maonyesho ya vitendo. Imani katika Mungu ni kwa ajili ya kuokolewa na ni kwa ajili ya kuyaridhisha mapenzi yake.” Nyinyi nyote mtakuwa mmesema haya mambo awali, sivyo? Je, kweli mnalewa haya maneno? Hapana, bado hujayaelewa kwa kweli. Imani ya kweli katika Mungu si kuhusu kumwamini Yeye ili kuokolewa na hata zaidi si kuhusu kuwa mtu mzuri. Pia si kuhusu kumwamini Mungu tu kwa ajili ya kuwa na taswira ya binadamu. Kwa kweli, watu hawapaswi kuangalia imani yao katika Mungu kama tu imani ya kwamba kuna Mungu, na kisha hakuna zaidi; si kwamba unapaswa kuamini tu kuwa Mungu ni ukweli, njia, uhai na kisha hakuna zaidi. Wala si tu ili umkubali Mungu, hata zaidi si tu kuamini kwamba Mungu ni Mtawala juu ya kila kitu, kwamba Mungu ni mwenyezi, kwamba Mungu aliumba vitu vyote katika dunia, kwamba Mungu ni wa kipekee na kwamba Mungu ni mkuu. Si tu ili wewe uamini ukweli huu, bali mapenzi ya Mungu ni ili nafsi yako yote na moyo wako wote–lazima vipewe Mungu na vimtii Mungu, yaani, unapaswa kumfuata Mungu, umruhusu Mungu akutumie, kuwa radhi kumfanyia huduma, na kwamba unapaswa kufanya kitu chochote kwa ajili ya Mungu. Siyo kusema kwamba Mungu huamua kabla na huchagua hawa watu kumuamini Yeye. Kwa kweli, wanadamu wote wanapaswa kumwabudu Mungu, kumsikiza Yeye na kumtii, kwa sababu binadamu waliumbwa na Mungu. Hili sasa linagusia suala la kiini. Kawa wewe daima huongea kuhusu nia zako za kumwamini Mungu, ukisema, “Hatumwamini Mungu ili kupata uzima wa milele? Hatumwamini Mungu ili kuokolewa” kana kwamba imani yako katika Mungu ni kama aina ya jambo la ukingoni, kuamini tu ili upate kitu, basi huu sio mtazamo unaofaa kuwa nao kuhusu imani yako katika Mungu. Kuhusu kila mojawapo ya ukweli, watu wanapaswa kutafuta, kujaribu kuelewa na kuchunguza ni nini maana ya ndani ya ukweli, jinsi ya kutenda hicho kipengele cha ukweli, na jinsi kinaweza kuingiwa ndani–haya ni mambo watu wanafaa kumiliki. Katika vipengele vyote vya ukweli ambavyo mnafaa kuvimiliki sasa, mnaelewa tu mafundisho ya juu juu, sura ya nje, na hamuelewi kiini cha ukweli, kwa vile bado hamjakipitia. Kwa mfano: Ni kiasi gani cha ukweli kiko ndani ya kipengele cha kutimiza wajibu wa mtu? Je, kuna ukweli mwingi ndani ya kipengele cha mwanadamu kumpenda Mungu? Kujijua, watu lazima waelewe ukweli mwingi. Kuna ukweli mwingi wa umuhimu na siri ya kupata mwili ambao lazima pia ueleweke. Kuna ukweli mwingi ndani ya masuala kama jinsi watu wanafaa kumwabudu Mungu, jinsi wanafaa kuishi kama binadamu, jinsi wanafaa kumtii Mungu, kile wanafaa kufanya ili kufuata mapenzi ya Mungu na jinsi wanafaa kumhudumia Mungu. Mnafikiri vipi au kujaribu kuelewa maswali ya vipengele hivi vyote vya ukweli? Kuna ukweli ambao hasa ni wa ndani kabisa katika kila kipengele, na vinahitaji watu kuvipitia. Usipovipitia na daima uzungumze tu kuhusu sehemu ya juu ya maneno, bila kuwahi kuvielewa ama kuvipitia kutoka katika vina vyake, utaishi daima juu juu ya maneno, na utakosa uwezo wa kubadilika.
Wakati watu wa kawaida hutoa maoni kuhusu nyinyi ambao ni viongozi, nyinyi husema: “Mmh, ni nini kinakufanya kuwa na sifa zinazostahili kutoa mawazo hunihusu? Je, ni mahubiri mangapi unaweza kutoa? Je, unaweza kuongea kwa kiasi gani? Je, ni watu wangapi unaweza kuwaongoza? Je, unaweza kufanya nini?” Ni kama mna sifa zinazostahili. Mkiendelea kwa njia hii mtakuwa katika shida; mnaweza kuhudumu kwa muda fulani lakini kisha mtakosea. Kuhusu nyinyi nyote, kama makanisa katika sehemu au yamepewa kwenu na hakuna anayewasimamia kwa miezi sita, mnaanza kupotoka. Kama hakuna anayekusimamia kwa mwaka mmoja, unawaongoza mbali na kuwapotosha. Miaka miwili inapita na bado hakuna anayekusimamia, na unawaleta watu hao mbele yako. Kwa nini hivi? Je, mmewahi kufikiri swali hili awali? Niambieni, mnaweza kuwa hivi? Maarifa yenu yanaweza kuwakimu watu kwa muda tu. Wakati unapoendelea, ukiendelea kusema kitu kile kile, watu kadhaa wataweza kutambua; watasema wewe ni mtu wa juu juu sana, aliyekosa kina sana. Hutakuwa na budi ila kujaribu kuwadanganya watu kwa kuongea mafundisho, na kama wewe daima huendelea hivi, wale walio chini yako watafuata namna yako, nyayo, na mfano wa kumwamini Mungu na kupitia, na watatia maneno na mafundisho hayo katika vitendo, na hatimaye, unapoongea katika njia hii, watakutumia kama mfano. Unachukua mwongozo kuongea mafundisho, na wale walio chini yako watajifunza mafundisho kutoka kwako, na vitu vinapoendelea utakuwa umechukua njia ambayo si sawa. Wale walio chini yako wanafuata njia yako, na wote wanajifunza kutoka kwako na hukufuata, hivyo unahisi; “mimi ni mwenye nguvu sasa; watu wengi sana hunisikiza, na dunia iko chini ya amri yangu.” Asili hii ya usaliti ndani ya binadamu bila kujua hukufanya umbadili Mungu kuwa mkubwa wa jina tu, na kisha wewe mwenyewe basi unaanzisha madhehebu kadhaa, faraka kadhaa. Je, madhehebu na faraka hutokea vipi? Zinatokea kwa njia hii. Tazama viongozi wa kila madhehebu na faraka. Wote ni wa kujigamba na kujisifu, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ujuzi fulani, na wanaweza kuongea mafundisho kiasi, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa, ambao kupitia kwake wamewaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu—lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na wale wanaohubiri njia ya kweli, baadhi yao wangesema, “Lazima tutafute ushauri kwake kuhusu imani yetu katika Mungu.” Tazama jinsi wanavyohitaji ridhaa ya mtu ili kumwamini Mungu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli? Watu wa aina hii ni wa aina sawa na Paulo. Kwa nini kusema hivi? Barua zilizoandikwa na Paulo ziko takriban umri wa miaka elfu mbili na zilisambaa kote katika Enzi nzima ya Neema. Watu wote walikula na kunywa maneno haya yake na kuchukua maneno yake kama kawaida, kama vile kuteseka, kuudhibiti mwili wa mtu mwenyewe, na kupokea taji la mwisho la haki. Watu walimwamini Mungu kulingana na maneno yake na mafundisho yake. Je, ni kiasi gani cha mapenzi ya Mungu ambacho watu wangeweza kuelewa katika Enzi ya Neema? Hata hivyo, wale ambao walimfuata Yesu katika wakati huo walikuwa katika walio wachache, na wale ambao walimjua walikuwa hata wachache zaidi—hata wanafunzi Wake kadhaa hawakuwa wanamjua kwa kweli. Mtu hawezi kusema kwamba mwanga kidogo mwanadamu huona ndani ya kurasa za Biblia huwakilisha mapenzi ya Mungu. Hata zaidi hakuwezi kusemwa kwamba kupata nuru kidogo kunamaanisha ufahamu wa Mungu. Watu ni wenye kujigamba na wenye majivuno na hawamshikilii Mungu katika mioyo yao. Wakiwa na uelewa mdogo wa mafundisho, wanajianzishia wenyewe na kuanzisha madhehebu mengi. Kwa bahati, hiyo ilikuwa Enzi ya Neema na Mungu hakuwa mkali na binadamu; madhehebu na faraka zote katika jina la Yesu zilifanyiwa kazi na Roho Mtakatifu isipokuwa wakati maalum ambapo kazi ya mapepo wachafu ilifanywa, hivyo wengi wa watu bado walifurahia neema ya Mungu.
Bila kujali kama ulimfuata mtu mwingine au hukuyakidhi mapenzi ya Mungu wakati ulimwamini Mungu awali, lazima uje mbele za Mungu katika kipindi cha hatua hii ya kazi ya siku za mwisho. Kama unaendelea kumfuata mtu kwa msingi wa kupitia hatua hii ya kazi, basi wewe utafikiriwa asiyesameheka, na utaishia kama tu Paulo. Kutoka mwanzoni, Niliwatumia Paulo na Petro kama mifano. Kwa nini? Hizi ni njia mbili tofauti. Kama mtu katika imani yake katika Mungu hatembei njia ya Petro, basi anatembea njia ya Paulo. Hizi ndizo njia mbili tu. Bila kujali kama wewe ni mfuasi aliye chini ama kiongozi, yote ni sawa. Usipoanza katika njia ya Petro, basi unatembea njia ya Paulo. Haliwezi kuepukwa, na hakuna njia ya tatu ya kutembea. Kama watu hawayaelewi mapenzi ya Mungu, hawamjui Mungu, hawatafuti kuuelewa ukweli na hawawezi kumtii Mungu kabisa, basi mwishowe lazima waishie kama Paulo. Kama hutafuti kumjua Mungu, hutafuti kuyaelewa mapenzi ya Mungu, lakini unatafuta tu kuongea na kujitayarisha na mafundisho, basi unaweza tu kumwasi na kumsaliti Mungu, kwa sababu asili ya binadamu ni kumsaliti Mungu. Vitu hivyo ambavyo havifuati ukweli vinaahidi kuwa vimetokea katika mapenzi ya binadamu. Mtu hawezi kusema yeye bado si mbaya sana, licha ya yeye kutoufuata ukweli. Baadhi husema: “Ingawa vitu hivi havijafanywa kulingana na ukweli, bado sifikiri kwamba vinamwasi Mungu.” Ukifanya chochote ambacho hakilingani na ukweli, basi kanaahidi kumwasi Mungu. Kama hakifanywi kulingana na ukweli, basi kimefanywa kulingana na mafundisho na mapenzi ya binadamu. Kitakuwa kimetokea kwa Shetani au kutoka kwa mapenzi ya binadamu. Huu ni uasi wa Mungu. Wale ambao hawautafuti ukweli, ingawa wanamwamini Mungu, hawana uwezo wa kumtii Mungu na wana uwezo tu wa kumwasi Yeye.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi MunguChanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni